Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 38 of 38
    1. #1
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,611
      Rep Power : 15262
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2868

      Default Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake




      WANAWAKE wengi hasa waishio nchi zinazoendelea wamekuwa wakipanga uzazi kwa kutumia dawa wanazopewa na ushauri wa namna ya kuzitumia. Lengo la ushauri huo ni kuepuka kuzaa bila mpangilio huku wakiaminishwa kuwa dawa hizo zinawasaidia.

      Dawa hizo licha kuwapatia madhara, lakini wengi wao wamekuwa wakikaa kimya na kuugulia madhara wanayoyapata, tena bila kujaza fomu ambazo baadhi ya watumiaji wamedai kuwa hawafahamu lolote kuhusiana nazo. Mbali na shirika hilo kutetea uhai nchini, pia huwa linazunguka barani Afrika kueleza na kutetea madhara yatokanayo na dawa hizo, utoaji mimba, elimu kwa vijana, usafi wa roho na mambo mengine.


      Katika utafiti niliofanya mkoani Mbeya na vitongoji vyake, ukiandaliwa na kudhaminiwa na Shirika la Kutetea Uhai wa Binadamu Tanzania (PROLIFE), niligundua kuwapo kwa wanawake wengi ambao wamepata madhara baada ya matumizi ya dawa hizo. Kabla sijaendelea na namna utafiti ulivyofanyika na madhara waliyoyapata, nianze kwa kueleza aina ya dawa na vidhibiti mimba vitumiwavyo.


      Kuna aina tano ya vidhibiti mimba, nazo ni vidonge vya majira vitumiavyo chachu za bandia za projestorini na estrojeni zilizotengenezwa katika maabara ambapo mwanamke humeza kila siku. Zipo aina mbalimbali za vidonge, majina ya vidonge hutegemea aina na kiwango cha chachu zilizowekwa.

      • Vidonge vyenye chachu ya estrojeni pekee huitwa vidonge na

      • vidonge vyenye mchanganyiko wa chachu ya estrojeni na projestini huitwa vidonge mchanganyiko.


      Vidonge vyenye chachu aina ya projestini pekee huitwa: Progestorene Only Pills (POP) au Low Dose Pill au Mini Pill. Leo hii vidhibiti mimba vingi vimetengenezwa kwa chachu hii pekee ambayo ni morning After Pills, RU486, Emmergency Contraceptives.
      Aina ya pili ni vipandikizi ambapo mashirika yanayoendeleza njia za kisasa za kupanga uzazi wanasifia vipandikizi, kama ni njia nzuri na salama kwa wanawake wanaotumia.

      Mashirika hayo yanadai kuwa, njia hii ni rahisi kwani inaondoa ile adha ya kumeza vidonge kila siku, zoezi ambalo baadhi ya watumiaji husahau.
      Hii ni chachu au homoni iitwayo ‘levonorgestrel’ inayowekwa katika vifuko 6. Baada ya kuwekwa, huanza kufanya kazi saa 24 hadi miaka 5. Kila kifuko huwekwa mg 36 za chachu ya ‘crystalline levonorgestrel’ na kila kimoja kina urefu wa mm 34 na upana wa mm 2.4. Kiasi cha mg 30 ya projestini husambazwa katika damu kila siku.

      Aina ya tatu ni kondomu inayotumika kwa mwanaume na mwanamke pia. Kwa kawaida kifaa hiki hubana kufuatana na umbile la mtu.
      Kondomu zimegawanyika katika aina tatu; ya kwanza ni zile zilizotengenezwa kwa utumbo wa kondoo zinazosemekana kuwa hazina uwezo mkubwa zikitumika kama kidhibiti mimba.

      Aina ya pili ni zile zilizotengenezwa kutokana na mpira wa latex. Watengenezaji wanazisifia kuwa na ubora mkubwa zinapotumika au kama kidhibiti mimba au kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa maambukizo ya magonjwa ya zinaa ikiwemi virusi vya ukimwi (VVU). Aina ya tatu ni kondomu zilizotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mpira na vitu vingine ziitwazo “polyurethane.” Soko la kondomu limepata umaarufu zaidi kuanzia miaka ya 1980 kufuatia kuzuka na kuenea kwa janga la ukimwi.


      Aina ya nne ya vidhibiti mimba ni kitanzi. Hiki ni kifaa kidogo cha plastiki chenye vinyuzi mwishoni, ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba kupitia uke. Mtumiaji anaweza kugusa nyuzi hizo kama anataka kujua kitanzi alichoweka bado kipo. Baadhi ya wanawake ambao nilipata kuzungumza nao baada ya Mkurugenzi wa Prolife, Emil Hagamu kutoa mafundisho, walieleza madhara na kusema kuwa mwanzo hawakujua wanaumwa nini, na matatizo yao yanatokana na nini.


      Scola Yusuph alieleza:
      “Mimi nilitumia vidonge, lakini nikawa natoa harufu mbaya katika sehemu zangu za siri na nilipimwa nikaambiwa nina fangasi.” Naye Agness Raphaely anasema baada ya kutumia sindano aina ya depo provera akawa hajisikii hamu ya tendo la ndoa japo kabla ya kutumia alikuwa akifurahia.


      Zawadi Kilembe ameeleza kuwa, alichoma sindano Januari 13 mwaka huu na akaanza kupata siku zake mfululizo hadi Aprili 17.
      Anasema alikuwa anaumwa sana kila siku hadi kufikia kulazwa, na kusema madhara mengine aliyopata ni kukonda, kichefuchefu, kichwa kuuma, kuumwa tumbo na chembe moyo.

      Katika tafiti ya kwanza iliyoshirikisha zaidi ya wanawake 350, wanawake 150 kati yao walieleza madhara waliyoyapata kutokana na dawa hizo.
      Tafiti hii pia iliendelea hadi Mbeya vijijini ambako nilibahatika kukutana na wanawake wa Kanisa la Moravian katika Kijiji cha Igoma, ambao wanaeleza matatizo wanayoyapata baada ya kutumia dawa za uzazi wa mpango.

      Elizabeth Brayson anasema baada ya kutumia vidonge alipata matatizo ya kuumwa kichwa na kutoka damu mfululizo. Anasema baada ya kupata shida hiyo, aliamua kwenda hospitali na kushauriwa abadilishe na kuweka vipandikizi maarufu vya vijiti. Imelda Mwakilasa anasema baada ya kuchoma sindano moja alikosa hamu ya tendo la ndoa hali iliyosababisha kuwa na mgogoro wa mara kwa mara na mumewe, na ilimchukua miaka minne na alipata kizunguzungu na kichwa kuuma, kiasi kwamba hata alipokunywa dawa kilikuwa hakiponi.


      Hao ni baadhi tu ya wanawake ambao wameumizwa na matumizi ya dawa hizo. Mkurugenzi wa Prolife, Hagamu, anaeleza dhima nzima ya shirika hilo na kusema kuwa ni kulinda, kutetea na kudumisha uhai wa binadamu, kutetea hadhi na heshima yao kwani vidhibiti mimba vinaharibu hekalu la Mungu. Dhima nyingine ni kufundisha njia za uzazi wa mpango kupitia maumbile ya mwanamke, elimu ya usafi wa moyo, na kutengeneza taifa la mtetezi wa uhai.

      Njia mbalimbali zitumikazo kuzuia mimba


      Fertility awareness-based methods—or natural family planning—are all about tracking your menstrual cycle to determine the days that you can get pregnant. The tricky part is actually knowing when those days are. To do that, you'll need to pay very close attention to your body and its patterns. Here we list all the different ways you can monitor your day-to-day fertility.


      "The Pill" is a pill. (How's that for stating the obvious?) Some people call it "oral contraception." You take it once a day, at the same time every day. There are lots of different kinds of pills on the market, and new ones come out all the time. They all work by releasing hormones that keep your ovaries from releasing eggs. The hormones also thicken your cervical mucus, which helps to block sperm from getting to the egg in the first place.


      A female condom is a pouch you insert into your vagina. It's not the prettiest thing in the world (it looks a bit like a floppy, clear elephant trunk) but it does give you more control than a male condom when it comes to preventing STIs. Female condoms work the same way that male condoms do, except that you wear one on the inside instead of sticking it on a penis. They keep the guy's sperm inside the condom and out of your vagina.


      A diaphragm is a shallow, dome-shaped cup made of latex or silicone. (Honestly, it looks like Meg Griffin's hat on The Family Guy. Except it's off-white and only a few inches in diameter.) You insert the diaphragm into your vagina. Then it covers your cervix and keeps sperm out of your uterus. One super important thing to remember: For a diaphragm to work effectively, you need to use it with spermicide.
      Last edited by Candid Scope; 23rd June 2012 at 05:34.
      Elli, Fadhili Paulo, Yummy and 2 others like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      sister's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Location : MBEZI YA KIMARA, DSM
      Posts : 1,443
      Rep Power : 959
      Likes Received
      450
      Likes Given
      470

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Quote By Candid Scope


      Njia bora kabisa na ambayo haina madhara ya pekee ni utumiaji wa kalenda. Mwanamke ndiye anayetakiwa kuijua vema njia hii kwani ndiye atakayekuwe mwepesi kusoma mwenendo wa kalenda yake na kumwekea alama ya hatari au salama mumewe. Tofauti na madawa madhara yake huwezi kuyajua nini kitakutokea kwa sababu kila mmoja reaction mwilini inatofautiana na wengi.
      ahsante

    4. #22
      kindogile's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd May 2012
      Location : Mafinga
      Posts : 18
      Rep Power : 356
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Na kama siku zako zimetofautiana sana yaan hazieleweki njia ipi ni salama? Kwakua calendar hapa nadhani itasumbua? Naomba ushauri tafadhali

    5. #23
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,969
      Rep Power : 2371
      Likes Received
      962
      Likes Given
      172

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Nilipokuwa 4th year nafanya OB& GY Clerckship niliwahi kumuuliza mwalimu kuhusu papai ... inajulikana kwamba papaya ina uwezo wa kutoa mimba ... je mtu akila papaya after intercorse je inaweza ikawa ni njia nzuri ya birth control ...?! hakunijibu nikasahau kumuuliza badaye but still najiuliza hilo swali...

      kila njia ya kuzuia mimba ina side effects zake ... nyingine si kubwa sana nyengine ni kubwa sana inategemea mtu na mtu ! calender ni njia nzuri though pia sio 100% safe
      nyumba kubwa likes this.
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    6. #24
      The secretary's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2012
      Posts : 2,728
      Rep Power : 19054
      Likes Received
      1460
      Likes Given
      129

      Default

      Quote By njiwa
      Nilipokuwa 4th year nafanya OB& GY Clerckship niliwahi kumuuliza mwalimu kuhusu papai ... inajulikana kwamba papaya ina uwezo wa kutoa mimba ... je mtu akila papaya after intercorse je inaweza ikawa ni njia nzuri ya birth control ...?! hakunijibu nikasahau kumuuliza badaye but still najiuliza hilo swali...

      kila njia ya kuzuia mimba ina side effects zake ... nyingine si kubwa sana nyengine ni kubwa sana inategemea mtu na mtu ! calender ni njia nzuri though pia sio 100% safe
      Papai bichi na si lililoiva

    7. #25
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,969
      Rep Power : 2371
      Likes Received
      962
      Likes Given
      172

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Quote By The secretary
      Papai bichi na si lililoiva
      ah! mkuu don't get me wrong aim not sure papaya can be used as a birth control but aim sure it is used to induce abortion na local people also it has been documented papaya can induce abortion esp India... kuhusu as a birth control aim not sure about this

      click hii link ya wiki answrs for more info
      hapa
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    8. Miaka 50

    9. #26
      Mamatalim's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 26th June 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake


      The contraceptive implant is a small flexible tube that's inserted under the skin of your upper arm. It releases the hormone progestogen to prevent pregnancy.You can have the implant removed at any time, and your natural fertility will return very quickly.

      This means that once the implant is removed, you could get pregnant as easily as if you'd never had the implant. It's very useful for women who know they don't want to get pregnant for a while.

      Once the implant is in place, you don't have to think about contraception for three year. In the first year after the implant is fitted, your periods may become irregular, lighter, heavier or longer. This usually settles down after the first year. Side Effects ndo hizi-A common side effect of the implant is that your periods stop (amenorrhoea).

      It's not harmful, but you may want to consider this before deciding to have an implant.

    10. #27
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,611
      Rep Power : 15262
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2868

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Quote By kindogile
      Na kama siku zako zimetofautiana sana yaan hazieleweki njia ipi ni salama? Kwakua calendar hapa nadhani itasumbua? Naomba ushauri tafadhali
      Nadhani njia hii ni bora kwa vile yai likikaribia kuangua dalili za ute mgumu hujitokeza, ukishaona hivyo uwe na tahadhari na pengine bora kusitisha kaibisa. Na ute laini ukishaanza ujue red tag, la sivyo ukavu ni salama zaidi for 95%.

    11. #28
      kajumula.'s Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Location : iringa.
      Posts : 32
      Rep Power : 354
      Likes Received
      0
      Likes Given
      7

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Ni taarifa nzuri sana..lakini elimu ya afya bado inahitajika sana

    12. #29
      Mhindih's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 205
      Rep Power : 456
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Je somo la jinsi ya kutumia hiyo kalenda mmetoa? Au ni assuming tu kuwa kila mtu anajua matumizi ya kalenda.

    13. #30
      Nivea's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 5,696
      Rep Power : 16250
      Likes Received
      3146
      Likes Given
      4068

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Quote By Elli
      Mpwa ujumbe wako umekuja wakati muafaka kabisa, naomba unishauri sasa njia gani tutumie na shemeji yako maana hii imenitisha sana, ntafurahi kama utanijibu kwa PM au hata hapa hapa jamvini ili na wengine wafaidi, maana najua wako wengi
      ni kwelu tupo kibao woga tele
      Elli likes this.
      Kosea njia utaelekezwa,lakini usikosee mtu wakuoa /kuolewa naye,vinginevyo majuto yatakuwa sehemu ya maisha yako.tuliza kichwa unapochagua mwenzi wa maisha.

    14. #31
      Elli's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,574
      Rep Power : 2551
      Likes Received
      2142
      Likes Given
      1862

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Umeona eeeh mi nilijua tu
      Quote By nivea
      ni kwelu tupo kibao woga tele
      ...but what MAN is entirely without Evil intent in the Silence of his Soul???

    15. #32
      manuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2009
      Posts : 711
      Rep Power : 656
      Likes Received
      263
      Likes Given
      185

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Je kuna njia ya kuondoa hiyo sumu mwilini kama mtu anahitaji kubadili njia na kutumia Calender ili isije kuwa unatumia Calender na kiwango cha sumu mwilini kianaendelea kuongezeka kutokana na PILLS ulizikwisha kutumia.
      Sababu nahisi hii ni tatizo kwa my wife coz tunapiga yale mambo yetu ili tufanye product lakini hakuna matokeo chanya
      yaani hadi nimefanya kama ndio home work yangu after job nikupiga mambo yetu tu hadi sasa napungua uzito bila mafanikio.
      Fadhili Paulo likes this.
      TO BE HURT ITS YOUR OWN WILLING

    16. #33
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,611
      Rep Power : 15262
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2868

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Quote By manuu
      Je kuna njia ya kuondoa hiyo sumu mwilini kama mtu anahitaji kubadili njia na kutumia Calender ili isije kuwa unatumia Calender na kiwango cha sumu mwilini kianaendelea kuongezeka kutokana na PILLS ulizikwisha kutumia.
      Sababu nahisi hii ni tatizo kwa my wife coz tunapiga yale mambo yetu ili tufanye product lakini hakuna matokeo chanya
      yaani hadi nimefanya kama ndio home work yangu after job nikupiga mambo yetu tu hadi sasa napungua uzito bila mafanikio.
      Umeuliza swali zuri sana. Wengi wenye kutumia hizi pills za majira pengine huchanganyikiwa na wengine hata kuvunja mahusiano kwa sababu ya kuhangaika kupata kiumbe kipya bila mafanikio. Ukweli sumu hubaki muda mrefu, na kama huna subira unaweza kufanya makosa kuchukua uamuzi wa haraka na ukashtukia baadaye unapata nafsi ya yai kurutubishwa vizuri, hili wengi limewatokea sana, ila yataka uvumilivu na uelewa. Hii inawasaidia zaidi uwezekana wa kupata kwa vijana wenye umri mdogo chini ya 30, lakini ukianza kutumia pills hizo umri kuanzia 30 and up wengi hupata shida kurudisha neema ya kurutubishiwa.

      Kutoa sumu mwilini kwa namna fulani ni kuongeza sumu nyingine kwa kumia pills ambazo zinaweza zikafanya mchanganyiko wa madawa kutengeneza kitu kingine chenye kukuletea madhara mengine. Labda cha msingi ni kujiepusha na matumizi ya pills na hivyo kutumia njia ya kalenda ambapo for 100% haikuletei madhara kama ya utumiaji wa njia nyiingine.

    17. #34
      Jeji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2011
      Location : hapa hapa
      Posts : 1,479
      Rep Power : 695
      Likes Received
      217
      Likes Given
      288

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      hizi njia kwa kweli si nzuri zina madhara, ni bora kuwa makini na utumiaji wa kalenda tu. mimi pia nina mifano ya wadada watatu waliopata madhara kutokana na njia za uzazi wa mpango. wawili walitumia kijiti au kipandikizi na mmoja alitumia sindano.
      Candid Scope likes this.
      Yeremia 33:3

    18. #35
      Muangila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2010
      Posts : 817
      Rep Power : 633
      Likes Received
      186
      Likes Given
      497

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      hii njia ya ku release spams nje ni nzuri kwa wadada lkn kwetu wanaume inataka moyo

    19. #36
      Fadhili Paulo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2011
      Location : maajabuyamaji.net
      Posts : 1,117
      Rep Power : 794
      Likes Received
      281
      Likes Given
      996

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      Mkuu Candid scope, mi nikupongeze kwa maelezo yako mazuri, ubarikiwe sana mkuu, kusema ukweli haya ni moja ya madudu nisiyoyapenda kabisa maishani. Mi na wife hatutumii kabisa madudu hayo, tunafuatilia tu kalenda na ku-withdraw out pale tarehe zinapokaribia.
      Maji ni Uhai. Tembelea www.maajabuyamaji.net kujifunza namna ya kutumia maji kujikinga na kujitibu na maradhi mbalimbali.

    20. #37
      kilikou's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 25th April 2012
      Location : dareesalaam
      Posts : 9
      Rep Power : 358
      Likes Received
      0
      Likes Given
      10

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      wakuu wa msaada vp? mwanamke ambae anatumia kalenda alafu anasumbuliwa na tatizo la kwenda hedhi almost two weeks sasa naomba msaada wenu

    21. #38
      kilikou's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 25th April 2012
      Location : dareesalaam
      Posts : 9
      Rep Power : 358
      Likes Received
      0
      Likes Given
      10

      Default Re: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

      wadau nini sababu ya breeding inayochukua zaidi ya wiki mbili kwa msichana ambae hajawahi kutumia njia ya uzazi wa mpango
      Last edited by kilikou; 11th July 2012 at 13:21. Reason: typing error

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...