SALAD YA KUKU (CHICKEN SALAD)
Leo nina waletea salad ya kuku.
Kama unavyoona pichani nina vitu vifuatavyo1.chicken breast(nyama ile ya eneo la kifuani la kuku)2.maharage machanga3.mahindi machanga kabisa.4.Hoho za njano,nyekundu na kijani japo haipo pichani5.Karoti6.Broccoli sijui kiswahili chake7.Squash hizo zinazofanana na matango8.Kitunguu maji
MATAYARISHO NA UPISHI WENYEWEUnachukua vipande vya kuku unaviosha vizuri na kuvitia ndimu na tangawizi kisha unachemsha kwa dk 20 maana ni laini sana na rahisi kuiva.Unapochemsha weka chumvi kiasi.Zikiiva unaipua unaweka pembeni.Zikiwa pembeni lile joto ndio unatumia kuivishia kitunguu inamaana hapa ndio utaweka kitunguu maji.
Hakikisha mboga mboga zako umeziosha vizuri kwa maji ya uvugu vugu.Kisha zikate kate weka kwenye sufuria zote kwa pamoja.Baada ya hapo chemsha kwa dk 5 tu ili usiiiue ile kijani lakini zinakuwa zimeiva.Usisahau kuweka chumvi wakai wa kuchemsha.Ipua na weka kwenye bakuli halafu chukua ile kuku kata vipande vidogo vidogo au vikubwa itategemea unapenda vipi.Changanya vizuriiii na inakuwa tayari kuliwa.Unaweza kuongezea ndimu kidogo au veniger itategemea unapendaje.
Ikiwa bado haijapoa unainyunyizia olive oil kwa juu na unaichanganya vizuri.
Pia unaweza kununua jiko maalum la kusteem mboga mboga,nyama,samaki,kuku kwa mvuke wa maji.Yapo yenye muonekano tofauti tofauti mfano ni kama hili.
Try it! and enjoy it!




Reply With Quote




Follow Us Here