JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Punyeto: Nini madhara yake?

  Report Post
  Page 1 of 38 123 11 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 742
  1. Konzogwe's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Location : Bujumbura
   Posts : 228
   Rep Power : 667
   Likes Received
   23
   Likes Given
   1

   Default Punyeto: Nini madhara yake?

   Nimeshindwa kuacha punyeto. Nilifikiri nikioa ntaacha cha ajabu bado naendelea tena kwa kasi mpya. Niponeje balaa hili?

   ======================

   BBC Wanaeleza hivi:

   Punyeto

   Ni nini?

   Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.

   Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.

   Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.

   Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.

   Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.

   Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.

   Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.

   Kwa nini punyeto huonekana kuwa makosa?

   Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.

   Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

   Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.

   Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.


   Lakini kuna sehemu wanaeleza hivi:

   Punyeto (kujitoa manii kwa mkono):

   “Punyeto” ni: Dhana inayowakilisha tendo la kujitoa/kushusha manii kwa njia isiyo jimai. Kupiga punyeto kwa kutumia kiungo/zana yo yote ile ni tendo la haramu mbele za Mafaqihi walio wengi. Na hiyo ndio kauli ya Mafaqihi wa madhehebu ya Imamu Maalik, Shaafiy na Abu Haniyfah. Lakini uharamu wa punyeto mbele zao uko chini ya uharamu wa zinaa; yaani zinaa ni haramu zaidi kuliko punyeto ingawa vyote ni haramu. Kwa muono wao huu, lau mtu ataangukia katika mtelezo wa kutenda mojawapo ya haramu mbili hizi; zinaa na punyeto. Basi hapana makindano kwamba aegemee zaidi janibu ya punyeto ili kuilinda nafsi yake dhidi ya uchafu wa zinaa. Atafanya hivyo kwa mazingatio ya msingi wa Fiq-hi usemao: “lenye madhara khafifu baina ya yenye madhara mawili” na “lenye shari kidogo baina ya yenye shari mawili”.

   Ama madhehebu ya Imamu Ahmad na maimamu wengineo-Allah awarehemu-ni kuhalalisha punyeto kwa kuizingatia kuwa ni nyenzo inayoweza kumsaidia muhusika kujikinga na zinaa. Na wala hapa hatukusudii na wala hatuna nafasi ya kutaja mkururo wa dalili za kauli mbili hizi; haramishi ya kundi kubwa na ile halalishi ya kundi dogo. Bali tunalazimika na kutosheka na kuashiria kwamba waliosimamia kauli ya uhalali. Hawakusema hivyo ila ni kwa sababu wameona tendo hili linampa kinga ya kiasi fulani mwanadamu dhidi ya kutenda uchafu na uoza wa zinaa. Hili ndilo walilolizingatia na kulijengea kauli yao hii ya uhalali, lakini hapo hapo hawalioni tendo hili kuwa ni halali iwapo litageuzwa kuwa ndio ada/desturi na mazoea ya mtu. Akawa analifanya zoezi hili kwa kuendelea kiasi cha kuifanya punyeto kuwa maradhi ya nafsi/siha. Kwa sababu hakuna hata mwanachuoni mmoja anayehalalisha madhara hata kama hicho chenye kudhuru kilikuwa halali katika asili yake. Mathalan tendo la kula, asili yake ni halali na wakati mwingine huwa ni wajibu kwa kiwango cha dharura/ulazima wa kuhifadhi uhai. Lakini tendo hili hili linaweza likawa haramu pale mtu atakapokula zaidi ya uweza/shibe yake na akasababisha kuidhuru nafsi yake. Kwa msingi wa maelezo haya basi, hapana makindano baina ya maulamaa wetu-Allah awarehemu-katika suala zima la kuharamisha punyeto. Kwa sababu tendo hili linaidhuru kano/mishipa ya nguvu ya muendekeza tendo hilo na kulifanya kuwa ndio mchezo wake. Kama linavyoudhuru mfumo mzima wa viungo vyake vya uzazi (reproductive system) na afya yake kwa ujumla. Kwa hivyo basi, si Imamu Ahmad wala imamu mwingine anayehalalisha kile kinachosababisha madhara kwa hali yo yote. Kwa mapenzi mema kabisa, tunawasihi na kuwanasihi vijana wetu wa kiume na wale wa kike kutoendekeza zoezi hili la kujitoa manii kwa njia isiyo ya jimai. Tena waache kabisa hata kufikiria kulitenda, kwa sababu tendo hilo ni hatari kwa afya zao.

   Mwanachuoni mkubwa; Sheikh Muhammad Al-Haamid-Allah amrehemu-katika kitabu chake {RUDUUDUN ‘ALAL-ABAATWIYL}, ametaja maneno kima kuhusiana na maudhui hii, tunamnukuu: “Hakika tene (kichwa cha dhakari) ina hisia kali sana na hapo ndipo patokapo hisia (za raha na ladha) wakati wa tendo la jimai kwenda kwenye kifuko cha manii (spermatic vesicle). Na kusababisha kijibinye ili kitoke humo kiasi fulani cha manii na kuchanganyika na kitu kinachoitwa “prostate gland”. Na hapo katika mchanganyo huo ndipo huundika mmiminiko maji huu ambao kutoka kwake huzipoza na kuzituliza shahawa/ashiki/matamanio. Sasa basi mtu atakapodumu na zoezi la kuichezea dhakari yake, ngozi ya tene huwa ngumu na kusababisha kudhoofika kwa nguvu-hisia zake. Na kuyafanya manii kutoka bila ya kuchanganyika na ute wa “prostate” ambao una athari na mchango mkubwa katika kutuliza kiamshi-shahawa. Kwa hivyo basi manii yanapokuwa hayakuchanganyika na ute huo, kupoa kwa shahawa huwa ni kwa muda mfupi tu, kisha huamka tena kwa nguvu kubwa. Kwa ajili hii humlazimisha mpiga punyeto kupiga tema mara ya pili, tatu.... na kama hivi. Mpaka mwishowe humwaga damu (badala ya manii), kwa sababu ya kumaliza kabisa kile kiitwacho “spermatic cord/funiculus” na kuudhoofisha kwake mfumo-uzazi kutokana na wingi wa kupiga punyeto. Kinachotokea kutokana na udhaifu wa hisia wa tene kwa sababu ya wingi wa kupiga punyeto: Ni kwamba mwenye kuzoea kupiga punyeto, hutokezea akashindwa kufanya jimai kwa namna anayoweza kufanya mtu asiyefanya mchezo huo. Hii ni kwa sababu tene iliyodhoofika kutokana na wingi wa kupiga punyeto haiathiriki (na tendo la jimai) kwa kiwango kihitajiwacho kutokana na msuguano ndani ya uke. Kwa hivyo basi hawezi kushusha manii ila kwa kujichua na mkono. Ndani ya tendo hilo kuna madhara kwa nafsi yake na mkewe ambaye ana haki ya kutoshelezwa nae (ili asifikirie/kufanya machafu) kwa jimai halali”. Mwisho wa kumnukuu sheikh-Allah amrehemu.

   Kwa kuungia maneno kima haya ya sheikh tunaongezea: Kwamba manii ni kimiminika muhimu mno cha mwili na mfumo mzima wa uzazi. Chini ya maana hii Muingereza Dr. Mary Stoubis anasema katika kitabu chake {MARRIED LOVE}: “Kwa yakini mchanganuo wa kikemia wa kimiminika hiki manii, umedhihirisha kwamba pamoja na vitu vingine unahodhi kiwango kikubwa cha “phosphoric acid” na “calcic acid”. Na zote mbili hizi ni maada kima zenye taathira adhimu katika ujenzi wetu wa kimwili (kama wanadamu). Hili likisihi (kuwa sahihi), basi kwa hakika kosa kubwa analolifanya mwanadamu ni kudhania kuwa maada manii ni kitu ambacho kunasihi kujitakasa nacho baina ya kipindi kifupi na kingine. Na kuimwaga hovyo bila ya malengo na kuona haja ya kuihifadhi”.

   Ni mazuri yaliyoje maneno ya mshairi huyu anayesema na vijana:

   {Yahifadhi manii yako kiasi uwezavyo kwani hayo *** Ni maji ya uhai yamwagwayo katika matumbo ya uzazi}.


  2. X-PASTER's Avatar
   Moderator Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Firdaws (Paradise)
   Posts : 11,854
   Rep Power : 7734
   Likes Received
   1502
   Likes Given
   0

   Default Re: Punyeto

   Quote By Konzogwe View Post
   Nimeshindwa kuacha punyeto. Nilifikiri nikioa ntaacha cha ajabu bado naendelea tena kwa kasi mpya. Niponeje balaa hili?
   Nakushauri nenda ukapate ushauri nasaa kwa wataalam husika.

   Madhara mengine kuhusiana na punyeto au kujichuwa tafadhari tembela thread ya hii:

   http://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=10486
   MziziMkavu likes this.
   “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

   'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

   (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


  3. PastorPetro's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th February 2008
   Location : Boston, MA USA
   Posts : 139
   Rep Power : 649
   Likes Received
   6
   Likes Given
   13

   Unhappy Re: Punyeto

   Kijana, Punyeto ni DHAMBI! Acha hiyo tabia na kuiwaza mara moja ili kuokoka roho yako.

  4. Injinia's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Location : Seriously? In your CPU
   Posts : 853
   Rep Power : 792
   Likes Received
   16
   Likes Given
   11

   Default Re: Punyeto

   hey,lets not condemn this poor guy, Padre! U shud b d 1st to ofa help, seeing as u r a padre n shd there4 b an 'expert' in keeping your thoughts 'pure' thereby avoiding 2 do what he duz!
   Kijana, mi nakushauri
   1. Dont think 2 much abt sex
   2. Ask ur wife 4 d real thing, Neno la Mungu lasema 'Msinyimane ktk ndoa'
   3. Muombe Mungu
   4. Tafuta ushauri wa ana kwa ana eg kwa psychologist
   Pole, al d best
   HILLARY MUSHI likes this.

  5. BAK's Avatar
   JF Tanzanite Member Array
   Join Date : 11th February 2007
   Location : Mfaranyaki
   Posts : 31,479
   Rep Power : 19996345
   Likes Received
   13174
   Likes Given
   14371

   Default Re: Punyeto

   Quote By Konzogwe View Post
   Nimeshindwa kuacha punyeto. Nilifikiri nikioa ntaacha cha ajabu bado naendelea tena kwa kasi mpya. Niponeje balaa hili?
   Badala ya kupiga punyeto kwa siri itakuwa vizuri ukimwambia mkeo akupige nyeto yeye kwa mikono yake. Unampa maelezo jinsi unavyotaka akufanyie na unamwacha afanye vitu vyake. Kingine unaweza kupiga punyeto mbele ya mkeo lakini ni vizuri akiwa uchi wa nyama....'nasikia' huwa ni turn on kubwa sana kwa wanawake... na badala ya kuwa 'balaa' inaweza kuwa ni part of your love making activities which will be enjoyable to both of you. Please try both ideas and let's know of the outcome.
   rogers26tz likes this.
   Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

  6. JF SMS Swahili

  7. DMussa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2007
   Location : Dar es salaam
   Posts : 1,010
   Rep Power : 846
   Likes Received
   48
   Likes Given
   37

   Default Re: Punyeto

   Quote By Bubu ataka kusema View Post
   Badala ya kupiga punyeto kwa siri itakuwa vizuri ukimwambia mkeo akupige nyeto yeye kwa mikono yake. Unampa maelezo jinsi unavyotaka akufanyie na unamwacha afanye vitu vyake. Kingine unaweza kupiga punyeto mbele ya mkeo lakini ni vizuri akiwa uchi wa nyama....'nasikia' huwa ni turn on kubwa sana kwa wanawake... na badala ya kuwa 'balaa' inaweza kuwa ni part of your love making activities which will be enjoyable to both of you. Please try both ideas and let's know of the outcome.
   Duh... from the expatriate!!

   Kozongwe,
   Ningependa kujua ni kwa nini unataka kuacha hiyo tabia maana yawezekana kabisa imetokana na mambo flani katika malezi/ukuaji wako!
   Nakushauri kama kweli una nia ya kuacha punyeto jitahidi uwe busy cos inavyoonekana kila unapokuwa idle ndo mawazo kama hayo yanakujia na hii inaweza kuja kukuletea athari kubwa sana mbeleni maana unaweza jikuta uko in love with your hands! ukiangalia tu mikono yako unakuwa turned on which will lead to breaking ur relationship(ndoa)!
   Piga moyo konde uachane na hilo tatizo....
   It is not the strongest species that survive, nor the most intelligent, but the ones most responsive to change - Charles Darwin

  8. Kidzogolae's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 20th April 2008
   Posts : 142
   Rep Power : 642
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Punyeto

   Hivi hii ina madhara gani katika uzazi wa mwanaume?inaweza ikakufanya usizae?

  9. Titus's Avatar
   Member Array
   Join Date : 28th July 2007
   Posts : 81
   Rep Power : 668
   Likes Received
   0
   Likes Given
   1

   Default Masturbation: nini madhara yake.

   Habari zenu JF Docs! naomba kujua masturbation ina madhara gani kiafya na nini mtu anaweza kufanya ili aweze kuacha. naombeni msaada wenu wa kitalaamu.
   A true soldier is more worried in tents than in a battle field

  10. MwanajamiiOne's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 24th July 2008
   Location : On My Seat
   Posts : 10,097
   Rep Power : 1385553
   Likes Received
   6063
   Likes Given
   5449

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Mimi si mtaalamu wala daktari ila nadhani ina madhara kama itazidi kipimo kwani si wanasemage anything in excess ina madhara.... no?
   Serebuka unaweza pendwa tena, serebuka unaweza penda tena - Mwasiti, 2014

  11. Yo Yo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st May 2008
   Posts : 11,196
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1434
   Likes Given
   2625

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Quote By titus View Post
   Habari zenu JF Docs! naomba kujua masturbation ina madhara gani kiafya na nini mtu anaweza kufanya ili aweze kuacha. naombeni msaada wenu wa kitalaamu.
   Mkuu haina MADHARA YOYOTE liendeleze libeneke tu.Ina tatizo moja ambalo naliona kama si tatizo ni kuwa ukiendekeza hii kitu itafikia unaanza dili zako na kwenda kukung'uta kamoja.......inawezekana kama wewe ni mwanafunzi uko class ukakacha masomo na kwenda kukitupa kimoja....

   Inaaminika wanaume 98% wamepiga au wanapiga hii kitu duniani.....na takwimu za sasa zinasema kuwa ndio njia salama kabisa ya kujiridhisha hasa ukiangalia magonjwa lukuki.....mkuu kama ulisoma boys school unafahamu mengi juu ya hii kitu.....Good lucky

  12. Congo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th March 2008
   Posts : 507
   Rep Power : 720
   Likes Received
   68
   Likes Given
   67

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Masturbation ina madhara ingawa yanaweza kuonekana kuwa sio ya kiafya. Ukiendekeza sana hutakuwa na hamu ya kukutana na mwanamke kabisa na hata ukikutana naye unakuwa na nguvu kidogo sana ya kujamiiana. Na ukimaliza hicho kimoja ndio mpaka wiki ipite. Na hata kama ukiacha hutakuwa na nguvu kwa muda mrefu kitu ambacho hakitakuletea furaha ya mapenzi na mwanamke. Ni vema kutofanya kabisa kama inawezekana.

  13. Mchola's Avatar
   Member Array
   Join Date : 30th October 2007
   Posts : 88
   Rep Power : 656
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Niongezee hapo kwa alichosema Congo,
   Punyeto inasababisha early ejacultaion unapokutana na mwanamke hivyo hutoweza kumridhisha mkeo. Madhara yake utaachwa na mkeo kwa vile humpi stahili yake. Chunga sana!!!!! Nakuhakikishia hakuna madhara makubwa kama hilo la kutoridhisha mkeo au mpenzio. Itakudhalilisha utajiona mdogooooo ka sisimizi mbele ya mkeo/mpenzio
   Sambula kiswaga likes this.
   Do not Agonize, Organize. -Kwame Nkrumah

  14. walter's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 22nd August 2008
   Posts : 2
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   ya kweli kabisa masturbation inaweza kukuharibia kabisa hamu ya kufanya ngono na mwanamke

  15. Kevo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th June 2008
   Location : Around the World
   Posts : 1,345
   Rep Power : 875
   Likes Received
   17
   Likes Given
   14

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Quote By Yo Yo View Post
   Mkuu haina MADHARA YOYOTE liendeleze libeneke tu.Ina tatizo moja ambalo naliona kama si tatizo ni kuwa ukiendekeza hii kitu itafikia unaanza dili zako na kwenda kukung'uta kamoja.......inawezekana kama wewe ni mwanafunzi uko class ukakacha masomo na kwenda kukitupa kimoja....

   Inaaminika wanaume 98% wamepiga au wanapiga hii kitu duniani.....na takwimu za sasa zinasema kuwa ndio njia salama kabisa ya kujiridhisha hasa ukiangalia magonjwa lukuki.....mkuu kama ulisoma boys school unafahamu mengi juu ya hii kitu.....Good lucky
   Mimi siyo Doctor ila I got these through Wikipedia!

   Blood pressure
   Both sex and masturbation lower blood pressure. A small study has shown that in one test group, recent full intercourse resulted in the lowest average blood pressure in stressful situations. Masturbation then led to lower blood pressure than did no recent sexual activity.

   Problems for males

   A man whose penis has suffered a blunt trauma or injury during intercourse may rarely sustain a penile fracture or suffer from Peyronie's disease.Phimosis is "a contracted foreskin (that) may cause trouble by hurting when an attempt is made to pull the foreskin back".In these cases, any energetic manipulation of the penis can be problematic.

   Lawrence I. Sank thought that masturbating prone (lying face downward) could be responsible for sexual problems in some men including anorgasmia and erectile dysfunction. He based this theory on four men he examined and coined the term traumatic masturbatory syndrome to describe it. As of 2008, no follow-up research has been conducted and the idea is not familiar or widely-held within the medical community. Some authors, however, continue to give it credence.
   dickson longo likes this.
   'I could have annihilated all the Jews in the World,but I left some of them so you will know why I was killing them'-Adolf Hitler;Mien Kampf

  16. Hofstede's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th July 2007
   Posts : 3,604
   Rep Power : 21389
   Likes Received
   1002
   Likes Given
   988

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Duh!,
   Hapo hapo na mimi niulize je na wanawake wanapojidobola mpaka kupata orgasm ina madhara gani kiafya hasa katika afya ya uzazi.

  17. Yo Yo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st May 2008
   Posts : 11,196
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1434
   Likes Given
   2625

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Quote By hofstede View Post
   Duh!,
   Hapo hapo na mimi niulize je na wanawake wanapojidobola mpaka kupata orgasm ina madhara gani kiafya hasa katika afya ya uzazi.
   Enhe....waulize hao....hii kitu haina madhara yoyote imedhibitika haina madhara kiafya hilo la kusema kuwa bao linakuja fasta hakuna ukweli wowote.

   kwanza inajulikana kuwa wanao practice hii kitu huwa very strong kwenye game.....nikiwa naa maana mzunguko wa kwanza wanaweza kwenda mpaka dakika 15-20......
   24hrs likes this.

  18. Titus's Avatar
   Member Array
   Join Date : 28th July 2007
   Posts : 81
   Rep Power : 668
   Likes Received
   0
   Likes Given
   1

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   naona kama napata mchanganyiko wa mawazo, lakini from what i see, it sounds like madhara ni mengi kimtindo, labda niulize, kama unahisi nguvu zako za kiume zinapungua je hakuna dawa ambayo imedhibitishwa inayoweza kusaidia? achilia izi za kibongo Mkuyati na nyingine nyingi ambazo waganga wetu wa kienyeji wa kibongo wanatangaza kila kukicha.
   A true soldier is more worried in tents than in a battle field

  19. Msanii's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th July 2007
   Posts : 6,369
   Rep Power : 2007
   Likes Received
   341
   Likes Given
   560

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Hakuna madhara labda ukiendekeza.
   niige mie ambaye huipiga once a month ili tu nipunguze masalia ya nguvu za uume.

   Ila ukizoea nasikia hata mbunye unakuwa huitaki tena hivyo elewa kila kitu kina side effects zake. hata chakula ukizidisha utavimbirwa na kujishuzisha kiasi cha kujikera
   Katiba mpya ituletee Taasisi imara na si viongozi imara- Msanii

   Kitendo Cha Kuitoa CCM Madarakani ni Kuwafumbua Macho na Kuwaonyesha Ukombozi wa Pili wenye Matumaini Kwa Uhai wa Taifa. - Kakobe
   [email protected]

  20. Nyerererist's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 455
   Rep Power : 734
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   Quote By Msanii View Post
   Hakuna madhara labda ukiendekeza.
   niige mie ambaye huipiga once a month ili tu nipunguze masalia ya nguvu za uume.

   Ila ukizoea nasikia hata mbunye unakuwa huitaki tena hivyo elewa kila kitu kina side effects zake. hata chakula ukizidisha utavimbirwa na kujishuzisha kiasi cha kujikera
   U deserve a ban,, ((MBUNYE????))!!!!
   Makuadi Hawana Hata Chembe ya Ujasiri mara Mambo yanapoharibika (Chachage, 2002)

  21. Mwana wa Mungu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th August 2008
   Posts : 1,013
   Rep Power : 799
   Likes Received
   27
   Likes Given
   6

   Default Re: Masturbation: nini madhara yake.

   HIli ni pepo kabisa, kama unafanya hivyo,omba Mungu akusaidie uache. ni roho, inaweza ikakaribisha hata roho chafu wenzie, ukajikuta haujakuwa mtu wa kueleweka kabisa. its sin and I rebuke it in the Mighty Name of Jesus Christ. Amin.
   mama yuva and bampami like this.

  22. JF SMS Swahili

  Page 1 of 38 123 11 ... LastLast

  Similar Topics

  1. CAR AIR FRESHENER na Madhara Yake
   By Kachanchabuseta in forum JF Doctor
   Replies: 6
   Last Post: 12th April 2010, 23:21

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...