Hii ni funika kombe mwanaharamua apite, Marekani kwa kuzua conspiracy stories ndiyo wenyewe:
- How war benefits USA Economy?
- Nani waliomuua John Fitzgerald Kennedy?
- Bay of Pigs invasion?
- 'Civil War in Congo, Sierra leone'
- Weapons of Mass destruction?
- USA Fighting marxist/communist idealogy in 1970s Latin America?
- Wikileaks
Mimi nadhani hapa hakuna kipya, kwani kila mmoja anaelewa kazi za maafisa ubalozi ni pamoja na ujasusi ndiyo maana kuna maafisa ubalozi wanaojificha chini ya majina haya 'military attaches', 'Education attaches', 'Economic Development attaches' n.k lakini kazi yao kubwa ni masikio na macho ya Usalama wa Taifa wa nchi zao.
Hapa dunia inafunukwa macho iweweseke na utamu wa story za Wikileaks huku Marekani inanufaika kwa kuchonganisha nchi kama Bahrain dhini ya Iran au kuchonganisha Saudia dhini ya Irani. Si tumesikia hii November 2010 wataalamu wa nuklia huko Iran wameshambuliwa na majasusi wa nje wakati wakielekea maofisini kwao na Iran inasema ni kazi ya Israeli na maswahiba wake wa nchi za Magharibi pamoja na Marekani.
Marekani inajua kuwa sasa kuna vyombo vikubwa vya habari ambavyo si vya kimagharibi vilivyo na heshima zaidi ya Voice of America (VOA) au BBC au CNN mfano vyombo ya RussiaToday, Aljazeera n.k
Hivyo hii Wikileaks ni chombo cha propaganda kusambaza habari za nchi za magharibi kujijengea hoja kuzishambulia nchi za kimapinduzi kama Venezuela, Iran, Cuba n.k
Hii Wikileaks habari zake mbona hazipewi uzito mkubwa na vyombo vya habari ndani ya Marekani yenyewe? hii ni kwa sababu Wa-Marekani wanajua na wameshastukia mikakati inayosukwa na serikali yao yenyewe kuhalalisha kuanzisha vita katika maeneo mengine ya dunia mfano kifo cha Rais J.F Kennedy kilisukiwa hoja kuwa Fidel Castro wa Cuba anahusika!
Uchumi wa Marekani na nchi za Magharibi unaendeshwa kwa kusababisha vita kwa kuwa viwanda vya silaha ndivyo vinavyokuza uchumi wa nchi hizo pamoja na kuhodhi biashara ya mafuta. Hata Tanzania tumeathirika kwa kuuziwa radar na BAE na kisha serikali ya Uingereza kufukia kashfa chini ya zulia kwa kuwa Uingereza imenufaika kiuchumi na kiajira kwa kuuza radar hiyo ya kijeshi kwa Tanzania.
Hii Wikileaks ni conspiracy story nyingine ya kuitawala dunia kimawazo kwa kisingizio kuwa Wikileaks ipo huko nchi ya Skandinavia hivyo nchi za kibeberu hazihusiki na hivyo tuzame na kaamini habari hizi kijuu-juu.
Follow Us Here