JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

  Report Post
  Results 1 to 9 of 9
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,484
   Rep Power : 429504381
   Likes Received
   22048
   Likes Given
   68192

   Default Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

   “Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

   Maumivu kwenye matiti
   Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

   Maumivu mwilini
   Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

   Kutokwa damu bila kutegemea
   “Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Anaongeza kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

   Kuchoka
   Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

   “Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi,” anasema Goist.

   Chuchu kuwa nyeusi
   Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

   Kichefuchevu
   Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

   Mwili kuvimba
   Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea, na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito, na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

   Kwenda haja ndogo mara kwa mara
   Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

   Tamaa ya vitu mbalimbali
   Kutokana na mwili kuwa na ‘mzigo’ wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

   Kuumwa kichwa
   Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

   Kufunga choo
   Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.

   Kuwa na hasira
   “Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
   Kuongezeka kwa joto mwilini.

   Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna ‘mtoto anakuja’.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  2. Larusai Mux's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th October 2012
   Posts : 944
   Rep Power : 650
   Likes Received
   206
   Likes Given
   0

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Asante kwa elimu mkuu,

  3. TUKUTUKU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th September 2010
   Location : ISELAMAGAZI
   Posts : 11,845
   Rep Power : 429499370
   Likes Received
   3979
   Likes Given
   1443

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Mkuu wewe ni mwisho wa maneno,tunafaidika sana kupitia mabandiko yako!
   "A friend in need,is a friend indeed"

  4. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,166
   Rep Power : 138795851
   Likes Received
   23335
   Likes Given
   23325

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Huo mstari mzuri
   Dont study me, you won't graduate!!!

  5. KakaJambazi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th June 2009
   Posts : 11,070
   Rep Power : 119107432
   Likes Received
   3680
   Likes Given
   3133

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Huo mstari unamaanisha nn?

  6. Mgaya.com's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th June 2013
   Posts : 95
   Rep Power : 448
   Likes Received
   24
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By MziziMkavu View Post

   MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

   “Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

   Maumivu kwenye matiti
   Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

   Maumivu mwilini
   Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

   Kutokwa damu bila kutegemea
   “Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Anaongeza kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

   Kuchoka
   Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

   “Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtotzi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

   Tamaa ya vitu mbalimbali
   Kutokana na mwili kuwa na ‘mzigo’ wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

   Kuumwa kichwa
   Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

   Kufunga choo
   Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.

   Kuwa na hasira
   “Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
   Kuongezeka kwa joto mwilini.

   Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna ‘mtoto anakuja’.
   Tunashukuru kwa kutujuza

  7. 124 Ali's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th April 2010
   Posts : 3,015
   Rep Power : 2157664
   Likes Received
   818
   Likes Given
   669

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Quote By MziziMkavu View Post

   MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

   “Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

   Maumivu kwenye matiti
   Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

   Maumivu mwilini
   Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

   Kutokwa damu bila kutegemea
   “Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Anaongeza kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

   Kuchoka
   Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

   “Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi,” anasema Goist.

   Chuchu kuwa nyeusi
   Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

   Kichefuchevu
   Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

   Mwili kuvimba
   Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea, na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito, na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

   Kwenda haja ndogo mara kwa mara
   Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

   Tamaa ya vitu mbalimbali
   Kutokana na mwili kuwa na ‘mzigo’ wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

   Kuumwa kichwa
   Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

   Kufunga choo
   Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.

   Kuwa na hasira
   “Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
   Kuongezeka kwa joto mwilini.

   Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna ‘mtoto anakuja’.
   Asanye mzizi! ila bado sijakusamehe na links vituko zako za jana zisizofunguka!

  8. Mwana Mtoka Pabaya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd April 2012
   Posts : 5,101
   Rep Power : 2474
   Likes Received
   2487
   Likes Given
   763

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Aminia mkuu MziziMkavu, sasa fanya hisani: tumiminie jamvini dalili za mwanaume aliyetungisha mimba (ambaye amempa mwanamke mimba)
   Kama kweli bakora zinafundisha basi punda angekuwa profesa!

  9. Obama wa Bongo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th May 2012
   Location : mbagala
   Posts : 3,821
   Rep Power : 163307440
   Likes Received
   321
   Likes Given
   303

   Default Re: Dalili za kukujuulisha kuwa mwanamke ameshika mimba

   Quote By Mwana Mtoka Pabaya View Post
   Aminia mkuu MziziMkavu, sasa fanya hisani: tumiminie jamvini dalili za mwanaume aliyetungisha mimba (ambaye amempa mwanamke mimba)
   wewe mkali ndugu!kwani ulivyo mvimbisha shemeji ulijisikiaje?

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...