Si kawaida sana mtu kujielezea jinsi ulivyo: Mwonekano, tabia na vitu unavyovipenda bila ku-pretend.
Kuna watu hata kusema jinsi walivyo kwao ni vigumu sana pengine kwa hofu ya kudharauliwa, kutengwa, kuchekwa au hata kutishwa.
Kwa sababu twaonana kwa kutumia ID hebu tujiseme tulivyo.
Mimi naanza kusema na kujisema kwa ukweli kabisa:
1. Ni mwanaume, rangi maji ya kunde, mrefu kiasi lakini mwembamba.
2. Rahisi sana kupandwa na hasira lakini mwepesi kujizuia kuzionyesha.
3. Sipendi mtu anidanganye kwa sababu huwa nahisi ananidharau au kuniona mjinga
4. Ni msiri sana..hata nikikuona unafanya jambo baya naweza kupotezea tu labda kama litaniathiri mimi na jamaa zangu.
5. Ukiniomba fedha/kukopa huwa sina maneno ya kuzungusha..nakwambia sina kama sina.
6. Naweza kujua kitu lakini nikajifanya sijui ili nisikie maoni ya upande wa pili.
7. Simwamini mpenzi wangu kwa 100%
Hebu na wewe sema ulivyo, kwa kuanzia akina Erickb52, sweetlady, Erotica, Asprin, Bishanga TANMO, EMT, Mwali N.K.

Reply With Quote



Follow Us Here