Attachment 54654
Kipindi hiki kinaanza na Mzee wetu Bishanga, ambaye baada ya kunizungusha sana kukubali mualiko wangu, hatimaye leo amekubali mualiko wangu na kuja hapa Studio kwa mahojiano haya ambayo yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.
Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza Mzee Bishanga swali lolote na yeye bila shaka atayajibu mwaswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.
Kwa kuanza ninayo maswali kumi ambayo ningependa kumuuliza Mzee Bishanga:
1. Je umezaliwa msimu gani?
2. Je Ulijisikiaje uliposhiriki tendo la kujamiiana kwa mara ya kwanza?
3. Je Umewahi Kutendwa
4. Je umewowa? Kama umewowa, Je una watoto wangapi, na kama hujawowa, Je nini mustakabali wako wa maisha ya uzeeni?
5. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
6. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana
7. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
8. Je unapenda chakula cha aina gani?
9. Ukipata fursa ya kupata staftahi na mheshimiwa Rais ungemweleza jambo gani linalokukera katika uongozi wake?
10. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Mzee wetu Bishanga atakuja kuyajibu maswali yenu.
Karibuni sana

Reply With Quote




Follow Us Here