Nimesikia mengi kuhusiana na mti wa Mlonge lakini hii ni kali zaidi
CAPE TOWN, (IPS). Wakati tatizo linalipolikabili Bara la Afrika, watu wanaangalia uwezekano wa kupata misaada kutoka kwenye mashirika ya kimataifa kutoka nje ya bara hilo.
Lakini hali ya ukame inayoongezeka kwa kasi, miti yenye kuhimili ukame huku ikiwa na majani yenye viini lishe vingi inaweza kuwasaidia watu maskini, pia maeneo ya usalama wa chakula na utapiamlo, wao wenyewe.
Shamba lenye hekta 15 lilipandwa miti ya Mlonge au wengine huuita mti wa miujiza ambao kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera, tayari umeshaanza kuleta mabadiliko katika jimbo moja maskini zaidi la Afrika Kusini la Limpopo.
Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi ya kiasi kile kinachopatikana kwenye spinachi. kiasi cha vitamani A mara nne zaidi ya kile kinachopatikana kwenye karoti na kiasi cha protini mara mbili zaidi ya kile kinachopatikana kwenye maziwa. Ukiwa na mti wa Mlonge ni sawa na kuwa na Supermarket kwenye mti.
Mavis Mathabatha aliyewahi kuwa mwalimu kutoka Tooseng, amekuwa akifanya bidii ya kufungua mashamba ya Mlonge kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ambalo litamuwezesha kuzalisha majani ya kutosha ya Mlonge ili kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii yake.
"Nataka kuleta mabadiliko katika jimbo langu na nchi nzima kupitia mradi huu," alisema.
Mwaka 2009, alianza kuvuna na kuyakausha na kisha kuyasaga majini ya Mlonge kutoka kwenye miti michache aliyokuwa ameipabnda.
Unga huo wa Mlonge alikuwa ukiwachanganyia watoto 400 kutoka katika familia masikini waliokuwa wakipata chakula kutoka kwenye kituo maalum.
Kituo hicho kinalisha watoto wanaotoka katika familia zenye kipato kidogo ambacho kiko chini ya dola 250 kwa mwezi.
Hii inahusuisha watoto wote wa kike na kiume kutoka kwenye jamii hiyo ambayo ina tatizo la ukosefu wa ajira, umasikini na utapiamlo, wengine wana maambukizi ya UKIMWI.
"Matokeo yake yalikuwa dhahiri kwa muda mfupi sana, Afya za watoto ziliboreka kwa muda mfupi.
Anasema Elizabeth Serogole, meneja wa kituo hicho cha kulisha watoto ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na Mathabatha.
Anasema watoto wengi waliokuwa wakionesha kuwa na utapiamlo, kama vile vidonda kwenye ngozi walianza kupona mara baada ya kula mlo huo uliochanganywa na unga wa Mlonge.
Nyongeza hiyo ya Mlonge kwenye chakula chao iliwasaidia kupambana na magonjwa mengine yaliyojitokeza, pia iliwasaidia kuboresha uwezo wao wa kiakili," anasema Seregole.
"Wengi sasa wanaweza kusoma vizuri shuleni," anasema. Walichokuwa wanahitaji ni kjiko kimoja cha unga wa molonge katika chakula chao kwa siku. Dk.Samson Tesfay anayseoma Afrika Kusini kwenye chuo kikuu cha Zulu Natal idara inayohusika na masuala ya mbogamboga na matunda,alisema Mlonge ni mmea wenye kutenda maajabu kwenye lishe.
"Mlonge ni mmea wa kipekeeunaoweza kuutumia kwa faida nyingi, kama vile dawa, chakula, kuponyesha viungo mwilini na kusaidia kupambana na utapiamlo," anasema.
Source-Gazeti la Nipashe Ijumaa Februari 24, 2012
Binafsi nimeshasikia kuwa Mlonge unatibu magonjwa 300, bila ya kusahau kansa,maralia,vidonda vya tumbo,kuondoa sumu mwilini na hata kuongeza nguvu za kiume. Maderava wengi wa safari ndefu hutumia Mlonge kuondoa uchovu. Mlonge watu wa kule Tanga wanatumia kama mti wa kujengea fensi, Uzaramoni umepandwa karibu kabisa na vyoo vyao, Dodoma na Morogoro umejaaa tele. Dar mbegu zake zinauzwa kwa Shilingi 1000 kwa pakti.
Mbegu hizo zina dozi ya 3x3x3 na ukizila kwa wingi huweza kukufanya kuhalisha na kutoa uchafu mwilini. Tafakari ndugu yangu dawa tunazo tunatimia madawa yenye sumu yaliyotayalishwa na wazungu.... Tafakari.

Reply With Quote



SIYO WOTE WANAOTANGATANGA WAMEPOTEA

Follow Us Here