JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Pata elimu kuhusu ugonjwa wa kuota vinyama sehemu za siri (Bawasiri, Hemorrhoids)

  Report Post
  Page 1 of 31 123 11 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 620
  1. Kanyafu Nkanwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th July 2010
   Location : Kaporogwe Falls
   Posts : 758
   Rep Power : 703
   Likes Received
   52
   Likes Given
   61

   Default Pata elimu kuhusu ugonjwa wa kuota vinyama sehemu za siri (Bawasiri, Hemorrhoids)

   Mara ya kwanza kuregister na nimeanza kimatatizo.

   Mwana JF mwenzenu kwa kipindi cha miezi kama miwili hivi, nimekuwa nikipata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa. Maumivu haya yanakuja nikiwa na choo kigumu au chepesi.

   Huwa ni maumivu kama kuna kitu kinakwanguliwa au kuna kidonda hivi. Lakini pindi nikimaliza haja kubwa sisikii tena na wala sihisi kama kuna maumivu!

   Hivi karibuni nilipata vurugu tumboni baada ya food poisoning, ile combination ya maumivu kwa kweli hailezeki. sehemu inayouma ni kwenye outlet (anus) pale pale na si kwingine.

   Maana ningekuwa nayasikia hata kwente rectum ningeweza sema, ila ni juu kabisa wakati wa defacation.

   Nilikwenda mwona Doctor, yeye aliniandikia flagyls ambazo nilizinywa wala sijapata nafuu. Alihisi kuna infection au inflammation. Sasa niko njia panda, nifanyeje? Sijui hata huko hospital nielezeje hasa hali yangu?!

   Naomba mawazo pa kuanzia. Asanteni.

   ========= Majibu========

   Quote By MziziMkavu View Post
   BAWASIRI (HEMORRHOIDS)

   Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

   Kuna aina mbili za Bawasiri

   Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

   Ndani
   : Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
   Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
   Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
   Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
   Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
   Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

   Je bawasiri husababishwa na nini?

   Bawasiri husababishwa na;

   • Tatizo sugu la kuharisha
   • Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
   • Ujauzito
   • Uzito kupita kiasi (obesity)
   • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
   • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
   • Umri mkubwa

   Dalili za bawasiri

   • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
   • Maumivu au usumbufu
   • Kinyesi kuvuja
   • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
   • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
   • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

   Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

   • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
   • Strangulated hemorrhoids

   Vipimo na uchunguzi   • Digital rectal examination
   • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
   • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

   Matibabu
   Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

   • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
   • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
   • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
   • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy   Njia za kuzuia Bawasiri

   • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
   • Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
   • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.   Kutibu kwa kutumia njia Mbadala Maradhi ya BAWASIRI:

   Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

   TIBA 1:
   MAKAL-ARZAK

   Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).

   Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.

   Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

   MWIKO
   : Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.

   TIBA 2:

   Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

   TIBA 3:

   Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.
   Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au “castor oil”. Mkuu.@
   gedoTumia kisha unipe Feedback.

  2. KiparaDar's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th March 2007
   Posts : 36
   Rep Power : 735
   Likes Received
   1
   Likes Given
   1

   Default Re: Matatizo ya Bawasir

   ugonjwa uliotapakaa sana kwa wanaume wengi ktk nchi zetu za kitropiki,hali ya hewa,joto jingi,kutokunywa maji kwa wingi,choo kigumu nakujikamua sana,mwisho bawasir,kuna sababu nyingine,kurithi ugonjwa etc,stages tofauti,inaweza kutibika ama kwa vidonge au ikiwa kubwa opersheni ni lazima.

  3. Mfumwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th August 2008
   Posts : 1,470
   Rep Power : 946
   Likes Received
   19
   Likes Given
   1

   Default Re: Matatizo ya Bawasir

   Quote By Zakayo View Post
   Nataka kujua hivi ni nini kinachosababisha bawasir au haemorhoids kwenye njia ya haja kubwa?
   Kwanza "Hemorrhoids" ama "Piles" husababishwa zaidi na mtu anapotumia nguvu kupata haja kubwa (naomba mnisamehe kama lugha si nzuri), ina maana kama unapata choo kigumu, msukumo huwa mkubwa na kutokea mkwaruzo na kusababisha veins kuvimba. Kukosa choo (constipation), mimba na umri mkubwa pia husababisha hii kitu, hasa kuanzia miaka 50. Pia kuingiliwa kinyume na maumbile husababisha. Pia leo ndio nimejua hii kitu kiswahili inaitwa Bawasir.

   Ziko aina ngapi ya bawasir?.
   Kwa kungalia uvimbe uliko, ziko za aina mbili, zinazotokea nje ama chini ya ngozi ya sehemu ya haja kubwa, na kuna zinazotokea ndani ya sehemu ya haja kubwa.

   Je inatibika bila ya operation?
   Yaweza kutibika bila kufanyiwa upasuaji, muhimu ni kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha nyuzinyuzi (fiber). Pia kunywa maji mengi. Hii inasaidia kukifanya choo kiwe laini na hivyo kupunguza msuguano na pia kupunguza msukumo wakati wa kutoa haja kubwa. Pia inatakiwa unapojisikia tu haja kubwa ukajisaidie, sio kuahirisha nayo ina madhara makubwa. Kuna dawa unaweza pewa, siwezi kukutajia hapa, zinasaidia na kumaliza kabisa wakati fulani.

   Wanawake nao huwa wanaupata ugonjwa huu?
   Ni ugonjwa unaotokea kwa jinsia zote.

   Kwa nini baada ya kumaliza haja kubwa huanza kuwasha na kuwa kero?
   Sana sana ukiona inawasha, huwa ni zile vimbe za nje, vimbe za ndani huwa hazina matatizo sana, kama muwasho. Lakini kwanini huwasha baada ya haja?, ni kwamba baada ya haja ile sehemu huwa imesuguliwa ama wakati unasukuma unachokoza zile vimbe katika veins.

   Na kwa nini wakati mwingine huwa haitokei? Has it to do with type of foods/drinks?
   Hii kitu inaweza kutokea, ikapotea kwa siku, wiki, miezi, mwaka, miaka na kurudi tena. Hivyo ni vizuri kubadili aina za vyakula na kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi, muhimu zaidi ni kunywa maji mengi iwezekanavyo.

   Pia kupunguza vyakula vyenye pilipili na binzari (hot and spicy foods) inaweza kusaidia.

   Muhimu: Ni vizuri kwenda hospitali ili upate kuchunguzwa zaidi.
   Maundumula and Code like this.

  4. #4
   Sipo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th July 2008
   Location : SIPAJUI
   Posts : 2,167
   Rep Power : 1090
   Likes Received
   22
   Likes Given
   0

   Default Re: Matatizo ya Bawasir

   Asante mtoa mada na zaidi asante bra Mfumwa kwa elimu uliyotoa,
   "Ficha Upumbavu wako, husifiche hekima yako'' Invisible

  5. Freetown's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2008
   Location : Tsim Sha Tsui
   Posts : 890
   Rep Power : 851
   Likes Received
   49
   Likes Given
   232

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Pole ndugu, unasumbuliwa na ugonjwa unaitwa "Hemorrhoid" jaribu kuingia kwenye internet utapata kuujua zaidi na namna ya kuutibu
   You can be whatever you make up your mind to be. What's in your mind is all that counts

  6. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 35,455
   Rep Power : 429504150
   Likes Received
   21393
   Likes Given
   66313

   Thumbs up re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Kutafuta njia ya Cure Hemorrhoids?

   Maelfu ya watu kutafuta njia ya tiba hemorrhoids, ingawa ni aibu pia kipaji kuuliza daktari wao. Baada ya yote, dhana ya kuwa na familia yako na daktari poke prod "chini kuna" ni wa kutosha kuwafanya shudder. Hivyo wengi kwenda katika kutafuta dawa nyumbani hemorrhoids ambayo kuwapa unafuu Wanahitaji katika siri ya nyumba zao wenyewe.

   Zaidi ya dawa kwa hemorrhoids kwamba kuona kwenye TV ni kutumika kutibu dalili tu, na sio tiba yao. Hii ni kwa nini watu wengi kutafuta dawa ambayo tiba yake badala ya relieving tu ya Ikiwachwa, moto, na kwamba wao kusababisha maumivu.

   Hemorrhoids ni pia hujulikana piles "" muda misimu ambayo inahusu kuonekana unsettling ya advanced hemorrhoids Ni kuangalia kama mwili piled juu ya mwili. Kwa hiyo dawa ya piles itakuwa kitu Same kama tiba ya hemorrhoids. Nilidhani I'd kutupa tidbit katika pale ili usipate kuchanganyikiwa wakati kutafuta jibu la tatizo lako chungu.

   Watu wengi kutafuta om korrigerande åtgärder yao nyumbani kwa hemorrhoids badala ya kuruka haki katika upasuaji. Baadhi ya sababu ni uwezo wao ama hawezi au tu wala 'wanataka upasuaji au matibabu Je, hupendelea zaidi ya asili badala ya boriti laser Kulenga saa nyuma yao.

   Hemorrhoids kutafuta dawa ya kuokoa nyumba Maelfu Njia ya dola katika bili ya matibabu. Hata kwa bima ya afya, mara tu takwimu katika deductible na asilimia 20 ya kawaida na subira ina kulipa, wewe ni kuangalia muswada sizable. Na kama huna bima ya afya, kusahau kuhusu hilo. Kama wewe ni kama watu wengi hemorrhoids utapata dawa ambazo zitakusaidia kuishi na hemorrhoids yako na kuweka kwenye mfuko wako pesa yako.

   Unaweza kutibu hemorrhoids na dawa leo. na ni Pia Uwezekano wa kufanya hivyo kwa dawa Home ambayo inaweza Urahisi Found kwenye wavuti. Unaweza kupata unafuu wa kudumu kutoka hemorrhoids bila kutumia tani ya fedha na bila aibu ya. Pamoja nanyi na kwamba taarifa aibu katika faili yako ya matibabu. Unaweza kupata matibabu kwa hemorrhoids yako kutoka kwa faraja ya nyumba yako mwenyewe.

   tarehe ya kuanza kwa njia yako ya kutibu hemorrhoids wako kwa ajili ya mema, wala kuishi pamoja na maumivu tena. Je, kuendelea kutumia dawa za juu-ya kukabiliana na kwamba kwa kufanya kazi. Kufanya utafiti wako dawa ya nyumbani na kuanza maisha maumivu bure.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  7. Kanyafu Nkanwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th July 2010
   Location : Kaporogwe Falls
   Posts : 758
   Rep Power : 703
   Likes Received
   52
   Likes Given
   61

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Mtimkavu, nashukuru kwa message. Ila lugha uliyotumia hapa ni ya kidaktari? Au ndiyo shorthand? kwa kweli nimeungaunga tu na wala sijaelewa kabisa. Can you come back again in summaried simple information? Thank you in advance.

  8. Abdulhalim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th July 2007
   Location : 67P
   Posts : 16,976
   Rep Power : 85903738
   Likes Received
   1741
   Likes Given
   795

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By kanyafu nkanwa View Post

   Muungwana cha msingi procure huduma za daktari wa kueleweka mwenye caliber ya kujua anachofanya. Kuendelea kusubiria majibu ya copy & paste yaliyotafsiriwa na google za akina Mzizimkavu utapoteza muda wako.
   ..."Dullah One, muzee ya triple distilled" ...

  9. Bawa mwamba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th March 2010
   Posts : 354
   Rep Power : 641
   Likes Received
   27
   Likes Given
   67

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   You are a courageous man/woman Most people dont talk about such issues to public,.....
   Hata hivyo tukianza kutoa maswali elekevu wakati mwingine yanasound Rather peculiar ,...au unaweza kujiona abused psychologically,...Cha kufanya kama uko abroad Nenda kamuone Daktari anayeitwa Proctologist,...au endoscopist,...

   Kama upo bongo basi nenda kamuone surgeon na ukifika mwambie ukweli na uombe kipimo cha Endoscopy AU proctoscopy kwanza ,..halafu baadaye utayapata majibu
   ANYWAY KABIBU JFFFFFFFFF,..........Tunasubir i post zako siku zijazo

  10. Mwanamayu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th May 2010
   Location : Manzese
   Posts : 4,325
   Rep Power : 1429
   Likes Received
   643
   Likes Given
   296

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By Bawa mwamba View Post

   Tumia kipimo alichosema Bawa.

  11. Mwanamayu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th May 2010
   Location : Manzese
   Posts : 4,325
   Rep Power : 1429
   Likes Received
   643
   Likes Given
   296

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Je, tatizo ili limekupata baada ya kuwa na 'loose motion' yaani kuendesha? Kama ndiyo, loose motion uleta michubuko kwenye rim ya njia ya haja kubwa, choo kigumu pia uleta michubuko; hivyo basi jisafishe kila baada ya kutumia choo kwa maji safi, fanya 'sit-bath (sitting in the warm water in the water dish/ basin for at least five minutes twice a day after a shower - don't mix that water with dettol)', kula matunda hasa mapapai, mboga za majani na mikate aina ya 'brown', pia usiache kunywa maji ya kutosha kila siku, halafu anagalia baada ya wiki hivi kama bado inaendelea muone Dk na uombe kipimo cha 'endoscopy' kitaonyesha kila kitu kunanzia kwenye rim ya njia ya haja kubwa mpaka kwenye mlango wa tumbo - hapo utapata majibu ya uhakika kama ni hemorrhoids au minyoo au fissures nk.

  12. Fredwash's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th October 2009
   Posts : 443
   Rep Power : 684
   Likes Received
   42
   Likes Given
   136

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By MziziMkavu View Post
   Kutafuta njia ya Cure Hemorrhoids?
   Maelfu ya watu kutafuta njia ya tiba hemorrhoids, ingawa ni aibu pia kipaji kuuliza daktari wao. Baada ya yote, dhana ya kuwa na familia yako na daktari poke prod "chini kuna" ni wa kutosha kuwafanya shudder. Hivyo wengi kwenda katika kutafuta dawa nyumbani hemorrhoids ambayo kuwapa unafuu Wanahitaji katika siri ya nyumba zao wenyewe.

   Zaidi ya dawa kwa hemorrhoids kwamba kuona kwenye TV ni kutumika kutibu dalili tu, na sio tiba yao. Hii ni kwa nini watu wengi kutafuta dawa ambayo tiba yake badala ya relieving tu ya Ikiwachwa, moto, na kwamba wao kusababisha maumivu.

   Hemorrhoids ni pia hujulikana piles "" muda misimu ambayo inahusu kuonekana unsettling ya advanced hemorrhoids Ni kuangalia kama mwili piled juu ya mwili. Kwa hiyo dawa ya piles itakuwa kitu Same kama tiba ya hemorrhoids. Nilidhani I'd kutupa tidbit katika pale ili usipate kuchanganyikiwa wakati kutafuta jibu la tatizo lako chungu.

   Watu wengi kutafuta om korrigerande åtgärder yao nyumbani kwa hemorrhoids badala ya kuruka haki katika upasuaji. Baadhi ya sababu ni uwezo wao ama hawezi au tu wala 'wanataka upasuaji au matibabu Je, hupendelea zaidi ya asili badala ya boriti laser Kulenga saa nyuma yao.

   Hemorrhoids kutafuta dawa ya kuokoa nyumba Maelfu Njia ya dola katika bili ya matibabu. Hata kwa bima ya afya, mara tu takwimu katika deductible na asilimia 20 ya kawaida na subira ina kulipa, wewe ni kuangalia muswada sizable. Na kama huna bima ya afya, kusahau kuhusu hilo. Kama wewe ni kama watu wengi hemorrhoids utapata dawa ambazo zitakusaidia kuishi na hemorrhoids yako na kuweka kwenye mfuko wako pesa yako.

   Unaweza kutibu hemorrhoids na dawa leo. na ni Pia Uwezekano wa kufanya hivyo kwa dawa Home ambayo inaweza Urahisi Found kwenye wavuti. Unaweza kupata unafuu wa kudumu kutoka hemorrhoids bila kutumia tani ya fedha na bila aibu ya. Pamoja nanyi na kwamba taarifa aibu katika faili yako ya matibabu. Unaweza kupata matibabu kwa hemorrhoids yako kutoka kwa faraja ya nyumba yako mwenyewe.

   tarehe ya kuanza kwa njia yako ya kutibu hemorrhoids wako kwa ajili ya mema, wala kuishi pamoja na maumivu tena. Je, kuendelea kutumia dawa za juu-ya kukabiliana na kwamba kwa kufanya kazi. Kufanya utafiti wako dawa ya nyumbani na kuanza maisha maumivu bure.

   KAKA naomba usitumie hiyo translator kweli imetuchanganya... jaribu kuisummarize au ipost katika lugha ya kingereza walau tunaweza kuambulia ila hiyo translator inaharibu.

  13. Kanyafu Nkanwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th July 2010
   Location : Kaporogwe Falls
   Posts : 758
   Rep Power : 703
   Likes Received
   52
   Likes Given
   61

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By Abdulhalim View Post
   Muungwana cha msingi procure huduma za daktari wa kueleweka mwenye caliber ya kujua anachofanya. Kuendelea kusubiria majibu ya copy & paste yaliyotafsiriwa na google za akina Mzizimkavu utapoteza muda wako.
   Nakubalia nawe Abdulhalim. Ila kumbuka kuwa nimeshaenda hospital already kwa daktari mzuri sana lakini si bingwa. Nikapewa flagyls ambazo hazijasaidia. hapa JF kuna mabingwa wengi tu ambao wanaweza kutoa ushauri appropriately wa namna ya ku-approach hii issue. Kwa mfano, kuna mtu kaniambia jaribu Endoscopy AU proctoscopy. Saa hii nisingeweza fikiria hata siku moja kwani sijui. Then kutokana na ushauri wao na mimi pia nachanganya na za kwangu then naamua.

  14. Mokoyo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd March 2010
   Location : KILIMO KWANZA
   Posts : 10,618
   Rep Power : 9546714
   Likes Received
   2667
   Likes Given
   2245

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Pole sana mgeni wetu kwa kuumwa na hayo maumivu makali

   Sasa kama umefuatilia vizuri niliwahi kuleta mada kama hii kuhusiana na tatizo la mshikaji wangu. Kupitia hapa JF alipata ushauri na alielekezwa kwenda zahanati moja ipo maeneo ya Banana eneo linaloitwa Bonanza ambayo wanatumia dawa za mitishamba. Jamaa yangu huyo kwasasa aanaendelea na matibabu na kuna maendeleo makubwa sana tofauti na mwanzoni. Jitahidi kufuatilia tiba hii nawe kama vipi. Jina la hospitali yenyewe silikumbuki ila nitamuuliza mshikaji na nitalipoti hapa
   Opportunities favor those who have prepared well..........

  15. Rubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2009
   Posts : 1,602
   Rep Power : 915
   Likes Received
   246
   Likes Given
   197

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   jaribu pia kuacha kula vyakula vya nafaka zilizokobolewa yaani kila siku badala yake ongeza kula nafaka ambazo hazijakobolewa, maji kwa wingi, matunda na pia tumia Juisi ya Ukwaju nzito glass mbili mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu utaona mabadiliko.
   Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

  16. Bawa mwamba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th March 2010
   Posts : 354
   Rep Power : 641
   Likes Received
   27
   Likes Given
   67

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By CKABULA View Post
   jaribu pia kuacha kula vyakula vya nafaka zilizokobolewa yaani kila siku badala yake ongeza kula nafaka ambazo hazijakobolewa, maji kwa wingi, matunda na pia tumia Juisi ya Ukwaju nzito glass mbili mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu utaona mabadiliko.
   SCABULA UNAMSHAURI MSHIKAJI KUHUSU UKWAJU,,..MATE YAMENITOKA,..huku hamna mzeee,,..namiss na ubuyu pia,..du bora nikanywe bia,...ina uchachu,...mzee

  17. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 35,455
   Rep Power : 429504150
   Likes Received
   21393
   Likes Given
   66313

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By Abdulhalim View Post
   Muungwana cha msingi procure huduma za daktari wa kueleweka mwenye caliber ya kujua anachofanya. Kuendelea kusubiria majibu ya copy & paste yaliyotafsiriwa na google za akina Mzizimkavu utapoteza muda wako.
   Unaona wivu akitaka ushauri wangu? wewe Abdulhalim unaleta ubishi hata huku?
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  18. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 35,455
   Rep Power : 429504150
   Likes Received
   21393
   Likes Given
   66313

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By kanyafu nkanwa View Post
   Mtimkavu, nashukuru kwa message. Ila lugha uliyotumia hapa ni ya kidaktari? Au ndiyo shorthand? kwa kweli nimeungaunga tu na wala sijaelewa kabisa. Can you come back again in summaried simple information? Thank you in advance.
   Kinachotakiwa uende kwa doctor Mtaalamu wa haya Maradhi ya Hemorrhoids akufanyie Uchunguzi na hata ikiwezekana ufanyiwe Operation ndogo kwa kuikata hicho kinyama kilichotoka sehemu yako ya siri. Huo ndio ni ushauri wangu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  19. Abdulhalim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th July 2007
   Location : 67P
   Posts : 16,976
   Rep Power : 85903738
   Likes Received
   1741
   Likes Given
   795

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By MziziMkavu View Post
   Unaona wivu akitaka ushauri wangu? wewe Abdulhalim unaleta ubishi hata huku?
   Wewe ni mngoni au mtu wa Kigoma nini? lol

   Yaani unaweka post ya google translator ambayo hata sentensi moja haileti mantiki halaf ukiambiwa unaanza kubisha na kuleta visingizio !
   ..."Dullah One, muzee ya triple distilled" ...

  20. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 35,455
   Rep Power : 429504150
   Likes Received
   21393
   Likes Given
   66313

   Default re: Kupata maumivu makali wakati wa haja kubwa

   Quote By Abdulhalim View Post
   Wewe ni mngoni au mtu wa Kigoma nini? lol

   Yaani unaweka post ya google translator ambayo hata sentensi moja haileti mantiki halaf ukiambiwa unaanza kubisha na kuleta visingizio !
   Naona wewe utakuwa ni Mzanzibar tena mtu wa CUF kama ni Mtu wa Bara utakuwa ni Mchaga wewe. kila Mahali upo tulia Mkuu
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment....(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')

  Page 1 of 31 123 11 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 5
   Last Post: 28th April 2014, 11:29
  2. Bawasiri/ kuota vinyama sehemu ya haja kubwa
   By adata5 in forum JF Doctor
   Replies: 2
   Last Post: 8th January 2014, 02:53
  3. Replies: 12
   Last Post: 29th December 2012, 13:49
  4. Replies: 2
   Last Post: 10th November 2012, 17:18
  5. Replies: 6
   Last Post: 2nd December 2011, 15:18

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...