
By
X-Paster
Bwana Balozi wa Lamu:
Mtu huyo mrefu, ambaye hadithi zake nyingi zilisimuliwa katika nchi ya wazulu, na ambaye katika watu wake huitwa “Gogota,” na “Mchinjaji” alishtuka, na shoka lake la vita lenye kipini kirefu lilikuwa karibu kumponyoka kwa mshangao na mara ile alinitambua akawa ananiamkia.
Mkuu, mkuu wa zamani, mkuu, mkuu! Baba! Makumazahn, mzee mwindaji, mwuaji wa tembo! mla simba, mwerevu! akeshaye! hodari! mwepesi! ambaye risasi zake kabisa hazikosi shabaha, apigaye shabaha ya kweli, rafiki mwaminifu. Mkuu! Baba! Ile methali ya kikwetu isemayo 'Milima haikutani lakini wanadamu ukutana,' ni ya kweli kabisa na yenye busara. Tazama! tarishi alikuja toka Natal, akalia, 'Makumazahn amefariki! Nchi haitamwona Makumazahn tena.' Haya yalitokea zamani sana. Na sasa, tazama hapa katika nchi ngeni ya harufu mbaya namwona tena Makumazahn, rafiki yangu. Ndiye bila shaka. Manyoya ya mzee bweha yameingia mvi; lakini macho yake na meno yake ni makali kama zamani. Ha! Ha! Makumazahn, unakumbuka namna ulivyoipeleka risasi katika jicho nyati aliyekuwa akishambulia... unakumbuka..."
Basi, nilikuwa nirnemwacha aendelee hivyo, kwa sababu niliona ya kuwa wale Wakazi watano walionekana kwamba wanaweza kufahamu maneno mengine katika yale aliyoyasema, tena yanawatia fikira; lakini sasa niliona inafaa kumkomesha, maana hakuna kitu kinachonichukiza kuliko desturi ile ya Wazulu iitwayo kubonga, yaani kusifu kupita kiasi. Nikasema, "Nyamaza! Ala, maneno yako yenye kelele yamezibwa tokea tulipoachana, na hii ndiyo sababu yanabubujika na kutugharikisha hivi? Unafanya nini hapa pamoja na watu hawa, wewe ambaye tulipoachana ulikuwa mfalme katika nchi ya Wazulu? Umekujaje hapa katika nchi iliyo mbali na kwenu, na kukaa pamoja na wageni?"
Umslopogaas aliliegemea shoka lake refu la vita, ambalo kipini chake ni kipande kizuri cha pembe ya kifaru, na uso wake ulikuwa umejaa huzuni, kisha akawatazama wale wakazi, akasema, “Baba yangu, ninazo habari nitakazo kuambia, lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyone hawa, maneno yangu ni baina ya mimi na wewe tu.
Mwanamke alinihaini mautini, akalifunika jina langu kwa aibu, ndiyo, mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi, alinihaini, lakini niliokoka na mauti;
ndipo rnlipoponyoka katika mikono ya wale waliokuja kuniua. Nilipiga mapigo matatu tu kwa shoka langu hili Inkosikazi- hakika baba yangu atalikumbuka moja upande wa kuume, moja upande wa kushoto, na moja mbele yangu, na hata hivyo niliwaacha watu watatu wamekufa. Kisha, nilikimbia, na kama baba yangu ajuavyo, ingawa mimi ni mzee, lakini miguu yangu ni myepesi kwenda mbio kama ile ya paa, wala hapana anaye weza kunigusa tena niishapo kutoka mbavuni pake. Mbele nilikimbia na matarishi wa mauti waliniandama nyuma, na sauti zao zilikuwa kama sauti za mbwa wanaowinda, Kutoka nyumbani kwangu nilikimbia; nikampita yule aliyenihaini alikuwa akiteka maji kisimani. Nilimpita upesi kama kivuli cha mauti, na nilipokuwa nikipita nilimpiga dharuba moja kwa shoka langu, tahamaki! kichwa chake kilimtoka, kikaangukia kisimani. Kisha, nilikimbilia kaskazini. Siku baada ya siku nilisafiri; kwa miezi mitatu nilisafiri, nisipumzike, nisisimame, ila nilizidi kukimbilia kwenye usahaulifu, mpaka nilipoonana na safari ya yule mwindaji mweupe aliyekwisha kufa, nami nimekuja hapa pamoja na watumishi wake. Wala sikuleta kitu pamoja nami. Mimi niliye mtoto wa watu, ndiyo, wa damu ya mfalme mkuu Chaka, mimi niliye mkuu mwenyewe, jemadari katika kikosi cha Nkomabakosi, sasa mimi ni mgaagaa, mtu asiye na nyumba. Wala sikuleta kitu pamoja name ila shoka ili langu; kwa nguvu zake ambazo kwazo nilitawalawatu wangu.
Wamewagawanya ng’ombe zangu; wamewatwaa wake zangu; na watoto wangu hawautambui uso wangu tena. Hata hivyo, kwa shoka lili hili nitakata njia nyingine nifike mpaka kwenye ustawi. Nimesema!” Basi, akalizungusha shoka lake kichwani likalialia lilipokuwa likiikata hewa.
Follow Us Here