Re: Cooking Spaghetti Mixed with Eggs
Kuna mchanganyo katika haya maelezo! Ninadhani:
Hatua ya kwanza ni kuchemsha maji yakishachemka, weka kiasi cha spagheti kulingana na mahitaji
Kaanga vitunguu na nyanya mpaka upate mchuzi mzito, ongezea viungo vingine kadri ya mahitaji (black pepper etc...)
Spagheti ikishakuwa tayari unaweza kuchuja maji na kuchanganya na sauce yako na ongeza vikiwa bado vya moto, ongeza mayai ambayo utakuwa tayari umeshayakoroga na koroga mpaka yai liive na mchanganyiko kuwa tayari.
Kimsingi yai linaivishwa na lile joto, kwa hiyo hakuna haja ya kuweka kwenye moto.
Usije ukasahau kuweka chumvi, labda kama sio mtumiaji wa chumvi
Ndivyo nilivyomwelewa, japo hakueleweka katika maelezo yake.
"If you are going through HELL, keep going..."-W.Churchill
Follow Us Here