naomba kujua dalili na visababishi na first aid kabla ya kufika hospital
naomba kujua dalili na visababishi na first aid kabla ya kufika hospital
Wapi msaada
first aid hutolewa kwenye matatizo ya dharura sidhani kama pneumonia inaweza kuwa tatizo la dharura.
COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND
hilo sio tatizo la dharula maana huanza taratibu na matokeo yake huonekana kikubwa nikwenda hospital unapoona dalili zake
dalili zake ni zipi?
tembelea Wanetu.com :: Elimu kuhusu Ujauzito na Uzazi, Malezi na makuzi ya watoto, Afya ya watoto, Saikoljia, Tabia na Haki za Watoto kwa msaada wa kitaalam kutoka kwa wataalam, unaweza kupost swali lako hapo na doctor akalijibu. nenda kwenye category ya magonjwa na maambukizi utakuta hizo habari.
Pneumonia ni ugonjwa unaotokana na maambukizi ktk mapafu(yanaweza kuwa yote au moja).Husabishwa na bacteria,virusi au hata fangasi.Dalili zinahusisha kukohozi chenye makoozi,mafua,homa,kupumulia ndani(breathing in) ambayo huambatana na sauti zisizo za kawaida kufuani n.k.Hili sio tatizo la dharura nenda hospitali watachukua makohozi(sputum culture) au kitu kinaitwa pleural effusion,ikithibitika matibabu yataanza.
Ngahekapahi naona umefika mbali saana....Pneumonia ni ugonjwa unaowapata both watoto na watu wazima, sina hakika unaongelea kwa group gani sasa, maana baadhi ya dalili zaweza tofautiana.
Naomba niongelee kwa watoto (mimi ni mdau mkubwa wa afya za watoto). Pneumonia kwa watoto ni ugonjwa simple sana (lakini unaongoza kwa kuua) ambao wala hauhitaji ujuzi mwingi na test sophisticated kuugundua na kutoa matibabu husika. Dalili kubwa kwa watoto ni kikohozi, na/au mafua, na/au homa, na kupumua kwa shida na/au haraka. Daktari atamchunguza kwa kuhesabu idadi yake ya pumzi kwa dakika, kama imevuka kiwango cha kawaida basi ni Pneumonia. Daktari pia anaweza msikiliza mtoto kifua kwa stethoscope na kusikia crepitations.
Udharura wa Pneumonia unakuja kama ni Pneumonia kali (kuna vigezo vya kusema hivyo)...mara nyingi hakuna first aid unayoweza kutoa nyumbani zaidi ya kumuwaisha mtoto hospitali akapate huduma husika. Pneumonia sasa hivi inaua watoto wengi zaidi hata ya Malaria.
NB:
Sputum Culture ni kipimo ambacho unatoa makohozi ili kutambua ni vijidudu gani (microbacteria) wamesababisha hiyo Pneumonia, mara nyingi hufanyika kwa Pneumonia Sugu na/au Tuberculosis.
Pleural Effusion ni complication ya Pneumonia pale inapoendelea kiasi cha mapafu kujaa maji kwenye pleural cavity...hii ni complication late sana ya Pneumonia sugu au Tuberculosis, na hayo maji maji yanaweza kutolewa kwa sindano ili kupima kujua ni vijidudu gani vinasababisha.
All things are DIFFICULT before they are EASY - Thomas Fuller
pneumonia(kichomi) ni uvimbe katika tisssue za mapafu, ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu au unaweza kutokea kutokana na magonjwa mengine , bacteria wanajulikana kwa kusababisha pneumonia ni kama Streptococcal pneumoniae, Hemophilus infl uenza, Staphylococcus aureus, and Mycoplasma pneumoia, virus na parasite husababisha pia kama Pneumocystis carinii
Dalili kwa watoto chini ya miaka mitano
dalili kubwa kwa watoto ni kikohozi na kupumua kwa shida
ili kutambua ni pneumonia kwa watoto
1/tazama uwezo wa upumuaji huwa mtoto anapumua haraka haraka sana na ukihesabu R. rate inapozidi 50 kwa wale chini ya miaka 5 na kwa wale chini ya miezi mitatu kiwango cha upumuaji huwa ni zaidi ya 60
2/sehemu ya chini ya kifua hubonyea na kuingia ndani mtoto anapopumua
DALILI KWA WALE MIAKA ZAIDI YA 5 NA KWA WAKUBWA
-homa
-maumivi ya kifua
-kupumua kwa shida
-mafua
-joto kupanda
-mapigo ya moyo kupanda kufikia kiwango cha 125beat/kwa dakika
-kubadika rangi ya ngozi kwanye lips za mdomo na kuwa za blue
first aid
ni kumuwaisha hospitali na kuhakikisha njia za upuaji hazijaziba anapumua vizuri
tiba
-benzylpenicillin
-chloramphenicol
-amoxicillin
-gentamycin
supportive tiba
-salbutamol
paracetamol 10mg/kg every 4-6 hours kamaanahoma
NOTE: ukiona Dalili kama hizo tafadhali wahi hospitali ukachukue vipima na umuone DOCTOR au NURSE kwa matibabu na ushauri
vipimo
-FBP(full blood picture)
-x-ray
-sputum culture
Follow Us Here