Maambukizi kwenye njia ya mkojo
Information Description
Wanawake na wanaume wanaweza kupata maambukizo kwenye njia ya mkojo, lakini zaidi kwa wanawake kwa sababu ni rahisi bakteria kuingia kwenye njia ya mkojo. Dalili za maambukizo ni:
• Kutaka kukojoa mara kwa mara
• Kusikia maumivu makali wakati wa kukojoa
• Mkojo kuchanganyikana na damu.
Maambukizi haya yanaweza kuepukwa kwa kujiweka safi hasa kwa kusafisha eneo la via vya uzazi kila siku na kuhakikisha unanawa baada ya kwenda haja kubwa. Wakati wote unasafisha kutoka mbele kuelekea nyuma. Ukisafisha
kutoka nyuma kwenda mbele unaweza kusambaza bakteria kutoka kwenye haja kubwa kwenda kwenye tundu la
mkojo. Hatua nyingine za kuchukua ili kuepuka maambukizo haya ni kunywa maji mengi; kukojoa mkojo mara kwa mara (usijaribu kubana mkojo kwa muda mrefu) na hasa baada ya ujamiiana, na kuvaa chupi za pamba na nguo pana zinazoweka sehemu za siri kavu.
Iwapo unafikiri unayo maambukizo kwenye mrija wa kupitisha mkojo, kunywa maji mengi na nenda
kamwone mhudumu wa afya kwa ajili ya matibabu. Usijamiiane mpaka dalili zote ziwe zimetoweka.
Follow Us Here