Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

    Report Post
    Results 1 to 5 of 5
    1. #1
      armanisankara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2011
      Posts : 273
      Rep Power : 676
      Likes Received
      43
      Likes Given
      108

      Default Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

      MAMLAKA ya Kudhibiti Chakula na Dawa Nchini Marekani (FDA), imethibitisha na kupitisha matumizi ya kifaa kipya cha kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa kutumia mate.

      Kifaa hicho kilichotengenezwa na wanasayansi wa nchini humo, kimeelezwa kuwa na uwezo wa kutoa majibu sahihi kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kati ya dakika 20 na 40 baada ya kupima.
      Imeeleza kuwa kifaa hicho kilichopewa jina la OraQuick, kimebuniwa sio tu kwa ajili ya matumizi ya hospitalini bali pia nyumbani na kitaanza kupatikana katika maduka ya dawa nchini Marekani kuanzia Oktoba mwaka huu kabla ya kusambazwa nchi mbalimbali duniani.

      Serikali ya Marekani imesema inaamini kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia ya watu wanaoishi na virusi hivyo bila kujua.
      Wataalamu mbalimbali wa afya wamekielezea chombo hicho kuwa ni hatua nyingine kwa dunia katika jitihada zake za kudhibiti maambukizi ya VVU
      .
      Kinavyotumika
      Kwa umbo OraQuick hakina tofauti na vipimo vingine vya kisasa ambavyo vimebuniwa kwa ajili ya kupima magonjwa kwa haraka kama vile malaria, Ukimwi na kisukari.
      Lakini badala ya kuwa na sehemu ya kudondoshea tone la damu, kina sehemu laini iliyojitokeza, maalumu kwa ajili ya kunyonya mate.

      Mtumiaji hapaswi kukitemea mate, bali kwa kutumia sehemu hiyo maalumu, atakiingiza kifaa hicho mdomoni na kuchukua mate katikati ya fizi na midomo chini au juu.

      Sehemu hiyo laini italoa mate na kuyanyonya. Hapo mpimaji atapaswa kukiondoa kifaa hicho na kukiweka sehemu kavu kusubiri kimpatie majibu ndani ya muda huo wa kati ya dakika 20 na 40.

      Gharama zake
      Hakuna uhakika juu ya bei kamili ya kipimo hicho. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa kitauzwa kwa Dola za Marekani 17.50 sawa na Sh 27,300.
      J Mbungi likes this.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Daudi Mchambuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 6,176
      Rep Power : 1951
      Likes Received
      2994
      Likes Given
      13624

      Default

      Hicho ndo safi, nitakuwa najipima kila baada ya siku mbili bila uoga.

      Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

    4. #3
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,476
      Rep Power : 1115
      Likes Received
      467
      Likes Given
      952

      Default Re: Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

      uwezo kwa watanzania itakuwa janga gharama tu ndio inagomba maana wengi wanahongwa/kuhonga 1000-5000 wanaridhika kwa hii more 27000 ni ngumu sijui

    5. C6
      #4
      C6's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th April 2011
      Location : Mtaa Wa Saba
      Posts : 3,079
      Rep Power : 19360
      Likes Received
      1774
      Likes Given
      1513

      Default Re: Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

      mimi nilisikia muda kuhusu idea ya kifaa hiki pia nilisoma jinsi kinavyofanya kazi, wataalamu waligundua kuwa chembe chembe ambazo hupigana na virusi kama vinavyosababisha ukimwi etc, hupatikana pia kwenye mate, kwa kutumia kifaa hiki inakuwa rahisi kujipima since huitaji kujitoboa, wala damu coz watu wengine huogopa kuona damu

    6. #5
      bornagain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Location : Nyakanazi - Biharamulo
      Posts : 1,612
      Rep Power : 692
      Likes Received
      438
      Likes Given
      320

      Default Re: Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

      Kitakachofaa ni cha kupima kwa macho lakini hata walete cha kipima sijui hewa ni kazi bure maana kinachotakiwa ni namna ya kuzuia maambukizi yasienee kwa kasi.Sasa hata icho cha kupima mate kikija hapa bongo msaada wake nini hasa tofauti na hivi tulivonavo vinavopima damu
      There is a saying in aviation "You haven't crashed until you've crashed. Until then, keep flying the plane".

    7. RukaaJuu Final

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...