| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 763
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Penny hongera sana kwa kuwa mama mtarajiwa, Hiyo ni hatua muhimu sana kwenye maisha yako na ni vizuri kwa kuwa inaonesha umejiandaa kimwili na kiakili. Ni vizuri pia kama mwenzi wako pia akawa karibu na wewe kipindi hiki muhimu cha maisha yenu kama wazazi watarajiwa.
Kwa kawaida kipindi cha ujauzito kimegawanywa katika makundi matatu ya takriban miezi mitatu kila kundi. Miezi mitatu ya kwanza ni kipindi muhimu kuliko vyote kwa sababu ndo viungo vya mtoto vinaundwa na vipindi vingine ni ukuaji wa kawaida. Utumiaji wa dawa na vyakula vyenye kemikali ambazo zinaathiri mgawanyiko wa chembechembe za mwili ( cell division) haitakiwi kabisa kwa sababu zaweza kuharibu maumbile ya kiumbe au hata kuharibu mimba. Ni vizuri kupata maelekezo ya daktari kabla ya kutumia aina yoyote ya dawa. Kwa upande wa vyakula ni vizuri kutumia chakula bora ( balanced diet) ni muhimu kwa ukuajia wa mtoto na kwa afya yako pia. Vyakula vinavyoongeza damu ni muhimu sana matunda na mboga za majani, ni muhimu pia kunywa maji kwa wingi. Ukifikisha miezi mitano ya ujauzito anza clinic ya wajawazito kwenye hospitali au kituo karibu nawe. mambo muhimu ya kuzingatia: Damu au maji kutoka ukeni mtoto kupunguza kucheza maumivu makali ya tumbo Homa Kuvimba miguu Kuongezeka uzito kwa kasi sana ( > 5kg per month) etc.......... Uwaone wataalamu mapema. Otherwise kwa niaba ya wana JF nakutakia miezi tisa yenye utulivu na kila la kheri kwa kipindi chote cha ujauzito wako. regards |
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Penny
Hongera kwa kuwa Mama Mtarajiwa. |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Penny, Hongera sana mama.
|
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Penny hongera sana. uashauri aliokupa M/Jadi ni mzuri na cha kuongezea ule samaki kwa wingi na usifanye kazi nzito
|
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Kwa kuongezea tu fanya mazoezi ya kutembea kila siku hii itasaidia kupunguza uvimbe wa miguu na kuwa na nguvu mungu akikujalia kufika siku husika ya kupush. Be good woman hapo ndo sehemu pa kumshukuru mungu kwa kuweza kuhakikishiwa uzima wa kizazi chako.Kama mnyaji wa bia tumia pia Guness bia walau chupa moja kwa wiki inasaidia sana kuongeza damu kwa wingi ila ina alcohol content 7.5.Nazungumzia hivyo kwa kuwa mke wangu naye amepitia hatua hizo na sasa tuna mtoto wa kiume ambaye alizaliwa akiwa na kg 5. one week ago. God bless you Penny. |
|
#7
|
|||||||||||||||
|
|||||||||||||||
Kutofanya kazi nzito inategemeana na tabia za mimba. Reolaston.Kila mama mjamzito huwa anabehave tofauti kuna mwingine kuanzia day one mpaka mwisho ni mchapa kazi hivyo inategemeana na aina ya kazi uisemayo kama ni ya kutumia akili sana au uzito wa ukubwa (kgs tani) Mke wangu kuanzia day one mpaka mwisho alikuwa akifanya kazi na hakupa bed rest hata moja na wala hajawahi kutapika na uchungu umeaupatia kazini hivyo inategemana kwakweli siyo uniform kwa kila mtu. Nawasilisha. |
|||||||||||||||
|
#8
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Jamani nashukuruni sana tena sana. Simnaujua tena ukiwa tena mbali na wazazi inabidi mtu uulize mambo kwa wazoefu. Yani kwa kweli nimejisikia kama niko nyumbani kweli. Umoja wa JF uendelee hivi hivi jamani. Nitayafanyia kazi maushauri yenu ya nguvu. Mungu awabarikini sana tena sana.
|
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
|
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Wana JF hapo juu wamekupa ushauri mzuri wa ujumla kuhusu matunzo ya mimba, ushauri zaidi utaupata kiliniki kulingana hali yako, jitahidi kuuliza maswali bila kuogopa, kwa kuwa ushauri mwingine utakuwa specific kwako kulingana na watakavyokupima. Pia hakikisha vipimo vifuatavyo vimefanyika- Uwingi wa damu (Hb), kundi la damu na rizazi (BG&Rh), Kaswende (VDRL) na HIV. KUMBUKA HAKUNA MIMBA ILIYO SALAMA MPAKA UMEJIFUNGUA SALAMA, Nakutakia safari njema kuelekea LABOUR ROOM.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 10:27 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||