JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

  Report Post
  Page 1 of 7 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 135
  1. GAZETI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Location : ILALA
   Posts : 2,633
   Rep Power : 1636
   Likes Received
   1472
   Likes Given
   1743

   Default Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Habarini wanajukwaa, kwa wale wenzangu ambao kidogo mmegusa Biology Huwa nikila parachichi hususani ninaposhushia na ubwabwa, nahisi hali ya msisimko wa mwili kuongezeka.

   Nimefanyia majaribio kama mara tatu hivi Nimegundua nikila parachichi na wali kwa pamoja msisimko unakuwa mkubwa ajabu.

   Naomba Darasa lenu parachichi linaongeza nguvu za kiume?

   Quote By MziziMkavu View Post
   Attachment 243278

   FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
   Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

   TINDIKALI
   Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.

   Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

   VITAMINI “E” NA B6
   Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

   Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

   FAIDA ZA PARACHICHI
   Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

   Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

   Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.

   HEDHI
   Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

   Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

   Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

   Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

   Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

   Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
   Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.

   Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.
   Quote By MziziMkavu View Post
   MSIMU wa matunda ya Parachichi umeshaingia. Kama yalivyo matunda yote kwa ujumla kuwa yana faida sana katika mwili wa binadamu, vivyo hivyo na Parachichi. Tunda hili lina maajabu makubwa katika kupambana na maradhi hatari ya moyo na sataratani ya matiti kutokana na virutubisho ilivyonavyo.

   Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya tunda hili, awali ya yote tunda hili lina kirutubisho
   aina ya Aloic Acid ambayo ni aina fulani ya mafuta mazuri yanayosaidia kushusha kolestrol mwilini. Katika utafiti mmoja waliofanyiwa watu kadhaa waliokuwa na matatizo ya kolestro mwilini, baada ya

   kutumia maparachichi kwa muda wa siku saba, walionesha mabadiliko mazuri katika afya zao kwa kupungua kiwango cha kolestro mbaya mwilini.

   Aidha, parachichi lina kiwango kikubwa sana cha madini aina ya potasium ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha mzunguruko wa damu mwilini.

   Inaelezwa kwamba ulaji wa kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu, hutoa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa yatokanayo na mzunguruko mbaya wa damu mwilini, kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kiharusi.


   Mbali ya madini hayo, parachichi lina virutubisho vingine kama vile
   Folate (Folic acid) ambacho ni muhimu sana kwa afya na ustawi wa moyo, kwa maana hiyo watu ambao wanakula sana vyakula kama parachichi lenye kirutubisho hicho, watukuwa salama dhidi ya magonjwa ya moyo au kiharusi kwa asilini 55.

   Kirutubisho kingine kinachopatikana kwa wingi kwenye parachichi ni
   Fatty Acids, ikiwemo Oleic Acid. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, imedhihirika kwamba virutubisho hivyo ni kinga tosha dhidi ya Saratani ya matiti. Kwa maana nyingine, wanawake wanaokula kwa wingi

   Maparachichi, wanaipa miili yao kinga dhidi yaSaratani hiyo ambayo hivi sasa imekuwa tishio miongoni mwa wanawake nchini.
   Parachichi linaweza kuliwa kama mtu atakavyopenda, wapo watu wanaopenda kula bila kuchanganya na kitu kingine, lakini pia parachichi linaweza kuliwa kwa kupaka kwenye mkate badala ya Blue Band. Halikadhalika parachichi linaweza kuliwa kwa kuchanganya na nyanya, vitunguu, ndimu na chumvi kidogo kama kachumbari ya kipekee.

   VIRUTUBISHO VYA PARACHICHI


   Kwa ujumla, parachichi ni chanzo kizuri cha
   Vitamini K, Vitamini B6 na Vitamini C.
   Aidha, tunda hili lina kiwango kizuri cha virutubisho aina ya Folate, kopa na ufumwele (Fiber). Fiber ni muhimu katika kuwezesha mtu kupata choo

   laini na bila matatizo. Bila kusahau kwamba tunda hili ni chanzo kizuri pia cha madini ya Potasiamu: ina kiwango kikubwa kuliko hata ndizi.

   Ingawa parachichi ni tunda, lakini lina kiwango kikubwa cha mafuta (fats) ambayo yanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 71 – 88, kiwango ambacho ni cha juu kwa asilimia 20 ukilinganisha na matunda mengine. Kwa wastani, parachichi moja lina gramu 30 za mafuta, lakini kati ya hizo, gramu 20 ni za

   mafuta mazuri kiafya
   (Monounsaturated fats na Aloic Acid) ambayo husaidia kujenga afya bora mwilini.
   Utafiti zaidi kuhusu tunda hili unamalizia kwa kusema kwamba parachichi lina takribani aina 20 za Vitamin, madini na virutubisho muhimu

   (Phytonutriens) ambavyo hutuo kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mengi hatari. Baadhi ya Vitamini zilizomo na asilimia zake kwenye mabano ni pamoja na Vitamin E (4%), Vitamin C (4%), Folate (6%), Fiber (4%), Iron (2%) na Potasium (4%).

   Kwa ujumla tunda la Parachichi lina faida nyingi kiafya na tunatakiwa tuyale kwa wingi, hasa ukizingatia huu ndiyo msimu wake. ni jambo la kushangaza sana kuona kwamba watu wengine msimu wa maparachichi unaingia hadi unakwisha, mtu hajala hata moja.

   ''KUMBUKA KINGA NI BORA KULIKO TIBA''! (Prevention is Better Than Cure)
   Quote By ngoshwe View Post
   Health Benefits of Avocado

   Avocado fruits are getting very popular anywhere in the world. Throughout the year, you can find avocado in your nearby supermarkets. Avocado is sometimes called “avocado pear” or “alligator pear”, and “Aguacate Palta” in Spanish.

   The world, especially in developing countries, is trying to adapt avocado as one of substitutes to cope for the shortage of nutritious food production.
   We believe that avocados have originated in Mexico and Central America. However, today, avocados are being planted and harvested in countries such as Indonesia, Philippines, Thailand, Vietnam, USA, Sri Lanka, Brazil, India, China, Japan, Peru, Uruguay, Argentina, Bolivia, Chile, Ethiopia, Spain, Palestine, South Africa, Australia, New Zealand, Malaysia, and Hawaii. Oh, yes, you can plant it even in your backyard garden and it is adaptable as long as the climate does not go below 5°C during winter season.

   In fact, I myself planted four avocado trees 25 years ago, and just a year ago, I added another two in my backyard. One tree bears about 200 pieces of fruit.

   Avocado is one of the most recommended fruits as well as a food for bodybuilding and medicine for cholesterol-related heart diseases.

   Also, did you know that avocado or an avocado extract is good for prevention or treatment of “breast cancer” as well as “prostate cancer”? Some information states that a toxin found in avocado can kill cancer cell. However, the toxin mentioned here is not identified completely. Scientists believe that the toxin has a great effect on the myocardium (heart muscle tissue) as well as on tissues of the lactating mammary gland.

   Although many farmers believe that fresh and dried leaves, bark, skin, and seeds are toxic to cattle, goats, horses, rabbits, and birds, there is no definite scientific explanation for that.

   Do not worry about the fruit meat of avocado. There are no dangerous toxic elements for human consumption as well as for animals.

   Creamy rich avocado is considered the world's healthiest fruit, because of its nutrient contents such as vitamin K, dietary fiber, potassium, folic acid, vitamin B6, vitamin C, copper, and reasonable calories in it.

   Avocados contain “oleic acid”, a monounsaturated fat that may help lower cholesterol.

   In our studies, patients with high cholesterol levels who ate avocados showed clear health improvements. After a week of avocado diet, patients had significant decrease in cholesterol contents.

   Avocado is a good source of potassium, a mineral that helps regulate blood pressure. Adequate intake of potassium can help guard against circulatory diseases, like high blood pressure, heart disease, or stroke.

   Diets containing foods that are good sources of potassium and low in sodium may reduce the risk of high blood pressure and stroke. One cup of avocado has about 23% of the Daily Value for folate, a nutrient important for heart health.

   Another study showed that individuals who consume folate-rich diets have a much lower risk of cardiovascular disease or stroke than those who do not consume much of this vital nutrient.

   Not only avocado has a rich source of monounsaturated fatty acids including oleic acid, which has recently been shown to offer significant protection against breast cancer, but it is also a very concentrated dietary source of the "carotenoid lutein". It also contains measurable amounts of related carotenoids plus significant quantities of vitamin E.

   A few slices of avocado in salad, or mixing some chopped avocado into salsa will not only add a rich, creamy flavor, but will greatly increase your body's ability to absorb the health-promoting carotenoids that vegetables provide.

   Compared to other fruits or vegetables such as carrots and spinach, just a slice of avocado improves your body's ability to absorb carotenoids.
   At first, you can try to start planting a seed in your room. You will love it as seen in the photos below.   After eating avocado, don't throw the seed. Place it in the garden soil in your container garden. The soil should always be with water. In about three weeks, you will enjoy seeing leaf buds growing. If you cannot keep it in your room, plant it in your backyard. You will enjoy seeing it growing again.
   Ways to Eat an Avocado

   There are hundreds of ways or recipes for avocado. Here are some that you can try to enjoy eating avocado.

   Chopped avocado with tofu, tomato, and mayonnaise dressing

   Avocado juice mixed with honey or sugar and milk
   Cool it. It is so tasty. Good for all ages.

   Avocado and tuna fish salad with lemon

   Avocado and salmon salad with mayonnaise

   Avocado with chicken and tomato

   Avocado, chicken, and fried garlic

   The simplest way is just slice the avocado and place ham and mayonnaise to make a bread sandwich. Probably, you can add a proverb, "One avocado a day, doctors away".

   To preserve, mash and place the avocado in the freezer. In this way, you can keep it for several months. Do not keep the avocado fruit as is in the freezer.

   Again and again, some critics might write us complaining about the article saying that avocado is toxic. Avocado toxicity is not scientifically well established up to now.

   Avocado poisoning has been a source of controversy and confusion among animal breeders. Some breeders have voiced an opinion that avocado fruit may be toxic, while other breeders have fed avocados to their animals with no abnormal incidences at all.

   Most avocados grown in the United States and other countries are sold for human consumption in the form of fresh fruit or processed paste products. Also, many parts of it are used for various products including animal feeds and baby consumption.

   Avocado poisonings in humans and animals are fairly limited, however, the avocado tree can be toxic. They say that toxic chemical is found in leaves, bark, pits, and skin of the avocado tree. Although some people claim that avocado fruit can cause skin allergy, it is just the same as banana, walnut, and kiwi allergy.

   Anyway, if you are a delicate person, just don't eat avocado. Once again, one avocado a day may save your life from cardiomyopathy and heart failure.
   In addition, if you're suffering from a serious illness, we recommend you to use the PYRO-ENERGEN. PYRO-ENERGEN is proven effective in eradicating viral diseases, cancer, and diseases of unknown cause.


  2. Roulette's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2010
   Posts : 5,646
   Rep Power : 172829250
   Likes Received
   5325
   Likes Given
   5923

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Ndio, inaongeza nguvu. Wali pia by the way, hasa kama unapika uji wa mchele. Sasa wewe ulipiga combo lunch pack so...
   Information is not knowledge

   Albert Einstein

  3. Mamndenyi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Location : Mafinga
   Posts : 25,729
   Rep Power : 429502116
   Likes Received
   14710
   Likes Given
   30237

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Angalia maparachichi ukila mengi unaweza kujisaidia kwenye shuka kwa kuwa yanalainisha sana tumbo.

  4. ndetichia's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th March 2011
   Location : Mwime - Buswangili
   Posts : 27,405
   Rep Power : 98146805
   Likes Received
   4352
   Likes Given
   383

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Ni kweli ngoja niende NIMR nikawaulize wanasayansi kama ni kweli..

  5. The Boss's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th August 2009
   Location : DARESALAAM
   Posts : 30,556
   Rep Power : 429503168
   Likes Received
   30830
   Likes Given
   29184

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   duh.....bado makande tu sasa...lo

   mara matikiti,mara asali,mara matango,sasa parachichi..lol

   mkirudi mtakuja na mapera lol
   Whenever you find yourself on the side of the majority, it is time to pause and reflect.


  6. Husninyo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th October 2010
   Posts : 23,292
   Rep Power : 344358669
   Likes Received
   8325
   Likes Given
   5194

   Default

   Hivi msisimko ndio nguvu za kiume.

  7. mikatabafeki's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th December 2010
   Posts : 10,242
   Rep Power : 171804228
   Likes Received
   2395
   Likes Given
   1745

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   sasa ukishapata huo msisimko hizo nguvu za kiume unazipimaje kwa kupiga punka u???

  8. GAZETI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Location : ILALA
   Posts : 2,633
   Rep Power : 1636
   Likes Received
   1472
   Likes Given
   1743

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Unajua kuna watu wana aleji ya vitu fulani mimi nikila nyama ya ng'ombe mimi embe, mimi tango..... Ili mradi wsatu hawa hudhurika kwa vitu ambavyo
   ni vya kawaida katika jamii, Hata kwa hili wakati mewingine huwa nahisi kuna watu wananufaika zaidi na vyakula fulani kuliko wengine kwa hiyo nafikiri ni bora ukianza kufanya utafiti wa vyakula gani vina manufaa mwilini mwako!

  9. GAZETI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Location : ILALA
   Posts : 2,633
   Rep Power : 1636
   Likes Received
   1472
   Likes Given
   1743

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By Husninyo View Post
   hivi msisimko ndio nguvu za kiume.
   Quote By mikatabafeki View Post
   sasa ukishapata huo msisimko hizo nguvu za kiume unazipimaje kwa kupiga punka u???
   Wakati mwingine tuwe tunaelewa mapema kuna lugha zinakuwa ngumu
   kutumia kwa hiyo unaweza kuelewa tu. Kwa kifupi kila stimulation husababishwa
   na msisimko lakini si kila msisimko husababisha stimulation . Huo ni mtazamo wangu tu!!

  10. Leonard Robert's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd April 2011
   Posts : 6,836
   Rep Power : 1911
   Likes Received
   1323
   Likes Given
   222

   Default

   Quote By GAZETI View Post
   Kuna wanaosema usichanganye dini na siasa sijui nitakosea nikisema
   usichanganye dini na sayansi? Au hilo pepo linapatikana kwenye parachichi
   au mchele?
   hapo hakuna sayansi yoyote ni mambo ya kiroho.dalili mojawapo ya hili pepo ni hiyo uliyotaja.karibu..

  11. King Kong III's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Location : Enaboishu-Umenyeni
   Posts : 23,599
   Rep Power : 168829829
   Likes Received
   9030
   Likes Given
   3536

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Mkuu GAZETI huo utafiti wako upeleke UDSM hili nawe upewe PHD kama Mzee wa kaya

  12. Mswahilina's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th April 2008
   Posts : 172
   Rep Power : 733
   Likes Received
   15
   Likes Given
   5

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By Leonard Robert View Post
   pepo la ngono,njoo maombezi mlima wa moto..mikocheni B..
   Mpendwa, hivi wewe unajua unachoamini? Au unaamini unachojua?
   Kama swali alilouliza huyu ndugu ni pepo la ngono, basi kufanya tendo la ndoa na mkeo/mumeo wa ndoa ni pepo la ngono pia.
   "BETTER IS NOT GOOD ENOUGH, THE BEST IS YET TO COME"

  13. Mswahilina's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th April 2008
   Posts : 172
   Rep Power : 733
   Likes Received
   15
   Likes Given
   5

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By Leonard Robert View Post
   hapo hakuna sayansi yoyote ni mambo ya kiroho.dalili mojawapo ya hili pepo ni hiyo uliyotaja.karibu..
   Hivi ilivyoandikwa Mithali 5:18 (Chemchem yako ibarikiwe nawe umfurahie mke wa ujana wako) hili nalo ni pepo la ngono?
   Kweli Mhe. Dr. Mama Getrude Rwekatare anatakiwa afundishe waumini wake kwa kina zaidi.
   "BETTER IS NOT GOOD ENOUGH, THE BEST IS YET TO COME"

  14. Daffi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th June 2011
   Location : Chuga.
   Posts : 3,534
   Rep Power : 1237
   Likes Received
   669
   Likes Given
   258

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Sure!parachichi inamwongezea sana mtu hamu la tendo la ndoa!kula parachi ili ndoa yako iwe salama

  15. Leonard Robert's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd April 2011
   Posts : 6,836
   Rep Power : 1911
   Likes Received
   1323
   Likes Given
   222

   Default

   Quote By Mswahilina View Post
   Mpendwa, hivi wewe unajua unachoamini? Au unaamini unachojua?
   Kama swali alilouliza huyu ndugu ni pepo la ngono, basi kufanya tendo la ndoa na mkeo/mumeo wa ndoa ni pepo la ngono pia.
   mwache aje apate maombezi,sisi waliokoka tuna mengi ya ziada mpendwa.hakika bwana anaweza,na anaweza kufanya makubwa juu ya huyu mwenye hili tatizo.mtumishi na wewe karibu hakika hutarudi kama ulivyokuja...pili usitetee ngono kwa kutumia vitabu vya mungu.

  16. Mchaka Mchaka's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 20th July 2010
   Location : A - CITY
   Posts : 4,540
   Rep Power : 1583
   Likes Received
   1326
   Likes Given
   687

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By RussianRoulette View Post
   Ndio, inaongeza nguvu. Wali pia by the way, hasa kama unapika uji wa mchele. Sasa wewe ulipiga combo lunch pack so...
   Ahaaaaa ndio maana hata maji yaliooshea mchele yananukia kama naniii!
   Miili ya waliokufa katika ajali ya Meli ya Spice Islander ipimwe DNA ili kutambua Ndugu zao - Dk. Jakaya .M. Kikwete,, September 2011.

  17. valid statement's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th September 2011
   Posts : 2,589
   Rep Power : 1036
   Likes Received
   446
   Likes Given
   8

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   mbona parachichi na wali nayalaga mara nyingi na sijawahi huo msisimko?huo utafiti huoo...

  18. GAZETI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Location : ILALA
   Posts : 2,633
   Rep Power : 1636
   Likes Received
   1472
   Likes Given
   1743

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By kikahe View Post
   Tofauti ya stimulation na msisimko iko wapi?
   Tofauti ya stimulation na msisimko iko wapi? an erection of the penis + Exciting.

  19. GAZETI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2011
   Location : ILALA
   Posts : 2,633
   Rep Power : 1636
   Likes Received
   1472
   Likes Given
   1743

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By valid statement View Post
   mbona parachichi na wali nayalaga mara nyingi na sijawahi huo msisimko?huo utafiti huoo...
   Labda uongeze na karanga mbichi ikishindikana tia Pweza juu
   zaidi ya hapo onana na Wamasai kwa ushauri zaidi.

  20. ndyoko's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2010
   Posts : 4,684
   Rep Power : 1872
   Likes Received
   1310
   Likes Given
   1977

   Default re: Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

   Quote By Mamndenyi View Post
   angalia maparachichi ukila mengi unaweza kujisaidia kwenye shuka kwa kuwa yanalainisha sana tumbo.
   Haahahahahahaaaa! haki ya mungu, shetani na wahuni Mungu na waungwana, mweee!


  Page 1 of 7 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Faida ya tangawizi na asali katika mwili wa binadamu
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 51
   Last Post: 20th June 2014, 07:52
  2. Faida ya kula ndizi mbivu katika mwili wa binadamu
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 0
   Last Post: 24th June 2013, 20:26
  3. Replies: 5
   Last Post: 23rd April 2012, 10:39
  4. Faida ya Mwanga wa jua katika mwili wa binadamu
   By MziziMkavu in forum JF Doctor
   Replies: 0
   Last Post: 19th December 2011, 01:54

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...