Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

    Report Post
    Page 9 of 18 FirstFirst ... 7891011 ... LastLast
    Results 161 to 180 of 348
    1. #1
      Mrs Mtaba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st January 2009
      Location : Denmark
      Posts : 104
      Rep Power : 546
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Red face Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      #1:
      Za leo wandugu, naomba kuuliza na kutaka kujua.

      Mimi niko kwenye ndoa ya kama miaka 2 sasa. Kwa kweli imekuwa na furaha zake pia ni vikwanzo vingi. Imefikia sasa mimi najishangaa sana kuwa nimeishiwa hamu kabisa na mme wangu na ninamuona mbaya sana. Nakaa na kujiuliza ilikuwaje mpaka nikaolewa nae.

      Namefikia hatua yakufanya mambo ili nimuudhi aniache tuu.

      Sijui sasa nifanye nini zaidi cha kumuudhi, nisaidieni.

      #2:
      Quote By Najuah
      Natumaini wote ni wazima wa afya inshalaah.

      Kwa kifupi Nina rafiki yangu mpendwa (Msichana) ana tatizo ambalo kwa kweli mi sijui hata nimsaidiaje, ni meona si vibaya kuliweka hewani tukasaidiana mawazo.

      Ni binti mwenye umri wa miaka 23 tatizo lake kubwa hajawahi katika maisha yake yote toka avunje ungo kujiskia hamu ya kufanya mapenzi. Ana mpenzi ila mara nyingi wakiwa faragha huwa kama anamfurahisha mwezake kwa sababu hana anacho jiskia hata aguswe wapi. Mara ya kwanza kunieleza mi nilimshauri aende hospitali akaonane na dakatari wa wanawake huenda Homoni za kike zikawa zimepungua au akagundulika tatizo lingine lolote linalo weza kusababisha hiyo hali; Nashukuru Mungu kwani alinisikiliza na kwenda hospitali ya regency ila majibu yalipo toka alionekana kila kitu kiko normal.

      Sasa sijui hata nimsaidiaje coz kuna kipindi nilimuuliza kama huwa anaota ndoto za mapenzi mara kwa mara kwa sababu nilisha wahi kusikia hata kusoma kwenye vitabu kuwa kama una Jini Mahaba basi kuna uwezekano hali kam yake ikajitokeza; ila ilinihakikishia kuwa hajawahi hata siku mwoja kuota ndoto za namna hiyo. Jamaa yake anampenda sana na hivi majuzi jamaa ansema anataka kuja kutoa posa ili ajichukulie jumla jumla anahisi atateseka sana kwenye ndoa coz hata pata hiyo raha ya chakula cha ndoa.

      Naomba tumsaidie jamani afanyaje??
      #3:
      Quote By Brandon
      Habari za kazi wandugu,

      nipo tutani naomba msaada wenu ili niweze kumfurahisha mpenzi wangu. Lately nimekuwa sina hamu ya kufanya mapenzi kabisa hata nikifanya nakuwa natimiza wajibu tu ili mwenzangu asijisikie kua simjali coz ananipenda sana na ninampenda sana. Nifanyaje ili niweze pata hamu na kufurahia mapenzi?

      Asanteni sana.
      #4:

      Quote By PSI Factor
      Ni post yangu ya kwanza kwenye jukwaa hili na nimefikia uamuzi wa kuandika hapa kwakuwa nimeona wadau wengi wakitoa maoni ambayo kweli yanaonyesha kusaidia.

      Tatizo langu ni dogo kwa wengine lakini kwangu kubwa sana. Mke wangu hana hamu ya tendo la ndoa na inakuwa vigumu kuweza kumlazimisha tufanye tendo hilo kwani najiona kama namwonea. Mimi nakuwa na ashki sana lakini sina jinsi hivyo nalazimika kuvumilia. Sijafikiria kutoka nje ya ndoa kwani sidhani kuwa hili litakuwa suluhisho la tatizo langu.

      Kabla hajajifungua hali ilikuwa nzuri (kiasi) lakini baada ya kujifungua mtoto wa kwanza tu, hali imekuwa mbaya sana. Hana hamu kabisa, hata ninapojitahidi kumwandaa anaamua kuruhusu tufanye tu ili mradi niridhike.

      Tuna watoto wawili, wote wa kike.

      Tofauti na hili, sina tatizo jingine kwenye ndoa lakini kama sijajitutumua naweza kukosa tendo hili muhimu hata kwa mwaka kwakuwa yeye haoni umuhimu wake sana.

      Anatambua tatizo hili, tumelijadili mara kadhaa lakini hatujajua ni daktari gani tumwendee na dawa gani zaweza kutumika.

      Nampenda mke wangu, namwonea huruma kwa hali hii na naamini huenda siku moja nikapata tiba ya tatizo hili. Wenzangu mmewahi kukumbana na hali hii? Mliikabili vipi? Kuna dawa? Kuna daktari?

      #5:
      Quote By Bugota
      Habari za leo wana JF. Natumaini hamjambo wote.

      Ndugu zangu naombeni ushauri. Mimi nina miaka 2 kwenye ndoa yangu. Tumepata mtoto mmoja. Mke tangu mwanzo alikuwa ni mtu mwenye kuyaweza mambozi kweli kweli. Lakini tangu nilipoanza kazi za migodini, nikirudi likizo nimekuwa nikiona mke wangu haoneshi kuwa na hamu ya kukutana na mimi kana kwamba tulikuwa wote muda wote. Pia ukifanya majambozi nagundua kuwa ishu yake imelegea, ina maji maji kibao tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa tight, kavu tena ya moto; haoneshi ushirikiano wakati wa majambozi.
      Nilipomuulika akaanza kudai o mara unajua nakuwa na mawazo juu ya nyumbani mara oh unajua mtoto ananinyonya sana.

      Nakuwa na wasiwasi huenda anachakachuliwa.

      Naomba ushauri jamani.
      Ushauri wa wadau:

      Soma hii post: http://www.jamiiforums.com/jf-doctor...ml#post4104552

      Quote By matambo
      Low libido

      Libido naturally diminishes as men age. Testosterone, the hormone primarily responsible for sex drive, begins to decline in the body by about 1 percent every year beginning around the age of 30. This is perfectly natural, though healthy men can take steps to boost libido at virtually any time in life. “There is no age beyond which sex drive is not possible or therapeutically helpful,” says Dr. David Plourd of the Naval Medical Center in San Diego.

      However, a drooping libido can also indicate an unhealthy body or mind. Most notably, low testosterone is a symptom of excess body fat, since fat both inhibits testosterone production and breaks down testosterone already in the system. Depression, anxiety and stress can each reduce libido, as can excessive alcohol intake.

      Note that sexual drive and erections are discrete physiological matters: Libido is determined by testosterone, while erections are dependent on blood flow and nerve sensitivity.

      Possible indications:
      • Obesity
      • Diabetes
      • Mumps
      • Tumors on pituitary or hypothalamus
      • Excessive alcohol intake
      • Sedentary lifestyle
      • Depression
      • Anxiety
      • Stress

      What to do:
      • Improve your diet and exercise
      • Reduce abdominal fat
      • Consider talking to a shrink
      • Get a blood test
      Quote By Kiroroma
      For men with little sexual desire it is sometimes enough to have one or a few conversations in which they can express their feelings and ask questions about the extent to which their situation is abnormal.

      Counselling about reduced desire in stressful situations like death, unemployment, disease of the partner or stress at work can be sufficient. If all sexual interest has disappeared, and there is no masturbation either, the hormonal regulation should be examined. When anomalies in this are found, medication can be prescribed.

      There are no standard treatments for a reduced interest in sex. Depending on the causes of the complaints a treatment will be set up. Physical causes are also treated depending on the cause. The lack of interest in making love due to certain medication is treated by using other medication or another dose. Psychological causes can best be determined and treated by a sexologist.

      Psychotherapy, which studies and treats the psychological causes, can be important in this. It is important to understand that thoughts often go through the mind while making love which negatively influence the interest in sex. Social influences, e.g relation problems, stress at work, etc. are treated by relation therapy or psychotherapy. A sexologist can use different forms of therapy to determine and possibly influence the thoughts about sex.
      AshaDii likes this.

    2. Miaka 50

    3. #161
      PSI Factor's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st April 2011
      Posts : 16
      Rep Power : 412
      Likes Received
      2
      Likes Given
      11

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Quote By Prissy k
      Pole sana kaka yangu itakuwa mkeo kaasirka kisaikolojia baada yakupata maumivu makal wakat wakujfungua jarbu kutafuta wataalamu wa magonjwa ya wanawake ila sikushauri uende kwa waganga tiba pekee mtafute gynacologist
      Asante Prissy,

      Gynacologist nitampata hospitali gani kwa Dar es Salaam?

      Quote By Leornado
      Wanawake wengi wanakumbwa na tatizo hilo, mara nyingi inasababishwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kifamilia, tohara, uzazi na malezi au kutokuridhishwa na mwenzi hivyo hawaoni umuhimu wa kufanya hilo tendo manake mwenza hamridhishi ipasavyo.

      Jaribu kumshauri mkeo amuone daktari wa wanawake au mtaalamu wa saikolojia pengine itasaidia.

      Pole sana mkuu.
      Leo,

      Mke wangu hajatahiriwa, hana shida kifedha, hana matatizo ya kifamilia ya kumfanya awe na msongo wa mawazo.

      Inawezekana simridhishi? Sidhani, labda, lakini nimemuuliza mara nyingi na anadai ni tatizo lake na si langu. Anajisikia vibaya kuwa hivi.

      Kama ni kwenda kwenye mzunguko wakati wa mechi, basi mi hata round 5 naenda bila kuchoka. Na si hivyo tu, naielewa kazi yangu kwa mke.

      Quote By First Born
      Mpaka mmekuwa na idadi hiyo ya wtoto kutakuwa na sababu zinazomfanya akose hamu ya tendo takatifu
      fikiria sana huenda umemuudhi mke wako, huenda hauko fresh kwenye kazi(inamfanya aone kama tendo hilo ni usumbufu tu)
      mkalishe chini mmbebeleze akuambie sababu kwa ajili ya kuboresha penzi lenu!!!!!!!!!
      Watoto ni wadogo bado, mmoja ana miaka 5, mwingine ana miaka 2. Wote wanasoma na kuna wafanyakazi wa ndani wanaowahudumia watoto kwakuwa mama watoto nilimshauri aende kujiendeleza walau apate hata Masters.

      Kama nilivyomjibu Leo hapo juu, sifikirii kuwa ni suala la kutojiweza kazini. Kwa usemi huu labda nijaribu nje ili niweze kuambiwa uwezo wangu ukoje huenda yeye ananificha?

      Natamani angekuwa anaingia JF akayaona maoni yenu.
      Quote By Bajabiri
      Pole sana mdau,wanandoa watakusaidia
      Asante mkuu, yanaweza kukuta haya ukioa/olewa.

      Quote By nyumba kubwa
      Pole sana. Umetoa maelezo ya kina na yatasaidia kupata mawazo ya kukusaidia. Ila labda ungesema watoto wenu wana umri gani nina maana kuwa kama ni wadogo sana labda wana mkeep busy na anakuwa amechoka sana.

      Otherwise muwe mnatafuta siku mna spend night or two mbali na watoto. Inawezekana watoto wamereplace feelings zake kwako au wanamchosha.

      Haya mambo najua yapo ila ni ya muda mfupi sana hasa mtoto akiwa mdogo, ila kama ni ya muda mrefu ni tatizo.

      Nimekumbuka kitu. Je mkeo anatumia njia za uzazi wa mpango? Nasikia zinapoteza hamu kabisa.
      Mkuu Nyumba Kubwa,

      Umri wa watoto nimeutaja hapo juu, mke wangu hapendi kwenda mbali na watoto, hatuwezi kusafiri pamoja mbali tukawaacha watoto akajisikia vema. Labda nimshawishi tena lakini nijuavyo hawezi kusafiri akawaacha, lazima tuwabebe.
      Quote By Nyangomboli
      Humridhishi au kuna kitu kikubwa ulimuudhi na hakupendi tena ila ndoa inamdhibiti na hawezi kuamua vinginevyo. Au alipata mtu nje anaemfanya akajisikia vizuri.

      Nilishawahi kumfanya mke wa mtu bila kujua na nilipojua ilikuwa too late ila aliniambia ukweli kama jamaa alikuwa hana hamu nae tena na akitaka uroda humutegea tu anahema zake mpaka basi kwani anamuona kama anamchafua tu.

      Fanya utafiti vyema utagundua tatizo liko wapi.
      Simridhishi? Naona wengi ndivyo mnavyofikiria kwa haraka.
      Anatembea nje? Hapana, ninavyomjua mke wangu hawezi kufanya hivyo. Ni mwaminifu sana, ni tatizo ambalo nahisi lina chanzo na huenda kuna aliyewahi kukumbana na hali hii anaweza kuiona hii thread na kunipa uzoefu wake
      I know that I am intelligent, because I know that I know nothing...

    4. #162
      Kimbojo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2009
      Posts : 298
      Rep Power : 573
      Likes Received
      40
      Likes Given
      26

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Pole mh. inatokea kwa baadhi ya wanawake hasa wanapokuwa na msongo wa mawazo,wako bize na watoto, au antumia vidonge vya uzazi wa mpango. Kwa nature ya kabila la mkeo haya yaweza kuwa sababu, chunguza kwa kuwa nae karibu saana.

    5. #163
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Kuna swali nimeuliza hujajibu. Anatumia dawa za uzazi wa mpango?? Mimi sijawahi tumia hizo dawa ila nina rafiki yangu alinambia alijaribu kutumia zilimfanya aone kama mumewe anambaka kwani hakuwa na feelings za kushiriki hilo tendo kabisa. Alipoamua kudrop kutumia hizo dawa amerudi kwenye hali yake ya zamani.

      Kingine umesema mkeo hawezi kuwaacha watoto lazima mwende nao. Hiyo tayari ni dalili ya tatizo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa ameamisha mapenzi kwa watoto. Anahitaji counselling.

      Watoto wa miaka 5 na 2 ni wakubwa mlitakiwa muwe mna enjoy life kwa sasa

    6. #164
      kisukari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th July 2010
      Posts : 2,574
      Rep Power : 3873
      Likes Received
      1380
      Likes Given
      645

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Je, mke wako ana umri gani?

      Je, ndoa yenu ina muda gani?

      Je, watoto wenu wana umri gani?

      Wamama wengi huwa na tatizo kama hilo, sababu kuu ni machovu, au kila siku style ni hizo hizo za sita kwa sita unaona kama ni kupoteza muda,au ulezi hasa kama watoto ni wadogo.

      Unakuwa na wasiwasi na watoto wako kwa vitu vidogo vidogo, watoto unawapa first priority kuliko tendo la ndoa, au pia age, wamama wengine age ikiwa kubwa hayo mambo wanakuwa hawana interest nayo tena.

      Suluhisho lake: Jaribu kubadilisha mazingira, nenda nae sehemu kama hoteli wewe na yeye tu, mkumbushie honeymoon yenu ilivyokuwa na mapenzi yenu yalivyokuwa mwanzo.na umuelezee jinsi unavyompenda, taraatibu mambo yatakuwa sawa tu.

    7. #165
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1523
      Likes Received
      1422
      Likes Given
      1828

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      hivi kwenda mizunguko mingi ndo kumridhisha mwenzio...wanaume wengi mnadhani maandalizi ni wakati wa tendo lenyewe,siku nzima umekaa hata kimeseji cha kumlainisha mtu hakuna unategemea nini!!!

    8. FemaTV & Radio

    9. #166
      ndetichia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Mwime - Buswangili
      Posts : 18,174
      Rep Power : 5095
      Likes Received
      2767
      Likes Given
      231

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      mkuu mnafanya na biashara au wote mnafanyakazi tofauti na biashara?

      wakati mwingine kama mtu yupo bize masaa yote inampelekea kutokufikiria hayo mambo zaidi ya shughuli zake kwa hiyo mjitahidi na kutoka out kidogo kila weekend nadhani itasaidia..

    10. #167
      genekai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Location : Loitering!
      Posts : 7,496
      Rep Power : 2078
      Likes Received
      1059
      Likes Given
      1568

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Pole sana kaka kwa yanayowapata. Dawa ipo na madaktari wapo dawa ya kwanza ni nyie wenyewe na madr wa kwanza ni nyie wenyewe vilevile. Nionavyo mimi mkeo anatatizo zaidi la kisaikolojia, na hili laweza kuwa limesababishwa na maumivu katika kujifungua ambapo mama zetu wanapata maumivu yasoweza elezeka na hii inaweza kumfanya asijisikie hamu hata kidogo. Lakini vilevile anahitaji kujikubali na kuanza ye mwenyewe kutengeneza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Shida niionayo hapa ni kuwa akiendelea na hii hali aweza kupata "ukavu wa sehemu za siri za mwanamke" a.k.a virginal dryness inayoweza kuleta matatizo makubwa hasa katika ndoa yake.

      Jaribu kumuandaa kwa muda mrefu hata usipofanya tendo la ndoa kisha muache, endelea hivyo hivyo mara nyingi iwezekanavyo hatimaye mambo yaweza kuwa mazuri.

      NB. Haya yakiendelea fuata ushauri wa daktari hasa wa magonjwa ya kina mama!
      PSI Factor likes this.
      The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders

    11. #168
      PSI Factor's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st April 2011
      Posts : 16
      Rep Power : 412
      Likes Received
      2
      Likes Given
      11

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Quote By Kimbojo
      Pole mh. inatokea kwa baadhi ya wanawake hasa wanapokuwa na msongo wa mawazo,wako bize na watoto, au antumia vidonge vya uzazi wa mpango. Kwa nature ya kabila la mkeo haya yaweza kuwa sababu, chunguza kwa kuwa nae karibu saana.
      Asante Kim,

      Hakuwahi kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Suala la asili ya kabila ndilo natilia shaka kwani kuna rafiki yangu naye ana tatizo kama langu na mkewe ni wa mkoa mmoja kama anaotokea wife.

      Quote By nyumba kubwa
      Kuna swali nimeuliza hujajibu. Anatumia dawa za uzazi wa mpango?? Mimi sijawahi tumia hizo dawa ila nina rafiki yangu alinambia alijaribu kutumia zilimfanya aone kama mumewe anambaka kwani hakuwa na feelings za kushiriki hilo tendo kabisa. Alipoamua kudrop kutumia hizo dawa amerudi kwenye hali yake ya zamani.

      Kingine umesema mkeo hawezi kuwaacha watoto lazima mwende nao. Hiyo tayari ni dalili ya tatizo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa ameamisha mapenzi kwa watoto. Anahitaji counselling.

      Watoto wa miaka 5 na 2 ni wakubwa mlitakiwa muwe mna enjoy life kwa sasa
      NK,
      Kama nilivyosema awali, hatumii vidonge wala dawa yoyote ya uzazi wa mpango. Tunapanga wenyewe.

      Hili tatizo lina zaidi ya miaka 5 sasa, mpaka naandika hapa maanake nimeona hali hii inanilazimisha kuwaza vibaya, nikaona huenda kuna waliowahi kumbana na maswahibu haya wanaweza kunipa ushauri.

      Suala la kuhamishia mapenzi kwa watoto naliona, nikimwambia ananiuliza kama nawaonea wivu watoto. Nakuwa mpole.

      Quote By kisukari
      Je, mke wako ana umri gani?

      Je, ndoa yenu ina muda gani?

      Je, watoto wenu wana umri gani?

      Wamama wengi huwa na tatizo kama hilo, sababu kuu ni machovu, au kila siku style ni hizo hizo za sita kwa sita unaona kama ni kupoteza muda,au ulezi hasa kama watoto ni wadogo.

      Unakuwa na wasiwasi na watoto wako kwa vitu vidogo vidogo, watoto unawapa first priority kuliko tendo la ndoa, au pia age, wamama wengine age ikiwa kubwa hayo mambo wanakuwa hawana interest nayo tena.

      Suluhisho lake: Jaribu kubadilisha mazingira, nenda nae sehemu kama hoteli wewe na yeye tu, mkumbushie honeymoon yenu ilivyokuwa na mapenzi yenu yalivyokuwa mwanzo.na umuelezee jinsi unavyompenda, taraatibu mambo yatakuwa sawa tu.
      Mke wangu ana miaka 31, ni mzee sana?
      Namweleza kila siku mke wangu nimpendavyo, na si kama namweleza kama maigizo hapana, sijaona mwanamke wa kunifanya nifurahi na kujisikia vyema kama mke wangu. Ni tatizo hili tu kwake ninaloliona, hana jingine.
      Kama ni kusafiri najitahidi sana, tunaenda nje ya nchi mara kwa mara kwa vacation, walau mara moja kila mwaka. Bado hawezi kwenda huko bila kubeba mtoto japo mmoja.
      Quote By shosti
      hivi kwenda mizunguko mingi ndo kumridhisha mwenzio...wanaume wengi mnadhani maandalizi ni wakati wa tendo lenyewe,siku nzima umekaa hata kimeseji cha kumlainisha mtu hakuna unategemea nini!!!
      Mkuu shosti,
      Kama ni zawadi nampa, kama ni ujumbe anapata kwa kila njia. Kama ni usafiri najitahidi kumbadilishia ili afurahie maisha. Kama ni mavazi, vidani nampa. Sijawahi kulalamikiwa hata siku moja, miaka 8 ya ndoa haijawa na tatizo na hata ukinikuta naye utatamani (kama wewe ni mwanamke) ungekuwa yeye, maana muda wote ni mwingi wa furaha na najitahidi kumhudumia.
      Kama suala ni kutomridhisha kama ninavyoona watu wanaandika basi itanibidi niende kujifunza upya, sijui nitumie misahafu gani kwani kama ni mitindo ya tendo lenyewe naweza kuwa naimudu mingi kwani umbo linaruhusu.
      Quote By ndetichia
      mkuu mnafanya na biashara au wote mnafanyakazi tofauti na biashara?

      wakati mwingine kama mtu yupo bize masaa yote inampelekea kutokufikiria hayo mambo zaidi ya shughuli zake kwa hiyo mjitahidi na kutoka out kidogo kila weekend nadhani itasaidia..
      Mkuu ndetichia,
      Mimi nina biashara zangu, yeye anasoma (nimesema hapo awali). Suala la kutoka nimeliongelea hapo juu
      I know that I am intelligent, because I know that I know nothing...

    12. #169
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Nimejifunza mengi JF. It is my firts time kusikia maumivu ya kujifungua yanapunguza hamu ya tendo. Nachojua maumivu mtu unayasahau muda mfupi tu baada ya kujifungua. Sasa kama kuna wamama wana ishi na kumbukumbu za maumivu hapo itakuwa kazi.

      Quote By genekai
      Pole sana kaka kwa yanayowapata. Dawa ipo na madaktari wapo dawa ya kwanza ni nyie wenyewe na madr wa kwanza ni nyie wenyewe vilevile. Nionavyo mimi mkeo anatatizo zaidi la kisaikolojia, na hili laweza kuwa limesababishwa na maumivu katika kujifungua ambapo mama zetu wanapata maumivu yasoweza elezeka na hii inaweza kumfanya asijisikie hamu hata kidogo. Lakini vilevile anahitaji kujikubali na kuanza ye mwenyewe kutengeneza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Shida niionayo hapa ni kuwa akiendelea na hii hali aweza kupata "ukavu wa sehemu za siri za mwanamke" a.k.a virginal dryness inayoweza kuleta matatizo makubwa hasa katika ndoa yake.

      Jaribu kumuandaa kwa muda mrefu hata usipofanya tendo la ndoa kisha muache, endelea hivyo hivyo mara nyingi iwezekanavyo hatimaye mambo yaweza kuwa mazuri.

      NB. Haya yakiendelea fuata ushauri wa daktari hasa wa magonjwa ya kina mama!

    13. #170
      PSI Factor's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st April 2011
      Posts : 16
      Rep Power : 412
      Likes Received
      2
      Likes Given
      11

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Quote By genekai
      Pole sana kaka kwa yanayowapata. Dawa ipo na madaktari wapo dawa ya kwanza ni nyie wenyewe na madr wa kwanza ni nyie wenyewe vilevile. Nionavyo mimi mkeo anatatizo zaidi la kisaikolojia, na hili laweza kuwa limesababishwa na maumivu katika kujifungua ambapo mama zetu wanapata maumivu yasoweza elezeka na hii inaweza kumfanya asijisikie hamu hata kidogo. Lakini vilevile anahitaji kujikubali na kuanza ye mwenyewe kutengeneza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Shida niionayo hapa ni kuwa akiendelea na hii hali aweza kupata "ukavu wa sehemu za siri za mwanamke" a.k.a virginal dryness inayoweza kuleta matatizo makubwa hasa katika ndoa yake.

      Jaribu kumuandaa kwa muda mrefu hata usipofanya tendo la ndoa kisha muache, endelea hivyo hivyo mara nyingi iwezekanavyo hatimaye mambo yaweza kuwa mazuri.

      NB. Haya yakiendelea fuata ushauri wa daktari hasa wa magonjwa ya kina mama!
      Si mkavu sehemu za siri.
      Nimekuelewa, kuna ya kufanyia kazi katika ushauri wako.
      Mungu akubariki
      I know that I am intelligent, because I know that I know nothing...

    14. #171
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Mke wangu hana hamu na tendo la ndoa

      Aisee pole sana. Nimeishiwa maneno. Kuna wamama nasikia ni makungwi labda awatafute sijuhi kama ita work. Si umesema hata yeye anajua kuwa ana tatizo. Pole maana umesema it is now 5 years toka tatizo lianze sasa hapo mbona kazi.

      Labda alilelewa kuona hilo tendo kama dhambi ndiyo maana hainjoi. Lakini hiyo miaka mitatu ya mwanzo ya ndoa yenu mbona ilikuwa poa. Embu mwambia aache kuwapa watoto nafasi yako. Hapo ndio kuna tatizo.

      Na mkiamua kwenda second honeymoon hamna kubeba watoto.

      Mwambie kuwa anakupa wakati mgumu uzalendo unakaribia kukushinda. Atakasirika lakini itaingia akilini.

    15. #172
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,163
      Rep Power : 31372
      Likes Received
      9571
      Likes Given
      683

      Default Re: Kuishiwa hamu

      Hivi Mrs. Mtaba ulipotelea wapi?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    16. #173
      fabinyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th August 2011
      Posts : 1,809
      Rep Power : 816
      Likes Received
      350
      Likes Given
      278

      Default Re: Kuishiwa hamu

      kwa nini usitafute namna ya kukutoa katika hali hiyo?mambo mengine hayatoki kwa shetani,ni sisi wenyewe!kila la heri katika kutafuta kwako kuachika,sababu zipo nyingi na utafanikiwa ila cha moto utakiona baada ya hapo..

    17. #174
      Kaitaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2009
      Posts : 862
      Rep Power : 675
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuishiwa hamu

      Uwezekano wa kukumbwa na shetani wa mahaba ni mkubwa sana, jifanye kama huna mume kaa naye, baada ya muda shetani huyo ataondoka, nawe utampenda kama mwanzo. tulia na mumeo

    18. ldd
      #175
      ldd's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2011
      Posts : 385
      Rep Power : 476
      Likes Received
      28
      Likes Given
      13

      Default Re: Kuishiwa hamu

      Mshkaj anataka tobo la taka kubwa, tobo la taka ndgo ni oversize! husituzngue km ni kumuacha si umuache kwan mpka uombe ushauri!? alafu kuwa m2 mzima bac, wakati anakupga sound mbona ukuomba ushaur jf?

    19. #176
      ndyoko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 4,505
      Rep Power : 1705
      Likes Received
      1199
      Likes Given
      1916

      Default Re: Kuishiwahamu

      Quote By Mrs Mtaba
      Range yety iko 35 kwa 46. mda ktk ndoa ni kariabia 2 years hivi! Mmmmh
      Umekaribia menopause dada! Aisee kwanini uliolewa ukiwa mzee hivyoo, why? Kwa kweli umri wako umeenda na hayo ndiyo madhara ya kuolewa na kibabu. Hiyo range ya umri wenu ni noma. Na kwa mwanaume mwenzio ndio kwanza ameanza kurudia ujana wake, yaani he is rejuvinating in terms of sexual practice.

    20. #177
      Konya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th June 2011
      Posts : 811
      Rep Power : 565
      Likes Received
      79
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By Mrs Mtaba
      Nimependa tuu yeye ndo aniache.
      jamani!na ile ahadi ya,ctakutosa kwenye shida na raha au ndo fungu lishakata,anyway.. kuna tatizo kt yenu...hebu kaeni na msolve iseee

    21. #178
      Kibukuasili's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th May 2010
      Location : Mbooni constituency, Kenya
      Posts : 798
      Rep Power : 617
      Likes Received
      134
      Likes Given
      104

      Default Re: Kuishiwa hamu

      Tafuta mwanamme mwingine, kwani umezaliwa nae huyo?
      Mapenzi ni ya watu wawili sasa ukianza kuingiza akina yesu, m'mad na wengineo utapotea. Fata moyo wako

    22. #179
      Mghoshingwa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th July 2011
      Location : lalati
      Posts : 182
      Rep Power : 434
      Likes Received
      19
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Mrs Mtaba
      Za leo wandugu, naomba kuuliza na kutaka kujua. Mimi niko kwenye ndoa ya kama miaka 2 sasa. Kwa kweli imekuwa na furaha zake pia ni vikwanzo vingi. Imefikia sasa mimi najishangaa sana kuwa nimeishiwa hamu kabisa na mme wangu na ninamuona mbaya sana. Nakaa na kujiuliza ilikuwaje mpaka nikaolewa nae. Namefikia hatua yakufanya mambo ilinimuuzi aniache tuu. Sijui sasa nifanye nini zaidi cha kumuuthi nisaidieni.
      ni pm nitakushauri kwa kina.

    23. #180
      Amyner's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2011
      Location : Somewhere..
      Posts : 2,329
      Rep Power : 7401
      Likes Received
      769
      Likes Given
      53

      Default Re: Kuishiwa hamu

      my dear fikiri kwa kina kwani mpaka mlipofikia hatua ya kuoana ina maana mnaelewana vizuri... falling out of love kwa muda kwa wanandoa nadhani ni jambo la kawaida...but kaa ukigundua baadae mapenzi yatarudi tena na kama ndio ukawa umeshamuacha akapata mwingine moyo utakuuma sana...BUT kama una uhakika humpendi na hautokuja kumpenda tena it gets me wondering kwanini ulikubali kuolewa nae??!!!! DIVORCES SUCK JAMANI KAMA WE ARE NOT SURE YET TUSIKUBALI KUOLEWA!!! YA NINI KUVAMIA NDOA THEN AFTER SOMETIME UMPE SHIDA MWENZIO!!

    24. Study Abroad
    Page 9 of 18 FirstFirst ... 7891011 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...