TiGo Maps
    Show/Hide This

    Topic: Jukwaa La Mapishi, Food Corner

    Report Post
    Page 5 of 7 FirstFirst ... 34567 LastLast
    Results 121 to 150 of 188
    1. #1
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Jukwaa La Mapishi, Food Corner

      Wana'JF Wote wenye kupenda kula na kunywa kwa Afya Bora, hapa ndio sehemu yako. Wote mnakaribishwa ili kubadirishana uzowefu wa MAPISHI, Mahanjumati na Makulaji.Jisikie Huru Kushirikiana na kila mwanachama katika kuboresha LISHE Bora.Aina zote za Mapishi yatapatikana hapa.ShukraniKaribuni Wote WanaJF
      ______________________________ __



      Virutubisho Vinavyopatikana Katika Vyakula

      Mwili wa binadamu (na viumbe vingine hai) ili uweze kukua na kunawili unahitaji vitu vinavyojulikana kama virutubisho au viinirishe. Kwa lugha ya kigeni virutubisho vinaitwa "Nutrients". Virutubisho hivyo vinapatikana katika vyakula mbalimbali.

      Vile vile tunajuwa kuwa, virutubisho vyote hugawanywa katika makundi makuu sita, ambayo ni kabohaidreti (wanga, sukari na nyuzi nyuzi), protini, mafuta, vitamini, maji na madini (minerals). Ili mwili uweze kukua na kunawili vizuri lazima upate virutubisho vyote.

      Chakula (kama cha asubuhi, mchana, jioni au usiku) chenye virutubisho vyote sita hujulikana kama mlo kamili au "balanced deit" kwa lugha ya Waingereza. Kwa vile takribani vyakula vyote tunavipata kwa gharama kubwa (fedha au kazi), swala la uchaguzi wa vyakula haliepukiki.

      Pia unategemea mazoea ya mlaji, radha na sura ya chakula, virutubisho na mambo kadhaa wa kadhaa. Ili kufikia uchaguzi sahihi wa vyakula, elimu ya chakula gani kina virutubisho gani ni ya msingi. Jukwaa La Mapishi, (Food Coner) linakusudia kukidhi haja hiyo kwa wasomaji wote. Katika kukidhi haja hiyo, vitataja aina ya chakula, virutubisho vya msingi na virutubisho vya ziada vinavyopatikana katika vyakula hivyo.

      Nafaka:
      Nafaka ni vyakula vya punje punje au chembechembe kama vile mtama, mahindi, ngano, uwele (mawele), mpunga n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula vya nafaka ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni Protini, vitamini (kundi la B) na baadhi ya madini.

      Vyakula jamii ya mizizi na matunda:
      Vyakula jamii ya mizizi (starchy roots) ni kama vile viazi (vitamu, mviringo, n.k) mihogo, n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula jamii ya viazi na matunda ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi (dietary fibres). Zaidi ya virutubisho hivyo ni baadhi ya madini, vitamini C (kama chakula hicho siyo kikavu) na vitamini A (kama chakula hicho kinarangi ya njano).

      Vyakula jamii ya maharage:
      Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k. Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na madini.

      Mbegu za mafuta:
      Mbegu za mafuta ni kama vile alizeti, pamba, ufuta, nazi, mawese (chikichi), kweme, maboga, tikiti maji, matango, n.k. Virutubisho vinavyopatikana kwa wingi katika mbegu za mafuta ni mafuta, protini na nyuzi nyuzi. Ziada kundi B. (B- Vitamins).

      Nyama/Samaki:
      Virutubisho vya msingi katika nyama au samaki ni protini, mafuta na madini ya chuma. Virutubisho vingine ni vitamini vya kundi B na madini (zaidi ya yale ya chuma).

      Ini:
      Ini linatupa virutubisho vya msingi vya protini, madini ya chuma na vitamini.

      Maziwa:
      Virutubisho tunavyovipata kwa wingi katika maziwa ni mafuta, protini, baadhi ya madini na vitamini.

      Mayai:
      Mayai yana virutubisho vya msingi vya protini na vitamini. Zaidi ya hivyo ni mafuta na madini (siyo ya chuma).

      Mafuta:

      Mafuta kama chakula yanatupa mafuta kama kirutubisho cha msingi. Zaidi ya hicho ni uwezekano wa kupata vitamini A.

      Mboga za majani:
      Mboga za majani hasa zile za kijani zinavirutubisho vya msingi vya vitamini A, C na B, Zaidi ya hivyo ni protini, madini na nyuzi nyuzi.

      Matunda jamii ya machungwa:
      Matunda jamii ya machungwa ni machungwa, machenza, n.k virutubisho vya msingi tunavyovipata kutoka katika matunda jamii ya machungwa ni sukari, vitamini A na C. Zaidi ya hivyo ni madini na nyuzi nyuzi.
      Last edited by X-PASTER; 17th January 2012 at 18:52.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)



    2. #121
      Lizzy's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Location : UngaLTD!
      Posts : 20,959
      Rep Power : 14456
      Likes Received
      7556
      Likes Given
      1967

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      LAT recipe hii hapa. . .
      Ntajitahidi niweke picha haraka iwezekanavyo kwasababu zitakuonyesha kila kitu kinavyotakiwa kufanyika na namna gani vionekane which is quite important.

      Mlo wa watu wanne (4)

      Mahitaji
      Nyama ya ng'ombe 1/2 kg
      Cream ya kupikia 1.5 - 2.5 dl /maziwa
      Uyoga kiasi upendacho
      Hoho 1- 3....mimi hua natumia rangi tatu tofauti (Nyekundu, kijani na njano).
      Kitunguu kimoja kikubwa
      Soy sauce kijiko kidogo 1
      Food coloring
      Pilipili manga (black pepper) au white pepper iliyosagwa
      Oregan
      Basil
      Chumvi
      Mafuta ya maji au siagi
      Maji ya kutosha
      Maandalizi

      Katakata nyama yako vipande vidogo vidogo na viungo vingine vyote baada ya kuviosha.

      Andaa frying pan yako na sufuria itakayotosha kuchemsha kila kitu pamoja. Ukimaliza nyunyuzia chumvi na pilipili manga (nusu kijiko cha chai of each) kwenye nyama yako kwa kuisambaza.

      Hatua inayofuata ni kuunguza nyama yako kidogo hivyo weka frying pan na mafuta kidogo jikoni mpaka vitakapopata moto. Vikishapata moto weka nusu ya nyama yako kwenye frying pan na ugeuze haraka haraka. Haitakiwi kutoa maji, inatakiwa iungue tu juu hivyo usije ukaweka kabla mafuta hayajapata moto vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama yako kwenye sufuria uliyoandaa mapema kisha urudishe kikaangio chako jikoni. Chukua maji nusu kikombe uweke kwenye kikaangio kikiwa jikoni iwe kama unakiosha vile. Hayo maji yakianza kuchemka changanya na ile nyama iliyopo kwenye sufuria. Rudia hatua hizo hizo kukaanga ile iliyobakia.

      Ukimaliza kaanga vitunguu, hoho, uyoga "mbalimbali" mpaka vitakapoanza kulainika kisha changanya na nyama.
      Baada ya hapo weka maji vikombe 4-6 vya chai, weka chumvi kidogo, funika na uweke motoni. Acha ichemke kwa dakika 40 - 50 mpaka utakapoona maji yaliyobaki hayazidi theluthi moja (1/3) ya kiasi ulichoweka mwanzo.

      Weka cream (ni nzuri zaidi kwasababu itafanya kitoweo chako kiwe kizito) au maziwa, koroga mpaka itakapoanza kuchemka. Kisha weka kijiko cha chai 1 soy souce na matone. . MATONE matatu tu ya food coloring ya brown/nyeusi, oregan na basil kiasi unachoweza kushika kwa vidole vyako viwili. Onja kujua kama kuna kitu ungependa kuongeza (pilipili manga/chumvi) kabla ya kufunika, kupunguza moto mpaka chini na kuacha cream iive taratibu kwa dakika 6 - 10.

      Unaweza ukala kwa wali, viazi vya kuchemsha pekee bila mafuta au hata pasta za aina yoyote ile.

      PS
      Soy sauce sio lazima ila food coloring ni muhimu ili kuipa mboga rangi ya kuvutia.

    3. LAT is online now
      LAT
      #122
      LAT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 4,481
      Rep Power : 1310
      Likes Received
      1110
      Likes Given
      1653

      Default

      Quote By Lizzy View Post
      LAT recipe hii hapa. . .
      Ntajitahidi niweke picha haraka iwezekanavyo kwasababu zitakuonyesha kila kitu kinavyotakiwa kufanyika na namna gani vionekane which is quite important.

      Mlo wa watu wanne (4)

      Mahitaji
      Nyama ya ng'ombe 1/2 kg
      Cream ya kupikia 1.5 - 2.5 dl /maziwa
      Uyoga kiasi upendacho
      Hoho 1- 3....mimi hua natumia rangi tatu tofauti (Nyekundu, kijani na njano).
      Kitunguu kimoja kikubwa
      Soy sauce kijiko kidogo 1
      Food coloring
      Pilipili manga (black pepper) au white pepper iliyosagwa
      Oregan
      Basil
      Chumvi
      Mafuta ya maji au siagi
      Maji ya kutosha
      Maandalizi

      Katakata nyama yako vipande vidogo vidogo na viungo vingine vyote baada ya kuviosha.

      Andaa frying pan yako na sufuria itakayotosha kuchemsha kila kitu pamoja. Ukimaliza nyunyuzia chumvi na pilipili manga (nusu kijiko cha chai of each) kwenye nyama yako kwa kuisambaza.

      Hatua inayofuata ni kuunguza nyama yako kidogo hivyo weka frying pan na mafuta kidogo jikoni mpaka vitakapopata moto. Vikishapata moto weka nusu ya nyama yako kwenye frying pan na ugeuze haraka haraka. Haitakiwi kutoa maji, inatakiwa iungue tu juu hivyo usije ukaweka kabla mafuta hayajapata moto vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama yako kwenye sufuria uliyoandaa mapema kisha urudishe kikaangio chako jikoni. Chukua maji nusu kikombe uweke kwenye kikaangio kikiwa jikoni iwe kama unakiosha vile. Hayo maji yakianza kuchemka changanya na ile nyama iliyopo kwenye sufuria. Rudia hatua hizo hizo kukaanga ile iliyobakia.

      Ukimaliza kaanga vitunguu, hoho, uyoga "mbalimbali" mpaka vitakapoanza kulainika kisha changanya na nyama.
      Baada ya hapo weka maji vikombe 4-6 vya chai, weka chumvi kidogo, funika na uweke motoni. Acha ichemke kwa dakika 40 - 50 mpaka utakapoona maji yaliyobaki hayazidi theluthi moja (1/3) ya kiasi ulichoweka mwanzo.

      Weka cream (ni nzuri zaidi kwasababu itafanya kitoweo chako kiwe kizito) au maziwa, koroga mpaka itakapoanza kuchemka. Kisha weka kijiko cha chai 1 soy souce na matone. . MATONE matatu tu ya food coloring ya brown/nyeusi, oregan na basil kiasi unachoweza kushika kwa vidole vyako viwili. Onja kujua kama kuna kitu ungependa kuongeza (pilipili manga/chumvi) kabla ya kufunika, kupunguza moto mpaka chini na kuacha cream iive taratibu kwa dakika 6 - 10.

      Unaweza ukala kwa wali, viazi vya kuchemsha pekee bila mafuta au hata pasta za aina yoyote ile.

      PS
      Soy sauce sio lazima ila food coloring ni muhimu ili kuipa mboga rangi ya kuvutia.
      Lizzy, thanks

      i know mushroom inavirutubisho vingi sana ambavyo ni free from colestral and other hazards

      wacha nikaitume na chakula cha uyoga

    4. #123
      Nsiande's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th July 2009
      Location : dar es salaam
      Posts : 1,093
      Rep Power : 670
      Likes Received
      428
      Likes Given
      35

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Quote By Lizzy View Post
      Nsiande unataka ladha iwe simple au spicey?
      Na samaki unaotaka kuoka ni wakubwa au wadogo? Niambie ili maelezo yangu yaendane na mahitaji yako.


      @LAT. . pole kwa kusubiri bana, recipe yako nimeshaiandaa sema nataka niweke nikiwa na pc ili niweze kuweka na picha vizuri. Jumatatu ndo ntaweka.
      Hi lizzy
      Oh so sorry sikuiona hii post,

      Ninaomba Recipe yenye spices lakini kwa foil, nimejaribu kutengeneza Mara 4 issue imebumaa jamani:
      embarassed:

      Yaani nitashukuru sana, ukinipatia kesho will do my fifth attempt
      Mhandisi wa mifumo na njia kuu za umeme.....

    5. #124
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Swahili Fish Curry (Mchuzi Wa Samaki)

      Swahili Fish Curry (Mchuzi Wa Samaki)
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    6. #125
      Fixed Point's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2009
      Posts : 1,879
      Rep Power : 813
      Likes Received
      381
      Likes Given
      409

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga:
      Mahitaji:
      1. bamia gram 250
      2. Majani ya maboga 200
      3. Nyanya chungu (kama utapenda) gram 100
      4. Magadi 1/4 kijiko cha chai
      5. chumvi - to taste
      6. nyanya ndogo 1
      7. Karanga zilizosagwa gram 100
      8. maji - kikombe 1

      Matayarisho:
      1. Osha na kata bamia na nyanya chungu vipande vidogovidogo
      2. Osha na kata majani ya maboga ndogondogo

      Jinsi ya kupika
      1. Bandika maji mpaka yachemke
      2. weka chumvi na magadi
      3. Weka majani ya maboga, bamia, na nyanya chungu
      4. vikishachemka kwa kama dakika 5, weka nyanya, acha ichemke kidogo.
      5. weka unga wa karanga na acha uchemke kwa kama dakika 5 - 7.
      Tayari kwa kuliwa.
      Mboga hii inapendeza kuliwa na ugali
      No one could ever earn your love, Your Grace and Mercy is free
      Lord these words are true, so is my love for You

    7. LAT is online now
      LAT
      #126
      LAT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 4,481
      Rep Power : 1310
      Likes Received
      1110
      Likes Given
      1653

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      tofauti ya lamb na mutton

      mfano utatofautishaje lamb curry na mutton curry

    8. #127
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Quote By LAT View Post
      tofauti ya lamb na mutton

      mfano utatofautishaje lamb curry na mutton curry
      Lamb: Wakazi wa UK, New Zealand na Australia, wao wanatumia haya majina kama nyama ya Kondoo na Mbuzi ambaye ajakomaa bado ambaye yupo si zaidi ya mwaka tangia kuzaliwa kwake.


      Hogget: ni nyama ya Kondoo ambaye amepita mwaka mmoja tangia kuzaliwa.


      Mutton: Nyama ya Kondoo ambaye amekomaa (an adult sheep).


      Haya majina ya Lamb, mara nyingi utumika kwa Kondoo mdogo na Mutton ni nyama ya mbuzi, na jina lingine ni chevon.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    9. LAT is online now
      LAT
      #128
      LAT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 4,481
      Rep Power : 1310
      Likes Received
      1110
      Likes Given
      1653

      Default

      Quote By X-PASTER View Post
      Lamb: Wakazi wa UK, New Zealand na Australia, wao wanatumia haya majina kama nyama ya Kondoo na Mbuzi ambaye ajakomaa bado ambaye yupo si zaidi ya mwaka tangia kuzaliwa kwake.


      Hogget: ni nyama ya Kondoo ambaye amepita mwaka mmoja tangia kuzaliwa.


      Mutton: Nyama ya Kondoo ambaye amekomaa (an adult sheep).


      Haya majina ya Lamb, mara nyingi utumika kwa Kondoo mdogo na Mutton ni nyama ya mbuzi, na jina lingine ni chevon.
      asante mheshimiwa X-PASTER

      je? unaweza kutofautishaje nyama hizi zinapokuwa zimepikwa?

    10. #129
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Quote By LAT View Post
      asante mheshimiwa X-PASTER

      je? unaweza kutofautishaje nyama hizi zinapokuwa zimepikwa?
      Kila nyama na radha yake... Ukipata nafasi nunua zote ndipo utakapojuwa... Kwa maelezo itakuwa ngumu kidogo.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    11. #130
      Bweri's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th August 2011
      Posts : 40
      Rep Power : 347
      Likes Received
      6
      Likes Given
      2

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      X PASTER mwisho wa wiki nataka kula pizza ya kuku au nyama ya ng،ombe ila sijui hata nianzia wapi mwenye ujuzi plz nisaidie

    12. #131
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Pizza

      Vipimo:
      • Unga.......................... ..4 Vikombe
      • Maziwa ya unga.............2 vijiko vya supu
      • Mafuta ya zaituni...........½ kikombe
      • Hamira........................ .1 kijiko cha supu
      • Chumvi kiasi
      • Sukari........................ ..1 kijiko cha chai
      • Maji vugu vugu..............2 kikombe


      Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Unga
      • Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
      • Ufunike na uache uumuke.


      Sosi Ya Pizza
      1. Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo .. 1
      2. Thomu iliyokatwa ndogo ndogo ....... 3 chembe
      3. Sosi ya HP .............................. .... 3 vijiko vya supu
      4. Sosi ya tomato ............................. 3 vijiko vya supu
      5. Pilipili manga .............................. ... 1 kijiko cha chai
      6. Oregano .............................. ........ ½ kijiko cha chai
      7. Parsley (ukipenda) ......................... ½ ukipenda

      1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
      2. Epua kwenye moto.


      Upendavyo Katika Hivi Au Vyovyote Vinginevyo
      1. Tuna
      2. Nyama ya kusaga iliyopikwa
      3. Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande
      4. Sauage zilizokatwa
      5. Salami
      6. Vipande vya nanasi

      Vitu Vya Kujaza Juu Ya Pizza
      • Nyanya zilizokatwa vipande vipande
      • Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
      • Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
      • Cheese ya Mazorella


      Jinsi Ya Kutayarisha

      1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size kama kwenye picha.
      2. Paka sosi juu ya unga
      3. Tia kiteo upendacho
      4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
      5. Mwagia cheese
      6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive pizza.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)



    13. #132
      Adharusi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd January 2012
      Posts : 111
      Rep Power : 340
      Likes Received
      12
      Likes Given
      1

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Mi napenda wali(biriliani)ila sijui kupika naomba mnielekeze tafadhari
      Iwa mwema
      Wakatabahu
      Adharusi

    14. #133
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      Quote By Adharusi View Post
      Mi napenda wali(biriliani)ila sijui kupika naomba mnielekeze tafadhari
      Iwa mwema
      Wakatabahu
      Adharusi
      Nadhani ukitafuta kwenye hii thread, unaweza kuona mapishi ya biriani.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    15. #134
      snochet's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st March 2011
      Posts : 232
      Rep Power : 611
      Likes Received
      78
      Likes Given
      67

      Default Re: Jukwaa La Mapishi, Food Coner

      JINSI YA KUPIKA KUKU WA KUPAKA

      Kuku katika mchuzi wa nazi)
      viungo
      kata kuku katika vipande 8
      1 kijiko vitunguu
      Kijiko 1 cha tangawizi
      pilipili hoho 2
      pilipili 2
      Juisi ya limau vijiko 4
      1/2 kijiko manjano
      vikombe 2 vya tui
      vitunguu maji 3
      nyanya 2
      chumvi kutegemeana na ladha upendayo
      rosemary


      Method
      Marinate vipande kuku katika vitunguu, tangawizi, pilipili, ndimu, chumvi na mafuta kijiko kimoja na kuloweka kwa muda wa dkk 30. Pika vitunguu kwa kijiko kimoja cha mafuta, kuongeza nyanya changanya vizuri kwenye joto la kati.ongeza pilipili, ndimu na maziwa ya nazi na kuchochea wakati wotei. weka kando. roast Vipande vya kuku juu ya mkaa au katika jiko kwa dakika 10 -1 5 hadi kuiva. weka kuku katika sahani, mimina mchuzi wa nazi nene juu ya kuku wa kuchoma na tena kuweka sahani katika tanuri kwa dakika 10 ,sasa yupo tayari kwa kumtafuna,kuku anafaa na supu mara kwa nyingi.andaa na wali, chapati, mandazi au mkate na kupamba na coriander(optional).mbinu hii inaweza kutumika kwa ajili ya samaki waku paka,pia hata nyama nyingine yoyote

    16. #135
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Smile How to bake rock buns

      Ingredients:

      • 225g Odlums Self Raising Flour
      • 125g Margarine or Butter
      • 75g Caster Sugar
      • 125g Mixed Dried Fruit (to include candied peel)
      • 1 Egg (beaten)
      • 2 tablespoons of Milk
      • Granulated Sugar for topping




      How to bake:
      1. Pre-heat oven to 200°C/400°F/Gas 6. Lightly grease a baking tray.
      2. Sieve flour into a bowl and add the margarine or butter. Rub into the flour until mixture resembles breadcrumbs.
      3. Add the sugar and dried fruit and mix well.
      4. Finally, add the egg and milk and mix thoroughly to give a stiff dough.
      5. Using two forks, lift up small portions of the mixture and place on the baking sheet about an inch and a half apart. The buns should be rough looking, do not smooth them down.
      6. Shake a little sugar on top of each bun and place in the pre heated oven for 10 to15 minutes until golden brown. Leave on tin for about five minutes, then transfer to a wire tray to cool.

      Rock buns are a specific type of pastry, distinguished by the hard, crust-like texture and sweet taste.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    17. #136
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Last edited by Young_Master; 20th April 2012 at 10:24.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    18. #137
      Kongosho's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 12,990
      Rep Power : 3838
      Likes Received
      4956
      Likes Given
      3441

      Default Re: How to bake rock buns

      Asante kwa recipe, do you like cooking?
      This silence tells me you are gone...

    19. #138
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By Kongosho View Post
      Asante kwa recipe, do you like cooking?
      I like it I think more than anything in this world.
      Kongosho likes this.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    20. #139
      Kongosho's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 12,990
      Rep Power : 3838
      Likes Received
      4956
      Likes Given
      3441

      Default Re: How to bake rock buns

      Lucky you.

      Itabidi niwe najichanganya na watu wanaopenda kupika japo na mie nitakuwa interested.

      Quote By Young_Master View Post
      I like it I think more than anything in this world.
      Young_Master likes this.
      This silence tells me you are gone...

    21. #140
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By Kongosho View Post
      Lucky you.

      Itabidi niwe najichanganya na watu wanaopenda kupika japo na mie nitakuwa interested.
      Karibu. Nitakupa somo zuri sana la upishi. By da way why u are not interested in cooking?
      Kongosho likes this.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    22. #141
      BlackBerry's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd March 2011
      Location : Down Town
      Posts : 1,789
      Rep Power : 718
      Likes Received
      893
      Likes Given
      690

      Default Re: How to bake rock buns

      Mimi jeeeee ai wewe
      Young_Master likes this.
      Simple Look But Tough in Wallet

    23. #142
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,734
      Rep Power : 1426
      Likes Received
      1271
      Likes Given
      1727

      Default Re: How to bake rock buns

      itabidi nihamie kwako kama mambo yenyewe ndo haya...weye wapika mie nala au wasemaje?
      Kipipi and Young_Master like this.

    24. #143
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By BlackBerry View Post
      Mimi jeeeee ai wewe
      And you too my dear @BlackBerry
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    25. #144
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By shosti View Post
      itabidi nihamie kwako kama mambo yenyewe ndo haya...weye wapika mie nala au wasemaje?
      Dah! itakuwa poa sana mimi mpishi nikikuangalia ukifaidi huku nikibaki8 namezea mate tu.
      shosti likes this.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    26. #145
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,734
      Rep Power : 1426
      Likes Received
      1271
      Likes Given
      1727

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By Young_Master View Post
      Dah! itakuwa poa sana mimi mpishi nikikuangalia ukifaidi huku nikibaki8 namezea mate tu.
      wamezea mate nini sasa nnavyotafuna au?
      Young_Master likes this.

    27. #146
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By shosti View Post
      wamezea mate nini sasa nnavyotafuna au?
      Hapana ni jinsi unavyonyonya kwa hisia.
      shosti likes this.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    28. #147
      shosti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : M'nyamala
      Posts : 4,734
      Rep Power : 1426
      Likes Received
      1271
      Likes Given
      1727

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By Young_Master View Post
      Hapana ni jinsi unavyonyonya kwa hisia.
      mwe haya si mapishi tena....
      Young_Master likes this.

    29. #148
      Young_Master's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Location : Arusha, Tanzania
      Posts : 3,643
      Rep Power : 1015
      Likes Received
      449
      Likes Given
      173

      Default Re: How to bake rock buns

      Quote By shosti View Post
      mwe haya si mapishi tena....
      Mapishi hayo shosti. Kwani mtu akinyonya kidole kwa hisia si inamaana chakula cha mpishi ni kitamu?
      shosti likes this.
      E-mail: meezy@youngmaster.co.tz

    30. #149
      FirstLady1's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 12,986
      Rep Power : 3061
      Likes Received
      1898
      Likes Given
      2786

      Default Re: How to bake rock buns


      asante sana Young_Master

      Hii nitaijaribu nikipata muda wa kutosha Jpili..
      Nitakutumia Picha
      Zaburi 35:1 Ee Bwana utete nao wanaoteta nami Upigane nao wanaopigana nami.

    31. #150
      Kongosho's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 12,990
      Rep Power : 3838
      Likes Received
      4956
      Likes Given
      3441

      Default Re: How to bake rock buns

      I started cooking when I was an infant.
      Nikachukia kupika moja kwa moja.

      Quote By Young_Master View Post
      Karibu. Nitakupa somo zuri sana la upishi. By da way why u are not interested in cooking?
      Young_Master likes this.
      This silence tells me you are gone...

    Page 5 of 7 FirstFirst ... 34567 LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 3
      Last Post: 1st August 2011, 22:44
    2. Jukwaa la mapishi (food corner)
      By ndetichia in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 6
      Last Post: 19th July 2011, 11:56
    3. Mapishi ya maandazi.
      By Mamndenyi in forum JF Chit-Chat
      Replies: 9
      Last Post: 13th July 2011, 20:57
    4. Mapishi
      By Kimbweka in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 7
      Last Post: 12th November 2010, 09:01

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...