JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Faida ya mdalasini na asali

  Report Post
  Page 1 of 7 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 134
  1. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Thumbs up Faida ya mdalasini na asali

   MDALASINI NA ASALI
   Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
   Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

   Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

   Kama ifuatayo:

   1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.

   Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

   Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

   Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

   2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
   Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

   3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
   Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

   4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
   Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

   5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
   Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
   Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

   6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
   SORES}.

   Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
   nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.
   Mahmood, jamadari, utafiti and 2 others like this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)


  2. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   7. Helemu {CHOLESTERAL}
   Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.

   Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

   Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

   8. Mafua {COLDS}
   Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.

   9. Ugumba {INFERTILITY}
   Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa anglao vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.

   Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi kwa kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

   Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.

   Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

   10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
   Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

   ll.Esidi/Gesi-Co2. Hco3. Hcl.
   Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.
   jamadari and amkawewe like this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  3. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}
   Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa.

   Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja ulionyesha.

   13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}
   Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini. Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha
   ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za tiba hii ya ajabu.

   14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}
   Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja - wataalamu wanasema.

   Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho} na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na {bacteria}.

   15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}
   Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.

   Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.

   16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}
   Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula chakula} huondoa kiungulia na wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.

   17.Flu {INFLTJENZA}
   Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vairasi {vimelea} waletayo Flu.

   18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}
   Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
   jamadari likes this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  4. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   19.Chunusi {PIMPLES}
   Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
   Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.

   20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} wenye sumu Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinatoweka.

   21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}
   Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.

   22.Kupungua kwa uzito
   Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala.

   Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.

   23.Saratani {CANCER}
   Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani.

   Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya kawaida".

   24.Uchovu {FATIGUE}
   Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji, nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii itajionyesha".

   25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}
   Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu} nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila asubuhi halafu nawisha nyayo kwenye maji baridi na vaa viatu.

   26.Harufu mbaya kutoka mdomoni
   Waamerica wa kusini wanasukutua kwa kutumia asali na mdalasini pamoja na vuguvugu kila asubuhi ili kufanya harufu toka mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya kusini mashariki, watu hula kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni {halitosis}. Wataalamu wanaamini kwamba uwezo wa kuua bacteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni.

   27.Kupungua kwa usikivu {HEARING LOSS}
   Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani.

   MDALASINI NA ASALI vinaweza kukufanya uonekane kama picha yenye afya nzuri kama ile ya mwonyeshaji mitindo ya mavazi na muigizaji sinema Jocqol Bell.
   Mdalasini


   Last edited by MziziMkavu; 18th January 2011 at 05:46.
   jamadari and Asamwa like this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  5. Mafuluto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2009
   Posts : 989
   Rep Power : 3072
   Likes Received
   224
   Likes Given
   358

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   mdalasini ndiyo cinamon au ?
   MziziMkavu likes this.

  6. Kansime

  7. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Quote By Mafuluto View Post
   mdalasini ndiyo cinamon au ?
   ndio mdalasini kwa kiingereza unaitwa Herb Cinnamon   tpaul likes this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  8. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Thumbs up Re: Faida ya mdalasini na asali

   Custard Ya Mdalasini


   VIPIMO

   Maziwa 2 1/2 Vikombe

   Mdalasini wa unga 1 Kijiko cha chai

   Mayai 3

   Asali 1/4 Kikombe

   Chumvi Kidogo (dash)

   Vanilla 1 Kijiko cha chai
   NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

   1. Washa oveni moto wa 375F.


   2. Weka vibakuli 6 maalum (remekins) vya kupikia kwenye oven , katika trei ya kuvumbika (bake).

   3. Pasha moto maziwa, mdalasini na vanilla katika sufuria.

   4. Chukuwa bakuli na uchanganye mayai, asali na chumvi pamoja.

   5. Endelea kukoroga, huku unamimina ule mchanganyiko wa maziwa
   kidogo kidogo hadi ichanganyikane vizuri.

   6. Mimina custard kwenye vibakuli ulivyovitayarisha, kisha weka treya
   kwenye mlango wa oveni na umimine maji ya moto (yaliyochemka) ili
   itapakae chini ya vile vibakuli nusu yake.

   7. Pika (bake) katika oven kwa muda wa dakika 30-40 au mpaka ukitovya kisu kitoke kisafi.

   8. Ikisha iiva na kupoa, weka ndani ya friji na ikishapata ubaridi
   itakuwa tayari kwa kuliwa.

   jamadari likes this.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  9. utiyansanga's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 19th May 2010
   Posts : 214
   Rep Power : 561
   Likes Received
   6
   Likes Given
   0

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Safi sana mzizi mkavu naona umetoka kivingine ..upo kwenye baridi au vumbi!
   MziziMkavu likes this.

  10. MAMMAMIA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Location : Near You
   Posts : 3,789
   Rep Power : 3317
   Likes Received
   1497
   Likes Given
   1207

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Very Nice. This may help the us of natural medicine instead of inorganic and chemicals. Thanks
   MziziMkavu likes this.

  11. #10
   Rubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2009
   Posts : 1,560
   Rep Power : 863
   Likes Received
   237
   Likes Given
   189

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Thanx, lakini mbona yule nyani mfuta bangi tulikuwa tumemzoea.
   MziziMkavu likes this.
   Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

  12. Mafuluto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2009
   Posts : 989
   Rep Power : 3072
   Likes Received
   224
   Likes Given
   358

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Hii ya kupakaa asali ktk mtalimbo ndo naiskia leo. Scientfically imekaaje hii na unapakaa wakati wa game au kabla ?
   MziziMkavu likes this.

  13. tzjamani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th October 2010
   Posts : 999
   Rep Power : 706
   Likes Received
   25
   Likes Given
   96

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   This is great. I have read alot of articles about honey, cinammon na green tea.
   MziziMkavu likes this.
   The more anger towards the past you carry in your heart, the less capable you are of loving in the present- Barbara De Angelis

  14. Kunta Kinte's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th May 2009
   Location : DAR
   Posts : 3,046
   Rep Power : 539562
   Likes Received
   809
   Likes Given
   1001

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Thanks Buddy!
   MziziMkavu likes this.

  15. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Quote By utiyansanga View Post
   Safi sana mzizi mkavu naona umetoka kivingine ..upo kwenye baridi au vumbi!
   nipo huku Ughaibuni baridi kali sana Mkuu
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  16. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Quote By Mafuluto View Post
   Hii ya kupakaa asali ktk mtalimbo ndo naiskia leo. Scientfically imekaaje hii na unapakaa wakati wa game au kabla ?
   Wakati wa kucheza game ndio unapakaa mtalimbo wako basi huyo mwanamke atajisikia raha tupu na joto litazidi na ndizi yako itakuwa na nguvu zaidi.
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  17. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 30,977
   Rep Power : 429503210
   Likes Received
   18019
   Likes Given
   55413

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Quote By Rubi View Post
   Thanx, lakini mbona yule nyani mfuta bangi tulikuwa tumemzoea.
   nimemtowa yule nyani mvuta bangi
   Only Do What Your Heart Tells You

   Allah
   Has Not Revealed A Disease without Treatment.... (Prevention is Better Than Cure)

  18. mamakunda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th July 2010
   Posts : 364
   Rep Power : 584
   Likes Received
   9
   Likes Given
   14

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Nakushukuru sana mkuu, katika asali mie ni mmojawapo nimethibitisha hii kwa upande wa kupanda pressure, toka nimeanza kunywa mchanganyiko wa asali na maji ya moto asubuhi kwa kweli kuna mabadiliko ya hali ya juu, ila sikujua kama na mdalasini unachangaya, nitaanza pia kuuchanganya,
   MziziMkavu and jamadari like this.

  19. Mafuluto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2009
   Posts : 989
   Rep Power : 3072
   Likes Received
   224
   Likes Given
   358

   Default Re: Faida ya mdalasini na asali

   Mkuu,

   Bado sioni kupaka asali ktk mtalimbo kunawezaje sababisha mtalimbo uwe wima, au na nguvu za ziada. Sana sana labda kuongeza/rahisisha friction, vinginevyo kisayansi bado haijakaa sawa. Maybe we need to do an experiment lol..
   MziziMkavu likes this.

  20. Uncle Jei Jei's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th January 2011
   Posts : 540
   Rep Power : 593
   Likes Received
   92
   Likes Given
   3

   Default Naomba kufahamu nguvu ya mdalasin ktk kuongeza nguvu za kiume.

   Asalaam aleykum, Hongereni nyote mliopata tiba ya "babu" na wale ambao bado mjitahd kwenda folen imepungua! Baada ya hayo, naamin hum ndan kuna wataalam wa aina zote wakiwemo wa afya.

   Nimekuwa nikisikia sana kuwa mdalasin unasaidia kuongeza nguvu za kiume,lakin tatizo linakuja kujua ni kwa kiasi gan kuna ukweli ndan yake kwan mara nyng unatumka kama kuongeza radha ya chakula. Vile vile ni upi hasa unafaa; wa unga utumiwapo kama chai au wa magamba unaochemshwa na kuachwa upoe kama baadhi wanavyodai? Na je,mhuska atumie mara ngapi kwa siku na kwa mda gani(duration)!?

   Ni iman yangu kuwa thread hii itachangiwa na watalaam wenye timamu wenye uwezo wa kupambanua mambo, na wasio leta MZAHA na KEBEHI kwenye mambo ya msingi kwan hao wana FORUM yao!! Natanguliza shukran zangu.
   MziziMkavu likes this.

  21. KYALOSANGI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st January 2011
   Location : town
   Posts : 857
   Rep Power : 654
   Likes Received
   219
   Likes Given
   199

   Default Re: Naomba kufahamu nguvu ya mdalasin ktk kuongeza nguvu za kiume.

   peruzi ilshaandikwa mara nyingi humu


  Page 1 of 7 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Jamani asali asali asali eehhh!!
   By Sajenti in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
   Replies: 30
   Last Post: 15th December 2011, 03:51
  2. Replies: 4
   Last Post: 4th August 2011, 09:44
  3. Asali asali asalai
   By Masika in forum JF Chit-Chat
   Replies: 2
   Last Post: 19th July 2011, 20:08

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...