JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

  Report Post
  Results 1 to 20 of 20
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,969
   Rep Power : 429503208
   Likes Received
   18015
   Likes Given
   55396

   Thumbs up Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo, kukosa choo

   Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.

   Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana tiba. Watu wa michezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu sana katika kuipa miili yao nguvu.

   KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, ndizi ni chanzo kikubwa cha Potassium, madini ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na ufanyaji kazi mzuri wa moyo. Kwa kuwa ndizi moja ina wastani wa 467mg za madini aina ya Potasiamu na 1mg ya sodiamu (chumvi), ndizi moja tu kwa siku inaweza kukupa kinga ya maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

   Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya Potasiamu katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu na kirutubisho cha Fiber (Ufumwele), wako katika hatari ndogo ya kupatwa na kiharusi.

   Aidha, utafiti mwingine uliofanywa na taasisi moja ya masuala ya tiba ijulikanayo kama Archives of Internal Medicine, ya nchini Marekani, pia ilithibitisha kwamba ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha ufumwele (fiber) kama vile ndizi, husaidia sana kutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo. Na katika suala hili, zaidi ya watu 10,000 walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 19.

   KINGA DHIDI Y VIDONDA VYA TUMBO

   Kwa muda mrefu sana imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (stomach Ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilkibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na maziwa freshi, huzuia utokaji wa asidi tumboni inayosababisha vidonda vya tumbo.

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya suala hili, ndizi hutoa kinga na ahueni ya vidonda vya tumbo kwa njia mbili. Mosi: virutubisho vilivyomo kwenye ndizi huzipa uhai seli zenye kazi ya kutengeneza utandu ambao hutoa aina fulani ya urojo (mucus) unaotumika kama kizuizi dhidi ya asidi tumboni.

   Pili: kuna virutubisho vingine kwenye ndizi ambavyo kwa kitaalamu vinajulikana kama ‘Protease’ ambavyo husaidia kuondoa bakteria tumboni ambao wanaelezewa kuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo. Hivyo kama wewe hujaptwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

   NDIZI KAMA TIBA KWA WENYE MATATIZO YA CHOO

   Ndizi ni muhimu sana katika kulainisha na kusafisha tumbo na kumuwezesha mtu kupata choo. Mbali ya kusaidia upatikanaji wa choo kwa wenye matatizo hayo, lakini pia hutoa ahueni kwa wagonjwa wa kipindupindu. Mtu aliyepatwa na kipindupindu hupoteza kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu, hivyo kwa kula ndizi ataweza kurejesha mwilini maidni yake yaliyopotea na kuupa mwili nguvu yake.

   UIMARISHAJI WA NURU YA MACHO

   Wakati ulipokuwa mdogo, bila shaka uliwahi kuambiwa na mama kuwa mtu akila karoti, atakuwa akiona vizuri. Bila shaka hakukosea, lakini sasa ukiwa mtu mzima unaambiwa kwamba ulaji wa matunda, ikiwemo ndizi, ndiyo kinga hasa dhidi ya matatizo ya kutokuona vizuri uzeeni. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba ulaji wa matunda kwa wingi kila siku, hupunguza kwa asilimia 36 matatizo ya kutokuona vizuri kutokana na mtu kuwa na umri mkubwa.

   KINGA DHIDI YA SARATANI YA FIGO

   Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Jarida la Kimataifa la masuala ya Saratani (International Journal of Cancer) la nchini Marekani, umeonesha kwamba ulaji wa mara kwa mara wa matunda halisi, hasa ndizi mbivu, ni kinga madhubuti ya mwili. Zaidi ya wawake 50,000 wenye umri kati ya miaka 40 na 76 waliofanyiwa utafiti, ulionesha kuwa wale waliokula wastani wa milo 2.5 ya matunda na mboga kila siku, walipunguza hatari ya kupatwa na saratani ya figo kwa asilimia 40.

   Baadhi ya vitamini na madini yaliyomo kwenye ndizi ni pamoja na Vitamini B6, Vitamin C, Potassium, Dietary Fibre na Mnganese. Hivyo utaona kwamba tunda la ndizi ni muhimu kwa sababu limesheheni vitamini na madini muhimu katika mwili wa binadamu. Kuanzia leo itazame ndizi kama tunda muhimu sana katika ustawi wa afya yako na ni kinga dhidi ya maradhi unayoweza kuyaepuka kesho kwa kula tunda hili kwa wingi leo!
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  2. dubu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2011
   Posts : 2,578
   Rep Power : 903
   Likes Received
   628
   Likes Given
   143

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   sawa asante mm.
   MziziMkavu likes this.

  3. harakat's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th July 2011
   Posts : 1,842
   Rep Power : 963
   Likes Received
   399
   Likes Given
   4

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   poa kamanda
   MziziMkavu likes this.

  4. WILSON MWIJAGE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2011
   Posts : 277
   Rep Power : 595
   Likes Received
   72
   Likes Given
   0

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Ndugu,

   Shukrani Kamanda wengine tunakula bila kujua
   MziziMkavu likes this.

  5. nxon's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th July 2011
   Posts : 767
   Rep Power : 611
   Likes Received
   173
   Likes Given
   14

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   hata mimi nna vidonda vya tumbo ngoja niekee mkazo kula ndizi
   MziziMkavu likes this.

  6. Clean9

  7. Siasa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th May 2009
   Posts : 29
   Rep Power : 576
   Likes Received
   5
   Likes Given
   4

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   inabidi mtu ale ngapi kwa siku? asije akajioverdose
   MziziMkavu likes this.

  8. Martinbayport's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 8th March 2012
   Posts : 1
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Duu doctor
   MziziMkavu likes this.

  9. Shine's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th February 2011
   Posts : 11,511
   Rep Power : 2955
   Likes Received
   1291
   Likes Given
   504

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Nimeekupata vizuri kabisa mkuu ni wajibu wangu kutimiza ushauri wako na kuwashauri ndugu jamaa na marafiki kuufuatilia
   MziziMkavu likes this.

  10. mathematics's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st February 2012
   Location : MY PLACE
   Posts : 2,822
   Rep Power : 1311
   Likes Received
   762
   Likes Given
   900

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Dah, ngoja nianze kula ndizi kwa fujo... Faida zote hizooooo!!!!
   MziziMkavu likes this.

  11. Foundation's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th November 2010
   Location : MAHAMENI
   Posts : 720
   Rep Power : 707
   Likes Received
   134
   Likes Given
   256

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Mimi huwa nakula sana.Mara nyingi huwa nakula usiku kama chakula
   MziziMkavu likes this.

  12. mayenga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th September 2009
   Posts : 2,361
   Rep Power : 1027
   Likes Received
   640
   Likes Given
   863

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   ahsante mkuu.
   MziziMkavu likes this.

  13. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,969
   Rep Power : 429503208
   Likes Received
   18015
   Likes Given
   55396

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   NDIZI mbivu ni tunda linalofahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wote wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini.

   Kama ulikuwa hujui umuhimu na faida za ndizi mbivu mwilini, naomba usome makala haya na baada ya kusoma naamini utakuwa na mtizamo tofauti kuhusu tunda hili.

   KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO
   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi kuhusu tunda hili, ndizi ni chanzo kikubwa cha madini aina ya ‘Potassium’, ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na huboresha utendajikazi mzuri wa moyo. Ndizi moja tu kwa siku inaweza kukukinga na maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

   Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya ‘Potassium’ katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye ‘Potassium’ na ‘Fiber’ (kambalishe), wamejiepusha na kupatwa na kiharusi.

   KINGA DHIDI YA VIDONDA VYA TUMBO
   Kwa muda mrefu imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (Stomach ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na maziwa huzuia utokaji wa asidi tumboni inayosababisha vidonda vya tumbo.

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya suala hili, ndizi hutoa kinga na ahueni ya vidonda vya tumbo kwa njia mbili. Mosi: virutubisho vilivyomo kwenye ndizi huzipa uhai seli zenye kazi ya kutengeneza utandu ambao hutoa aina fulani ya urojo (mucus) unaotumika kama kizuizi dhidi ya asidi tumboni.

   Hivyo kama wewe hujapatwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

   TIBA KWA WENYE MATATIZO YA CHOO
   Ndizi ni muhimu sana katika kulainisha na kusafisha tumbo na kumuwezesha mtu kupata choo laini. Mbali ya kusaidia upatikanaji wa choo kwa wenye matatizo hayo, lakini pia hutoa ahueni kwa wagonjwa wa Kipindupindu. Mtu aliyepatwa na maradhi hayo hupoteza kiasi kikubwa cha madini ya ‘Potassium’, hivyo kwa kula ndizi ataweza kurejesha mwilini haraka madini yake yaliyopotea.

   UIMARISHAJI WA NURU YA MACHO
   Wakati ulipokuwa mdogo, bila shaka uliwahi kuambiwa na mama kuwa mtu akila karoti, atakuwa akiona vizuri. Bila shaka hakukosea, lakini sasa ukiwa mtu mzima unaambiwa kwamba ulaji wa matunda, ikiwemo ndizi ndiyo kinga hasa dhidi ya matatizo ya kutokuona vizuri uzeeni.

   Ndizi hujenga kwenye utumbo mwembamba uwezo mzuri wa kunyonya madini ya ‘calcium’ na virutubisho vingine na hivyo kuwezesha virutubisho kuingia mwilini na kuzunguka katika mfumo wa damu bila matatizo.

   Baadhi ya vitamini na madini yaliyomo kwenye ndizi ni pamoja na Vitamini B6, Vitamin C, ‘Potassium’, ‘Manganese’ na Fibre (kambalishe). Hivyo utaona kwamba tunda la ndizi ni muhimu kwa sababu limesheheni vitamini na madini muhimu katika mwili wa binadamu. Kuanzia leo itazame ndizi kama tunda muhimu sana katika ustawi wa afya yako. Ndizi pia hutia mwili nishati, unaposikia uchovu, kula ndizi moja na utajisikia mchangamfu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  14. georgeallen's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2011
   Location : Seattle, WA, USA
   Posts : 3,152
   Rep Power : 0
   Likes Received
   844
   Likes Given
   571

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Quote By MziziMkavu View Post

   Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo, kukosa choo

   Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.

   Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana tiba. Watu wa michezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu sana katika kuipa miili yao nguvu.

   KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, ndizi ni chanzo kikubwa cha Potassium, madini ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na ufanyaji kazi mzuri wa moyo. Kwa kuwa ndizi moja ina wastani wa 467mg za madini aina ya Potasiamu na 1mg ya sodiamu (chumvi), ndizi moja tu kwa siku inaweza kukupa kinga ya maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

   Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya Potasiamu katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu na kirutubisho cha Fiber (Ufumwele), wako katika hatari ndogo ya kupatwa na kiharusi.

   Aidha, utafiti mwingine uliofanywa na taasisi moja ya masuala ya tiba ijulikanayo kama Archives of Internal Medicine, ya nchini Marekani, pia ilithibitisha kwamba ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha ufumwele (fiber) kama vile ndizi, husaidia sana kutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo. Na katika suala hili, zaidi ya watu 10,000 walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 19.

   KINGA DHIDI Y VIDONDA VYA TUMBO

   Kwa muda mrefu sana imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (stomach Ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilkibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na maziwa freshi, huzuia utokaji wa asidi tumboni inayosababisha vidonda vya tumbo.

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya suala hili, ndizi hutoa kinga na ahueni ya vidonda vya tumbo kwa njia mbili. Mosi: virutubisho vilivyomo kwenye ndizi huzipa uhai seli zenye kazi ya kutengeneza utandu ambao hutoa aina fulani ya urojo (mucus) unaotumika kama kizuizi dhidi ya asidi tumboni.

   Pili: kuna virutubisho vingine kwenye ndizi ambavyo kwa kitaalamu vinajulikana kama ‘Protease’ ambavyo husaidia kuondoa bakteria tumboni ambao wanaelezewa kuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo. Hivyo kama wewe hujaptwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

   NDIZI KAMA TIBA KWA WENYE MATATIZO YA CHOO

   Ndizi ni muhimu sana katika kulainisha na kusafisha tumbo na kumuwezesha mtu kupata choo. Mbali ya kusaidia upatikanaji wa choo kwa wenye matatizo hayo, lakini pia hutoa ahueni kwa wagonjwa wa kipindupindu. Mtu aliyepatwa na kipindupindu hupoteza kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu, hivyo kwa kula ndizi ataweza kurejesha mwilini maidni yake yaliyopotea na kuupa mwili nguvu yake.

   UIMARISHAJI WA NURU YA MACHO

   Wakati ulipokuwa mdogo, bila shaka uliwahi kuambiwa na mama kuwa mtu akila karoti, atakuwa akiona vizuri. Bila shaka hakukosea, lakini sasa ukiwa mtu mzima unaambiwa kwamba ulaji wa matunda, ikiwemo ndizi, ndiyo kinga hasa dhidi ya matatizo ya kutokuona vizuri uzeeni. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba ulaji wa matunda kwa wingi kila siku, hupunguza kwa asilimia 36 matatizo ya kutokuona vizuri kutokana na mtu kuwa na umri mkubwa.

   KINGA DHIDI YA SARATANI YA FIGO

   Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Jarida la Kimataifa la masuala ya Saratani (International Journal of Cancer) la nchini Marekani, umeonesha kwamba ulaji wa mara kwa mara wa matunda halisi, hasa ndizi mbivu, ni kinga madhubuti ya mwili. Zaidi ya wawake 50,000 wenye umri kati ya miaka 40 na 76 waliofanyiwa utafiti, ulionesha kuwa wale waliokula wastani wa milo 2.5 ya matunda na mboga kila siku, walipunguza hatari ya kupatwa na saratani ya figo kwa asilimia 40.

   Baadhi ya vitamini na madini yaliyomo kwenye ndizi ni pamoja na Vitamini B6, Vitamin C, Potassium, Dietary Fibre na Mnganese. Hivyo utaona kwamba tunda la ndizi ni muhimu kwa sababu limesheheni vitamini na madini muhimu katika mwili wa binadamu. Kuanzia leo itazame ndizi kama tunda muhimu sana katika ustawi wa afya yako na ni kinga dhidi ya maradhi unayoweza kuyaepuka kesho kwa kula tunda hili kwa wingi leo!
   je MziziMkavu mtu mwenye kisukari anaruhusiwa kula ndizi mbivu au zilizopikwa?
   Arrogance come before the fall

  15. Eliezar Mlwafu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th January 2013
   Posts : 350
   Rep Power : 448
   Likes Received
   118
   Likes Given
   3

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Tunashukuru dk kwa Elimu yako nzuri

   Sent from my BlackBerry 9780{katefar}
   MziziMkavu likes this.

  16. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,969
   Rep Power : 429503208
   Likes Received
   18015
   Likes Given
   55396

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Quote By georgeallen View Post
   je MziziMkavu mtu mwenye kisukari anaruhusiwa kula ndizi mbivu au zilizopikwa?
   Mgonjwa wa kisukari anaruhusiwa kula ndizi zilizopikwa georgeallen
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  17. MadamG's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 1st February 2013
   Posts : 113
   Rep Power : 399
   Likes Received
   36
   Likes Given
   32

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Asante sana mkuu
   MziziMkavu likes this.

  18. Shimilimana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 12th March 2013
   Posts : 45
   Rep Power : 381
   Likes Received
   11
   Likes Given
   0

   Default

   [QUOTE=MziziMkavu;5955678][SIZE=3]NDIZI mbivu ni tunda linalofahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wote wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini.

   Kama ulikuwa hujui umuhimu na faida za ndizi mbivu mwilini, naomba usome makala haya na baada ya kusoma naamini utakuwa na mtizamo tofauti kuhusu tunda hili.

   KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO
   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi kuhusu tunda hili, ndizi ni chanzo kikubwa cha madini aina ya ‘Potassium’, ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na huboresha utendajikazi mzuri wa moyo. Ndizi moja tu kwa siku inaweza kukukinga na maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

   Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya ‘Potassium’ katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye ‘Potassium’ na ‘Fiber’ (kambalishe), wamejiepusha na kupatwa na kiharusi.

   KINGA DHIDI YA VIDONDA VYA TUMBO
   [COLOR=#4E4E54][FONT=Gill Sans]Kwa muda mrefu imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (Stomach ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na ma
   MziziMkavu likes this.

  19. Shimilimana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 12th March 2013
   Posts : 45
   Rep Power : 381
   Likes Received
   11
   Likes Given
   0

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Asante sana mkuu kwa kutusaidia kuhusu faida ya kula ndizi mbivu hasa kwenye eneo la vitamin c ambayo ndiyo mlinzi wa miili yetu, be blessed
   MziziMkavu likes this.

  20. kabanga's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 12th December 2011
   Location : Kisarawe
   Posts : 13,456
   Rep Power : 291570482
   Likes Received
   4379
   Likes Given
   574

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   elimu kubwa hii kaka mkubwa ... ubarikiwe..!!
   MziziMkavu likes this.

  21. Mhandisi Mzalendo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd August 2010
   Location : mjini
   Posts : 807
   Rep Power : 666
   Likes Received
   210
   Likes Given
   63

   Default Re: Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu

   Asante sana kwa elimu hii mimi ni mlaji mzuri wa ndizi ingawa kuna aina ya ndizi huwa zinavimbisha tumbo linakua ndindi...
   again asante sana
   MziziMkavu likes this.

  22. Kansime

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...