Re: Ugonjwa wa kisukari (diabetes mellitus).
Idadi ya milo ya kila siku
Si busara kula rundi la maakulati bora kupendelea kula milo midogo midogo
ya mara kwa mara. Njia hii inasaidia kupunguza uzito wa mtu vile vile na
kuifanya insulin kufanya kazi kwa kasi au bora zaidi.
Tahadhari na kukwepa chai au mlo wa asubuhi kwa vile unahitaji kuanza siku ukiwa na chochote tumboni. Baada ya mlo wa asubuhi unaweza kuendelea kula mara mbili zaidi kwa kutwa ikiwa umezoea kula hivyo. Lakini hakikisha kwamba unakula kiwango kidogo kidogo, tofauti na ulivyozoea.
Kula ndimba kubwa kubwa asoruka paka hazina tija kwa siha yako.
Inawezekana kuwa huna njaa baina ya nyakati za kula, lakini inafaa
utambuwe kwamba ni vyema ukila vitu vidogo vidogo vikavu kama ya ngano nzima na ule pamoja na tunda moja. Ulaji huu wa udoho udoho utakufanya usiwe na njaa kali wakati wa milo mikuu na kwa hivyo utakula kidogo zaidi.
Matunda
Matunda ni chakula bora, lakini mengi yao yana sukari nyingi, kwa hivyo ni
vizuri kula si zaidi ya mawili-matatu kwa siku ukihakikisha kupunguza
ulaji wa zabibu, embe, ndizi mbivu, matunda makavu kama tende, zabibu kavu,zeituni kwa vile matunda haya yana sukari nyingi.
Maziwa na mitindi
Maziwa yana sukari-ya-maziwa (lactose) , kwa hivyo mtu anahitajiwa asinywe zaidi ya nusu liter kwa siku, hii ina maana maziwa ya aina mbali mbali kama mtindi na yoghurt bila ya matunda.
Vidonge vya utamu haviathiri kiwango cha sukari katika damu kwa hivyo mtu anaweza kutumia vidonge hivi kwa kutayarishiya maakulati badala ya kutumia sukari ya kawaida. Vidonge hivi viko vya aina tafauti kwa mfano saccharin (sakkarin), cyclamate, acesulframe, aspartame (Nutra-sweet) n.k.
Cyclamate na acelsulframe zinaweza kuchemshiwa bila ya kuharibu ladha.
Nutra-sweet inapoteza ladha yake tamu ikiwa itachemshwa au kubekiwa kwa zaidi ya dakika chache. Sakkarin inageuka kuwa chungu ikiwa itachemshwa zaidi ya digrii 70 kwa muda mrefu.
Epuka na vitu vilvyo tiwa ladha ya utamu kwa matumizi ya sorbitol na au
fructose kwa vile vina ongeza sukari katika damu.
Inafaa mtu anywe vinyaji vilivyo punguzwa utamu au kutiwa utamu wa vidonge yaani vinyaji bila ya sukari. Hakikisha kusoma kama sharubati fulani ina sukari au haina sukari.
Epuka na vyakula vya utamu-utamu kama vile haluwa, jelebi, laddu-laddu,
peremende-pipi, asali, matunda ya kuchemsha, jamu, makeki-keki, kashata
n.k. na ujizoweshe kula vyakula visivyo vitamu tamu.
Mboga-mboga ni vyakula bora na haziongezi sukari katika damu :
mabilingani, mabamia, vitunguu, squshi, kebeji, kerot, tungule/nyanya, tango, koliflower, fiwi, kisamvu, mchicha n.k.
Njegere, kunde, mbaazi, maharage, njugu mawe, muhogo, ndizi mbichi,
majimbi, viazi vikuu ni vyakula vyenye mizizi mizizi ambavyo vinateremsha
sukari katika damu. Tahadhari na ndizu mbivu, za mkono wa tembo, boga na viazi vitamu.
Ukila jibini hakikisha kwamba haijajaa shahamu yaani iwe ya kiasi cha 18%
ambayo itakuwa na shahamu ya kiasi cha gramu 18 kwa kila gramu 100 za
jibini. Kwenye pakiti unaweza kusoma kiasi cha asili mia ya shahamu kwenye jibini.
Samaki ni wenye manufaa makuu kisiha na aina zote zinaruhusiwa
Usile mayai zaidi ya 2-3 kwa wiki.
Wasia wa Chakula bora
Punguza utumiaji wa mafuta, siagi, samli na margarini
Kula mboga mboga kwa wingi, ama za kuchemsha au mbichi
Kula vyakula vya mizizi mizizi
Kula vyakula vyenye ngano nzima na chapati za ngano nzima
Pale inapomkinika soma kwenye paketi/chupa kuhusu kuwemo au kutokuwemo sukari ndani
Maakulati/machopo chopo
Ikiwa mtu atafuata mapendekezo ya hapo juu, anaweza mara 1-2 kwa mwezi kula maakulati kama vile kwenye shughuli, maaliko, sherehe yenye vyakula vyenye mafuta/siagi na sukari kwa wingi.
Matatizo
Baadhi ya nyakati mtu anaweza kufikwa na maafa kama misiba, matatizo ya kifamilia n.k. Na kwa hivyo mtu hupendelea kujiliwaza kwa kula zaidi au
kupoteza hamu ya kula kabisa. Hali hizi zina athiri ugonjwa wa kisukari na
kwa hivyo mtu inambidi aendelee na kula kama ilivyopendekezwa ingawa mara nyengine inaweza kuwa ni vigumu.
Magonjwa mengine
Hutokea kwamba mtu anapata magonjwa mengine juu ya ugonjwa wake wa kisukari, anatakiwa aendelee na matibabu yake ya kisukari kama kawaida.
Na anategemewa apime sukari katika damu mara kwa mara zaidi kuliko kawaida kwa vile magonjwa mengine yanaweza kuifanya sukari ikapanda zaidi ingawa matibabu yanaendelea kwa kawaida. Kwa hivyo kumbuka kuwasiliana na tabibu wako pindi sukari ikipanda.
Safarini
Jambo la mwanzo kumubuka kuchukuwa dawa yako na kipima sukari chako.
Kwa msaada mkubwa wa toka kwa Dr. Y. Salim
__________________
“I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”
'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.
|