Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 52
    1. #1
      Shapu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2008
      Location : Citizen of the World
      Posts : 1,586
      Rep Power : 897
      Likes Received
      167
      Likes Given
      302

      Default Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

      Nimekuwa nikipata maelezo meengi kuhusiana na hizi bidhaa za GNLD na Forever living Products (FLP). Hasa za forever, jamaa wako mahiri sana katika kuelezea faida utakazo zipata pindi utakapo jiunga na wanayoiita network marketing. Huwa wanafocus zaidi kwenye faida mtu atakayoipata once anajiunga na business.

      Hawaongei sana kuhusu bidhaa zenyewe. Mimi kidogo ni mshamba kwenye hizo bidhaa/suppliments. Napenda kurusha mjadala huu niweze kupata mawazo yakinifu hasa katika utumiaji wa hizo bidha, pia biashara yenyewe kama kweli inalipa na mwisho nataka kujua kama kuna ukweli watu wana oanisha this business na ushetani.

      Swali, kuna haja sana sisi watu wa kijijini kutumia hizi bidha wakati tunazo fresh mboga, matunda etc ambazo zingeweza kutusaidia tu bila ya hizi bidhaa?

      Wanaongelea Alo Vera! What is the big deal na huo mmea? Mbona tunao hapa lakini sijawahi kuona mtu hata akisema autumie kama mboga?

      Au ni kiini macho cha wenzetu walioendelea kutukandamiza kiuchumi kama kawaida wanatudanganya eti zitatusaidia kuondoa magonjwa etc etc?

      Wakuu naomba niwakilishe ili nipate maoni toka kwenu!
      Pasco and nyumba kubwa like this.
      "WHEN YOU REFUSE TO GIVE UP COMPETELY, THATS WHEN GOOD THINGS TEND TO HAPPEN! Never give up!" Shapu

    2. Reply With Quote

    3. MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Mimi baba yangu yupo hapa Dar na an miaka 85 hatumii GNLD wala nini....piga zoezi kula matunda na vyakula fresh tu ndugu yangu!

    Sina uzoefu na GNLD ila naona kama wako kibiashara zaidi
    nyumba kubwa likes this.
    Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

  • #3
    Pasco's Avatar
    JF Premium Member Array
    Join Date : 22nd September 2008
    Posts : 9,839
    Rep Power : 7368
    Likes Received
    6154
    Likes Given
    22277

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Suplements ni virutubisho ziada. Sio siri kama unapata mlo kamili, unajitosheleza kabisa hivyo huhitaji hivyo virutubisho ziada. Ili kupata mlo kamili, ni kupota chakula chenye viini lishe vinavyohitajika kwa ajili ya aina ya mwili wako na shughuli unaifanya na mwili huo.
    Mwili ukishafyonza viini lishe vya kutosha, unaweza kufyonza na ziada kidogo halafu kila vilivyosalia vinageuzwa makapi na kutolewa nje kwa njia kuu 4 za kawaida ambazo ni kutoa hewa,jasho na haja K na haja N.
    Chakula bora sio lazima kiwe ni chakula kingi wala huna haja ya kushiba kuvimbisha tumbo kwani sehemu ya mahitaji halisi ni ndogo tuu na nyingine yote ni ziada na makapi.
    Kila mtu ana mwili wa aina yake wenye mahitaji na viango vyake vya virutubisho. Kama una mwili mkubwa mahitaji ni makubwa kuliko mwili mdogo. Kuna watu wana miili ya kunenepa mahitaji yao ni tofauti na vimbau mbau, siku hizi kwa madada zetu vimbambau ni dili. Unene au wembamba sio viwango vya afya, kuna wanene wenye afya mbaya mpaka unene ugonjwa. Na kuna wemba ni fiti kama chuma cha nondo. Mahitaji ya virutubisho pia vitategemeana na shughuli zako. Kama ni mbeba zege/box sio sawa na washika kamu. Nk.

    Baadhi ya hivi virutubisho vya GNLD na Forever ni kama mbolea. Mwili ukipata virutubisho hivi huwa na afya bora, utapendeza, utang'aa na kuwaka. Kwa kifupi utaelezewa kuwa unakula kuku kwa mrija. Walio na miili isiyo na shukrani, utaambiwa una sura ya njaa njaa tuu.

    Kuku wa kizungu ndio wenye kuhitaji hivyo virutubisho zaidi. Kuku wa kienyeji hahitaji virutubisho na bado ana afya njema.

    Kama kawaida ya mmea uliozoea mbolea ukikosa mbolea unasinyaa na kudorora na ndivyo yatawakuta hawa watumiaji wa haya madawa. Lazima uyatumie siku zako zote za maisha yako.
    Ushetani wa matumizi yake ni utumwa wa kuchangamkia pesa. Hata ukipenda sana movies, unakuwa mtumwa wa movies ama wapenda game wanajikuta wanaabudu gemu kuliko chochote, Mungu anawekwa kando. Kitu chochote kinachomuweka Mungu kando ni kazi ya shetani.
    Visenti likes this.
    style="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="https://www.jamiiforums.com/clear.gif" alt="Reply With Quote" /> Reply With Quote

  • #4
    Mama's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 24th March 2008
    Posts : 2,916
    Rep Power : 41157
    Likes Received
    13
    Likes Given
    0

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Hizi supplements ni nzuri kwa wanaohitaji kama vile wagonjwa, kina mama wajawazito na wanyonyeshao na pia wazee. Zitumiwe pale inapolazimu tu.

    Kumbuka kila kitu kikizidi mwilini kila madhara. Na hizi supplements mara nyingi ni vitamins na essential metals ambazo huwa hazina mahitaji makubwa sana kwa mtu wa mwenye afya. Zinaweza kupatikana kwa lishe tu isipokuwa kwa makundi yaliyotajwa hapo juu.

    Epuka kuwapa watoto.
    Visenti and nyumba kubwa like this.

    Reply With Quote

  • #5
    Mwanjelwa's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 29th July 2007
    Location : Chenorbly
    Posts : 677
    Rep Power : 739
    Likes Received
    28
    Likes Given
    26

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    [QUOTE=Pasco;343702]........ Kama ni mbeba zege/box sio sawa na washika kamu. Nk.
    Wakina nani hawa?
    Pasco likes this.

  • RukaaJuu Final

  • #6
    Nyikanavome's Avatar
    JF Gold Member Array
    Join Date : 3rd March 2008
    Posts : 287
    Rep Power : 630
    Likes Received
    24
    Likes Given
    27

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Pengine inaweza kuwa unfair kuongelea bidhaa za makampuni hayo zote kwa ujumla na kusema ni hatari; nafahamu makampuni hayo yana bidhaa mbalimbali za kula ambazo nyingi zina supply micronutrients mwilini and nyingine wanaclaim kuwa zina therapeutic effect kwa magonjwa mbalimbali. Pia wana bidhaa ambazo sio za kula. Kinachofanya uhatari uwepo ni jinzi wavyo zisambaza bidhaa zao na kuwashawishi watu wazitumie kwa vishawishi vya kupata utajiri na afya bila kuwapa ushauri wa kutosha wa kitaalamu wa kwa wateja wao.
    Ninavyo fahamu mie, ulaji wetu wa kitanzania unaweza usiweze kutupatia wengi wetu kiwango cha kutosha cha vitamini na madini nakupelekea kitu kinachoitwa hidden hunger (njaa iliyojificha). Katika hali ya kawada mtu anaweza kuishi akiwa na kiwango cha chini cha vitamini na madini mbali mbali bila kujitambua. Unaweza kutambua kuwa hupati micronutrients za kutosha kwa kupitia ulaji wako a kilasiku kama unakidhi haja na pia unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa chakula na lishe aliyeko karibu nawe.

    Mimi
    Haika and Kiruke cha Ibwe like this.

  • #7
    Pasco's Avatar
    JF Premium Member Array
    Join Date : 22nd September 2008
    Posts : 9,839
    Rep Power : 7368
    Likes Received
    6154
    Likes Given
    22277

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    [QUOTE=mwanjelwa;343784]
    Quote By Pasco
    ........ Kama ni mbeba zege/box sio sawa na washika kamu. Nk.
    Wakina nani hawa?
    Wabeba zege ama wabeba box ni watumiaji wa more mascular job, manual laboures ambao wanatumia nguvu nyingi na akili kidogo wanamahitaji yao ya viini lishe tofauti na washika kalamu, wafanyakazi maofisini, watumia compyuta ambao wanatumia akili zaidi na nguvu kidogo nao wanamahitaji yao.

  • #8
    MwalimuZawadi's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 1st September 2007
    Posts : 623
    Rep Power : 723
    Likes Received
    50
    Likes Given
    3

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Wajinga ndio wali-wao...werevu pilau-lao!
    manasa likes this.
    Sent from my Nokia rinGo using JamiiForums

  • #9
    Shapu's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 17th January 2008
    Location : Citizen of the World
    Posts : 1,586
    Rep Power : 897
    Likes Received
    167
    Likes Given
    302

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Quote By MwalimuZawadi
    Wajinga ndio wali-wao...werevu pilau-lao!
    Naomba ufafanuzi hapo.
    "WHEN YOU REFUSE TO GIVE UP COMPETELY, THATS WHEN GOOD THINGS TEND TO HAPPEN! Never give up!" Shapu

  • #10
    Next Level's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 17th November 2008
    Location : Pwani
    Posts : 3,151
    Rep Power : 1171
    Likes Received
    76
    Likes Given
    42

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Quote By Shapu
    Nimekuwa nikipata maelezo meengi kuhusiana na hizi bidhaa za GNLD na Forever living Products (FLP). Hasa za forever, jamaa wako mahiri sana katika kuelezea faida utakazo zipata pindi utakapo jiunga na wanayoiita network marketing. Huwa wanafocus zaidi kwenye faida mtu atakayoipata once anajiunga na business.
    Si mtumiaji wa bidhaa hizo japo nimeshazisikia sana, na hata kuletewa DVD inayoelezea kwa undani products hizo....two me ukiacha kuwa products hizo zina supplements....GNLD na FLP hazinatofauti na DECI or any Pyramid Scheme...so be careful!

    Wanaongelea Alo Vera! What is the big deal na huo mmea? Mbona tunao hapa lakini sijawahi kuona mtu hata akisema autumie kama mboga?
    Mimi babu yangu (kafariki 1999..RIP akiwa na miaka 120), alikuwa mganga wa kienyeji, mpaka anakufa ktk maisha yake hakuwahi kutumia hata panadol au modern medicine yoyote ile...mojawapo ya mmea aliokuwa anatumia kutengeneza dawa zake ni huu wa Alo vera aka Litembatemba.....so 2 me hao FLP hawajaleta kitu kipya hapa!

    walioendelea kutukandamiza kiuchumi
    Hili nakubaliana na wewe...soma hapo juu zaidi!
    Visenti likes this.
    “When the missionaries came to Africa they had the Bible and we had the land. They said ''Let us pray'' we closed our eyes. When we opened them we had the Bible and they had the land.
    - Rev.Bishop Desmond Tutu.

  • #11
    Makonyagi's Avatar
    Member Array
    Join Date : 16th April 2009
    Posts : 40
    Rep Power : 523
    Likes Received
    1
    Likes Given
    0

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Wizara ya Afya hawajatoa tamko
    Mamlaka ya dawa na vyakula wanahangaika na metakeflin wanasahau hii piramidi scheme kwenye sekta ya afya.
    Nashangaa ktk maelezo yoooote ya hizi tianshi sijui forevago and whateva hakuna side effects.
    Hic!
    Kula kilaji pata afya
    Msingida likes this.
    Aliyekamatwa na Ng'ombe ndiye mwizi wa Konyagi ...Hic!

  • #12
    Shapu's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 17th January 2008
    Location : Citizen of the World
    Posts : 1,586
    Rep Power : 897
    Likes Received
    167
    Likes Given
    302

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Quote By Next Level
    ....GNLD na FLP hazinatofauti na DECI or any Pyramid Scheme...so be careful!
    Hapo Next level umenena... I smell something like that, kabisa kabisaaaaa. Thaks
    "WHEN YOU REFUSE TO GIVE UP COMPETELY, THATS WHEN GOOD THINGS TEND TO HAPPEN! Never give up!" Shapu

  • #13
    Makonyagi's Avatar
    Member Array
    Join Date : 16th April 2009
    Posts : 40
    Rep Power : 523
    Likes Received
    1
    Likes Given
    0

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Utakuta mpaka maprofesa wamo humo.
    na wachungaji wakisindikizwa na maaskofu wanawahimiza waumini kuingia ktk hizi scheme za madawa ambayo hayajaruhusiwa
    Aliyekamatwa na Ng'ombe ndiye mwizi wa Konyagi ...Hic!

  • #14
    LazyDog's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 10th April 2008
    Posts : 2,186
    Rep Power : 21022
    Likes Received
    16
    Likes Given
    33

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Quote By Makonyagi
    Wizara ya Afya hawajatoa tamko
    Mamlaka ya dawa na vyakula wanahangaika na metakeflin wanasahau hii piramidi scheme kwenye sekta ya afya.
    Nashangaa ktk maelezo yoooote ya hizi tianshi sijui forevago and whateva hakuna side effects.
    Hic!
    Kula kilaji pata afya



    Mamlaka ya chakula na dawa ungetaka wafanye nini?
    Tizama hii orodha,
    Orodha ya vipodozi vinavyotambuliwa na mamlaka ya chakula na dawa


    Kuna pyramid schemes za aina nyingi, and not all are illegal. Some are illegal only in some countries.
    A person who won't read has no advantage over one who can't read. -Mark Twain

  • #15
    Mundu's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 26th September 2008
    Posts : 1,680
    Rep Power : 879
    Likes Received
    228
    Likes Given
    22

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Nilipoangalia title ya huu mjadala niliogopa na kusema kulikoni tena kwa taasisi hizi mbili. Anyway yaelekea wote waliojadili hapo juu hawana uelewa wa kutosha wa bidhaa hizi na network marketing business.

    Kwa uchache nawaomba mtafute kitabu kiitwacho '"Business school, for people who like helping other people" cha Robert Kiyosaki anayeelezea network marketing business kwa urefu na pia ame ireccomend kwa watu wote ambao wanapenda kuboresha maisha yao na ya jamaa zao na kuacha utegemezi wa viajira kama vya GTV. Robert pia ni mtunzi wa kitabu maarufu cha 'Rich Dad, Poor dad"

    Mwenye kuweza kupata link ya hicho kitabu na aiweke hapa. Lakini tatizo liko palepale je, MTASOMA?
    Kiruke cha Ibwe and busy05m like this.

  • #16
    tbahemuka's Avatar
    Junior Member Array
    Join Date : 28th January 2010
    Posts : 1
    Rep Power : 0
    Likes Received
    1
    Likes Given
    0

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Ninakubaliana na mchangiaji asilimia mia. Kwa ujumla kuna kampuni zingine zimeiga mfumo huu wa biashara na kuifananisha na "pyramid". Mtoa hoja ninampogeza sana kwa kutoa hisia zake na kutaka kusaidiwa. Kuna waandishi wengi wamekuwa wakieleza biashara hii na namna inavyoweza kumsaidia mtu wa kawaida kumfikisha mahali ambapo atafurahia maisha kwa kuwa na fedha na muda wa kutosha katika maisha yake. Kama utakuwa mwajiriwa kwa kipindi cha miaka 10, mafanikio utakayoyapata ndani ya miaka hiyo, waweza kuyapata ndani ya mwaka mmoja katika biashara hii kama ukimaanisha hasa na kwa kanuni zilizowekwa na kampuni. Hapa kuna bidhaa au huduma inayofanywa kwa kuwatumia watu moja kwa moja - "Direct Sales". Hebu bofya kwenye website hii, utapata jibu la swali lako kutoka kwa mtu ambaye amefanya biashara hii zaidi ya miaka 15.
    http://www.networkmarketingtimes.com/blog/why-i-believe-in-mlm/#ixzz0MFc33h5f
    busy05m likes this.

  • REX
    #17
    REX's Avatar
    Senior Member Array
    Join Date : 24th March 2012
    Location : KCMC-MOSHI
    Posts : 182
    Rep Power : 397
    Likes Received
    24
    Likes Given
    2

    Default

    Baada ya kusoma kichwa cha habari nimeogopa sana na kujiuliza kulikon? Kwa wasiofaham TFDA wamezipisha bidhaa za forever baada ya tafiti zao kukamilika na shirika la sayans ya aloe vera la dunia limethibitisha uhalari wa bidhaa hizo kwa matumiz ya binadam.ni bidhaa zisizo na matatizo hao wanaobisha na kulaan they hav a negativ attitude and its more likely they are career critics wao muda wote wanaangalia ubaya tu by the way marketing plan yao siyo pyramidal kama ilivoripotiwa ni multilevel marketing (mlm) and this is the compasation schemes na pia hata ktk ulipaji kod tazania forever kwa awards za TRA imekuwa ya pil baada tu ya miaka mitano,for real its a nyc opportunity for information conduct me 0752720276
    len and gorretti54 like this.

  • #18
    manasa's Avatar
    Member Array
    Join Date : 2nd April 2012
    Location : DUNIANI
    Posts : 88
    Rep Power : 377
    Likes Received
    6
    Likes Given
    31

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    4 sure wajinga ndo waliwao

  • #19
    bebiwilli's Avatar
    Member Array
    Join Date : 4th March 2011
    Posts : 69
    Rep Power : 429
    Likes Received
    15
    Likes Given
    2

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Sina imani na hizo dawa,nilishawahi kumnunulia mdogo wangu dawa ya meno ya forever kwa ajili ya shule,alianza kuumwa na ganzi ya meno 2lipompeleka hosp doct alimwambia aache kuitumia na tatizo likaisha.ingiwa cjajua kwa hizo dawa zingine

  • #20
    Njowepo's Avatar
    JF Gold Member Array
    Join Date : 26th February 2008
    Location : Santiago
    Posts : 7,624
    Rep Power : 22060
    Likes Received
    1002
    Likes Given
    793

    Default Re: Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

    Hayo mambo ya ulaya Africa itachukua mda kuyaaply ktk level ya Taifa.
    Wee dawa ya mswaki elfu kumi
    Kwa watu wa mjini na wenye ela ya ziada mnaweza zichangamkia.
    Sisi tuanaoshindia mlenda na ugali unakazia na futa la alizeti hazitufai as vitu vyote apo vimetoka shambani
    WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

  • Page 1 of 3 123 LastLast

    Similar Topics

    1. Kwa wanaoifahamu kampuni ya'GNLD'
      By Babu mchumi in forum Business & Economic Forum
      Replies: 9
      Last Post: 5th December 2012, 15:30
    2. Forever Living and GNLD Products Business
      By Kaniki1974 in forum Business & Economic Forum
      Replies: 72
      Last Post: 28th April 2012, 17:07
    3. Living my dream vs Living in dreams
      By Mlachake in forum JF Chit-Chat
      Replies: 2
      Last Post: 24th August 2011, 10:41
    4. Utumiaji wa mpira
      By Kimbweka in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 17
      Last Post: 18th June 2010, 12:13

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...