Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Maradhi ya kiharusi (stroke)

    Report Post
    Results 1 to 14 of 14
    1. #1
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Maradhi ya kiharusi (stroke)

      Maana ya Kiharusi











      Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.


      Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo na ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24. Muda wa masaa 24 umechukuliwa ili kutofautisha kiharusi na kiharusi cha kukosa oksijeni katika ubongo (ischemia) ambacho hutokea na kudumu kwa muda mfupi yaani (transient ischemic attack).


      Kwa kawaida dalili za TIA hupotea na mtu kurudia hali yake ya kawaida ndani ya masaa 24.





      Aina za kiharusi


      Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea (visababishi vyake). Aina hizo ni


      1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)


      Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.


      Aina hii ya kiharusi husababishwa na nini?


      Aina hii ya kiharusi husababishwa na


      Damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis) au
      Kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism)
      Kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla kwa mfano shock.
      Vena thrombosis
      2. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya Ubongo (Haemorrhagic Stroke)


      Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.


      Visababishi vya Kiharusi (kwa ujumla)


      Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis) hiyo. Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza kuathirika na tatizo hili ni pamoja na arteri za common carotid na interior carotid arteries, na arteri za vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo.
      Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgojwa wa sickle cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha Kiharusi.
      Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis) huweza kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.
      Upungufu wa usafirishaji damu mwilini (systemic hypoperfusion) - Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha (Ischaemic Heart Diseases) au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje (pericardial effusion) au kupungua kwa damu mwilini, kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa. Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.
      Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo (Intracerebral hemorrhage).
      Dalili za kiharusi


      Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa.


      Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa ( Cerebellum) itaadhirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.
      Iwapo sehemu ya ubongo wa kati (cerebral cortex) itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea,kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri, kuwa na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wakw wa kufikiri, kuchanganyikiwa, na kubadilika kwa mwendo wa harakati za hiari.
      Iwapo mgonjwa ataadhirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona; kulegea kwa misuli ya macho (ptosis); kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande); kupungua uwezo wa kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja; kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti; mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.
      Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na hisia mtetemo.
      Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.


      Vipimo


      Mionzi
      CT-scan
      MRI
      PET
      SPECT
      Vipimo vingine ni;


      ECG, ECHOCARDIOGRAM huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo
      Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi
      Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.
      Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu
      Vihatarishi vya kiharusi


      Vitu vinavyoweza kumuweka mtu katika hatari ya kupata kiharusi ni pamoja na


      Shinikizo la damu lisilothibitiwa
      Kisukari
      Uvutaji sigara
      Unywaji pombe kupita kiasi
      Kutofanya mazoezi kabisa
      Fetma (obesity)
      Kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu
      Atrial fibrillation
      Matibabu


      Matibabu ya kiharusi hutegemea pia aina na visababishi vyake .


      1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke)


      Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.


      2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke)


      Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Angalizo: ni hatari kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana uhatarisha maisha ya mgonjwa badal ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.


      Huduma na Matunzo kwa mgonjwa wa Kiharusi


      Mojawapo ya mambo muhimu ya kufanya kwa mgonjwa aliyepata kiharusi ni kumuongoza na kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Hapa uhitaji ushirikiano wa wauguzi, wataalamu wa viungo, wataalamu wa ushauri wa kazi na daktari. Kuna umuhimu pia wa kuwaelimisha ndugu kuhusu hali ya mgonjwa ili waweze kumsaidia katika matunzo yake nyumbani na kwenye jamii inayomzunguka.


      Matarajio (prognosis)


      Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao na kuajiriwa. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja.


      Ulemavu wa kimwili ni pamoja na


      Ulegevu wa misuli
      Kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika
      Kujikojolea
      Kutoona vizuri
      Kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku
      Vichomi
      Vidonda shinikizo
      Kukosa hamu ya chakula.
      Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama


      Mgonjwa kuwa na wasiwasi
      Hofu ya mashambulizi, na
      Unyongovu.
      Jinsi ya kuzuia kiharusi


      Zuia au tibu shinikizo la damu
      Dhibiti kisukari
      Fanya mazoezi
      Acha kuvuta sigara
      Punguza uzito
      Acha kunywa pombe kupita kiasi
      Tumia Junior Aspirin
      Kula chakula kisichokuwa na mengi na kisicho na chumvi nyingi.
      Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini (statins)kwa mfano Simvastatin
      http://www.tanzmed.com/index.php/mag...iharusi-stroke
      Boflo and Red Giant like this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      Asante; je chance ya kupona kwa watu waliopata stroke ikoje. Kupona nikiwa na maana ya kutokufa, hata kama atakuwa mlemavu?
      MziziMkavu likes this.

    4. #3
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      Quote By nyumba kubwa
      Asante; je chance ya kupona kwa watu waliopata stroke ikoje. Kupona nikiwa na maana ya kutokufa, hata kama atakuwa mlemavu?
      ipo chance ya kupona ikiwa kama atawahi kutumia dawa za tiba mbadala.

      Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao na kuajiriwa. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja.




      Ulemavu wa kimwili ni pamoja na




      Ulegevu wa misuli
      Kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika
      Kujikojolea
      Kutoona vizuri
      Kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku
      Vichomi
      Vidonda shinikizo
      Kukosa hamu ya chakula.
      Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama




      Mgonjwa kuwa na wasiwasi
      Hofu ya mashambulizi, na
      Unyongovu nyumba kubwa
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    5. #4
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,669
      Rep Power : 21308
      Likes Received
      10026
      Likes Given
      13923

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      binafsi nashukuru sana naleo nirudie for the second time kukushukuru MziziMkavu u played your role on ma moms treatment and now she walks and talk as normal. Hakuna tena kutetemeka wala kushindwa kutumia sehem za mwili wake and hata uso umerudi to its normal position.

      Mkuu ktika watu ambao huwa najiskia kuwaombea kwa Mungu ni wewe you said it nikajaribu now mma ni mzima kabisa. Umeshiri katika kuisimamia furaha yangu duniani MziziMkavu.

      nawashauri wana jf doctors wawe wanatilia maanani ushauri wanaopewa na madatari hapa huwa unasadia sana.
      MziziMkavu and Mwanaweja like this.

    6. #5
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      Quote By gfsonwin
      binafsi nashukuru sana naleo nirudie for the second time kukushukuru MziziMkavu u played your role on ma moms treatment and now she walks and talk as normal. Hakuna tena kutetemeka wala kushindwa kutumia sehem za mwili wake and hata uso umerudi to its normal position.

      Mkuu ktika watu ambao huwa najiskia kuwaombea kwa Mungu ni wewe you said it nikajaribu now mma ni mzima kabisa. Umeshiri katika kuisimamia furaha yangu duniani MziziMkavu.

      nawashauri wana jf doctors wawe wanatilia maanani ushauri wanaopewa na madatari hapa huwa unasadia sana.
      Asante na wewe Mama yetu Mwenyeezi Mungu atampa afaya njema inshallah. gfsonwin
      gfsonwin likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    7. Miaka 50

    8. #6
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      Unajua nimekuwa interested na hii thread kwa kuwa my dady amepatwa na stroke recently ya upande mmoja, yeye ni aged kiasi 73 years na naweza sema ni over weight. Yani nimetoka ku google kuhusu stroke tu naingia JF doctor nakuta huu uzi.

      Napenda baba yangu apone hata kama atakuwa na ulemavu that's why nimeuliza chance ya kupona. Yeye aligunduliwa kuwa ana pressure hata mwaka haujaisha amepata stroke. Mimi niko mbali lakini najua yuko na madaktari bingwa ingawa these days naamini kuwa tunapaswa kutafuta additional medical information whenever possible, hasa katika ulimwengu wa sasa wa IT.

      Nashukuru sana kwa kunipa moyo kuwa anaweza kuishi au hata kupona.
      MziziMkavu likes this.

    9. #7
      Red Giant's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2012
      Posts : 730
      Rep Power : 3610
      Likes Received
      233
      Likes Given
      282

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)

      mkuu mzizi big up sana. pale umesema ni vizuri kuwa makini kutoa dawa za kuyeyusha damu ni kweli kabisa kama vile asprin au clopidogrel sababu utaifanya damu kuwa nyepesi zaidi na hivyo kuvuja kirahisi kwenye ubongo.
      MziziMkavu likes this.
      COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND

    10. #8
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)



      What Is a Stroke?

      Stroke is a medical emergency and a leading cause of death in the U.S. It occurs when a blood vessel in the brain bursts or, more commonly, when a blockage develops. Without treatment, cells in the brain quickly begin to die. The result can be serious disability or death. If a loved one is having stroke symptoms, seek emergency medical attention without delay.




      Stroke Symptoms

      Signs of a stroke may include:

      • Sudden numbness or weakness of the body, especially on one side.
      • Sudden vision changes in one or both eyes, or difficulty swallowing.
      • Sudden, severe headache with unknown cause.
      • Sudden problems with dizziness, walking


      Stroke Test: Talk, Wave, Smile

      The F.A.S.T. test helps spot symptoms. It stands for:
      Face. Ask for a smile. Does one side droop?
      Arms. When raised, does one side drift down?
      Speech. Can the person repeat a simple sentence? Does he or she have trouble or slur words?
      Time. Time is critical. Call 911 immediately if any symptoms are present.


      Stroke: Time = Brain Damage

      Every second counts when seeking treatment for a stroke. When deprived of oxygen, brain cells begin dying within minutes. There are clot-busting drugs that can curb brain damage, but they have to be used within three hours of the initial stroke symptoms. Once brain tissue has died, the body parts controlled by that area won't work properly. This is why stroke is a top cause of long-term disability.

      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    11. #9
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)


      Diagnosing a Stroke

      When someone with stroke symptoms arrives in the ER, the first step is to determine which type of stroke is occurring. There are two main types, and they are not treated the same way. A CT scan can help doctors determine whether the symptoms are coming from a blocked blood vessel or a bleeding one. Additional tests may also be used to find the location of a blood clot or bleeding within the brain



      Ischemic Stroke

      The most common type of stroke is known as an ischemic stroke. Nearly nine out of 10 strokes fall into this category. The culprit is a blood clot that obstructs a blood vessel inside the brain. The clot may develop on the spot or travel through the blood from elsewhere in the body.


      Hemorrhagic Stroke

      Hemorrhagic strokes are less common but far more likely to be fatal. They occur when a weakened blood vessel in the brain bursts. The result is bleeding inside the brain that can be difficult to stop.

      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    12. #10
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)



      'Mini-Stroke' (TIA)

      A transient ischemic attack, often called a "mini-stroke," is more like a close call. Blood flow is temporarily impaired to part of the brain, causing symptoms similar to an actual stroke. When the blood flows again, the symptoms disappear. A TIA is a warning sign that a stroke may happen soon. It's critical to see your doctor if you think you've had a TIA. There are therapies to reduce the risk of stroke.


      What Causes a Stroke

      A common cause of stroke is atherosclerosis -- hardening of the arteries. Plaque made of fat, cholesterol, calcium, and other substances builds up in the arteries, leaving less space for blood to flow. A blood clot may lodge in this narrow space and cause an ischemic stroke. Atherosclerosis also makes it easier for a clot to form. Hemorrhagic strokes often result from uncontrolled high blood pressure that causes a weakened artery to burst.


      Risk Factors: Chronic Conditions

      Certain chronic conditions increase your risk of stroke. These include:

      • High blood pressure
      • High cholesterol
      • Diabetes
      • Obesity

      Taking steps to control these conditions may reduce your risk.

      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    13. #11
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)


      Risk Factors: Behaviors

      Certain behaviors also increase the risk of stroke:

      • Smoking
      • Getting too little exercise
      • Heavy use of alcohol



      Risk Factors: Diet

      A poor diet may increase the risk for stroke in a few significant ways. Eating too much fat and cholesterol can lead to arteries that are narrowed by plaque. Too much salt may contribute to high blood pressure. And too many calories can lead to obesity. A diet high in fruits, vegetables, whole grains, and fish may help lower stroke risk.



      Risk Factors You Can't Control

      Some stroke risk factors are beyond your control, such as getting older or having a family history of strokes. Gender plays a role, too, with men being more likely to have a stroke. However, more stroke deaths occur in women. Finally, race is an important risk factor. African-Americans, Native Americans, and Alaskan Natives are at greater risk compared to people of other ethnicities.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    14. #12
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)



      Stroke: Emergency Treatment

      For an ischemic stroke, emergency treatment focuses on medicine to restore blood flow. A clot-busting medication is highly effective at dissolving clots and minimizing long-term damage, but it must be given within three hours of the onset of symptoms. Hemorrhagic strokes are more difficult to manage. Treatment usually involves attempting to control high blood pressure, bleeding, and brain swelling.


      Stroke: Long-Term Damage

      Whether a stroke causes long-term damage depends on its severity and how quickly treatment stabilizes the brain. The type of damage depends on where in the brain the stroke occurs. Common problems after a stroke include numbness in the arms or legs, difficulty walking, vision problems, trouble swallowing, and problems with speech and comprehension. These problems can be permanent, but many people regain most of their abilities.


      Stroke Rehab: Speech Therapy

      Rehabilitation is the centerpiece of the stroke recovery process. It helps patients regain lost skills and learn to compensate for damage that can't be undone. The goal is to help restore as much independence as possible. For people who have trouble speaking, speech and language therapy is essential. A speech therapist can also help patients who have trouble swallowing.





      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    15. #13
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)


      Stroke Rehab: Physical Therapy

      Muscle weakness, as well as balance problems, are very common after a stroke. This can interfere with walking and other daily activities. Physical therapy is an effective way to regain strength, balance, and coordination. For fine motor skills, such as using a knife and fork, writing, and buttoning a shirt, occupational therapy can help.


      Stroke Rehab: Talk Therapy

      It's common for stroke survivors and their loved ones to experience a wide range of intense emotions, such as fear, anger, worry, and grief. A psychologist or mental health counselor can provide strategies for coping with these emotions. A therapist can also watch for signs of depression, which frequently strikes people who are recovering from a stroke



      Stroke Prevention: Lifestyle

      People who have had a stroke or TIA can take steps to prevent a recurrence:

      • Quit smoking.
      • Exercise and maintain a healthy weight.
      • Limit alcohol and salt intake.
      • Eat a healthier diet with more veggies, fish, and whole grains.


      Stroke Prevention: Medications

      For people with a high risk of stroke, doctors often recommend medications to lower this risk. Anti-platelet medicines, including aspirin, keep platelets in the blood from sticking together and forming clots. Anti-clotting drugs, such as warfarin, may be needed to help ward off stroke in some patients. Finally, if you have high blood pressure, your doctor will prescribe medication to lower it.



      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    16. #14
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8048
      Likes Given
      26489

      Default Re: Maradhi ya kiharusi (stroke)



      Stroke Prevention: Surgery

      In some cases, a stroke results from a narrowed carotid artery -- the blood vessels that travel up each side of the neck to bring blood to the brain. People who have had a mild stroke or TIA due to this problem may benefit from surgery known as carotid endarterectomy. This procedure removes plaque from the lining of the carotid arteries and can prevent additional strokes.




      Stroke Prevention: Balloon and Stent

      Doctors can also treat a clogged carotid artery without major surgery in some cases. The procedure, called angioplasty, involves temporarily inserting a catheter into the artery and inflating a tiny balloon to widen the area that is narrowed by plaque. A metal tube, called a stent, can be inserted and left in place to keep the artery open.





      Life After a Stroke

      More than half of people who have a stroke regain the ability to take care of themselves. Those who get clot-busting drugs soon enough may recover completely. And those who experience disability can often learn to function independently through therapy. While the risk of a second stroke is higher at first, this risk drops off over time.

      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    17. Study Abroad

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...