Wanawake nchini
wametakiwa kubadilika
kwa kuacha kutumia
vipodozi vyenye madhara
mwilini na kuachana na
dhana kuwa ukiwa
mweupe au kuwa na
mapaja manene
unapendwa zaidi.
Hayo yamesemwa na
Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA), Kanda ya
Kati, Florent Kyomo.
Kyomo amesema kuwa,
asilimia kubwa ya
waathirika wa vipodozi ni
wanawake hasa wale
wenye uelewa mdogo
ambao hawataki
kubadilika kwa kudhani
kuwa weupe ni moja ya
mafanikio na kupendwa
zaidi na wanaume.
Ameongeza kuwa,
changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo ni
uelewa wa wananchi juu
ya matumizi ya vipodozi
vyenye madhara ambapo
wengi wao wanashindwa
kuacha kutumia kutokana
na kutumia madawa hayo
kwa muda mrefu na
kufafanua kuwa, hata
hivyo kuwa wataendelea
na mikakati ya kutoa
elimu zaidi ili watu wengi
wajue madhara na kuwa
na dhamira ya kuacha
kutumia vipodozi hivyo.

Reply With Quote

Follow Us Here