Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kabichi ni kinga zidi ya Ugonjwa wa Kensa Cancer Disease

    Report Post
    Results 1 to 4 of 4
    1. #1
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8047
      Likes Given
      26489

      Default Kabichi ni kinga zidi ya Ugonjwa wa Kensa Cancer Disease


      Ugonjwa wa saratani
      (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo.

      Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.

      Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya.

      Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana wanaopenda kula mboga hii.

      Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

      KINGA DHIDI YA SARATANI
      Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.

      Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

      Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;
      ‘Antioxidant’, ‘Anti-inflammatory’ na ‘Glucosinolates,’ ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

      Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

      AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO

      Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

      HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
      Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

      VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI

      Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

      Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    2. Study Abroad

    3. #2
      BornTown's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2008
      Location : ???
      Posts : 1,482
      Rep Power : 863
      Likes Received
      283
      Likes Given
      104

      Default Re: Kabichi ni kinga zidi ya Ugonjwa wa Kensa Cancer Disease

      Asante Mkuu! Mie ninatatizo la vidonda vya tumbo sasa hiyo juisi ya kabichi ndio inatengenezwaje
      "DONT BE A WOMAN THAT NEEDS A MAN BE A WOMAN A MAN NEEDS!!!!"

    4. #3
      shin's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kabichi ni kinga zidi ya Ugonjwa wa Kensa Cancer Disease

      sawa dk lakin kwa mfano kebich ukipika iive sana au na pia nasikia kebich nyekundu ndio nzuri au ilimradi iwe kebich na je kama kachumbari iweje?

    5. #4
      shin's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kabichi ni kinga zidi ya Ugonjwa wa Kensa Cancer Disease

      Ninatatizo linanisumbua muda mrefu takriban 5yrs mimi ni mweupe wa asili, lakini nimepatwa na mabaka meusi kwenye paji la uso na kwenye mashavu. Hali hii ilianza tangu kushika ujauzito hadi sasa. Nimeenda kwa specialist wa ngozi akahihi ugonja na kuniandikia vipimo, lakini majibu kutoka ugonjwa sina. akanieleza huwa watu weupe wnaathirika na mionzi ya jua kwa kua ngozi zao ni lain. akaniandikia nitumie sunblock kwa ajili ya kuzuia jua. lakin haikunisaidia kwa kweli nimetumia vitu vingi wakati wengine wananiambia nijaribu kutumia sonaderm itanisaidia lakini nimegonga mwamba.

      Alama hizi kwa sasa nikiwa mwezini (kwenye hedhi) zinakolea sana, na wakati mwingine zinaisha kabisa. Bado mpaka sasa sijapata majibu kwani hata siki hizi ukipita njian watu weupe utawaona na alama hizi.

      Nipen pole mwenzenu sura inaharibika sana.

    6. FemaTV & Radio

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...