Ndugu ukiona unatumia dawa huponi. ujue unapata maambukizi mapya, kila wakati au kila siku. Fungus wanapaswa kupona ndani ya wiki 1.
Mimi nilisumbuliwa takribani miaka 5 na hao wadudu. Na nimeshamaliza hospitali zote mpka nje ya nchi. Nilichoma pesa mpaka South Afrika. Mpaka kuna kipindi niliamini watu wamenitupia uchawi. Nilijaribu kila dawa ninayoisikia na kuamini.
Ndugu yangu, fungus dawa yake ni usafi. Ukiwa msafi, fungus wanapaswa kukimbia, hata kama hutumii dawa. Maana watashindwa kuzaliana.
Kuna daktari mmoja alinipa mfano, akaniambia "huwezi kupulizia dawa ya kufukuza mbu chumbani wakati mlango na madirisha iko wazi". Ni sawa na kujaza maji kwenye ndoo iliyotoboka.
Jaribu haya yafuatayo: alafu utaniambia.
1) Hakikisha unaoga mara 2 kwa siku, au zaidi(kwa kutumia medicated soap) na maji safi, zingatia usafi wa ndoo yako ya kuogea, na usafi wa bafu pia.
2) Usirudie nguo za ndani. Fua nguo zako za ndani na maji ya moto na kuzianika juani. Usirudie taulo, na suruali pia. Maana hao wadudu watakuwa wameshatapakaa kwenye nguo zako zote hata mashuka ya kulalia, na inawezekana wameshakuwa sugu. Hakikisha nguo zote unafua mara kwa mara tena na maji ya moto.
3)Jitahidi unakauka vizuri baada ya kuoga. Jikaushe na feni ikiwezekana.
4)Epuka sehemu zenye joto. Fungus wanazaliana sana kwenye unyevu unyevu. Hasa sehemu zinatoka jasho jingi.
5)Usitumie vyakula vyenye sukari, mfano soda, juicy, nk. Vyakula hivyo vinafanya uongeze sukari nyingi mwilini. Jasho lenye kiwango kikubwa cha sukari ni chakula kikubwa cha fungus.
6) Usivae nguo za kubana. Ambazo haziruhusu hewa kupita kirahisi. Hakikisha unavaa nguo za cotton.
Follow Us Here