Show/Hide This

  Topic: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

  Report Post
  Page 1 of 3 123 LastLast
  Results 1 to 20 of 42
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 34,222
   Rep Power : 429503890
   Likes Received
   20613
   Likes Given
   63334

   Thumbs up Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)
   FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
   Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

   TINDIKALI
   Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
   Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

   VITAMINI “E” NA B6
   Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

   Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

   FAIDA ZA PARACHICHI
   Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

   Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

   Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.


   HEDHI
   Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

   Aidha, tunda
   hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

   Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

   Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

   Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

   Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
   Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.

   Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.
   Kibunango, BAK, Mahmood and 25 others like this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)


  2. Rutashubanyuma's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 24th September 2010
   Location : Arusha
   Posts : 40,012
   Rep Power : 623274
   Likes Received
   5076
   Likes Given
   7928

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   thanks MziziMkavu
   MziziMkavu likes this.
   John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

   John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

  3. kijana makini's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 47
   Rep Power : 535
   Likes Received
   4
   Likes Given
   15

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Very well said..
   MziziMkavu likes this.

  4. miksel's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th January 2011
   Location : Mwaza
   Posts : 57
   Rep Power : 528
   Likes Received
   3
   Likes Given
   20

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Good job.Thnks.
   MziziMkavu likes this.

  5. Mtoto wa Mbwa's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 29th April 2012
   Posts : 6
   Rep Power : 449
   Likes Received
   1
   Likes Given
   2

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   MziziMkavu likes this.


  6. R CHUGGA's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 28th November 2011
   Posts : 124
   Rep Power : 494
   Likes Received
   13
   Likes Given
   17

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   I get you mzizimkavu thanx a lot..
   MziziMkavu likes this.

  7. Babkey's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th December 2010
   Posts : 2,526
   Rep Power : 1114
   Likes Received
   561
   Likes Given
   250

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   ...achante chana NziziNkavu.
   MziziMkavu likes this.

  8. ummu kulthum's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th February 2012
   Location : singida
   Posts : 2,790
   Rep Power : 7132
   Likes Received
   1294
   Likes Given
   677

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   nayapendaga haya matunda yaan hapa mzzmkavu unanitamanisha je?
   MziziMkavu likes this.
   ASIYEUMBA HAUMBUI

  9. Evarm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2010
   Location : totoroni
   Posts : 1,235
   Rep Power : 873
   Likes Received
   374
   Likes Given
   180

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Senkyu bro!
   MziziMkavu likes this.
   Everything in your life is a reflection of a choice you have made. If you want a different result, make a different choice.

  10. Mwanaweja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th February 2011
   Posts : 3,570
   Rep Power : 1226
   Likes Received
   498
   Likes Given
   1121

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   mzizimkuu nimekupata kweli tunda hili ni muhimu sana ila tu watanzania hatauana utamaduni wa kutumia sana natural food ninaimani tunaweza kuepukana na aina nyingi sana za magonjwa kwa kutumia vitu vya asili na vinavyopatikana kwa urahisi kwenye mazigira yetu
   MziziMkavu likes this.

  11. manasa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 2nd April 2012
   Location : DUNIANI
   Posts : 88
   Rep Power : 469
   Likes Received
   6
   Likes Given
   31

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Faida zake zimenifurahisha nitazidi kulitumia
   Swali- mafuta yake je hatanenepeshi?
   MziziMkavu likes this.

  12. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 34,222
   Rep Power : 429503890
   Likes Received
   20613
   Likes Given
   63334

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   PENDA MWILI WAKO: PARACHICHI KINGA YA SUMU MWILINI NA KUZEEKA   Kwa muda mrefu sana wanawake wamekuwa wakitumia parachichi kama nyenzo mojawapo ya urembo ima kwa kupaka kwenye uso au nywele bila kuwa na uhakika kama kweli parachichi husaidia katika kurutubisha nywele na ngozi ya kwenye uso, swali ni je ni wangapi wanajua faida za parachichi kiafya, hususani faida ya kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana?

   Wanasayansi wa chuo kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wamesema ya kwamba parachichi husaidia katika kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari (free radicals) na hivyo kuweka kinga dhidhi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana (fight against ageing). Wanasayansi hao wamesema kwamba mafuta yanayopatikana katika parachichi yanauwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama mitochondria.

   Free radicals ni kemikali zinazosababisha magonjwa mengi yakiwemo baadhi ya saratani, huharibu mishipa ya damu ya ateri (arteries), pamoja na kumfanya mtu kuzeeka haraka. Mafuta yanayopatikana katika baadhi ya mboga za majani, matunda na nyanya/tungule (tomatoes) yanauwezo wa kupambana na kemikali hizi hatari lakini mafuta haya hushindwa kuingia ndani ya mitochondria ambapo ndio kuna kemikali hizi hatari kwa wingi. Mtafiti Christian Cortes-Rojo kutoka chuo kikuu hicho cha Mexico ambaye ndiye alifanya utafiti huu, alisema ‘’Anti-oxidants zinazopatikana katika mboga za majani na matunda mengi haziwezi kupenya ndani ya mitochondria na hivyo kushindwa kudhibiti kemikali hatari ndani ya mitochondria hizo. Hivyo kusababisha kemikali hizo hatari kuendelea kushambulia mitochondria na kuziharibu, matokeo yake ni kuwa nishati haitolewi tena kutoka kwenye mitochondria na seli hushindwa kufanya kazi na kufa.”

   Matokeo ya utafiti huu yalitolewa katika kongamano la kila mwaka la chama cha wataalamu wa mambo ya biochemistry na bayolojia ya viumbe hai kutoka nchini Marekani (American society of biochemistry and molecular biology annual conference).

   Kemikali hizi hatari ni uchafu (natural waste products) zinaotolewa na mwili wakati wa kusaga chakula (metabolism), na huweza kutolewa kwa wingi kwa mtu anayevuta sigara,mtu anapokumbana na mionzi (radiation) na hata wakati kukiwa na uchafuzi wa mazingira (pollution). Kemikali hizi uharibu mpangilio wa protini katika muundo wa vina saba (DNA structure).


   Wanasayansi hao wakati wanafanya utafiti waliweza kuona ya kwamba mafuta ya parachichi yaliwezesha seli za yeast kuishi kwa muda mrefu kwenye madini chuma licha ya kuwekewa kiwango kikubwa cha madini hayo (exposed tohigh concentration of iron) ambayo ndio hutoa kemikali hizi hatari (free radicals) kwa wingi.

   Mtafiti Christian Cortes-Rojo alisema “Tunahitaji kuthibitisha ya kwamba kile tulichoona katika seli za yeast kinaweza kutokea kwenye seli za binadamu”. Katika tafiti ambazo ziliwahi kufanyika huko nyuma nchini Mexico, nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa parachichi duniani, zilionyesha ya kwamba parachichi hupunguza kiwango cha lehemu (blood cholesterol) mwilini na pia hupunguza baadhi ya mafuta yanayohusishwa na ugonjwa wa kisukari.


   Mafuta ya parachichi yana virutubisho sawa na mafuta ya olive oil yanayohusishwa kwa kusaidia kupunguza lehemu mwilini pamoja na kinga dhidhi ya magonjwa mengi sugu kama inavyoonekana kwa watu wanaoishi katika nchi za mediteranean ambao ni watumiaji wazuri wa mafuta haya ya olive oil.


   Parachichi hupatikana kwa wingi nchini Tanzania katika mikoa ya Tanga (Lushoto), na Mbeya hivyo ni muhimu kuboresha kilimo cha matunda haya ili kuweza kuboresha afya za wananchi. Kwa muda mrefu wanasayansi wamekuwa wakiita parachichi kama mfalme wa matunda kutokana na kuwa na virutubisho vingi kuliko tunda jingine lolote duniani.Hivyo, usisahau kula/kutumia parachichi mara kwa mara kwa afya njema.

   Penda Mwili Wako: Parachichi Kinga ya Sumu Mwilini na Kuzeeka
   Mamndenyi likes this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  13. nnunu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th March 2011
   Posts : 656
   Rep Power : 664
   Likes Received
   220
   Likes Given
   278

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Asante sana kwa elimu utupayo naamini wengi tunafaidika nayo.
   SAMAHANI, HIVI INAFAA KWA MTU MWENYE NGOZI YENYE MAFUTA MENGI USONI,
   KUPAKA UJI WA TUNDA HILI USONI ???. Jibu lako litani/tusaidia kupaka au kutokupaka usoni.

   Napenda kula hili tunda ksb nimezaliwa na kukulia sehemu ambayo,
   linapatikana hili tunda kwa urahisi sana, ila pia nimehamasika kulipenda zaid,
   baada ya kusoma kuwa linasaidia kutoa au kupunguza baadhi ya sumu mwilini,
   tupatazo baada ya kula red meat( japo nala kwa nadra sana).
   MziziMkavu and Mamndenyi like this.

  14. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 34,222
   Rep Power : 429503890
   Likes Received
   20613
   Likes Given
   63334

   Thumbs up Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   MSIMU wa matunda ya Parachichi umeshaingia. Kama yalivyo matunda yote kwa ujumla kuwa yana faida sana katika mwili wa binadamu, vivyo hivyo na Parachichi. Tunda hili lina maajabu makubwa katika kupambana na maradhi hatari ya moyo na sataratani ya matiti kutokana na virutubisho ilivyonavyo.

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya tunda hili, awali ya yote tunda hili lina kirutubisho
   aina ya Aloic Acid ambayo ni aina fulani ya mafuta mazuri yanayosaidia kushusha kolestrol mwilini. Katika utafiti mmoja waliofanyiwa watu kadhaa waliokuwa na matatizo ya kolestro mwilini, baada ya

   kutumia maparachichi kwa muda wa siku saba, walionesha mabadiliko mazuri katika afya zao kwa kupungua kiwango cha kolestro mbaya mwilini.

   Aidha, parachichi lina kiwango kikubwa sana cha madini aina ya potasium ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha mzunguruko wa damu mwilini.

   Inaelezwa kwamba ulaji wa kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu, hutoa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa yatokanayo na mzunguruko mbaya wa damu mwilini, kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kiharusi.


   Mbali ya madini hayo, parachichi lina virutubisho vingine kama vile
   Folate (Folic acid) ambacho ni muhimu sana kwa afya na ustawi wa moyo, kwa maana hiyo watu ambao wanakula sana vyakula kama parachichi lenye kirutubisho hicho, watukuwa salama dhidi ya magonjwa ya moyo au kiharusi kwa asilini 55.

   Kirutubisho kingine kinachopatikana kwa wingi kwenye parachichi ni
   Fatty Acids, ikiwemo Oleic Acid. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, imedhihirika kwamba virutubisho hivyo ni kinga tosha dhidi ya Saratani ya matiti. Kwa maana nyingine, wanawake wanaokula kwa wingi

   Maparachichi, wanaipa miili yao kinga dhidi yaSaratani hiyo ambayo hivi sasa imekuwa tishio miongoni mwa wanawake nchini.
   Parachichi linaweza kuliwa kama mtu atakavyopenda, wapo watu wanaopenda kula bila kuchanganya na kitu kingine, lakini pia parachichi linaweza kuliwa kwa kupaka kwenye mkate badala ya Blue Band. Halikadhalika parachichi linaweza kuliwa kwa kuchanganya na nyanya, vitunguu, ndimu na chumvi kidogo kama kachumbari ya kipekee.

   VIRUTUBISHO VYA PARACHICHI


   Kwa ujumla, parachichi ni chanzo kizuri cha
   Vitamini K, Vitamini B6 na Vitamini C.
   Aidha, tunda hili lina kiwango kizuri cha virutubisho aina ya Folate, kopa na ufumwele (Fiber). Fiber ni muhimu katika kuwezesha mtu kupata choo

   laini na bila matatizo. Bila kusahau kwamba tunda hili ni chanzo kizuri pia cha madini ya Potasiamu: ina kiwango kikubwa kuliko hata ndizi.

   Ingawa parachichi ni tunda, lakini lina kiwango kikubwa cha mafuta (fats) ambayo yanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 71 – 88, kiwango ambacho ni cha juu kwa asilimia 20 ukilinganisha na matunda mengine. Kwa wastani, parachichi moja lina gramu 30 za mafuta, lakini kati ya hizo, gramu 20 ni za

   mafuta mazuri kiafya
   (Monounsaturated fats na Aloic Acid) ambayo husaidia kujenga afya bora mwilini.
   Utafiti zaidi kuhusu tunda hili unamalizia kwa kusema kwamba parachichi lina takribani aina 20 za Vitamin, madini na virutubisho muhimu

   (Phytonutriens) ambavyo hutuo kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mengi hatari. Baadhi ya Vitamini zilizomo na asilimia zake kwenye mabano ni pamoja na Vitamin E (4%), Vitamin C (4%), Folate (6%), Fiber (4%), Iron (2%) na Potasium (4%).

   Kwa ujumla tunda la Parachichi lina faida nyingi kiafya na tunatakiwa tuyale kwa wingi, hasa ukizingatia huu ndiyo msimu wake. ni jambo la kushangaza sana kuona kwamba watu wengine msimu wa maparachichi unaingia hadi unakwisha, mtu hajala hata moja.

   ''KUMBUKA KINGA NI BORA KULIKO TIBA''! (Prevention is Better Than Cure)
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  15. FirstLady1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th July 2009
   Location : Mama Mwenye Nyumba
   Posts : 15,975
   Rep Power : 85937855
   Likes Received
   4285
   Likes Given
   7536

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Thank you

   Be Blessed
   MziziMkavu likes this.
   No one is in charge of your happiness except you...
   God time is the best..
   Tupo wangapi?

  16. The secretary's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th January 2012
   Posts : 4,074
   Rep Power : 96482407
   Likes Received
   2465
   Likes Given
   745

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Wabheja. hili tunda pamoja na yai la kienyeji huwa nalitumia kama steaming ya nywele
   MziziMkavu likes this.

  17. Malila's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd December 2007
   Location : Makete mjini
   Posts : 3,736
   Rep Power : 35922835
   Likes Received
   1900
   Likes Given
   830

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   Quote By Mwanaweja View Post
   mzizimkuu nimekupata kweli tunda hili ni muhimu sana ila tu watanzania hatauana utamaduni wa kutumia sana natural food ninaimani tunaweza kuepukana na aina nyingi sana za magonjwa kwa kutumia vitu vya asili na vinavyopatikana kwa urahisi kwenye mazigira yetu
   Ngoja niongeze juhudi ktk kuipanda miparachichi huko shambani kwangu,siku zijazo itakuwa deal la kuzeekea.
   MziziMkavu likes this.
   Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

  18. HAZOLE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2011
   Posts : 1,198
   Rep Power : 749
   Likes Received
   250
   Likes Given
   43

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   nipo mazingira ambayo parachichi hailimwi na hupatikana kwa bei juu. dawa ni kupanda mti tu. we ngoja tu. viva mzizi...
   MziziMkavu likes this.
   JANA SI NIMEKOSEA BOMA NIKAINGIA KWA MAMA MKWE, IMELEWA SANA JANA. CHIBOROIKWE IMECHOOOOKA SANA LEO!!

  19. Kambiaso's Avatar
   Member Array
   Join Date : 2nd April 2012
   Posts : 42
   Rep Power : 460
   Likes Received
   28
   Likes Given
   1

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   i like avocado,hayo maelezo mks me love t mo
   MziziMkavu likes this.

  20. BADILI TABIA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th June 2011
   Location : DUNIANI
   Posts : 21,604
   Rep Power : 171830338
   Likes Received
   9935
   Likes Given
   8223

   Default Re: Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)

   mzizi mkavu nisaidie, nikila avocado nashiba siku nzima, yaani haijalishi nimekula kiasi gani...... Inatokana na nini?
   MziziMkavu likes this.


  Page 1 of 3 123 LastLast

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...