Rais Kikwete akipanda ngazi kuangalia Pantoni inayotengenezwa huko Mwanza. Picha na Fredd Maro wa Ikulu
Kulikuwa na ulazima kweli na makamera yote hayo...??? mweh!!
Rais Kikwete akipanda ngazi kuangalia Pantoni inayotengenezwa huko Mwanza. Picha na Fredd Maro wa Ikulu
Kulikuwa na ulazima kweli na makamera yote hayo...??? mweh!!
[email protected]
Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji
Jamani suala la safety katika mambo ya uhandisi linapewa kipaumbele . Mtu yoyote aliyeko katika hilo eneo anatakiwa avae helmet achilia mbali kupanda ngazi . Inasikitisha sana kumwona rais wetu akifanya mambo ya kitoto kabisa ...No safety belt , No helmet . Nakumbuka kuna kipindi mkapa alifungua mgodi wa geita na mara alipoingia tuu ndani ya mgodi kitu cha kwanza walichompa ni helmet na safety shoes. Na hata waheshimiwa wengi waliokuwa wanatembelea pale wakiwa wamevaaa tai waliombwa kuvua kwani ni hatari sana katika yale maeneo
Kitu muungwana anachofanya ni kibaya sana kwa sababu anaweka maisha yake matatani na ya wale wanaomzunguka . Kusema ya kuwa mkapa ni mnene na asingeweza kupanda ngazi ni utoto ...Hoja sio unene bali ni kitu alichofanya Rais wetu ni sahihi , na jee ni ujumbe gani anaoutuma kwa watanzania wengine. Jamani ni lazima huyu mtu ajifunze kuongoza kwa mifano.
Hii picha inatufundisha kitu kimoja , kwama JK hayuko serious au hajui nini anachofanya PERIOD.
Last edited by Rufiji; 11th May 2007 at 14:40.
rufiji
chukua 5,kutembea ni kuona mengi.
TVT wametunyima raha yakuona raisi wete anapopanda kgazi.That would the best item of the News Broadcast today.
Sina tatizo na lengo la JK kukwea huko juu, ila najiuliza kwanini wataalamu wetu wanawaachia viongozi kuvunja sheria ama taratibu kwa kutumia madaraka yao? Tuwaseme hawa! Ni kasumba mbaya na hatari.
Pili, watu wausalama wanafundishwa nini katika mafunzo yao? Nadhani neno "hatari" linatakiwa kutanuliwa zaidi kwao.
I am still optimistic on the good of our land and the best of my people, only if few of us in the ring or wish to be in the ring ready to think, work, sacrifice not for us, only in the name of our grandchildren
Kama Muungwana alipangiwa ratiba ya kupanda huko, wahusika wa huo mradi(pantoni) wakishirikiana na wasaidizi wa JK walitakiwa waangalie suala la usalama(hasa helmet na ovaroli). Hata kama aliomba/aliamuru yeye mwenyewe bado wahusika walitakiwa waangalie kipengele cha usalama. Sitaki kuamini kama mafundi wanafanya kazi peku peku.
Vinginevyo, inaweza kuwa tabia ya wabongo kuwa waoga na wanafiki wa kupindukia kumweleza Muungwana kwamba kuna masharti/sheria za kufuata ukitaka kupanda huko.
Watanzania mbumbumbu wamemchagua raisi dhaifu ajenge taifa la watu wasiojiamini, 2010/2015 - Tafakari
Invincible,
Mnashangaa hayo?
Je, mnajua ya kwamba lile Ferry alilopanda kuvuka Kisorya (Mwibara) na kuingia Ukerewe halina/halikuwa na hata maboya!... watu huvuka kwa uwezo wa Mungu tu na sio kwamba haijawahi kutokea... Ferry hilo limewekwa baada ya la kwanza kuzama na kuua watu sii chini ya 100.
Exploration of reality
Amani Iwe Nanyi,
Camerlengo
Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka
"Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun
'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"
Huyu ndiye JK kwa mamilioni ya waliompigia kura.
Nyie wazee wa protocals, formalities na mengineyo mlishakuwa na wenu kwa miaka kumi iliyopita na mkamgeuka vilevile. Waachieni wengine ambao tupende tusipende ndio wengi wajinome na mwenziwao akiwa katika usukani.
Tanzanianjema
Pasipo na IMANI kuna Uovu, Pasipo na MISINGI kuna Ufedhuli, Pasipo na ITIKADI kuna Ujanjaujanja...Yote haya ni mazalia ya UFISADI
Pasipo na IMANI kuna Uovu, Pasipo na MISINGI kuna Ufedhuli, Pasipo na ITIKADI kuna Ujanjaujanja...Yote haya ni mazalia ya UFISADI
’’I came to this country (Tanzania) without a single penny; a beggar. True, I had not a single penny, but I was not a beggar. I came with a brain worth millions of dollars ... supported by education and exposure.’’
Hivi kulikoni yuko wapi..?maana najua anaweza kutupa "valid Explanation" ya hii kitu, inabidi wananchi wahoji hii kitu, ina maana watu wa PSU hawakujua Rais atakwea ngazi, katika pilika pilika zangu za kusoma vitabu vya SS when it comes to the President's safety there is a person who can always say No to the President and he listens to him or her.
Hating gets you no where, have a safe trip!
....we bongo unaweza kumwambia rais asifanye kitu fulani...wakati yeye keshavua nguo ayaoge maji!...sijui,mi sijasikia!
hivi?mtu ka jk unaweza kumwambia...."mh,hao watu ni wengi,usiwasalimie wote,tutachelewa safari" halafu akakukubalia?...yaani hiyo yote ndani ya bongo...sijui.
hata mi kwa uswahili wangu pale ningepanda bila hilo kofia....mbona minazi tunakwea bila shida...itakua hicho kipande kidogo tu.....utan'samehe uswahili wangu[at times we are very local]!
labda ulaya na si tz,ndugu yangu!
Dar na Lamu yote miji ya pwani, lakini haifanani!
Unajua sioni hata mtu kuzuia ile ngazi toka chini!.. ama ndio picha yenyewe haikuonyesha!...
Yote tisa hili ni kosa la nani?
Exploration of reality
...hivi walipokuwa wakiingia kwenye hiyo sehemu,kulikuwa hamna kofia?....au ndio hali halisi kama ilivyo kwa bongo....vifaa vya usalama hadimu maeneo ya kazi!
Dar na Lamu yote miji ya pwani, lakini haifanani!
Kama uliangalia Tarifa ya Habari - ITV ungeona sii pekeya alipanda hiyo ngazi.Walikuwa wengi nyumayake. Lakini hawakuoneswa wanapopada.Only when they were up there on the deck were they shown.They were playing "Follow The Leader".
kama mchangiaji mwingine alivyosema, kuna watanzania kibao, wanapanda minazi, na mikarafuu, bila vifaa vyovyote vya kujikinga.
kwenye site nyingi za ujenzi utakuta mafundi wamevaa mifuko ya sementi wanabeba zege wakiwa vifua wazi. tena hata hizo ngazi za kubebea zege ni za wasiwasi kuliko hiyo anayotumia raisi.
Raisi anafahamu kwamba hata akianguka na kuumia atapelekwa AFRIKA KUSINI au ULAYA kwa matibabu. Sioni sababu ya kumhoji. Sana sana najiuliza wale walalahoi wenzangu wanaovaa mifuko ya sementi na kandambili, wakiumia inakuwaje?
NB:ukiangalia vizuri hiyo picha utaona kuna mafundi wamevamaa nguo za blue. hakuna hata mmoja mwenye kofia ya kujikinga.
Follow Us Here