Mama yangu mpenzi gfsonwin! Mimi mwanao mzima kabisa. Kabla ya yote nikuhakikishie mapenzi ya kweli niliyonayo
kwako. Hapana mwingine kama mama! Wewe una nafasi ya kwanza moyoni mwangu na hakika ninakupenda daima mama
yangu mpenzi! Baba Kaizer hajambo hapo nyumbani?
Mama yangu mpenzi, wiki iliyopita nilipatwa na safari ya ghafla. Zilikuwepo dalili za waheshimiwa kutaka kumwaibisha
dhaifu kwa kuwaadhibu wateule wake. Hivyo akanipigia simu ili nikaweke mambo flani ya 'kitekiniko' sawa. Hii ilinilazimu
kujifungia kati ya moja ya vyumba vya mjengo wetu na kale 'kaofisi ketu kadogo' pale. Mawasiliano yangu ya simu na
internet yalizuiliwa kwa kiasi flani kwa sababu za 'kiintelijensia'. Kwasasa kazi nimemaliza kama mlivyoona wenyewe
jumamosi na jana tulikuwa tunajipongeza kidogo. . .
Ako zangu Eiyer, platozoom, Excellent, Mbimbinho na aunt Smile wamenitafuta bila mafanikio, sasa narudi.
Ila nimegundua Asprin hana nia njema nawe mama, anataka akugombanishe na mzee Kaizer. Halafu nimegundua
wakeze cacico, Yummy na BADILI TABIA wananizimikia maana nilipowasha simu nimekutana na msg zao tata
mama yangu. Nishauri niwafanyeje?

Reply With Quote





Follow Us Here