Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

    Report Post
    Results 1 to 8 of 8
    1. #1
      Sendeu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2009
      Posts : 60
      Rep Power : 520
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      Wadau naomba kujua infection kwenye mkojo kwa wanaume nini chanzo chake? Asanteni

    2. #2
      li sheng's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th September 2008
      Location : Tanzania.
      Posts : 47
      Rep Power : 558
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      Quote By Sendeu View Post
      Wadau naomba kujua infection kwenye mkojo kwa wanaume nini chanzo chake? Asanteni
      UTI= Urinary Tract Infection ni ugonjwa unaoambatana na mfumo mzima wa njia ya mkojo kutokea kwenye mafigo, mirija ya mkojo (ureter), kibofu, tunda (prostate gland ) na njia ya kupitia mkojo kwenye uume (urethra)
      Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:
      1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.
      2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana
      3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.
      4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
      5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo
      6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana,
      7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.
      Natumai nimejaribu kukutajia sababu kuu muhimu katika mazingira ya kawaida huenda zikakusaidia kukata kiu yako.
      Asante
      ZionTZ likes this.

    3. #3
      Sendeu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2009
      Posts : 60
      Rep Power : 520
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      Quote By li sheng View Post

      Shukran sana kwa ufafanuzi uliotulia -nini kifanyike ili kujikinga na ugonjwa huu ndugu zanguzi wadau-kinga nk.

    4. #4
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      G.o.v.i
      BINARY NO and habariyamujini like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    5. #5
      li sheng's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th September 2008
      Location : Tanzania.
      Posts : 47
      Rep Power : 558
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      Sorry kwa kuchelewa kukujibu,mambo ya ubizi.
      kinga ndugu yangu inaambatana na sababu za maradhi kama nilivyozieleza hapo juu, ila cha msingi ni pale unapopata tiba ni jambo la msingi Mtabibu / daktari kutafuta sababu ilipelekea tatizo hilo na sio kutibu dalili tu au kufata kipimo cha mkojo pekee, panahitajika ufatiliaji wa kina na kutibu sababu ya msingi, na kujiepusha na yale mambo yanayoweza kuzua mfumuko mwengine (predisposing factors)wa UTI mfano kunywa maji ya kutosha, kutojizuilia mkojo muda mrefu, kujisafisha baada tendo la ndoa, nk nk, jengine ni kujitibu mapema na kujifatilia /follow up mana unaweza kukaribisha compilication za UTI kama hutatibika kikamilifu ni vizuri kuongea na Daktari vya kutosha anapokutibu, atakusaidia njia ipi ilo bora kwako kujikinga kutokana na sababu aloigundua.
      Asante

    6. #6
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,842
      Rep Power : 19441
      Likes Received
      8646
      Likes Given
      28210

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I MWENYEWE..!

      U.T.I ni ugonjwa sugu unaosumbua sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa wadogo. U.T.I (Urinary tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na huweza kusababisha maumivu makali na unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na damu.

      Wataalamu wetu wa masuala ya tiba wanatueleza kuwa tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo inaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.

      UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA

      Kwa kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali. Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo halijawa sugu.

      Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia nyingine ya kuudhibitibi ugonjwa huu ni kunywa maji mengi au kwenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria wote ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.

      Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani.

      Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa kama unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa yanasababishwa na kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘antibiotics’, ambazo watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side effects). Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na ****liza dozi ili kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.

      KUZUIA

      Ili kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa akina mama.

      Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.

      DAYATI MUHIMU KUDHIBITI UTI

      Katika kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa vyakula vya ‘kupaki’ kama vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye ‘caffeine’, kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda.
      takashi likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You

      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    7. #7
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 815
      Rep Power : 684
      Likes Received
      143
      Likes Given
      822

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      Quote By MziziMkavu View Post

      Sawa sawa Dr,Mzizi Mkavu...nimefata maelekezo yako na sasa nimeanza kuona mabadiliko...Shukran sana.
      MziziMkavu likes this.
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    8. #8
      MAN PC's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2013
      Posts : 85
      Rep Power : 324
      Likes Received
      11
      Likes Given
      0

      Default Re: UTI kwa wanaume husababishwa na nini?

      madhara (effects ) za UTI ni zipi?

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...