Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'
Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.
Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.
Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.
Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
Follow Us Here