Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 35 of 35
    1. #1
      Pdidy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 12,283
      Rep Power : 3442
      Likes Received
      1322
      Likes Given
      855

      Default Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Jamani ningependa kuuliza kuna wanaume wengine wanakuwa na ama vijititi vidogo na wengine makubwa kabisa... Nikaona nipate ufahamu, maana kuna mdogo wetu nae amekutwa nayo...

      Naomba mtupe data zaidi wa medical

    2. Miaka 50

    3. #21
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,135
      Rep Power : 21609
      Likes Received
      13464
      Likes Given
      17776

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      ni percent ngapi?????
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    4. #22
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1523
      Likes Received
      1422
      Likes Given
      1828

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      haahhahahaha kuna kaukweli kabisa,,unaweza kutana na mkaka wa ukweli ngoja aongee!

    5. #23
      Preta's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : yaeda chini
      Posts : 14,718
      Rep Power : 15099
      Likes Received
      7172
      Likes Given
      6838

      Default

      Quote By shosti
      haahhahahaha kuna kaukweli kabisa,,unaweza kutana na mkaka wa ukweli ngoja aongee!
      anakukata stim muda huo huo
      shosti likes this.

    6. #24
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1523
      Likes Received
      1422
      Likes Given
      1828

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Quote By Preta
      anakukata stim muda huo huo
      yaani we acha tu mpendwa wangu....

    7. #25
      The Priest's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2010
      Location : Kimanzichana
      Posts : 989
      Rep Power : 625
      Likes Received
      186
      Likes Given
      155

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Ni kweli hlo tatizo lipo.

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Pat Gucci's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Location : Mbauda, Arusha, Tanzania
      Posts : 135
      Rep Power : 429
      Likes Received
      17
      Likes Given
      0

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Hilo nalo neno, Wanaume kama mabinti!

    10. #27
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,732
      Rep Power : 1366
      Likes Received
      280
      Likes Given
      142

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      mbona mimi kausauti kangu kembamba mchana lakini asubuhi ni bezi la kutisha

    11. #28
      Mamndenyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 11,886
      Rep Power : 31774
      Likes Received
      5869
      Likes Given
      19165

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Wababa fanyeni mazoezi ati, au mtaota manyonyo na mawowo ati manake ni gari - ofisi - gari - kitanda hapo utakosaje.

    12. #29
      MkimbizwaMbio's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Posts : 873
      Rep Power : 605
      Likes Received
      292
      Likes Given
      197

      Default re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Quote By shosti
      yaani we acha tu mpendwa wangu....
      Mbona na wewe una sauti nzito kama Mwanaume?
      Ulinikata stim muda uleule.
      We shall heal our wounds, collect our dead and continue fighting

    13. #30
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8046
      Likes Given
      26482

      Default Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto (gynecomastia)


      Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto limekuwa kubwa sana katika dunia ya leo. Inawezekana kabisa wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti makubwa ambapo watu wengi huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu gynecomastia ni kukuwa kuliko kawaida yake kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na wanaume waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.


      Ukubwa wa tatizo (epidemiology)
      Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo hili la kukuwa kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu kamatransient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.
      Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri wa kubaleghe imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na kuwepo kwa wingi kwa kimengenyo aina ya estradiol.Mara nyingi huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri ya zaidi ya miaka 17. Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa na tatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa kichocheo aina ya testerone kuwa estradiolna kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki cha testerone kutoka kwenye korodani zinazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testerone hutengenezwa katika korodani za mwanamume.

      Pathofiziolojia (Nini hutokea?)

      Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kamaestrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko(sensitivity) wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.Estrogen husababisha chembechembe zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi, kurefuka(ductal elongation) na kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta (ductal fibroblasts) na kuongezeka kwa mfumo wa damu kwenye matiti (increase vascularity).Estrogen hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya testerone naandrogen kwa kutumia kimengenyo kinachojulikana kama aromatase.


      Aina za gynecomastia
      •Puffy nipples – Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular tissue.
      •Pure glandular gynecomastia – Huonekana sana kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili (bodybuilders), kutokana na matumizi ya dawa za kujenga mwili (anabolic steroids) ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha kichocheo aina ya testerone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen. Kwa wanaume wembamba, tatizo hili hutokea kutokana na kuongezeka kwa breast tissue gland pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose tissue.
      Ni nani aliyekatika hatari ya kupata tatizo hili?
      •Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.
      •Wenye uzito uliopitiliza (Obesity)
      •Unywaji pombe kupindukia
      •Magonjwa sugu ya figo au ya Ini
      •Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.


      Visababishi vya kukuwa kwa matiti kwa wanaume


      •Pseudogynecomastia – Kuongezeka kwa tishu zinazozunguka chuchu za matiti na huambatana na kuwepo kwa wingi wa tishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye virutubisho sahihi huondosha tatizo hili.


      •Unilateral/asymetrical gynecomastia – Ni kuongezeka kwa titi moja pekee au la upande mmoja wa mwili wa mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. Titi la upande wa pili huwa kwenye umbile na saizi ya kawaida.Bilateral gynecomastia ni kuongezeka kwa matiti yote mawili.


      •Hypogonadism – Kutofanya kazi kwa korodani vizuri na kuwa ndogo. Hii husababishwa na magonjwa mbalimbali kama klinifelter'rs syndrome, pitituary insuffiency na nk.


      •Umri – Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili kutokana na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo cha testerone na kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza kwa wingi kwa kimengenyo aina ya estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya testerone. Pia mabadiliko ya mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.


      •Uzito uliopitiliza (Obesity) – Watu wenye uzito uliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen mwilini mwao na wakati huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya testerone.


      •Saratani – Baadhi ya saratani kama saratani ya kwenye korodani, kwenye tezi lililojuu ya figo (adrenal gland), saratani ya tezi la kichwa (pitituary tumor), huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa vichocheo kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).


      •Hyperthyroidism – Kukuwa kwa ukubwa wa tezi la koo (thyroid gland) na hivyo kutengeneza kwa wingi kichocheo aina yathyroxine.


      • Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi (Renal/Kidney failure) - Nusu ya wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa matiti kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance).


      •Matatizo ya Ini – Dawa za kutibu magonjwa ya kwenye Ini kama liver cirrhosis, liver failure husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana kwa uwiano sawa wa mfumo wa vichocheo mwilini.


      •Utapia mlo, ukame – Utapia mlo, ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa kichocheo aina ya testerone na kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa vichocheo mwilini. Hii hutokana na kukosekana kwa virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa mbalimbali pamoja na tatizo hili.


      •Madhara ya dawa za kurefusha maisha (Antiretroviral therapy) kwa wagonjwa wa ukimwi.

      •Utumiaji wa madawa ya kulevya kama bangi/marijuana.

      Vipimo vya Uchunguzi

      Vipimo hivi vitafanywa kulingana na historia ya mgonjwa, dalili na viashiria vya mgonjwa baada ya kupimwa na daktari.


      •Kipimo cha damu (Complete Blood Count) – Kuangalia wingi wake, aina mbalimbali za chembechembe za damu na uwepo wa maambukizi ya bakteria.


      •X-ray ya matiti (Mammogram) – Hutumiwa kuangalia tishu za kawaida na zile ambazo si za kawaida zilizo kwenye matiti. Husaidia kugundua uwepo wa saratani, cysts, na calcifications kwenye matiti.


      •Liver function test – Mjumuiko wa vipimo vya damu kuangalia aina mbalimbali za vichocheo na vimengenyo ili kuweza kutambua kama mgonjwa ana ugonjwa wowote ule wa Ini na chanzo chake, vipimo hivi huangalia albumin, Alanine transaminase (ALT), Aspartate transaminase (AST), Alkaline phosphatase (ALK), Total bilirubin (TBIL), Direct bilirubin (Conjugated Bilirubin), Gamma Glutamyl Transpeptidase (GGT), Lactate Dihydrogenase (LDH).


      •Tumor markers – Kipimo cha damu cha kuangalia viashiria vya saratani ya korodani kama AFP alpha feto 1 protein, Beta-HCG, LDH.

      •Kipimo cha damu cha kuangalia wingi wa kichocheo cha aina ya testerone (Total and Free Testerone) Hufanyika asubuhi ambapo kiwango cha testerone huwa juu. Kiwango cha kawaida cha kichocheo cha testerone ni 300 - 1000 ng/dl (Kiwango hiki hupungua kwa asilimia 13 wakati wa mchana).

      •Kipimo cha damu cha kuangalia vichocheo vinavyoonekana kwenye ugonjwa wa kukua ukubwa wa tezi la koo ( hyperthyroidism) kama kichocheo aina ya Thyroid Stimulating Hormone (TSH) ambacho huwa katika kiwango kidogo wakati wa kuugua ugonjwa wa hyperthyroidism, hutolewa na

      tezi la kwenye kichwa aina ya pitituary gland, vichocheo vyengine aina ya anti-TSH receptor antibodies (kwa wenye ugonjwa wa Grave’s disease), anti-thyroid – peroxidase (kwa wenye ugonjwa wa Hashimoto’s disease), na pia kuangalia wingi wa vichocheo aina ya T3 na T4. Kipimo cha

      Thyroid Scintigraphy
      pia huweza kutumiwa kutofautisha kati ya ugonjwa wa hyperthyroidism na ugonjwa wa thyroiditis. Kipimo hiki hutumia madini ya mionzi ya iodine (Iodine-131 ama Iodine-123).


      •Vipimo vya kuangalia kama figo zimeshindwa kufanya kazi vizuri kama;

      a)Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.
      b)Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)
      c)Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
      d)Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
      e)Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
      f)Renal biopsy.


      Tiba ya Gynecomastia


      Kama nilivyosema hapo awali, tatizo hili kwa vijana waliokatika umri mdogo au wa kubaleghe hupotea lenyewe taratibu ndani ya miezi 18. Kwa mzazi unatakiwa usihofu, lakini kama litaonekana kwa mtoto zaidi ya miaka 17, basi hapa mzazi unatakiwa kuchukua hatua za haraka ambazo ni kumuona daktari ili aweze kukusaidia kwa ufasaha zaidi.


      1.Tiba ya madawa

      •Tiba ya kutumia vichocheo (Testerone Replacement Therapy) – Kichocheo aina ya testerone hutolewa kwa mgonjwa kwa njia ya mdomoni, kwenye dripu, au kipachiko (patch forms). Hii hutolewa kwa wagonjwa ambao hawawezi kutoatesterone kutoka kwenye korodani zao kutokana na kupata ajali, ugonjwa au wale ambao hawana korodani kutokana na sababu mbalimbali.

      •Dawa aina ya Selective Estrogen Receptor Modulator (SERMs) kama Tamoxifen, raloxifen, husaidia kupunguza ukubwa(volume) wa matiti lakini haziondoi tishu zote kwa ujumla. Aina hii ya tiba hutumiwa kwa wale wenye tatizo sugu lagynecomastia au wale wenye kupata maumivu makali sana. Dawa hizi zina madhara na hivyo ni vizuri kutumia kwa maelekezo ya daktari.


      •Dawa aina ya Aromatase Inhibitors kama anastrozole, hufanya kazi kwa kuzuia kimengenyo aina ya aromatase na hivyo kuzuia utengenezwaji wa kichocheo aina ya estrogen. Tafiti nyingi zilizofanywa zimeshindwa kutoa majibu ya uhakika juu ya matumizi ya dawa hizi katika kutibu tatizo hili la kukuwa kwa matiti kwa wanaume.


      2.Tiba ya Upasuaji – Kwa wale wenye tatizo hili sugu, upasuaji wa kurekebisha matiti unaweza kufanyika. Hii humuongezea mwanamume hali ya kujiamini na hivyo kuwa katika hali nzuri kisaikolojia, na huongeza ufanisi wa maisha yake ya kila siku.

      3.Kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kula mlo wenye virutubisho vyote muhimu.
      4.Kutibu chanzo au magonjwa mbalimbali kama hyperthyroidism, ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi, saratani mbalimbali na nk.
      5.Kuacha kunywa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya kama bangi/marijuana.
      6.Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa baada ya kuona dalili za tatizo hili kwa wale wenye kutumia dawa za kutibu ugonjwa wa Ini, dawa za

      kurefusha maisha. Kwa wagonjwa wa Ukimwi, ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa mgonjwa dawa, kumfanyia mgonjwa kipimo cha fasting lipid profile, ili uweze kutambua kama dawa unazotaka kumpa zitamletea madhara au la. Na inashauriwa kurudia kipimo hiki kati ya miezi 3 hadi 6 baada ya

      kuanza dawa hizi za kurefusha maisha au baada ya kumbadilishia mgonjwa dawa. Hata hivyo sio dawa zote za kurefusha maisha zilizo na madhara haya, kwani zipo nyingine zinazopunguza kiwango cha mafuta mwilini na kwenye tishu.


      Madhara ya Gynecomastia


      1.Uwepo wa tatizo hili kwa muda wa zaidi ya miezi 12 au mwaka mmoja, husababisha matiti kutengeneza makovu au kwa kitaalamu scarring/fibrosis na hivyo kufanya tiba kwa kutumia dawa kuwa ngumu sana.

      2.Wanaume wenye tatizo hili wapo kwenye hatari zaidi ya mara tano ya kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wanaume ambao hawana tatizo hili.
      3.Kuathirika kisaikolojia (kuona aibu, kutojiamini, kujihisi tofauti na wanaume wenzake). Hali hii inaweza hata kumfanya mtu kuishi maisha ya huzuni au kushindwa kujumuika na watu katika shughuli mbalimbali kama michezo na nk.





      CHANZO: Tatizo la Kuota Matiti kwa Wanaume na Watoto (Gynecomastia)
      Hardman and CANCER like this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    14. #31
      The Priest's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2010
      Location : Kimanzichana
      Posts : 989
      Rep Power : 625
      Likes Received
      186
      Likes Given
      155

      Default Re: Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto (gynecomastia)

      Duh!hv surgery hapa bongo wanafanya?
      MziziMkavu likes this.

    15. #32
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,113
      Rep Power : 19194
      Likes Received
      8046
      Likes Given
      26482

      Default Re: Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto (gynecomastia)

      Quote By The Priest
      Duh!hv surgery hapa bongo wanafanya?
      Sijuwi ninafikiri wanafanya hiyo Surgery hapo bongo ,kwani mkuu The Priest unayo hayo matatizo ya kuota matiti?
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    16. #33
      Paxman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2010
      Location : MIT
      Posts : 1,067
      Rep Power : 1129
      Likes Received
      383
      Likes Given
      598

      Default Re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      Hivi sasa ukifanya hiyo surgery hisia za mapenzi zitakuwepo tena kweli?

    17. C6
      #34
      C6's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th April 2011
      Location : Mtaa Wa Saba
      Posts : 3,034
      Rep Power : 19350
      Likes Received
      1745
      Likes Given
      1500

      Default Re: Mwanaume kuwa na sauti nyembamba, kuota matiti, kuwa na mahips/wowowo yaliyotuna

      hiyo inaitwa gynacomastia, mara nyingi inatokana na matumizi ya dawa fulani fulani...

    18. #35
      Hardman's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th January 2011
      Posts : 113
      Rep Power : 446
      Likes Received
      15
      Likes Given
      8

      Default Re: Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto (gynecomastia)

      hongera kwa kuukata mzizi wa fitna

    19. Study Abroad
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    Similar Topics

    1. Na hii inawezekana kuwa sababu ya kuwa na matokeo mabaya alevel mwaka huu?
      By Mani H in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 5
      Last Post: 1st May 2011, 14:40
    2. Tetesi: Hizi kweli zinaweza kuwa kuwa dalili za mke msaliti katika ndoa?
      By Shada in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 13
      Last Post: 25th March 2011, 17:47
    3. Je unaweza kuota bila kuwa usingizini?
      By Mwanajamii in forum Jokes/Utani + Udaku/Gossips
      Replies: 4
      Last Post: 28th January 2011, 17:14
    4. Jee hii inaweza kuwa moja ya sababu ya kundi fulani kuwa mbele kitaaluma?
      By Gozigumu in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 17th May 2010, 12:41

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...