Inatokea mtu anakuwa na tabia mbaya na anajua kabisa kwamba tabia hiyo itamletea dhahama au itamuua, lakini yumo tu, inamtesa na hataki kuiacha kabisa, hata akionywa na kupewa mifano mingi ya majanga yanayowapata watu wenye tabia kama hiyo, yeye kila siku anaahidi kuwa ataacha lakini haachi na anaendelea nayo tu...........!
Mimi mwenzenu nilikuwa na tabia mbaya ambayo ilikuwa ikiniletea kisirani kwa Mama Ngina miaka kumi iliyopita lakini nikaipatia tiba baada ya kwenda kwa washauri wa kisaikolojia mpaka nikaiacha. Tabia yenyewe ilikuwa ni ya kuwa na shingo feni. Jamani ilikuwa asikatize binti mwenye kikalio na kihipsi cha kiushkaji, lazima nisuuze macho hata kwa kuibia ibia. Mama Ngina akapiga kelele wee, mpaka nikaamua kutafuta tiba na sasa nimekuwa huru, hata nione mwanamke mwenye kalio la namna gani wala hainishtui.......
Hebu wana JF wenzangu fungukeni, ni tabia gani mbaya mlizo nazo na mnashindwa kuziacha kabisa, huenda tukashauriana hapa na kupeana tiba.................!


Reply With Quote






Follow Us Here