Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

    Report Post
    Page 17 of 18 FirstFirst ... 715161718 LastLast
    Results 321 to 340 of 348
    1. #1
      Mrs Mtaba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st January 2009
      Location : Denmark
      Posts : 104
      Rep Power : 547
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Red face Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      #1:
      Za leo wandugu, naomba kuuliza na kutaka kujua.

      Mimi niko kwenye ndoa ya kama miaka 2 sasa. Kwa kweli imekuwa na furaha zake pia ni vikwanzo vingi. Imefikia sasa mimi najishangaa sana kuwa nimeishiwa hamu kabisa na mme wangu na ninamuona mbaya sana. Nakaa na kujiuliza ilikuwaje mpaka nikaolewa nae.

      Namefikia hatua yakufanya mambo ili nimuudhi aniache tuu.

      Sijui sasa nifanye nini zaidi cha kumuudhi, nisaidieni.

      #2:
      Quote By Najuah
      Natumaini wote ni wazima wa afya inshalaah.

      Kwa kifupi Nina rafiki yangu mpendwa (Msichana) ana tatizo ambalo kwa kweli mi sijui hata nimsaidiaje, ni meona si vibaya kuliweka hewani tukasaidiana mawazo.

      Ni binti mwenye umri wa miaka 23 tatizo lake kubwa hajawahi katika maisha yake yote toka avunje ungo kujiskia hamu ya kufanya mapenzi. Ana mpenzi ila mara nyingi wakiwa faragha huwa kama anamfurahisha mwezake kwa sababu hana anacho jiskia hata aguswe wapi. Mara ya kwanza kunieleza mi nilimshauri aende hospitali akaonane na dakatari wa wanawake huenda Homoni za kike zikawa zimepungua au akagundulika tatizo lingine lolote linalo weza kusababisha hiyo hali; Nashukuru Mungu kwani alinisikiliza na kwenda hospitali ya regency ila majibu yalipo toka alionekana kila kitu kiko normal.

      Sasa sijui hata nimsaidiaje coz kuna kipindi nilimuuliza kama huwa anaota ndoto za mapenzi mara kwa mara kwa sababu nilisha wahi kusikia hata kusoma kwenye vitabu kuwa kama una Jini Mahaba basi kuna uwezekano hali kam yake ikajitokeza; ila ilinihakikishia kuwa hajawahi hata siku mwoja kuota ndoto za namna hiyo. Jamaa yake anampenda sana na hivi majuzi jamaa ansema anataka kuja kutoa posa ili ajichukulie jumla jumla anahisi atateseka sana kwenye ndoa coz hata pata hiyo raha ya chakula cha ndoa.

      Naomba tumsaidie jamani afanyaje??
      #3:
      Quote By Brandon
      Habari za kazi wandugu,

      nipo tutani naomba msaada wenu ili niweze kumfurahisha mpenzi wangu. Lately nimekuwa sina hamu ya kufanya mapenzi kabisa hata nikifanya nakuwa natimiza wajibu tu ili mwenzangu asijisikie kua simjali coz ananipenda sana na ninampenda sana. Nifanyaje ili niweze pata hamu na kufurahia mapenzi?

      Asanteni sana.
      #4:

      Quote By PSI Factor
      Ni post yangu ya kwanza kwenye jukwaa hili na nimefikia uamuzi wa kuandika hapa kwakuwa nimeona wadau wengi wakitoa maoni ambayo kweli yanaonyesha kusaidia.

      Tatizo langu ni dogo kwa wengine lakini kwangu kubwa sana. Mke wangu hana hamu ya tendo la ndoa na inakuwa vigumu kuweza kumlazimisha tufanye tendo hilo kwani najiona kama namwonea. Mimi nakuwa na ashki sana lakini sina jinsi hivyo nalazimika kuvumilia. Sijafikiria kutoka nje ya ndoa kwani sidhani kuwa hili litakuwa suluhisho la tatizo langu.

      Kabla hajajifungua hali ilikuwa nzuri (kiasi) lakini baada ya kujifungua mtoto wa kwanza tu, hali imekuwa mbaya sana. Hana hamu kabisa, hata ninapojitahidi kumwandaa anaamua kuruhusu tufanye tu ili mradi niridhike.

      Tuna watoto wawili, wote wa kike.

      Tofauti na hili, sina tatizo jingine kwenye ndoa lakini kama sijajitutumua naweza kukosa tendo hili muhimu hata kwa mwaka kwakuwa yeye haoni umuhimu wake sana.

      Anatambua tatizo hili, tumelijadili mara kadhaa lakini hatujajua ni daktari gani tumwendee na dawa gani zaweza kutumika.

      Nampenda mke wangu, namwonea huruma kwa hali hii na naamini huenda siku moja nikapata tiba ya tatizo hili. Wenzangu mmewahi kukumbana na hali hii? Mliikabili vipi? Kuna dawa? Kuna daktari?

      #5:
      Quote By Bugota
      Habari za leo wana JF. Natumaini hamjambo wote.

      Ndugu zangu naombeni ushauri. Mimi nina miaka 2 kwenye ndoa yangu. Tumepata mtoto mmoja. Mke tangu mwanzo alikuwa ni mtu mwenye kuyaweza mambozi kweli kweli. Lakini tangu nilipoanza kazi za migodini, nikirudi likizo nimekuwa nikiona mke wangu haoneshi kuwa na hamu ya kukutana na mimi kana kwamba tulikuwa wote muda wote. Pia ukifanya majambozi nagundua kuwa ishu yake imelegea, ina maji maji kibao tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa tight, kavu tena ya moto; haoneshi ushirikiano wakati wa majambozi.
      Nilipomuulika akaanza kudai o mara unajua nakuwa na mawazo juu ya nyumbani mara oh unajua mtoto ananinyonya sana.

      Nakuwa na wasiwasi huenda anachakachuliwa.

      Naomba ushauri jamani.
      Ushauri wa wadau:

      Soma hii post: http://www.jamiiforums.com/jf-doctor...ml#post4104552

      Quote By matambo
      Low libido

      Libido naturally diminishes as men age. Testosterone, the hormone primarily responsible for sex drive, begins to decline in the body by about 1 percent every year beginning around the age of 30. This is perfectly natural, though healthy men can take steps to boost libido at virtually any time in life. “There is no age beyond which sex drive is not possible or therapeutically helpful,” says Dr. David Plourd of the Naval Medical Center in San Diego.

      However, a drooping libido can also indicate an unhealthy body or mind. Most notably, low testosterone is a symptom of excess body fat, since fat both inhibits testosterone production and breaks down testosterone already in the system. Depression, anxiety and stress can each reduce libido, as can excessive alcohol intake.

      Note that sexual drive and erections are discrete physiological matters: Libido is determined by testosterone, while erections are dependent on blood flow and nerve sensitivity.

      Possible indications:
      • Obesity
      • Diabetes
      • Mumps
      • Tumors on pituitary or hypothalamus
      • Excessive alcohol intake
      • Sedentary lifestyle
      • Depression
      • Anxiety
      • Stress

      What to do:
      • Improve your diet and exercise
      • Reduce abdominal fat
      • Consider talking to a shrink
      • Get a blood test
      Quote By Kiroroma
      For men with little sexual desire it is sometimes enough to have one or a few conversations in which they can express their feelings and ask questions about the extent to which their situation is abnormal.

      Counselling about reduced desire in stressful situations like death, unemployment, disease of the partner or stress at work can be sufficient. If all sexual interest has disappeared, and there is no masturbation either, the hormonal regulation should be examined. When anomalies in this are found, medication can be prescribed.

      There are no standard treatments for a reduced interest in sex. Depending on the causes of the complaints a treatment will be set up. Physical causes are also treated depending on the cause. The lack of interest in making love due to certain medication is treated by using other medication or another dose. Psychological causes can best be determined and treated by a sexologist.

      Psychotherapy, which studies and treats the psychological causes, can be important in this. It is important to understand that thoughts often go through the mind while making love which negatively influence the interest in sex. Social influences, e.g relation problems, stress at work, etc. are treated by relation therapy or psychotherapy. A sexologist can use different forms of therapy to determine and possibly influence the thoughts about sex.
      AshaDii likes this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #321
      by default's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2011
      Location : on my way
      Posts : 817
      Rep Power : 561
      Likes Received
      197
      Likes Given
      17

      Default Re: Msaada jamani!!!!!!!!!!!!kukosa hamu upendo kutoka kwa mwenzangu

      Mkuu wamba huyo mkeo ana umri gani isije kuwa ni age mate wako! Pole sana

    4. #322
      by default's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2011
      Location : on my way
      Posts : 817
      Rep Power : 561
      Likes Received
      197
      Likes Given
      17

      Default

      Quote By Mwanaweja
      kikubwa jitahidi upe mimba haya yote yatapungua kwa kiasi kikubwa sana
      kama ingekuwa kwenye maji nauakika angeshampa mnunulia lita 10

    5. #323
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,205
      Rep Power : 19214
      Likes Received
      8165
      Likes Given
      26639

      Thumbs up Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)









      Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano wa mwanamke na mpendwa wake. Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana sana kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.


      Visababishi vya tatizo hili kwa wanawake ni;


      Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili linaweza kutokea kutokana na msongo wa mawazo ambapo huchangiwa na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa

      uaminifu katika uhusiano {infedility} nk)
      na magonjwa mbalimbali.
      Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au ndoa

      Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana (sexual

      refractory period) kwa kuingiliana na ufanyaji kazi wa homoni/kichocheo chengine kinachojulikana kama dopamine (ambayo ndio humfanya mtu kufikia kilele wakati wa kujamiana). Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia
      huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi,

      kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu nyengine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo (anterior pitituary tumors). Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume (impotence).

      Kupungua mzunguko wa damu
      katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
      Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
      Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu

      Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote
      hupunguza hamu ya kujamiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.

      Ugonjwa wa kisukari
      Uvutaji sigara
      Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
      Uzito uliopitiliza (obesity)
      Ugonjwa wa mifupa (arthritis)
      Utumiaji madawa ya kulevya

      Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve damage) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
      Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu, antidepressant medication, dawa za saratani nk.
      Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo

      kusababisha uchovu.

      Ugonjwa wa moyo
      Saratani ya aina yoyote ile
      Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression nk.

      Historia ya kubakwa, au kupata maumivu wakati wa kujamiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari kujamiana au kutotayarishwa vyema kabla ya kujamiana au magonjwa ya zinaa.

      Tatizo la vaginismus – Hii ni tatizo ambalo husababisha tupu ya mwanamke kuwa ndogo wakati wa kujamiana na hivyo husababisha mwanamke kupata maumivu wakati wa kujamiana.

      Kupenda inataneti kupita kiasi (addiction) – Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchat au

      kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababishwa msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.






      Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?


      Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
      Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
      Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (menopause- miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri na depression.




      Kwa wanaume, visababishi vya tatizo la kupungua hamu au uwezo wa kujamiana ni kama ifuatavyo;


      Msongo wa mawazo kama nilivyoeleza hapo juu
      Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano/ndoa
      Unywaji pombe kupindukia kama nilivyoeleza awali
      Utumiaji wa dawa za kulevya

      Uvutaji sigara – Hupunguza kiwango na uzito wa shahawa kwa wanaume. Uzito wa shahawa (concentration of spermatozoa in semen) hupungua kwa asilimia 22-57 kwa wale wanaovuta sigara. Uwezo wa shahawa kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke pia nao hupungua kwa asilimia 20 kwa wale wanaovuta sigara ikilinganishwa na wale wanaume wasiovuta sigara.

      Tafiti nyengine zimethibitisha kuwa wanaume wanaovuta sigara wana asilimia kubwa ya kutoa shahawa ambazo hazina maumbile mazuri au ya kawaida na hivyo kuongeza uwezekano wa mimba kutoka (spontaneous abortion) au kuzaa mtoto mwenye maumbile ambayo sio ya kawaida (birth defects). Tafiti mbalimbali pia zimethibitisha kuwa uvutaji sigara huharibu mirija ya seminiferous tubules ambayo hupatikana kwenye korodani na ni sehemu ambapo shahawa hutengenezwa, hivyo uharibifu wake hupunguza wingi na uzito wa shahawa.


      Pia uvutaji sigara hupunguza vichocheo aina ya testerone, growth hormone, na nk.Wanaume wenye kiwango kidogo cha testerone huwa na tatizo la kupungukiwa uwezo wa kujamiana na kiwango kidogo cha shahawa.Uvutaji sigara hupunguza mzunguko wa damu unaopita/kwenda kwenye moyo na kwenye uume na hivyo basi kumfanya mwanamume kushindwa kusimika na kupata tatizo la kupungua uwezo wa kujamiana (vascular impotence).


      Katika tafiti zilizofanyika, asilimia 97 ya wale waliogunduliwa na tatizo la vascular impotence walikuwa wavutaji sigara na katika tafiti nyengine asilimia 87 ya wale wenye tatizo hili la vascular impotence walikuwa pia wavutaji sigara. Katika tafiti iliyohusisha wapenzi 290 hapo mwaka 1999, ilionyesha ya kwamba wanaume ambao walikuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa na wake zao mara 6 tu kwa mwezi mzima na wale ambao hawakuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa mara mbili zaidi ya wale wavutaji sigara.


      Uvutaji sigara, huusishwa pia na kuongezeka kwa chembechembe nyeupe za damu kwenye shahawa ambazo kwa kawaida hutolewa kukiwa na ugonjwa ndani ya mwili, chembechembe hizi ambazo zinakuwepo kwa wingi kwenye shahawa pasi na kuwepo kwa ugonjwa, hupunguza uwezo wa shahawa kuingia na kuungana na yai (ovum) kutoka kwa mwanamke na hivyo kusababisha kutotunga kwa mimba.


      Ugonjwa wa kisukari

      Uzito uliopitiliza (obesity) – Kutokana na kuongezeka kwa mafuta ambayo husababisha mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na uume kuwa midogo na kupungua uwezo wa kujamiana. Kupungua uwezo wa kujamiana au kufanya mapenzi kwa wanaume ni ishara mojawapo ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.
      Hypothyroidism – Matatizo ya vichocheo katika tezi la koo

      Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression
      Kupenda mambo ya intaneti kupita kiasi (addiction to internet) kama nilivyoeleza awali.
      Umri – Kuanzia miaka ya 40,kiwango cha kichocheo aina ya prolactin huongezeka na kusababisha kuongezeka kwa

      kichocheo chengine aina ya dihydro-testerone ambacho husababisha tezi dume kuongezeka na hatimaye kupunguza uwezo wa kusimika kwa mwanamume (rudia makala ya kuvimba tezi dume – Benign Prostate Hyperplasia, BPH)

      Madhara katika neva inayohusika na kusimika kwa uume (pudendal nerve damage)
      Kuendesha baiskeli muda mrefu (kwa kipindi kimoja) – Hii hugandamiza neva na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume na kusababisha tatizo la kupungua kwa uwezo wa kusimika kwa mwanamume kwa muda tu (temporary).




      Vipimo vya uchunguzi


      Kabla ya kufanya vipimo vya uchunguzi, Daktari atachukua historia ya mgonjwa inayohusisha matumizi ya dawa aina mbalimbali, historia ya magonjwa, sexual history pamoja na kuangalia dalili za magonjwa mbalimbali. Vipimo vya uchunguzi vitatokana na historia ya mgonjwa ambayo Daktari ameweza kuipata kutoka kwake. Vipimo hivyo vinaweza kuwa


      Vaginal swab – Kuangalia magonjwa kwenye tupu ya mwanamke au kama kuna bakteria aina yoyote.
      Vaginal swab – Kuangalia magonjwa ya zinaa
      Vipimo vya mkojo (urinalysis)

      Kipimo cha kuangalia mabadiliko yoyote kwenye tupu ya mwanamke (physical changes, thinning of genital tissues, decreased skin elasticity and scarring)

      Kumpima mgonjwa akili ili kuweza kutambua kiini cha tatizo
      Vipimo vya vichocheo kama T3, T4, testerone level, growth hormone, prolactin hormone nk.
      Semen analysis – Kipimo cha kuangalia shahawa, wingi wake (volume), kiwango chake, mvutano wake (liquefaction time), sperm count, maumbile yake (sperm morphology), PH yake, uwezo wake wa kuogelea (sperm motility), kiwango cha sukari na chembechembe nyeupe za damu.

      BMI – Kipimo cha kuangalia kama mtu anauzito unaolingana na urefu wake pamoja na umri wake au ana uzito uliopitiliza
      Vipimo vya ugonjwa wa shinikizo la damu – Kwa wale wenye shinikizo la damu au dalili zake au wanaotumia dawa za shinikizo la damu
      Vipimo vya ugonjwa wa kisukari – Fasting Blood Glucose test, Oral Glucose Tolerance Test (OGTT), glycosylated hemoglobin (Hb A1C) rudia makala ya Kisukari kwenye tovuti ya Tanzmed.
      Tiba ya tatizo hili


      Tiba ya tatizo hili inahusisha


      1.Kubadilisha mfumo wa maisha


      Kufanya mazoezi mara kwa mara – Mazoezi huongeza stamina, hupunguza uzito,humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiana
      Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha (fedha, nk) lazima yatafutiwe ufumbuzi.Kufanya mazoezi ya pelvic muscles kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa kujamiana kwa wanawake
      2. Kubadilisha mfumo wa maisha kwa wapenzi


      Zungumza na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao, kuwa wakweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja. Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati

      wa kujamiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishiwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.

      Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mupate kudumisha uhusiano wenu
      Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali wakati wa kujamiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile muliyoizoea wakati wa kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani)

      Kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, marriage counsellors na hata madaktari wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi yao.





      3.Tiba ya dawa


      Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk.
      Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazoleta madhara kama ya msongo wa mawazo, depression nk.

      Kutibu tatizo la depression na anxiety
      Kutumia dawa au jelly (vaginal lubricants) zinazolainisha tupu ya mwanamke wakati wa tendo la ndoa kwa wale

      wanaopata maumivu au kupunguza tupu kuwa kavu (dryness of vagina) au kuwasha (irritation).
      Tiba ya homoni au vichocheo – Estrogen Replacement Therapy (ERT) and androgen therapy.
      Dawa aina ya Yohimbine Hydrochloride
      4.Vyakula vinavyosaidia kupunguza tatizo hili


      Ikumbukwe ya kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia tu kupunguza ukubwa wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi na kuboresha kwa wale ambao hawana tatizo hili na hivyo kudumisha uhusiano.


      Kitunguu swaumu – Kitunguu swaumu kina kemikali aina ya allicin ambayo huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye uume, huongeza hamu ya kufanya mapenzi na utolewaji wa shahawa.

      Habat al soda (black caraway seeds au Nigella Sativa Seed) – Mafuta,mbegu,au unga wa habat soda kama wengi wanavyoita na ambazo zimetumika kwa miaka mingi sana kupunguza tatizo hili na waandishi wengi wameeleza umuhimu

      wake. Tumia kidogo kwenye chai au maji ya uvuguvugu mara mbili kila siku. Mbegu hizi hupatikana kwa wingi katika nchi za asia kama Saudi Arabia, Syria, Iran, Dubai (UAE), na hata Misri, Tanzania (Dar-es-salaam katika maduka ya dawa za asili ya kariakoo, mbagala, na Zanzibar)

      Celery au giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.

      Ndizi – kuwepo kwa wingi kwa enzyme aina ya bromelain na madini ya potassium huongezeka msisimko wa kufanya mapenzi kwa wanaume.Potassium pia hupatikana kwenye tikiti maji ambalo pia lina kemikali aina ya arginine ambayo huongeza wingi wa damu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kusimika kwa uume.

      Parachichi – Huwa na kiwango kikubwa cha folic acid ambayo huvunjavunja protini. Vitamini B6 kwenye parachichi huchochea kutengeza kichocheo aina ya testerone kwa wingi.
      Mayai – Mayai yana kiwango kikubwa sana cha vitamini aina ya B5 na B6, ambazo husaidia kuleta usawa wa viwango vya vichocheo mwilini na kupunguza msongo wa mawazo.

      Nyanya/Tungule (tomatoes) – Zina kiwango kikubwa cha virutubisho aina ya bio-active phyto-nutrients, lycopene, na beta carotene ambazo husaidia kuleta damu kwa wingi kwenye uume na hivyo kusaidia kusimika kwa uume
      Chocolate – Ina kiwango kikubwa cha kemikali aina ya theobromine na phenylethylamine ambazo huongezeka hamu ya kufanya mapenzi.

      Vitamin A – Husaidia katika kuweka usawa wa vichocheo vya mapenzi (sexual hormones). Vyakula venye wingi wa vitamin hii ni pamoja na karoti, maini,tikiti maji, spinach, maziwa nk.

      Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone ambacho husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake. Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi tamu, lentils,

      mboga za majani, parachichi (avocado), mayai, nyama aina ya tuna, bata mzinga, maini nk.
      Vitamin C – Tafiti zilizofanywa karibuni zimeonyesha ya kwamba vitamini C inapotumiwa pamoja na vitamini nyengine,

      husaidia L-enantiomer ya ascorbic acid kudhibiti msongo wa mawazo, wasiwasi (anxiety), utolewaji wa homoni ya prolactin na huongeza mzunguko wa damu pamoja na kutolewa kwa kichocheo cha aina ya oxytocin na hivyo

      kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa. Vyakula venye vitamin C ni ndimu, chungwa, limao, brussels sprouts, mapera, tikiti maji, nyanya, broccoli, kiwi, papai, strawberries, pilipili hoho na pilipili mbuzi nk.

      Vitamin E – Husaidia kudhibiti matamanio ya mwanamume pamoja na kusimika kwa uume kutokana na uwepo wa vichocheo aina androgens na estrogen ambavyo huchanganyikana na homoni za mayai (ovarian hormones) na testerone. Vyakula venye vitamin E ni pilipili hoho, nyanya, olives, tunda aina ya kiwi, papai, mafuta ya alizeti, karanga nk.

      Madini ya Zinc – Muhimu katika utengenezaji wa testerone
      Madini ya selenium – Huongeza uwezo na nguvu ya kufanya mapenzi kwa wanaume.

      Madini ya magnesium na calcium – Calcium ni muhimu katika kusaidia ufanisi wa kufanya mapenzi. Huweka mawasiliano ya karibu kati ya ubongo na tezi zinazotoa vichocheo vya mapenzi pamoja na kusaidia katika ufanyaji kazi wao. Madini

      ya magnesium husaidia kuondoa madhara ya madini ya calcium katika kusaidia kuhimili kusimika kwa uume. Vyakula venye madini ya calcium ni maziwa, mtindi, cheese, siagi, chungwa, almonds, walnuts, maharage meupe, ice cream, chocolate nk.
      Cinnamon stick (mdalasini) na Asali (Honey) – Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi

      kwa wale wenye tatizo hili. Jinsi ya kuandaa, chukua mdalasini robo na changanya na asali nusu lita kisha weka kwa siku tatu, baada ya siku tatu anza kunywa kwa kutumia kikombe cha kahawa mara tatu kwa siku kwa muda wa wiki mbili (kama utatumia mdalasini nusu basi changanya na asali lita moja).
      http://www.tanzmed.com/index.php/features/uzazi?start=5
      mama D likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    6. #324
      gody's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2010
      Posts : 734
      Rep Power : 726
      Likes Received
      161
      Likes Given
      18

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Leo nimekukubali mkuu yaana karibu nimefuatilia thread zako zote na zpo deep:
      MziziMkavu likes this.

    7. #325
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,205
      Rep Power : 19214
      Likes Received
      8165
      Likes Given
      26639

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Kuamsha tamaa ya kufanya tendo la ndoa kwa Mwanamme na Mwanamke Juisi ya tangawizi nusu kijiko pamoja na yai nusu iliochemshwa na asali. Tumia kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Hii dawa anaweza kutumia Mwanamke au Mwanamme.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    8. Miaka 50

    9. #326
      Remmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2009
      Location : home
      Posts : 4,342
      Rep Power : 7768
      Likes Received
      1546
      Likes Given
      1793

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Asante sana daktari!
      MziziMkavu likes this.

    10. #327
      mama D's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,501
      Rep Power : 735
      Likes Received
      395
      Likes Given
      1311

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      asante kwa elimu
      MziziMkavu likes this.
      Daily News halisomwi tandale kwa mtogole - MPOKI

    11. #328
      Paul mathew's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 116
      Rep Power : 394
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default

      [QUOTE=wamba;4068290]kingine kinachonipa mashaka ni kwamba hata kumgusa hataki kabisa yani ukitaka ugomvi basi mguse even hata nikitaka kutengeneza mazingira ya kufanya tendo hapo mnaweza kugombana tena mno na anasema kabisa 'sitaki kuguswa' it make me sick actually kwakuwa nakuwa kwenye wakati mgumu sn kwakweli. ME SINA MCHANGO HAPA LO! I HAVE GOT THE SAME CASE.

    12. #329
      Dena Amsi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 17th August 2010
      Location : Saayo
      Posts : 11,859
      Rep Power : 8730
      Likes Received
      3152
      Likes Given
      1572

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Hii kitu inahusu sana mmmhhh kukosa hamu ya mapenzi its not only mambo ya causes like magonjwa etc but remember kuna maumbile yanachangia especially for wanawake im one of them mie nilikwenda hospital nikajua where is the problem and my husband nows everything shida iko wapi usifiche nenda kwa daktari atakuelekeza........for me its normal I can stay for almost two years without anything and nothing happen cause I know where is the problem....
      A Little Impatience can spoil great plan!!!!!!!!!!!!!!! "Dont Loose your temper nobody need it"

    13. #330
      Xidian's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Posts : 131
      Rep Power : 377
      Likes Received
      24
      Likes Given
      34

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      tumia Soy Isoflavone Softgel Capsule
      Function:
      1.Balance estrogen level to improve female climacteric syndrome and promote bone metabolism to improve osteoporosis.
      2.Regulate cholesterol
      3.Nourish skin , anti aging
      4.Reduce risk of breast cancer and help ovaries function
      5.Improve sleeping
      6.Improve the quality of sex, nourish vaginal and flexibility of vaginal muscles

      Bei:48,000 tsh or 25 usd
      How To get : contact me

      Dawa Nyingine ni OceaPower Capsule
      Function:
      1.HelpFor sexual dysfunction and giving you a better sexual life
      2.Increase the power and vitality

      Price:30,720 tsh

      Hata Kama anatatizo gani huyo mwanamke ni lazima arudie hali yake.
      KaribuKwa ushauri zaidi .
      Last edited by Xidian; 1st July 2012 at 22:09.

    14. #331
      mchajikobe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2009
      Posts : 1,197
      Rep Power : 737
      Likes Received
      96
      Likes Given
      35

      Default Re: Kuishiwahamu

      Anzisha tabia ya kujikojolea kitandani!!!
      tired of being fooled!!

    15. #332
      situmai's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 78
      Rep Power : 546
      Likes Received
      16
      Likes Given
      9

      Default siku hz sina hamu ya kufanya mapenzi,whats happening?


    16. #333
      saita's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd June 2012
      Posts : 35
      Rep Power : 355
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuishiwahamu

      Hayo ndiyo maipact ya fgm au ukeketaji, laani hilo katika jamii yako

    17. #334
      Mtanzania haswa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 533
      Rep Power : 544
      Likes Received
      60
      Likes Given
      18

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      FOREVER MULTI-MACA ndio suruhisho. Inatokana na mmea, au Lepidium Meyenii kutoka nchi ya Peru wenye historia ya miaka zaidi ya 2000 kwa kuongeza stamina ya mwili. Haina madhara na ina faida kubwa sana kwa wanaume na wanawake. Wanawake wa Peru wanatumia maca kuanzia wakiwa miaka 3 ili wawe na nguvu, hamu ya tendo la ndoa na uwezo wa kuzaa ina protein nyingi ktk mfumo wa amino acids na virutubisho muhimu inavyosaidia kazi ya kuamsha ishara za hamu ya tendo la ndoa. unahitaji namba yangu ni 0713348165. nipo D

    18. #335
      Kanjunju's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 90
      Rep Power : 456
      Likes Received
      5
      Likes Given
      9

      Default Re: Kukosa hamu ya tendo la ndoa

      kwakweli sasa nimegundua kwamba wanawake wengi tuna tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.kinachosikitisha hakuna mtu ana jibu sahihi kuhusu tatizo hili.kimsingi mimi nipo kwenye ndoa kwa miaka 5,kwangu sio hamu ya tendo la ndoa tu,ila sipendi hata kuguswa sijui nina tatizo gani?umri wangu ni miaka28.tafadhari kwa yeyote mwenye jibu sahihi kuhusu tatizo langu anisaidie.imefikia hatua sasa mume wangu anadiriki kusema atatafuta mwanamke mwingine kwakuwa mie sitaki kubadilika.kimsingi sipendi kupoteza ndoa yangu ila natamani nirudi kwenye hali yangu ya kawaida.sipendi chochote kinachohusiana na tendo la ndoa.

    19. #336
      dennisrt88's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 27th July 2012
      Posts : 21
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1
      Likes Given
      4

    20. #337
      AGNETH's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 45
      Rep Power : 353
      Likes Received
      8
      Likes Given
      10

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Nakupa pole sana kaka yangu mapenzi gani hayo ya kuumizana achana naye mbona tupo hata kama unapenda hikusaidii bali unajitesa mwenyewe au siyo

    21. #338
      Mtanzania haswa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 533
      Rep Power : 544
      Likes Received
      60
      Likes Given
      18

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Maca, also known as Lepidium Meyenii, is an annual plant that is cultivated in the Peruvian central highlands. The edible root, which resembles a radish, is a staple food for the local population.
      Maca has been highly revered for over 2,000 years in Peru. According to legend, the Incan warriors ate Maca for strength and endurance before going to battle. The Spanish Conquistadors called it the “sex herb of the Incas.” Today it is known as “Peruvian Ginseng”. Modern studies suggest that Maca may promote libido, sexual potency and energy.

      Women in South America have also used Maca for thousands of years to help maintain their stamina and handle stress. Peruvian women begin using Maca at age 3, and remain strong, fertile and productive, well into their later life. Maca may increase a woman’s libido, and should be taken daily for best results.

      Forever Multi-Maca®combines legendary Peruvian Maca with other powerful herbs and select ingredients, to create one of the finest supplements of its kind!



      • Known as the sex herb of the Incas
      • Helps promote libido, stamina and energy



      IN NEED PLEASE PM

    22. #339
      pretty n's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2012
      Location : Arusha
      Posts : 273
      Rep Power : 394
      Likes Received
      60
      Likes Given
      18

      Default Re: Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi (low sexual libido or loss of libido)

      Unatafuta kuachwa ili upendwe na mwgne cyo? au ukataftie hamu kwngne, ukifanya kosa ukaachika, utakua 2 unazckia ndopa kwenye bomba... acha kufanya mambo ya kichekechea

    23. #340
      makoye78's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th February 2012
      Location : In my room
      Posts : 263
      Rep Power : 417
      Likes Received
      74
      Likes Given
      8

      Default

      Quote By Mrs Mtaba
      Nimependa tuu yeye ndo aniache.
      pumbavu.

    Page 17 of 18 FirstFirst ... 715161718 LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...