JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

  Report Post
  Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
  Results 21 to 40 of 46
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,470
   Rep Power : 429504379
   Likes Received
   22043
   Likes Given
   68192

   Default Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’


   Attachment 52332


   BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice’ huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added’ au ‘No preservatives’ (haikuongezwa sukari wala dawa)!

   Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!


   Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure’.

   NINI KINACHOTOKEA?
   Ni kweli kwamba ‘100% pure juice’ hutokana na matunda halisi kama vile machungwa, mananasi, embe, n.k, lakini mchakato wake wa kukamua, kuhifadhi na hatimaye kumfikishia mlaji ndiyo wenye dosari za kiafya.

   Kinachofanyika baada ya tunda kukamuliwa ni kuhifadhi juisi yake kwenye matanki maalumu makubwa ya viwandani. Ili juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, wanalazimika kuondoa hewa yake asilia ya oksijeni (mchakato unajulikana kitaalamu kama ‘deaeration’), kitendo ambacho huifanya juisi hiyo kupoteza ladha yake ya asili.

   NINI HUFANYIKA KUREJESHA LADHA YA MATUNDA?
   Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Food Renegade’ wa nchini Marekani unaojishughulisha na masuala ya lishe na kuhimiza ulaji wa vyakula asilia, makampuni yanayozalisha juisi hukodisha makampuni yenye ujuzi wa kutengeneza ladha mbalimbali za matunda na manukato.

   Makampuni hayo husimamia utengenezaji wa maboksi ya kuhifadhia juisi ambayo huwekwa ladha na harufu ya matunda husika. Inaelezwa zaidi kuwa makampuni hayo ndiyo yanayotengeneza pia manukato (perfumes) maarufu duniani, kama vile Dior na Calvin Klein.

   Lakini cha kushangaza, virutubisho vinavyotumika kutengenezea ladha hiyo bandia haviorodheshwi kwenye boksi na wenyewe wanajitetea kwa kusema kuwa ladha hiyo haiwezi kuorodheshwa kama sehemu ya ‘ingredients’ kwa sababu hutengenezwa kutokana na tunda lenyewe, ingawa wataalamu wengine wanadai utengenezaji wake huhusisha kemikali zingine ambazo siyo za asili.

   Mtaalamu mwingine kutoka Taasisi ya Sera ya Kilimo na Biashara nchini Marekani, Bi. Alissa Hamilton J. D (PhD), ameelezea kwa undani jinsi juisi ya machungwa inavyotengenezwa kiwandani. Undani huo umo kwenye kitabu chake cha; ‘Squeezed: What You Don’t Know About Orange Juice’. (Kitu usichokijua kuhusu juisi ya machungwa).

   Katika kitabu hicho, mwanadada huyo anasema kuwa ni muhimu kila binadamu kujua kwa undani jinsi chakula chake kinavyoandaliwa, kwa sababu maelezo au lebo inayowekwa kwenye boksi, siyo tu haisemi ukweli, bali pia hailezi ukweli wote.

   Anasema kwamba, kama kweli ‘pure orange juice’ tunayokunywa ilipatikana baada ya kukamuliwa chungwa peke yake na kuwekwa kwenye boksi, basi bila shaka ladha ingekuwa tofauti kati ya boksi moja na lingine, kwa sababu chungwa moja linatofautiana ladha na chungwa lingine. – mengine matamu, mengine makali.

   Mbali na hilo, kila kampuni inayotengeneza juisi ya machungwa ina ladha yake. Juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Tropicana ina ladha tofauti na juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Ceres, sababu ya tofauti hiyo inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.
   Last edited by MziziMkavu; 28th January 2014 at 09:59.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')


  2. nachid's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th April 2011
   Location : IRINGA
   Posts : 822
   Rep Power : 706
   Likes Received
   122
   Likes Given
   10

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   mi ni mnywaji mzuri wa juice za azam kuanzia leo napiga stop

  3. ngarambe's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 15th April 2012
   Posts : 100
   Rep Power : 509
   Likes Received
   11
   Likes Given
   0

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Asante sana

  4. Zion Daughter's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2009
   Location : Mlimani
   Posts : 8,934
   Rep Power : 28554457
   Likes Received
   4115
   Likes Given
   2167

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Quote By Mwanaweja View Post
   tusiinge mambo ya kigeni bali tutumie mazao yetu ya asili tutapunguza magonjwa mengi sana kwa kuwa nchi yetu imebarikiwa kila sehemu ina neema yake tuleni sana (Parachichi,Ndizi, machungwa,magimbi,zabibu, matango, tikitimaji,etc) yanapatikana pande zote za nchi
   Tuna tatizo kubwa.Hata hayo matunda nayo yameingiliwa kwani yamekaa KICHINA Mno.Siku hizi sio ajabu kuambiwa hili ni tikiti la kisasa au chungwa la kisasa n.k Na hayo matunda ya kisasa nayo yamejaa kemikos kibao...Hata hakieleweki siku hizi nini cha kufanya ili mradi hata hao TFDA na TBS wamelala usingizi...
   Blessed and highly favored

  5. Kimbori's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st February 2012
   Posts : 2,048
   Rep Power : 906
   Likes Received
   325
   Likes Given
   11

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Tujitahidi kula vyakula vyetu asilia. Hawa Wazungu watatuua, hata huko kwao, hivyo vyakula vinapigwa vita.

  6. Nchi Kavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Posts : 2,037
   Rep Power : 979
   Likes Received
   381
   Likes Given
   145

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Nalijua hili sema ubishi tu


  7. King'asti's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th November 2009
   Location : Masaini
   Posts : 26,131
   Rep Power : 429502269
   Likes Received
   20917
   Likes Given
   10494

   Default

   Tatizo ni kuwa unaacha juisi ya boksi unaanza kunywa konyagi ya chupa Husninyo
   Quote By Husninyo View Post
   Ahsante sana dokta mzizimkavu. Kuanzia leo nitaacha hizo juice za box.

  8. nyumba kubwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th October 2010
   Posts : 8,526
   Rep Power : 429498702
   Likes Received
   6434
   Likes Given
   8193

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Siko kuharibu biashara za watu ila mi nawashangaa sana wanaokunywa juice za Azam sijuhi anaweka sukari nusu kilo kwa box. Utasema yametengenezwa ili yawe diluted. Kuna watu unakuta wanaparamia box zima daily; kwa nini usinenepeane.

   Mimi ni mtu wa kutengeneza juice nyumbani, na wala si expensive kama kununua za box. 2500 napata matunda kibao mchanganyiko na tunakunywa nyumba nzima

   Quote By Foundation View Post
   Mimi nilacha kunywa juice hizi muda mrefu sana.Ziliniongeza uzito sana mpaka zikanigharimu muda na pesa kuushusha uzito sana

  9. MNYISANZU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2011
   Posts : 7,053
   Rep Power : 17398076
   Likes Received
   1038
   Likes Given
   83

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Ndio nimetoka kunywa juice ya namna hii muda huu!

  10. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,470
   Rep Power : 429504379
   Likes Received
   22043
   Likes Given
   68192

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Quote By KOMANDOO View Post
   mkuu mimi kwa sasa nakunywa maji tu, nina mwaka na miezi mitano tangia niache kutumia juice za makopo na soda, mkuu swali langu liko kwenye juce ya Rozela vipi hii juice ina faida zipi?

   Beverage

   Cuisine: Among the Bodo tribals of Bodoland, Assam (India) the leaves of both hibiscus sabdariffa and hibiscus cannabinus are cooked along with chicken, fish or pork, one of their traditional cuisines
   See also Hibiscus tea

   A roselle drink

   In the Caribbean sorrel drink is made from sepals of the roselle. In Malaysia, roselle calyces are harvested fresh to produce pro-health drink due to high contents of vitamin C and anthocyanins. In Mexico, 'agua de Flor de Jamaica' (water flavored with roselle) frequently

   called "agua de Jamaica" is most often homemade. Also, since many untrained consumers mistake the calyces of the plant to be dried flowers, it is widely, but erroneously, believed that the drink is made from the flowers of the non-existent "Jamaica plant". It is prepared

   by boiling driedsepals and calyces of the Sorrel/Flower of Jamaica plant in water for 8 to 10 minutes (or until the water turns red), then adding sugar. It is often served chilled. This is also done in Guyana, Antigua, Barbados, Dominica, Grenada, Jamaica and Trinidad and Tobago where it is called 'sorrel'. The drink is one of several inexpensive beverages (aguas frescas) commonly consumed in Mexico and

   Central America, and they are typically made from fresh fruits, juices or extracts. A similar thing is done in Jamaica but additional flavor is added by brewing the tea with ginger and adding rum. It is a popular drink of the country at Christmas time. It is also very popular in

   Trinidad & Tobago but cinnamon and cloves are preferred to ginger. In Mali, Senegal, The Gambia, Burkina Faso and Benin calyces are used to prepare cold, sweet drinks popular in social events, often mixed with mint leaves, dissolved menthol candy, and/or various fruit flavors. The Middle Eastern and Sudanese drink "Karkade"(كركديه) is a cold drink made by soaking the dried Karkade flowers in cold

   water over night in a refrigerator with sugar and some lemon or lime juice added.It is then consumed with or without ice cubes after the flowers have been strained.In Lebanon, sometimes toasted pine nuts are tossed into the drink.

   With the advent in the U.S. of interest in south-of-the-border cuisine, the calyces are sold in bags usually labeled "Flor de Jamaica" and

   have long been available in health food stores in the U.S. for making a tea that is high in vitamin C. This drink is particularly good for people who have a tendency, temporary or otherwise, toward water retention: it is a mild diuretic.


   In addition to being a popular homemade drink, Jarritos, a popular brand of Mexican soft drinks, makes a Flor de Jamaica flavored carbonated beverage. Imported Jarritos can be readily found in the U.S.


   In the UK the dried calyces and ready-made sorrel syrup are widely and cheaply available in Caribbean and Asian grocers. The fresh calyces are imported mainly during December and January in order to make Christmas and New Year infusions, which are often made into cocktails with additional rum. They are very perishable, rapidly developing fungal rot, and need to be used soon after purchase – unlike the dried product, which has a long shelf-life.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  11. MSEZA MKULU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd July 2011
   Posts : 767
   Rep Power : 680
   Likes Received
   448
   Likes Given
   773

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   nashukuru mkuu mzizi mkavu. Nakumbuak nimewahi kubishana sana kutetea juice ya CERES kuwa ni sahihi kabisa. Breki yangu ya kwanza ni kuwarudia watu niliowashawishi kutokana na kusoma rebo ya ingredients ili wajue wanachokunywa. mimi ndio naaga rasmi.

   thanks for adding value to my life.
   "The man who doesn't read good books, has no advantage over the one who can't read them" mark twain

  12. tpaul's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2008
   Posts : 8,125
   Rep Power : 302914552
   Likes Received
   2903
   Likes Given
   6752

   Default

   Quote By nachid View Post
   mi ni mnywaji mzuri wa juice za azam kuanzia leo napiga stop
   mkuu, hata azam embe sio 'natural' hata kidogo--ina kemikali za kufa mtu. juice halisi ni ile inayotokana na matunda halisi uliyochuma shambani wewe mwenyewe au uliyonunua kwenye soko kariakoo shimoni au tandale kwa bi nyau, basi!!!

  13. juve2012's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th October 2012
   Posts : 3,326
   Rep Power : 262840556
   Likes Received
   1540
   Likes Given
   628

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Artificial foods=artificial body=artificial mind=artificial man=artificial thinking=artificial actions=artificial world!Guess who want things to go this way?...ARTIFICIAL GOD!

  14. Sista's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th September 2013
   Posts : 2,957
   Rep Power : 25015076
   Likes Received
   830
   Likes Given
   195

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   MziziMkavu ibarikiwe. naomba kujua faida ya juice ya ubuyu na ukwaju

  15. nasalena's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 18th December 2013
   Posts : 146
   Rep Power : 431
   Likes Received
   34
   Likes Given
   6

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Muhimu kuliwek katika matendo kwa manufaa yetu

  16. ndupa's Avatar
   Banned Array
   Join Date : 25th January 2008
   Posts : 4,459
   Rep Power : 0
   Likes Received
   58
   Likes Given
   3

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Mweeee!! Sasa mimi najiuliza hatuna kitengo cha kuangalia yote haya?? Kama zina madhara kwanini zinauzwa?? Ila si mbaya mwenye masikio na asikie...mimi nshajitoa huko..sio soda wala juice ni mwaka wa pili huu!!

   Lakini naomba kujuzwa.. MziziMkavu na haya maji ya kilimanjaro sijui uhai nayo yakoje?? Ni salama kwa afya??

  17. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,470
   Rep Power : 429504379
   Likes Received
   22043
   Likes Given
   68192

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Quote By LORDVILLE View Post
   Mweeee!! Sasa mimi najiuliza hatuna kitengo cha kuangalia yote haya?? Kama zina madhara kwanini zinauzwa?? Ila si mbaya mwenye masikio na asikie...mimi nshajitoa huko..sio soda wala juice ni mwaka wa pili huu!!

   Lakini naomba kujuzwa.. MziziMkavu na haya maji ya kilimanjaro sijui uhai nayo yakoje?? Ni salama kwa afya??
   Kitu chochote kikitengenezwa na kuwekwa ndani ya chupa ya plastiki au box kinakuwa hakiko salama ndugu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  18. Pokofame's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th August 2012
   Posts : 827
   Rep Power : 18462262
   Likes Received
   347
   Likes Given
   27

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   ndicho kinanifanya niwe follower wako daima, sio kila siku CHADEMA na CCM, elimu kama hizi are more valuable, BIG UP mkuu MziziMkavu, keep it up, AND THANKS FOR NICEST CLASS
   Religion Is a Biological Father of Evil and Crimes

  19. mountain's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th July 2012
   Posts : 591
   Rep Power : 593
   Likes Received
   156
   Likes Given
   398

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   asante sana kwa taarifa hii mkuu ...ingawa washkaji wananiambia mm mgumu wa kununua juice za maboks kumbe naepuka madhara. watanzania tupige vita haya majuice masoda maaana vijana wanakunywa sana...sasa sipat picha tutakapokuwa watu wa umri mzima ,,,sizan kama tutakuwa normal

  20. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,470
   Rep Power : 429504379
   Likes Received
   22043
   Likes Given
   68192

   Thumbs up Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Quote By Sista View Post
   MziziMkavu ibarikiwe. naomba kujua faida ya juice ya ubuyu na ukwaju
   FAIDA YA UBUYU.

   UBUYU WENYEWE

   Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa

   kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini

   ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.

   Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu

   (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye

   unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa

   watu wenye matatizo ya figo.

   Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili (antioxidant) kutokana na

   kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa

   nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi,

   bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi

   usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha   UNGA WA UBUYU :


   * Hutumika kutengeneza juisi. ( Juisi ya ubuyu ina vitamnini C nyingi kuliko tunda lingine lolote duniani.


   *Husaidia kuongeza kumbukumbu.


   SABUNI YA UBUYU :


   * Huondoa mabaka, mmba, chunusi , madoadoa na mwasho wa ngozi


   * Hulainisha ngozi na kuifanya yenye mvuto daima.
   * Hutibu fangasi na huwasaidia walio haribiwa ngozi na vipodozi.
   * Huwasaidia wenye ulemavu wa ngozi.

   FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU.   Tunda la Ukwaju.
   Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

   Juisi ya Ukwaju.

   NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.

   Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets

   • andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu
   • baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni
   • uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
   • ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe
   • andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
   • weka sukari kwa kiasi unachopendelea
   • pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste
   • weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa


   FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.


   1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
   2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
   3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
   4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
   5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
   6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
   7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
   8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
   9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
   10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)


   NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!   Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name:	UBUYU1.jpg 
Views:	63 
Size:	82.5 KB 
ID:	135413  
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  21. Criss's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th March 2011
   Location : Kasungu
   Posts : 826
   Rep Power : 710
   Likes Received
   177
   Likes Given
   823

   Default Re: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

   Haya maelezo nitayaprint kisha naenda kuyasahau mezani makusudi naamini nitapata mrejesho kwenye fridge .
   There is no Success Or failure in Life , success or failure is a matter of attitude .....


  Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...