Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Punyeto: Nini madhara yake?

    Report Post
    Page 23 of 37 FirstFirst ... 13212223242533 ... LastLast
    Results 441 to 460 of 725
    1. #1
      Konzogwe's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : Bujumbura
      Posts : 164
      Rep Power : 606
      Likes Received
      11
      Likes Given
      0

      Default Punyeto: Nini madhara yake?

      Nimeshindwa kuacha punyeto. Nilifikiri nikioa ntaacha cha ajabu bado naendelea tena kwa kasi mpya. Niponeje balaa hili?

      ======================

      BBC Wanaeleza hivi:

      Punyeto

      Ni nini?

      Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.

      Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.

      Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.

      Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.

      Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.

      Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.

      Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.

      Kwa nini punyeto huonekana kuwa makosa?

      Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.

      Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

      Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.

      Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.


      Lakini kuna sehemu wanaeleza hivi:

      Punyeto (kujitoa manii kwa mkono):

      “Punyeto” ni: Dhana inayowakilisha tendo la kujitoa/kushusha manii kwa njia isiyo jimai. Kupiga punyeto kwa kutumia kiungo/zana yo yote ile ni tendo la haramu mbele za Mafaqihi walio wengi. Na hiyo ndio kauli ya Mafaqihi wa madhehebu ya Imamu Maalik, Shaafiy na Abu Haniyfah. Lakini uharamu wa punyeto mbele zao uko chini ya uharamu wa zinaa; yaani zinaa ni haramu zaidi kuliko punyeto ingawa vyote ni haramu. Kwa muono wao huu, lau mtu ataangukia katika mtelezo wa kutenda mojawapo ya haramu mbili hizi; zinaa na punyeto. Basi hapana makindano kwamba aegemee zaidi janibu ya punyeto ili kuilinda nafsi yake dhidi ya uchafu wa zinaa. Atafanya hivyo kwa mazingatio ya msingi wa Fiq-hi usemao: “lenye madhara khafifu baina ya yenye madhara mawili” na “lenye shari kidogo baina ya yenye shari mawili”.

      Ama madhehebu ya Imamu Ahmad na maimamu wengineo-Allah awarehemu-ni kuhalalisha punyeto kwa kuizingatia kuwa ni nyenzo inayoweza kumsaidia muhusika kujikinga na zinaa. Na wala hapa hatukusudii na wala hatuna nafasi ya kutaja mkururo wa dalili za kauli mbili hizi; haramishi ya kundi kubwa na ile halalishi ya kundi dogo. Bali tunalazimika na kutosheka na kuashiria kwamba waliosimamia kauli ya uhalali. Hawakusema hivyo ila ni kwa sababu wameona tendo hili linampa kinga ya kiasi fulani mwanadamu dhidi ya kutenda uchafu na uoza wa zinaa. Hili ndilo walilolizingatia na kulijengea kauli yao hii ya uhalali, lakini hapo hapo hawalioni tendo hili kuwa ni halali iwapo litageuzwa kuwa ndio ada/desturi na mazoea ya mtu. Akawa analifanya zoezi hili kwa kuendelea kiasi cha kuifanya punyeto kuwa maradhi ya nafsi/siha. Kwa sababu hakuna hata mwanachuoni mmoja anayehalalisha madhara hata kama hicho chenye kudhuru kilikuwa halali katika asili yake. Mathalan tendo la kula, asili yake ni halali na wakati mwingine huwa ni wajibu kwa kiwango cha dharura/ulazima wa kuhifadhi uhai. Lakini tendo hili hili linaweza likawa haramu pale mtu atakapokula zaidi ya uweza/shibe yake na akasababisha kuidhuru nafsi yake. Kwa msingi wa maelezo haya basi, hapana makindano baina ya maulamaa wetu-Allah awarehemu-katika suala zima la kuharamisha punyeto. Kwa sababu tendo hili linaidhuru kano/mishipa ya nguvu ya muendekeza tendo hilo na kulifanya kuwa ndio mchezo wake. Kama linavyoudhuru mfumo mzima wa viungo vyake vya uzazi (reproductive system) na afya yake kwa ujumla. Kwa hivyo basi, si Imamu Ahmad wala imamu mwingine anayehalalisha kile kinachosababisha madhara kwa hali yo yote. Kwa mapenzi mema kabisa, tunawasihi na kuwanasihi vijana wetu wa kiume na wale wa kike kutoendekeza zoezi hili la kujitoa manii kwa njia isiyo ya jimai. Tena waache kabisa hata kufikiria kulitenda, kwa sababu tendo hilo ni hatari kwa afya zao.

      Mwanachuoni mkubwa; Sheikh Muhammad Al-Haamid-Allah amrehemu-katika kitabu chake {RUDUUDUN ‘ALAL-ABAATWIYL}, ametaja maneno kima kuhusiana na maudhui hii, tunamnukuu: “Hakika tene (kichwa cha dhakari) ina hisia kali sana na hapo ndipo patokapo hisia (za raha na ladha) wakati wa tendo la jimai kwenda kwenye kifuko cha manii (spermatic vesicle). Na kusababisha kijibinye ili kitoke humo kiasi fulani cha manii na kuchanganyika na kitu kinachoitwa “prostate gland”. Na hapo katika mchanganyo huo ndipo huundika mmiminiko maji huu ambao kutoka kwake huzipoza na kuzituliza shahawa/ashiki/matamanio. Sasa basi mtu atakapodumu na zoezi la kuichezea dhakari yake, ngozi ya tene huwa ngumu na kusababisha kudhoofika kwa nguvu-hisia zake. Na kuyafanya manii kutoka bila ya kuchanganyika na ute wa “prostate” ambao una athari na mchango mkubwa katika kutuliza kiamshi-shahawa. Kwa hivyo basi manii yanapokuwa hayakuchanganyika na ute huo, kupoa kwa shahawa huwa ni kwa muda mfupi tu, kisha huamka tena kwa nguvu kubwa. Kwa ajili hii humlazimisha mpiga punyeto kupiga tema mara ya pili, tatu.... na kama hivi. Mpaka mwishowe humwaga damu (badala ya manii), kwa sababu ya kumaliza kabisa kile kiitwacho “spermatic cord/funiculus” na kuudhoofisha kwake mfumo-uzazi kutokana na wingi wa kupiga punyeto. Kinachotokea kutokana na udhaifu wa hisia wa tene kwa sababu ya wingi wa kupiga punyeto: Ni kwamba mwenye kuzoea kupiga punyeto, hutokezea akashindwa kufanya jimai kwa namna anayoweza kufanya mtu asiyefanya mchezo huo. Hii ni kwa sababu tene iliyodhoofika kutokana na wingi wa kupiga punyeto haiathiriki (na tendo la jimai) kwa kiwango kihitajiwacho kutokana na msuguano ndani ya uke. Kwa hivyo basi hawezi kushusha manii ila kwa kujichua na mkono. Ndani ya tendo hilo kuna madhara kwa nafsi yake na mkewe ambaye ana haki ya kutoshelezwa nae (ili asifikirie/kufanya machafu) kwa jimai halali”. Mwisho wa kumnukuu sheikh-Allah amrehemu.

      Kwa kuungia maneno kima haya ya sheikh tunaongezea: Kwamba manii ni kimiminika muhimu mno cha mwili na mfumo mzima wa uzazi. Chini ya maana hii Muingereza Dr. Mary Stoubis anasema katika kitabu chake {MARRIED LOVE}: “Kwa yakini mchanganuo wa kikemia wa kimiminika hiki manii, umedhihirisha kwamba pamoja na vitu vingine unahodhi kiwango kikubwa cha “phosphoric acid” na “calcic acid”. Na zote mbili hizi ni maada kima zenye taathira adhimu katika ujenzi wetu wa kimwili (kama wanadamu). Hili likisihi (kuwa sahihi), basi kwa hakika kosa kubwa analolifanya mwanadamu ni kudhania kuwa maada manii ni kitu ambacho kunasihi kujitakasa nacho baina ya kipindi kifupi na kingine. Na kuimwaga hovyo bila ya malengo na kuona haja ya kuihifadhi”.

      Ni mazuri yaliyoje maneno ya mshairi huyu anayesema na vijana:

      {Yahifadhi manii yako kiasi uwezavyo kwani hayo *** Ni maji ya uhai yamwagwayo katika matumbo ya uzazi}.

    2. Miaka 50

    3. #441
      mzalendofungo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th February 2011
      Posts : 46
      Rep Power : 428
      Likes Received
      4
      Likes Given
      1

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Mkuu acha akako katabia, maanake baada ya muda mrefu, hautaweza kusimamisha tena hata milele. kwani ulianza je mpaka kujichua mtoto wa kiume? Hii ni dalili ya ukosefu wa maadili, nenda kwa ndodi akakuombee mara moja.

    4. #442
      hashycool's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2010
      Location : network search....
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1457
      Likes Received
      559
      Likes Given
      141

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By iron finger
      Ni mwaka wa 4 sasa najitahidi niache ila nashndwa ata nikipata mwanamke naona hana ladha nisaidieni wakuu!
      uwe unapka pilipili mikono kila ukijisikia kupiga nyeto
      hivi vrusi vya H.I.V na wewe nani mchokozi?

    5. #443
      Kichwa Ngumu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Location : In the Computer
      Posts : 1,296
      Rep Power : 692
      Likes Received
      186
      Likes Given
      248

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      ukiwa unaoga mkono ukifika sehemu nyeti tu unaanza kufanya mambo yko.
      demu mkono hana likizo coz hableed si ndio
      Chezea nguvu ya umma wewe; utaumia

    6. #444
      Husninyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 17,200
      Rep Power : 24908
      Likes Received
      4186
      Likes Given
      636

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Endelea kujichua hadi uoe.
      zumbemkuu likes this.

    7. #445
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,242
      Rep Power : 31389
      Likes Received
      9619
      Likes Given
      684

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By Husninyo
      Endelea kujichua hadi uoe.
      Wewe unajichua?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    8. RukaaJuu Final

    9. #446
      Husninyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 17,200
      Rep Power : 24908
      Likes Received
      4186
      Likes Given
      636

      Default

      Quote By Nyani Ngabu
      Wewe unajichua?
      ndio. Wewe je?

    10. #447
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,242
      Rep Power : 31389
      Likes Received
      9619
      Likes Given
      684

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By Husninyo
      ndio. Wewe je?
      Ndiyo.

      Yako tamu?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    11. #448
      Husninyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 17,200
      Rep Power : 24908
      Likes Received
      4186
      Likes Given
      636

      Default

      Quote By Nyani Ngabu
      Ndiyo.

      Yako tamu?
      tamu kama yako.

    12. #449
      Alexism's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2011
      Location : Iringa Municipal TZ
      Posts : 843
      Rep Power : 565
      Likes Received
      119
      Likes Given
      18

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Kaka ongela sana kwahilo kwani unasaidia kutoongezeka watu(population growth) kitu ambacho ni poa lkn pia unajilinda dhidi ya maambukizi kama HIV,Kaswende,gono na dhambi ya uzinzi .keep it up!

    13. #450
      Gosbertgoodluck's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 2,863
      Rep Power : 1149
      Likes Received
      334
      Likes Given
      4

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By God bell
      Hilo ni pepo la ngono. Nenda kwenye maombi ukaombewe. Soma vitabu vya Mungu, hudhuria ibadani, na kwenye semina ya neno la Mungu. Hiyo ndo dawa pekee ya ugonjwa wako.
      Umenena. Siongezi neno.
      "Before God we are all equally wise and equally foolish"

    14. #451
      LE GAGNANT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2011
      Posts : 1,228
      Rep Power : 710
      Likes Received
      222
      Likes Given
      184

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Endelea kukung'uta tu ndugu yangu haina madhara yoyote kiafya na kimwili kwa ujumla, madhara ni ya kiasaikolojia tu.
      SI VYOTE VING'AAVYO NI DHAHABU

    15. #452
      MKUNGA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th December 2009
      Location : SIRTE
      Posts : 425
      Rep Power : 566
      Likes Received
      54
      Likes Given
      21

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Masturbation ni addiction kama vile sigara, pombe etc. watu wengi wamejaribu kuacha wameshindwa hadi wameoa bado wanajiraha tu. Ili uache kwanza anza kw kupunguza mf. kama ulikua unagonga daily inakua twice a week, then once a week huku ukiichukia tabia hiyo hadi inakwisha. Epuka upweke, acha kukaa maeneo hatarishi mf.room peke yako. sali sana kwa imani yako ukimwomba Mungu akuepushe na tabia hiyo na akupe mchumba uoe. Nadhani umenipata.
      Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao na wataungua katika huo moto.
      The Holy Quran 4:10

    16. #453
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 767
      Rep Power : 5117
      Likes Received
      584
      Likes Given
      111

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By gazeti
      niliomba ushsuri wakuu wameniambia sio vizuri so nimekaa kando!
      mke wa mtu sumu..
      Pathologically.."women must bear all loves" ..Atheisms .

    17. #454
      SHAROBALO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2011
      Location : DRIVE (C:)
      Posts : 585
      Rep Power : 536
      Likes Received
      211
      Likes Given
      125

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Sasa mkono wako ukipata mimba utafanyeje? loh acha ubakaji mkono una haki pia hadi ukubali wenyewe!!

      pole kijana Punguza kuangalia Ngono!! delete porn zote kwenye PC yako,. ni hilo tu
      MziziMkavu likes this.
      A hackerwith a new toy,the first thing he'll do is take it apart to figure out how it works.

    18. #455
      TUNTEMEKE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2009
      Location : Mombasa
      Posts : 4,504
      Rep Power : 11337
      Likes Received
      323
      Likes Given
      236

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      utafakari ukuu wa mungu kwanza vidole vinakazi yake mkuu na kuna raha ya kuwa na mwanamke iambie nafsi yako utaweza

    19. #456
      mysteryman's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 4th August 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 987
      Rep Power : 0
      Likes Received
      164
      Likes Given
      39

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Safi sana karibu CHAWAPUTA mkuu kuna nafasi nzuri tu tunakuandalia ktk chama...karibu sana

    20. #457
      Nzagamba Yapi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st September 2011
      Posts : 154
      Rep Power : 420
      Likes Received
      56
      Likes Given
      2

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Imeandikwa Ole wao wageuzao viganja vya mikono yao kuwa uchi wa mwanamke...maana watoto nusu uliowaua siku ya kiama watakulilia wakiwa viumbe ambavyo havijakamilika kwani manii hazikuungana na za mwanamke na ubinafsi wa kujifurahisha mwenyewe bila mwanamke(lwa of nature)itaandikwa kwenye paji la uso wako...Nzagamba 12:1-3

    21. #458
      c..rella Brains's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 66
      Rep Power : 399
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By mysteryman
      Safi sana karibu CHAWAPUTA mkuu kuna nafasi nzuri tu tunakuandalia ktk chama...karibu sana
      najuutaje!?!

    22. #459
      charndams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Posts : 393
      Rep Power : 510
      Likes Received
      96
      Likes Given
      86

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      Quote By GAZETI
      Narekebisha tu mkuu najua umekosea, Hapo kwenye RED sema TUNA na sio WANA na hapo chini ni UTATU badala ya UTAWA. Hilo tu!
      mwambie mkuu, hakuna kubebana hapa. kila mtu kwa miguu yake. hakuna wengi wenye tabia kama hii ni yeye mwenyewe na kama wapo kila mtu atajitetea kwa nafsi yake

    23. #460
      feis buku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2011
      Posts : 2,367
      Rep Power : 864
      Likes Received
      644
      Likes Given
      574

      Default Re: Jamani kujichua kutaniua nifanyeje?

      ukachomwe sindano 82 za kwinini! tiba tosha kabisa!

    Page 23 of 37 FirstFirst ... 13212223242533 ... LastLast

    Similar Topics

    1. CAR AIR FRESHENER na Madhara Yake
      By King of Kings in forum JF Doctor
      Replies: 6
      Last Post: 12th April 2010, 22:21

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...