Kwa kuanza ninayo maswali kumi ambayo ningependa kumuuliza Aunt
Lizzy:
1. Je umezaliwa msimu gani?
. . . . HEHEHE. . msimu nlozaliwa mie kiangazi, ndo maana watu hawaishi kulalamika Lizzy majibu yake DRY!!Jamani. . I can't help it.
2. Je Ulishawahi kucheza mchezo wa baba na mama na kupika pika utotoni?
. . .Khaa, kuna aliyeishi uswahilini akapitwa kweli? Ila tu niseme sie hatukua tunafanya matusi kama ambavyo nasikia wengine walikua wakifanya.
3. Je umeolewa? Kama umeolewa, Je una watoto wangapi, na kama hujaolewa, ina maana huna hata wa kuchombeza?
. . . Mara ya tatu hii.Niliwahi kuwa mama mchungaji, nikawa 'firstlady' wa mwenyekiti wa mtaa, na sasa hivi nimetulia kwa balozi wa wabeba box.
. . . Kila ndoa imenibariki watoto wawili, kwahiyo nnao sita mpaka sasa.
4. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
Kifo cha mwanaJF mwenzetu Regia na Chentutu.
5. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana
Ushindi wa MMU Queen. . .japo
Superman mpaka leo hajanipa zawadi yangu.
6. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
Vimini na jeans tight. . .ndio maana u'mama mchungaji ulinishinda.
7. Je unapenda chakula cha aina gani?
Kwanzia wali wa maharage mseto, ugali wa dagaa mpaka ndizi. machalari tunazopika sana kule kwetu Machame.
8. Ukipata fursa ya kupata staftahi na mheshimiwa Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Chadema jimbo la Arusha, utamshauri nini?
Asife moyo. . .yeye ni wa watu wa Arusha na watu wa Arusha ni wake.
9. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
. . . Nalipa kodi. . .japo inaishia kwa mafisadi ila na mie nimejaribu.
10. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….
. . .Huu ntakupa pembeni usije ukaacha kunikaribisha tena kwenye kipindi.
Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Aunt
Lizzy atakuja kuyajibu maswali yenu.
Karibuni sana
Follow Us Here