Well, hello guys!
It is Mei Mosi again, zamani zetu Rais wa Jamhuri ilikuwa ni lazima atoe hotuba kwa wafanyikazi, na matarajio yetu mara nyingi ilikuwa ni kupanda kwa viwango vya mishahara. Ikifika siku ya leo, mfanyakazi lazima uhakikishe redio yako ina betri za kutosha, na ume-tune Radio Tanzania Dar es salaam (kwani kulikuwa na stesheni nyingine?), au kama uko Dar es salaam ujue Karimjee panakuhusu. Sijui kipindi hiki hali ikoje, I mean uhusiano kati ya serikali na wafanyikazi katika siku yao hii, I don’t bother anyways!
Yangu mie leo sio hayo, ya kuwarudisha enzi za mwalimu, wala!
Leo nataka nitoe pongezi zangu kwa makundi ya wafanyikazi wa sekta zisizo rasmi, tena ambao ni kama wanasahaulika kila yanapotajwa makundi ya wafanyikazi wengine.
Wa kwanza ni mama lishe, au mama ntilie, kama hujanielewa, hawa ni watu wanaotoa huduma za chakula kwa bei nafuu katika vibanda vyao wenyewe, kama maisha yako ni safi au hauishi maeneo ya mjini, au kama umeoa huwezi kujua nazungumzia nini. Ndiyo, ili uwe mteja wa hawa kina mama kuna masharti kadhaa, kipato chako kiwe kidogo, uwe hujaoa na uwe mkazi wa mijini. Hawa ndio wanalisha kundi kubwa la wafanyakazi wa kiwango cha chini ambao ndio wengi na vijana. Kundi hili linalolishwa nao ndio nguvukazi ya taifa haswa, sipati picha bila huduma ya kinamama hawa maisha yetu yangekuwaje? Kazi yao ina changamoto nyingi, kushughulika na moto muda mwingi si mchezo, lakini bado hakujawa na tija sana katika biashara zao. Kutokana na kasumba, kinamama hawa hawakopesheki na mabenki, na ikitokea ni haya mashirika ya kina Iddi Simba, tena kwa riba ya asilimia 50. Biashara yao ni challenge tosha, achilia mbali matusi wanayovurumishiwa na wateja wao. Its realy painfull. My shout outs to you kinamama!
Kundi la pili ni vibarua wa ujenzi maarufu kama wabeba zege. Hivi umeshawahi kujitwisha mfuko wa saruji wa kg. 50? Ni mzito asikwambie mtu, sasa maisha ya vijana hawa ni zaidi ya kubeba huo mfuko, ni kazi ngumu na nzito kuwahi kutokea chini ya jua. Pamoja na dharau wanayoipata kutokana na kazi yao, achilia mbali malipo duni wanayopata (Sh.T 4000/= kwa siku), ukweli ni kwamba hili ndilo kundi muhimu kabisa katika sekta ya ujenzi, hasa miradi mikubwa. Pata picha ile mijengo yote kule Posta na kwingineko, mabarabara yote nchi nzima, uwanja mkuu wa Taifa, ni kazi ya mikono yao. But when it comes to credits, everyone turns to so called ‘wakandarasi’, ambao ndio kupitia kwao majengo yanaanguka, barabara zinaumuka na uwanja hauna viwango. Nitumie kalamu hii kuwatia moyo vibarua wote wa ujenzi, natambua mchango wenu kwa taifa hili.
Kundi la tatu ni wafanyabiashara wadogo wadogo wa vyakula na mbogamboga. Kwa sisi wakazi wa mjini tusiofuga wala kulima walau tuta moja la matembele, hawa ndio wakombozi wetu. Unajua mtu unaweza kuchukulia poa kwa vile ukihitaji nyama unaifuata tu buchani, hujui kuwa mwenzako ameamka saa tisa ya usiku kuwahi Vingunguti, na vibaka wote njiani, bado mvua haijanyesha hapo. Wauza genge vilevile huwalazimu kuamka saa 10 alfajiri ili kuwahi Kariakoo na Buguruni ili kuwaletea ninyi makulaji yenu ya kila siku, sijawasahau pia wafanyabiashara wa samaki ambao nusu ya maisha yao ni kukabiliana na lile shombo lenye harufu mbaya. Hawa niliowataja hapo juu wana maana kwenye maisha yangu ya kila siku kuliko Afisa Kilimo aliyehitimu SUA ambaye sioni delivery yake kwangu (samahani kama nimekukwaza).
Kundi linguine katika kumbo hii ni wafanyakazi wote wa mifumo ya takataka. Yaani kuanzia wasafisha mitaro, wazoa takataka mpaka wazibua vyoo. Hizi ni kazi za kinyaa kuwahi kutokea kwenye uso wa nchi, really shit job, lakini wameifanya kwa moyo na kwa bidii siku zote za uhai wao. Hawa wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya kuambukiza but no one cares, hata vijisemina vya safety and precaution jamani? Wanakaa kujilaza kwenye mahoteli makubwa mpaka wanaibiwa huko, wala hawaangalii maslahi ya hawa watu. Ushawahi kufanya kazi mahali ambapo chemba ya uchafu imezibuka, hakyanani hapakaliki mahala hapo, na kama una roho nyepesi utashinda njaa siku nzima, utakulaje chakula mbele ya kinyesi? Kuhusu wazoa taka wala sina haja ya kuwaelezea sana, nadhani wote mmeshawahi kukatiza karibu na gari la taka, and you know the msala here, zimeshawahi kupita siku kadhaa bila gari ya taka kupita mtaani kwenu? How was it look like, uhm? Naomba nitambue uwepo wenu na umuhimu wenu katika kuweka mazingira tulivu kwa ajili ya kazi, masomo, na shughuli zingine.
Wengine ni madereva, mtaani kwetu unawaita sukas. Hapa simaanishi kila mwenye leseni.\, nope! Namaanisha watu ambao udereva ndio kula yao, kuanzia madereva taksi, madereva wa daladala, wanaosafirisha abiria mikoani na wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi. Hii ni kazi ambayo hakuna uvivu, lazima unapokuwa nyuma ya usukani uwe macho muda wote na uweke akili yako barabarani, bado kuna changamoto za vyombo kupata hitlafu barabarani bila kusahau ajali, hakuna dereva anayependa ajali wakuu, hasa kwa vile na maisha yake nayo yanahusika. Na bado kikinuka, cha kwanza ni polisi kumtia pingu dereva, bila kujua kuwa si kila ajali inasababishwa na uzembe, ndo maana wengi wanakimbiaga. Bado kitengo cha usalama barabarani hakijishughulishi na kutoa elimu kwa madereva, wao ni kuandika notifikesheni tu na kupokea rushwa. Mwishoni mwa mwaka jana kama sikosei, ndio Said Salim Bakhressa aliandaa semina kwa ajili ya madereva wa mizigo wa kampuni lake na akakaribisha madereva wengine kujifunza bure, lakini waliopewa dhamana hiyo, wala hawana habari. Changamoto zingine kwa madereva ni pamoja na kuvamiwa na majambazi kwa wanaosafiri mbali na taxi drivers. Kingine ni ugonjwa wa UKIMWI hasa kwa madereva wa mizigo masafa marefu, wakati umefika kwa mashirika ya kupambana na UKIMWI yaandae semina zaidi kwa hawa madereva, wako katika hatari kwa kweli. Mbali na yote, natambua mchango wao katika kuendeleza taifa hili, wote mmeshuhudia adha ya mgomo wa madereva na mnajua madhara ya sekta ya usafirishaji kwa uchumi wa nchi.
Kundi la mwisho katika andiko langu hili, naomba niguse wafagizi wa barabara. Kwanza hawa mara nyingi ni kinamama wazee, sijui kwanini imekuwa hivyo? Miili yao imechoka na uwezo wa kuona umepungua kwa kiasi fulani, yet wanafanya kazi katika mazingira ya kupishana na magari, aloo? Yupo mmoja ambaye ni jirani yangu, kila baada ya siku kadhaa lazima anijie na stori ya koswakoswa za magari, what a risk? Thanks god madereva wanajitahidi wawezavyo kuwajali, na matukio ya hawa kugongwa si mengi sana. Pamoja na hatari hizo, bado maslahi ya kazi yao ni kiduchu, hardly wanalipwa Tsh. 40000/= kwa mwezi, hakuna tips, per diem wala sijui nini nini allowances, lakina maisha yanasonga. Natambua mchango wao katika kuweka mazingira ya miji yetu safi, hasa kutokana na sisi kutokuwa na ustaarabu wa utupaji taka njiani. My appreciatin to you!
Hao ndio nilioona ni vema niwaangazie katika andiko langu kwa leo, maana sidhani hata kama wanajua kuwa leo ni sikukuu yao. Hardly they work, hardly they earn!
Mei Mosi njema!
Mphamvu.

Reply With Quote

Follow Us Here