Leo nilikuwa na kaproject flan kalikosababisha nitembelee sehemu mbali mbali za dsm hasa kule kunakoitwa uswahilini. Kilichonishangaza nilipofika hayo maeneo na kupiga simu kwa line ya tigo nikawa napewa ujumbe kuwa nipo kwenye maeneo ambayo kuna punguzo kubwa sana la kupiga simu nje ya nchi!! Maeneo hayo ni kama MTONI MTONGANI NA KWA AZIZI ALI,MBAGALA, TANDIKA,TEMEKE MIKOROSHINI, AND TANDALE MANZESE AND THE LIKES! Hivi hayo maeneo tajwa yana idadi kubwa ya watu wenye connections nje?? Kwa nini hiyo ofa isiwe MASAKI,OBEY,MBEZI BEACH KIJITONYAMA AND THE LIKES