Re: Baba HIV+, Mama HIV+: Je, Mtoto anaweza kuzaliwa salama?
Darwin, ni kweli kinachoungana ni ile mbegu yenyewe sperm na ovum, ambazo hazina virusi- kwa hiyo kitoto (ki-zygote) kinachotokea kiko free of virus. Maambukizi yanaweza kutokea kuanzia wakati wa ujauzito (sio kama mchangiaji mmoja aliyesema haiwezekani kuambukizwa kwa sababu damu hazigusani)- kuna conditions kibao ambazo zinaharibu intergrity ya placenta kwa hiyo vijidudu vingi, HIV, malaria, n.k vinaweza kuingia upande wa mtoto, ingawa ni kweli maambukizi mengi yanatokea wakati wa kujifungua.
Kuna njia nyingi sasa za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto; sasa hivi 'nji' zilizoendelea ni kama hawana tena tatizo hilo lakini kwetu TZ bado tunajikongoja.
Tutafika, taratibu!
__________________
The more choices you have, the more unhappy you become
|