JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

  Report Post
  Page 1 of 3 123 LastLast
  Results 1 to 20 of 43
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Thumbs up Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

   Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

   KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

   TUFAHA, TANGO NA FIGILI
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

   NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
   TANGO CHUNGU,

   Click image for larger version. 

Name:	ImportanceofFruitsInDiet1.jpg 
Views:	1038 
Size:	119.2 KB 
ID:	40769


   TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

   CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

   NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

   TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI’
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.

   PEASI NA NDIZI

   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

   KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
   Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

   MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
   Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

   PAPAI, NANASI NA MAZIWA
   Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

   Click image for larger version. 

Name:	fruits22.jpg 
Views:	610 
Size:	34.8 KB 
ID:	40770


   NDIZI, NANASI NA MAZIWA

   Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

   Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya’.

   Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')


  2. Mtalingolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th August 2011
   Location : Mbeya
   Posts : 2,168
   Rep Power : 1152
   Likes Received
   383
   Likes Given
   130

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Kilicho baki ni utekelezaji tu kwa 2naopenda afya zetu.

  3. #3
   Evarm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2010
   Location : totoroni
   Posts : 1,263
   Rep Power : 917
   Likes Received
   380
   Likes Given
   187

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Asante sana mkuu, ngoja mimi nikatengeneze sasa hv.
   Everything in your life is a reflection of a choice you have made. If you want a different result, make a different choice.

  4. Alexism's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th August 2011
   Location : Iringa Municipal TZ
   Posts : 1,123
   Rep Power : 752
   Likes Received
   162
   Likes Given
   18

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Mkuu nipenda sana juisi mpaka basi lakini ngozi yangu hasa usoni ninapata chunusi saanaa why?

  5. SILENT ACtOR's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th April 2011
   Location : KANDA MAALUM!
   Posts : 551
   Rep Power : 652
   Likes Received
   115
   Likes Given
   142

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Lol, sasa nitaanza kutumia matunda kwa staili hii, aksante!
   SUCCESS MEANS; DOING THE BEST YOU CAN WITH WHAT YOU HAVE.


  6. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Quote By Alexism View Post
   Mkuu nipenda sana juisi mpaka basi lakini ngozi yangu hasa usoni ninapata chunusi saanaa why?
   Jaribu kutumia dawa hii ya Chunusi:
   Chukua unga wa habbasouda kwa kiingereza unaitwa (Nigella sativa seed)ukande katika mafuta ya ufuta (simsim) pamoja na kijiko kimoja cha unga wa ngano, jipake usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu osha kwa maji yenye uvuguvugu na sabuni. Endelea kufanya hivo kwa muda wa wiki moja. Na uwe unakunywa mafuta ya habbasouda(Nigella sativa oil) ndani ya maji ya Uvuguvugu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  7. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Thumbs up Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Juisi ni kinywaji bora, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali.


   Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.


   Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini:


   KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO
   Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.


   EPO+TANGO+FIGILI
   Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.


   NYANYA+KAROTI+EPO
   Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.


   CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO
   Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.


   NANASI+EPO+TIKITI MAJI
   Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.


   KAROTI+EPO+PEASI+EMBE
   Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.   PAPAI+NANASI+MAZIWA
   Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).


   NDIZI+NANASI+MAZIWA
   Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.


   Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumiwa kama ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali. Ili uone faida za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  8. #8
   ram's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2007
   Posts : 5,288
   Rep Power : 4566961
   Likes Received
   2344
   Likes Given
   1796

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   This is great! Tutajitahidi kutengeneza hizo juice, thanks mzizimkavu
   ''1 Samweli 7:12 - Eben-ezeri - Hata sasa BWANA ametusaidia''

  9. #9
   ram's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2007
   Posts : 5,288
   Rep Power : 4566961
   Likes Received
   2344
   Likes Given
   1796

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   This is great! Tutajitahidi kutengeneza hizo juice, thanks mzizimkavu
   ''1 Samweli 7:12 - Eben-ezeri - Hata sasa BWANA ametusaidia''

  10. tembeleh2's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th July 2010
   Posts : 765
   Rep Power : 732
   Likes Received
   157
   Likes Given
   13

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Ni somo zuri lakini kwa wasiojua kusoma wakiamua kutumia PICHA hizi wameumia, maana yake vitu vingine watakuwa hawajawahi hata kuviona. Hivi ulikosa picha za hivyo ulivyoviandika (picha kubwa inayoonekana vizuri)????? yaani vitu kama tangawizi, chungwa, karoti,papai, na mengineyo.

  11. CAMARADERIE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2011
   Location : 1 Luthuli Street
   Posts : 4,314
   Rep Power : 2881
   Likes Received
   1706
   Likes Given
   1169

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Hilo TUFAHA ndio tatizo..........halipatikani kwa wingi na ni ghali sana

   Tanganyika
  12. Katavi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st August 2009
   Location : Lyamba Lya Mfipa
   Posts : 31,863
   Rep Power : 271424177
   Likes Received
   5828
   Likes Given
   3414

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Asante sana mkuu, lakini vipi zile juisi zinazotengenezwa viwandani hazifai??

  13. Bonge's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th August 2007
   Posts : 329
   Rep Power : 796
   Likes Received
   84
   Likes Given
   9

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   TUFAHA ni tunda gani???

  14. #14
   Rubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2009
   Posts : 1,603
   Rep Power : 941
   Likes Received
   246
   Likes Given
   197

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Quote By Bonge View Post
   TUFAHA ni tunda gani???
   kusoma inaelekea ni shida kwako (samahani) rudi kwenye topiki mwenyewe kaishakupa maana.
   Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

  15. mshihiri's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 15th July 2011
   Location : zanzibar
   Posts : 119
   Rep Power : 551
   Likes Received
   30
   Likes Given
   195

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   safi sana

  16. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Quote By tembeleh2 View Post
   Ni somo zuri lakini kwa wasiojua kusoma wakiamua kutumia PICHA hizi wameumia, maana yake vitu vingine watakuwa hawajawahi hata kuviona. Hivi ulikosa picha za hivyo ulivyoviandika (picha kubwa inayoonekana vizuri)????? yaani vitu kama tangawizi, chungwa, karoti,papai, na mengineyo.
   Watu humu ndani mkuu hawafuati picha wanachofuata maelezo yako hebu na wewe toa hizo picha na utoe maelezo yake Watu wapate kukufuata.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  17. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Thumbs up Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Quote By Bonge View Post
   TUFAHA ni tunda gani???
   Tufaha ni jina la kiarabu kwa kiingereza hili tunda linaitwa Apple. Angalia hii picha


   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  18. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,466
   Rep Power : 429504378
   Likes Received
   22039
   Likes Given
   68192

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Quote By Katavi View Post
   Asante sana mkuu, lakini vipi zile juisi zinazotengenezwa viwandani hazifai??
   Hazifai tengeneza Juice yako mwenyewe tumia matunda yaliyo fresh na mashine ya Blenda Mkuu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  19. Mamzalendo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th December 2010
   Location : KASKAZINI
   Posts : 1,674
   Rep Power : 16537
   Likes Received
   535
   Likes Given
   387

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Ahsante sana ndugu,yaani familia yako ina raha

  20. kipusy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th May 2010
   Posts : 362
   Rep Power : 662
   Likes Received
   63
   Likes Given
   31

   Default Re: Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

   Safi sana MziziMkavu big up.....
   Problems are simply part of the curriculum that appear and fade away like algebra class but the lessons you learn will last a lifetime


  Page 1 of 3 123 LastLast

  Similar Topics

  1. Zijue faida za juisi za matunda mwilini
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 24
   Last Post: 14th March 2015, 21:39
  2. Faida ya vyakula na matunda tunayokula kila siku
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 12
   Last Post: 24th May 2012, 09:38
  3. Faida ya Mwanga wa jua katika mwili wa binadamu
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 0
   Last Post: 19th December 2011, 01:54
  4. Replies: 21
   Last Post: 6th December 2011, 06:01
  5. Mwili wa Binadamu unavyo fanya kazi
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 1
   Last Post: 17th October 2011, 07:10

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...