Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

    Report Post
    Results 1 to 10 of 10
    1. #1
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,198
      Rep Power : 19212
      Likes Received
      8161
      Likes Given
      26633

      Default VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa


      Maiti ya Gaddafi
      Video mpya imetolewa ikionyesha kwa

      ukaribu zaidi jinsi mwili wa aliyekuwa

      kiongozi wa Libya, Kanali Muammar

      Gaddafi ukichezewa na kuburuzwa

      buruzwa ndani ya gari huku watu wakiupiga picha kwa simu zao.
      Baada ya kukamatwa na kuuliwa kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi mwezi oktoba mwaka jana, video nyingi zilitolewa zikimuonyesha akiwa hai kabla ya kuuliwa huku shati lake likiwa limejaa damu.

      Katika video hii mpya ambayo imeingizwa kwenye internet wiki hii na kuwa gumzo duniani, maiti ya Gaddafi ikiwa kifua wazi inaonyeshwa kwa ukaribu zaidi huku wanajeshi wa kundi la waasi wakiichezea na kupiga nayo picha.

      Haijajulikana ni kwa nini VIDEO hiyo imetolewa sasa lakini video hiyo imekuwa gumzo duniani kufuatia mwanaharakati Sami al-Hamwi kuweka linki kwenye Twitter akisema kuwa rais wa Syria Bashar Assad aiangalie video hiyo kwa ukaribu ili ajifunze yaliyomkuta dikteta mwenzake wa Libya.

      Gaddafi aliitawala Libya kwa miaka 42 kabla ya utawala wake kupinduliwa mwaka jana na yeye mwenyewe kuuliwa na maiti yake kuzikwa jangwani.

      Angalia VIDEO ya maiti ya Gaddafi chini.



      VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa
      Mbuzi Mzee likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    2. Miaka 50

    3. #2
      Mbuzi Mzee's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th October 2011
      Posts : 5,185
      Rep Power : 3522
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      3590

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Hizi video zinatisha mkuu

    4. #3
      Father of All's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 3,093
      Rep Power : 1044
      Likes Received
      1829
      Likes Given
      3343

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Ni burdani tosha na somo kwa watawala wetu wezi na wajinga. Nimeiangalia zaidi ya mara saba na kujisikia furaha ingawa si vizuri kushabikia kifo cha binadamu. Hakuna film zenye kufurahisha na kufundisha kama ile ya mauaji ya Samuel Doe, kunyongwa kwa jahid Saddam na hii ya kufilishwa kwa Gaddafii. Malipo ni hapa hapa duniani. Heri mbwa kama Mobutu, Bongo, Eyadema, Banda, Kenyatta, Mengistu, Mugabe, Abacha na wengine yangewakuta haya.
      asigwa likes this.

    5. #4
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,420
      Rep Power : 5039
      Likes Received
      785
      Likes Given
      1796

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Duh, watu walikuwa wamekula si milungula au bangi! Lol kweli matendo ya mtu yana impact kwenye aina ya kifo.
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    6. #5
      Gosbertgoodluck's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 2,863
      Rep Power : 1149
      Likes Received
      334
      Likes Given
      4

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Laana hiyo itawatafuna walibya mpaka wakome.
      jamiif likes this.

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Daudi Mchambuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 6,190
      Rep Power : 1954
      Likes Received
      2997
      Likes Given
      13635

      Default

      Sasa hebu uliza maisha ya libya baada ya kifo cha gadaffi yakoje??
      watamkumbuka milele kenge maji hawa.

      Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
      jamiif likes this.

    9. #7
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 980
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Quote By Father of All
      Ni burdani tosha na somo kwa watawala wetu wezi na wajinga. Nimeiangalia zaidi ya mara saba na kujisikia furaha ingawa si vizuri kushabikia kifo cha binadamu. Hakuna film zenye kufurahisha na kufundisha kama ile ya mauaji ya Samuel Doe, kunyongwa kwa jahid Saddam na hii ya kufilishwa kwa Gaddafii. Malipo ni hapa hapa duniani. Heri mbwa kama Mobutu, Bongo, Eyadema, Banda, Kenyatta, Mengistu, Mugabe, Abacha na wengine yangewakuta haya.
      nakushauri sherehekea kila anapokufa mtawala mbaya maana ni njia ya ziada kuukomboa umma unaoonewa wakati wowote kifo cha muonezi ni kizuri na tuzidi kuwaombea umauti hata viongozi wetu wa kitanzania kwa maana ndio njia rahisi ya adhabu itakayowaondoa huku ikiliacha taifa likiwa salama bado.tofauti na sasa kama tukiamua kutumia nguvu tutaathiri hata watoto na mama zetu maana baadhi ya viongozi wetu hulinda madaraka hata kwa damu za watu mungu akubariki kwa kiboresha siku yangu.
      LIMPETA

    10. #8
      jamiif's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2012
      Posts : 956
      Rep Power : 547
      Likes Received
      242
      Likes Given
      511

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      ....dunia mapito jamani...tusijisahau na kuanza kuhukumu wenzetu...nasi hukumu yatungoja!!!!

    11. #9
      Ibnu Mussa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th June 2012
      Posts : 19
      Rep Power : 511
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Nyinyi walibya hamkumuua gaddafi mmejiua wenyewe . Poleni sana ndugu zangu mtakufa njaa sasa kama wasomali.

    12. #10
      Mtumzima's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th September 2008
      Posts : 13
      Rep Power : 548
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default Re: VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa

      Mimi nina mawazo tofautikidogo kuhusu kuuawa kwa Muammar Gadaffi.Mabeberu wa magharibi na washirika wao,walitumia kisingizio cha kukaa kwa muda mrefu madarakani kwa mtawala huyo.Lakini walinyang'anywa akili na muda mfupi baadaye Waingereza walisherehekea kwa mbwembwe nyingi kutimiza miaka 60 ya kiutawala ya malkia Elizabeth anayepoteza kumbukumbu kwa umri aliokuwa nao.Walishasahau kwamba Muamar Gadaffi alitawala miaka 42 tu.Nikimjibu member wa JF,Father of All,ni kwamba asifurahie hali hii kwani nyuma ya hili kuna uozo mkubwa sana.
      Magenge ya siri ulimwenguni yakitumia watawala walafi duniani wanaendesha kampeni chafu za kupora maliasili za watu,kwa kisingizio cha demokrasia na utawala bora.Ukirudi nyuma mwaka 1776 tarehe 01/05 ndipo Genge hili lilipoasisi katiba yake (GREAT SEAL).Ndani ya katiba hiyo haramu kuna maazimio mengi na taratibu nyingi walizoziandika ili kufanikisha azma yao ya kutawala kwa mabavu na dhuluma.Sisi huku tunaambiwa ni siku ya wafanyakazi duniani (May Day)!!Bila ya sisi kujua ya kwamba genge hili limetupatia jina la "USELESS EATERS"!Genge hili linalojulikana kama ILLUMINATI ni hatari kuliko unavyojua.Kwa kifupi Genge hili na mengineyo kama FREEMASON n.k ndiyo yanayodhibiti karibu kila kitu kisiasa,kiuchumi n.k.Hata vyombo vya habari na propaganda zote zinafanywa na magenge hayo.Pointi yangu ni kwamba sisi nchi maskini afrika tunaona yanayoendelea ni mageuzi ya kisiasa kwa faida yetu,lakini kumbe ni maangamizo yetu sisi na vizazi vijavyo.
      Tumeelezwa ya hao mahayawani kwamba wameanzisha gereza maarufu la GUANTENAMO kwa ajili ya magaidi,lakini ukweli hapo ni chuo cha kuwafundisha magaidi wanaotumiwa na mataifa makubwa kuingia na kuanzisha vurugu katika mataifa yale yenye raslimali kama mafuta na madini.Wakishaingia katika nchi fulani wanajulikana kama WAASI.Waasi hawa wanatokea kuwa na nguvu sana kisilaha na katika medani za kivita!Kwa kifupi ni kwamba LIBYA,MISRI ALGERIA na SYRIA ni katika wahanga wa operation hii ya kinyama.Mengine ni BOKO HARAM,AL QAEDA,JANJAWID na AL SHABAB.Yote haya ni magenge madogo yaliyotengenezwa na mataifa makubwa kwa maslahi yao.AMKENI JAMANI!!!Msishangilie tu mambo bila kuyaelewa kilichopo katika hilo.
      Vyombo vingi vya habari vipo chini ya Genge hili ILLUMINATI.
      Jaribu kutazama ni kwa nini wakati Gadaffi ameuawa walionekana wanaofurahia kifo chake!!Je ina maan ahakuna binadamu yoyote aliyehuzunika????Hili ni jambo la kufikiri kabla ya kushangilia.

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...