JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

  Report Post
  Page 1 of 7 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 122
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 29,414
   Rep Power : 19293254
   Likes Received
   16179
   Likes Given
   51109

   Thumbs down Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

   Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

   Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

   MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
   Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

   NINI HUSABABISHA TATIZO?
   Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

   NINI KIFANYIKE?
   Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda ******. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

   Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.


  2. Bongemzito's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 162
   Rep Power : 512
   Likes Received
   9
   Likes Given
   1

   Default Kukosa choo

   Nisaidieni dawa ya kuniwezesha kupata choo cha kawaida, maana ni miaka sasa imepita nimekuwa na hili tatizo la kuwa na choo kigumu kiasi kwamba nasikia haja kubwa na nikienda toilet kujisaidia napata taabu sana..

   Nilienda hospitali kumuona daktari akanipatia dawa nikazitumia na zilinisaidia sana na akaniambia ninywe sana maji na kwa kweli sasa ivi nakunywa sana maji...

   Nikikaa baada ya mda ilo tatizo huwa linanirudia nikinywa dawa huwa linaisha mimi ni mtu wa kunywa dawa....

   Imefikia hatua kale kanyama kwenye haja kubwa kametokeza kwa sababu ya kupata taabu wakati wa haja..

   Nisaidieni wanajamii wenzangu jinsi ya kuepukana na hili tatizo maana limekuwa kama ni sehemu ya maisha yangu naona kama litakuja kuniletea madhara makubwa mno...
   MziziMkavu likes this.

  3. Deck Joel's Avatar
   Member Array
   Join Date : 14th April 2010
   Posts : 32
   Rep Power : 516
   Likes Received
   2
   Likes Given
   22

   Default Re: Kukosa choo

   Pole sana mkuu, bila shaka hapa kuna wataalam watakusaidia.
   MziziMkavu likes this.
   "KUMCHA MUNGU NI KUEPUKA UOVU"

  4. Brandon's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th October 2010
   Posts : 336
   Rep Power : 551
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By deck joel View Post
   pole sana mkuu, bila shaka hapa kuna wataalam watakusaidia.
   pole sana. Jitahidi unywe juisi ya ukwaju mara tatu kwa siku glass moja.
   MziziMkavu likes this.

  5. #5
   Rubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2009
   Posts : 1,545
   Rep Power : 846
   Likes Received
   226
   Likes Given
   188

   Default Re: Kukosa choo

   he kama na kanyama kameisha anza kutoka ni hatari jiandae kufanyiwa oparesheni za mar kwa mara. huo ugonjwa unaitwa ugonjwa wa kuganda kwa choo (Hemoroids) kama sijakosea mimi sio dk. ila nina ufahamu kidogo kwa tatizo lako. mambo ambayo yamepelekea upatwe na tatizo hilo ni pamoja na
   1. kula sana vyakula vya nafaka vilivyokobolewa bila other vitamins zipatikanazo kwenye matunda na mbogamboga.
   2. kutokupenda kunywa maji mengi i.e bilauli nane kwa siku.
   3. kupendelea kula sana vyakula vya nyamanyama hasa nyekundu. na pengine kula bila mtiririko yaani masaa maalumu ya kula na pia kula usiku sana saa 3 usiku, nne .... na mengineyo ambayo wataalamu wanayajua.

   hali hiyo imekupelekea mfumo wa usagaji chakula tumboni mwako kutokuwa mzuri na mara nyingi kuwa na gesi tumboni, kutokujisikia kula kwa kujua umeshiba, kufunga choo na ukienda kigumu ka cha mbuzi. na matatizo mengi yatokanayo. na hizo dawa u nazotumia zinakupa nafuu lakini kutumia dawa kwa kila mara sumu zinazidi kulundikana mwilini kwa sababu kufunga choo maana yake uchafu hautoki nje unabaki ndani.

   Cha kufanya jaribu kubadili mwenendo wa maisha yako kwa kujaribu haya.
   1. Pendelea kula vyakula visivyo kobolewa kama ngano na ugali wa dona au uji wa dona.
   2. Katika maisha yako yote duniani kila siku jitahidi kunywa maji safi na salama bilauli zisizopungu nane au kumi na mbili kwa siku kutokana na muda wa utazigawa katika masaa ambayo ni muafaka kwako.
   3. kula matunda kwa wingi kama mapapai, mananasi, embe n.k pia mboga za majani kwa wingi zingatia uandaaji wa mboga za majani kwa afya na virutubisho katika mwili.

   4. Jitahidi kula chakula cha usiku mapema iwezekanavyo tena kisiwe kigumu sana.

   5. Kwa kuanza kujitibu mwenyewe nyumbani tumia Juis ya ukwaju glass mbili mara tatu kwa siku angalau kwa siku tatu mpaka tano mfululizo. jinsi ya kutengeneza chukua ukwaju kg 1 loweka katika maji ya moto uliyochemsha mikono yako ikiwa safi fikicha huo ukwaju upate juis nzito kisha changanya na asali mbichi (glass 1 kijiko kimoja cha asali kikubwa) kisha tumia hiyo juis yake. Kama una vidonda vya tumbo pengine ukwaju hutauweza jaribu kuchemsha bamia bila kuziunga pengine weka chunvi kidogo kwa ajili ya ladha kisha saga kwenye blenda unywe.

   6. Punguza kula mikate mikate na maandazi ya kwenye bekari ukiweza tengeneza mwenyewe vifungua kinywa kama viazi mchemsho mihogo n.k.

   7. Punguza mafuta mengi kwenye vyakula unavyokula hasa nyama na na mafuta unayotumia yawe yale ya mimea. Nafikiri ukifuata ushauri utaona mabadiliko ingawa sijamaliza yote ilahaya ni ya muhimu.

   Pia kuna thread humu ilikuwepo ya mtu mwenye tatizo kama lako jaribu kuitafuta utaona ushauri mwingi uliotolewa wenye faida.
   Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

  6. JF SMS Swahili

  7. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 29,414
   Rep Power : 19293254
   Likes Received
   16179
   Likes Given
   51109

   Thumbs up Re: Kukosa choo

   UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

   Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

   Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

   Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

   Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

   MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

   Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

   Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

   NINI HUSABABISHA TATIZO?

   Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

   NINI KIFANYIKE?

   Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

   Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

   Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

   Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

   Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  8. Bongemzito's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 162
   Rep Power : 512
   Likes Received
   9
   Likes Given
   1

   Default Re: Kukosa choo

   Nashukuru mno mkuu kwa ushauri wako nimekuelewa sana,juisi ya ukwaju nilikuwa siipendi ila sasa ntaanza kuinywa

  9. Andrew Nyerere's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th November 2008
   Posts : 1,592
   Rep Power : 2255
   Likes Received
   476
   Likes Given
   0

   Default Re: Kukosa choo

   Hii ni ''constipation'',na constipation ndiyo chanzo cha magonjwa yote duniani.

   Daktari atakueleza ufanye nini. Tatizo ni maji tu. Kunywa maji ya kutosha kusaidia peristalisis. Ukikaa muda mrefu sana,hii pia inaongeza constipation. Kama kazi yako ni kazi katika desk,basi uwe mwangalifu,na ufahamu unahitaji kufanya marekebisho baadaye.

   Usinywe uji wa aina yoyote. Sijui kwa nini hyo mtu anakushari kunywa uji. Hiyo itakuongezea tu constipation. Kunywa ukwaju,hii ni bitter drink. Ukwaju,ndimu,limau,vitu kama hivi vitasaidia vipi? Labda kama short-term solution,unatumia hii acidic diet kusaidia digestion.

   Kula vyakula laini,kama ugali lazima upikwe kiaina,uwe laini. Kama ukienda South Africa,utaona katika magenge yao ya chakula wanapika ugali laini kuliko wanavyopika hapa Tanzania.

   You must be alert. Kama unaanza kuona dalili za constipation,nenda kafanye jogging. Kwa sababu ukichelewa sana,it may be too late.
   MziziMkavu and utaifakwanza like this.

  10. Nanren's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th May 2009
   Posts : 1,287
   Rep Power : 815
   Likes Received
   446
   Likes Given
   598

   Default Re: Kukosa choo

   Hiyo ni Constipation ndugu yangu.
   Kikubwa ni kuwa unahitaji chakula chenye "dietary fibers" kama vila Dona, mboga za majani na matunda. Fanya utaratibu wa kupata matunda na mboga za majani kila siku pamoja na kunywa maji mengi. Punguza kula nyama na badala yake pendelea protein za kutoka kwenye mimea kama vile soya, mbaazi, maharage, choroko, njegere. Jaribu hivi kwa muda wa wiki mbili, utaanza kuona mabadiliko chanya. Kama hutapata mabadiliko, basi, constipation yako inahitaji utalaam zaidi.
   MziziMkavu likes this.

  11. Zipuwawa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th November 2010
   Posts : 2,849
   Rep Power : 25892
   Likes Received
   482
   Likes Given
   268

   Default Re: Kukosa choo

   Pole sana ndg yangu hata mimi nimejifunza mengi sana humu kwani hata kama sijui sasa nimejifunza na nitajitahizi......

   Tatizo lako kweli ni hatari na linawakumba wengi sana. Mimi mwenyewe sipendi kabisa kunywa maji naweza kaa hata siku 3 bila kunywa maji na kuhusu mboga za majani ndio sipendi kabisa hivyo kabla sijaingia katika dozi hizo bora nianze kuepukana na hatari hiyo.
   MziziMkavu likes this.

  12. YeshuaHaMelech's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th October 2010
   Posts : 2,630
   Rep Power : 1010
   Likes Received
   27
   Likes Given
   0

   Default Re: Kukosa choo

   Mpenzi wa Nyama Choma/Kukaanga?
   Punguza matumizi hayo hasa kama chakula kikuu. Ongeza kula maembe, mapapai na Avocado
   Ongeza kunywa maji hasa baada na kabla ya kula.
   MziziMkavu likes this.
   "For the Lord himself shall descend from heaven with a shout, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first, then we which are alive and remain shall be caught up together with them in the clouds, to meet the Lord in the air: and so shall we ever be with the Lord" (1Th 4:16-17)
   Even so, come Lord Jesus!

  13. kipipili's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th July 2009
   Posts : 1,332
   Rep Power : 813
   Likes Received
   82
   Likes Given
   19

   Default Re: Kukosa choo

   Quote By Bongemzito View Post
   Nisaidieni dawa ya kuniwezesha kupata choo cha kawaida,maana ni miaka sasa imepita nimekuwa na hili tatizo la kuwa na choo kigumu kiasi kwamba nasikia haja kubwa na nikienda ****** kujisaidia napata taabu sana..

   Nilienda hospitali kumuona daktari akanipatia dawa nikazitumia na zilinisaidia sana na akaniambia ninywe sana maji na kwa kweli sasa ivi nakunywa sana maji...

   Nikikaa baada ya mda ilo tatizo huwa linanirudia nikinywa dawa huwa linaisha mimi ni mtu wa kunywa dawa....

   Imefikia hatua kale kanyama kwenye haja kubwa kametokeza kwa sababu ya kupata taabu wakati wa haja..

   Nisaidieni wanajamii wenzangu jinsi ya kuepukana na hili tatizo maana limekuwa kama ni sehemu ya maisha yangu naona kama litakuja kuniletea madhara makubwa mno...
   ahahahahahah ndiyo maana umekuwa bonge, kun.ia huwezi.
   kwenye bold hiyo ni ndyamgongo
   "Annuntio vobis gaudium magnum... habemus papam!" - "I announce to you a great joy... we have a pope!"

  14. mwanaWaafrika's Avatar
   Member Array
   Join Date : 12th December 2010
   Posts : 26
   Rep Power : 480
   Likes Received
   2
   Likes Given
   2

   Thumbs down Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu

   nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?

  15. pmwasyoke's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th May 2010
   Location : Dar es Salaam
   Posts : 3,008
   Rep Power : 1129
   Likes Received
   501
   Likes Given
   552

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   Baadhi ya mambo yawezayo kukusaidia ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara, kunywa maji mengi, kula vyakula vyenye roughage mfano mboga za majani nk. Hayo yasipokusaidia nenda hospitali.

  16. masssaiboi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th February 2009
   Posts : 493
   Rep Power : 669
   Likes Received
   52
   Likes Given
   21

   Default

   Quote By mwanaWaafrika View Post
   nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?
   Kunywa juice ya ukwaju
   MziziMkavu and utaifakwanza like this.

  17. Saint Ivuga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2008
   Posts : 21,652
   Rep Power : 2900447
   Likes Received
   6016
   Likes Given
   12831

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   piga mapapai mengi sana
   MziziMkavu likes this.
   JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

  18. 2c2's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th November 2009
   Posts : 98
   Rep Power : 551
   Likes Received
   5
   Likes Given
   3

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   sna ushaidi wa ki science ila mahindi ya kuchoma malaini niliambiwa ni dawa safi sana na nilipotumia mkuu The results was Good
   MziziMkavu likes this.

  19. Mupirocin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th January 2011
   Location : Tanzania
   Posts : 1,584
   Rep Power : 856
   Likes Received
   543
   Likes Given
   418

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   Kunywa maji glas 2 asubuhi wakati wa kuamka, nusu saa kabla ya meal kunywa glas 1, kabla ya kwenda kuoga kunywa glas 1, kabla ya kulala kunywa glas 1. Hii inasaidia kusafisha digestive system na kukinga dhidi ya heart diseases. Pia kula vyakula vyenye lougheges kama alivyochangia mdau hapo juu. Ikiambatana na tumbo kuuma, kutapika na kuto jamba kabisa nenda hospitali yawezekana ikawa intestinal obstruction. Pole
   MziziMkavu likes this.

  20. Kang's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th June 2008
   Posts : 3,827
   Rep Power : 1464
   Likes Received
   647
   Likes Given
   26

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   Unahitaji vyakula vyenye fiber au fiber supplement.
   High Fiber Foods List for a High Fiber Diet
   MziziMkavu likes this.
   “Society is like a stew. If you don't stir it up every once in a while then a layer of scum floats to the top.”

  21. Gaga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th January 2011
   Location : Clarendon road
   Posts : 4,501
   Rep Power : 1417
   Likes Received
   1834
   Likes Given
   1891

   Default re: Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

   Maji ya uvuguvugu ukiamka tu kabla ya mswaki na maji mengi wakati wote, matunda hasa mapapai pia ni msaada mkubwa
   MziziMkavu and Lulu michael like this.
   You Only live Once....But if you do it right, Once is enough

  22. JF SMS Swahili

  Page 1 of 7 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Shule ya msingi Kambarage wilayani Serengeti yafungwa kwa kukosa choo
   By Mwl Ryoba in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 6
   Last Post: 29th October 2011, 12:32
  2. Replies: 9
   Last Post: 4th March 2011, 04:42

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...