Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dual Citizenship: Progress & Solutions

    Report Post
    Page 2 of 24 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 473
    1. #1
      Saidi Yakubu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th March 2006
      Location : colchester,united Kingdom
      Posts : 109
      Rep Power : 790
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Arrow Dual Citizenship: Progress & Solutions

      Naam wanajukwaa

      Nafurahi kujiunga na JF, nachukulia jukwaa hili kama ni sehemu ya kujifunza.

      Takwimu za tanzania zinaonyesha kuwa kuna watanzania zaidi ya 1.2m wanaoishi nje ya nchi [rejea ripoti ya Tanzania Law Review Commission]. Naam hii ni karibu 3% ya taifa zima.

      Nadhani wakati umefika sasa serikali ikapitisha sheria kuruhusu raia hawa kuweza kufaidi matunda ya uraia wa nchi mbili kwani kwa sasa wengi wanakwazwa na kuwa wakiamua kuchukua uraia mwingine inabidi waamue kuachia uzalendo wao.

      Swali hili niliwahi kumuuliza mheshimiwa Sumaye alipokuja hapa Uingereza mwaka jana akakiri kuwa ni muhimu kuruhusu lakini hakuweza kutoa sababu kwa nini hasa mpaka sasa Tanzania imeshindwa kuwa sheria ya kuruhusu uraia wa nchi mbili.

      Sasa hivi watanzania wengi wanaoishi Uingereza na nchi nyinginezo za Magharibi wanaweza kupata misaada kadhaa ya kuwekeza nchini mwao lakini kwa vile wengi wameamua kuwa na uraia wa nchi mbili bila kuachia uraia wao wa TZ basi inakuwa hawawezi kuwekeza nyumbani na kama watawekeza wataweka katika mfumo usio rasmi kama vile kuwatumia ndugu na jamaa pesa ili waweze kuwekeza,matokeo yake ni kuwa kwa vile ndugu hana uwezo wa biashara au kutokuwa muaminifu inakuwa ndio hivyo tena hela zinakwenda na hakuna linalofanyika,hii ina athari zaidi kwani mtu huyu hutotegemea akamhimiza mwenzie wa tanzania kuwa kawekeze nyumbani.

      Naam mniwie radhi wanajukwaa nadhani ngwe yangu hapa mtandaoni italelemea zaidi katika kuwawezesha na kuwajali raia wote wa tanzania na kwa vile tuna asilimia 3% ya hawa wapo nje basi nao inabidi waainishe hoja zao ikiwemo na matatizo wayapatao,mwishowe waweze kuwa nao ni washiriki wazuri wa shughuli za kiuchumi Tanzania.

      Mfano wa China ututoshe:
      Kuna wachina 48 milioni nje ya nchi yao.Kuna wizara ya kushughulikia wachina waliopo nje ambayo inakuwa ni kama kiambatanishi cha wizara ya mambo ya nje ambapo wana jukumu la kuhakikisha kila mchina mwenye uwezo wa kutoa mchango kwao anawezeshwa bila vikwazo na pia wachina waliopo nje waweze kuwa wanapata habari na taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi,siasa,jamii nk wakati wote.

      Angalia kwetu:

      Balozi zetu zipo mbali na watanzania au tusema baadhi zimejitenga sana,ni kwa sababu kuwa karibu au mbali kunategemea na hulka ya balozi husika,kama ni mtu wa watu basi watu 'watajichanganya' kama sivyo basi watu hola! Nukta ni nini hapa? ni kuwa inabidi kuwe na ainisho maalum kwenye kazi za balozi katika kuwashughulikia watanzania.

      Inatokea Rais anakuja kwenye nchi husika balozi anamkimbiza asionane na watanzania!

      Natumai Ari mpya haitokuwa hivi na mabalozi nao watawajali watanzania hawa. Maoni yanakaribishwa, ''i stand to be corrected''
      Last edited by PainKiller; 28th December 2007 at 19:49. Reason: altered icon


    2. #21
      Kamundu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2006
      Posts : 1,391
      Rep Power : 921
      Likes Received
      299
      Likes Given
      9

      Default

      Mwanakijiji, uraia wa nchi mbili una affect nchi postively, mfano itatuwezesha sisi kutokuogopa ku own land, bank accounts, etc kama mtu ukituma pesa nyumbani ina saidia serikali maana uliwatumia pesa wanaitumia nyumbani. Kuhusu account za watanzania walio nje je unajua mwaka jana watanzania wa nje wali deposit $2million CRDB, Je ukiruhusu uraia wa nchi mbili ni kiasi gani watu wata deposit??. Exchange rates zetu mnaziona zilivyo, huu ni wakati muafaka kuruhusu watanzania wote wenye uraia na wasio na uraia ku invest back home bila mashaka ya sheria.

    3. #22
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default

      Maneno ya bwana Said kweli kabisa... nilikuwepo hukooo! navyofahamu Duo ndio imesha pita washikaji kwa hiyo ni uzalishaji tu! kazi kwenu.
      Maneno hayo! hongera JK na EL kwa hili moja lakini tutakuja na mapungufu yake itakapo bidi.
      Exploration of reality

    4. #23
      Field Marshall ES's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 27th April 2006
      Posts : 13,740
      Rep Power : 0
      Likes Received
      329
      Likes Given
      208

      Default

      Mzee Yakubu "Gowon"

      Kama kawaida ndugu yangu heshima kwako mkuu,

      maneno mazito lakini hiyo tutawaachia nyie mlioko majuu muamue, lakini ninajua kuwa Mzee JK, alishawatuma wapambe kule Eritrea, kulisoma hili jambo kwa makni maana wao wanalo hilo tayari, na kwenye hili ninamuamini kuwa atalitimiza, sasa kazi kwenu!

    5. #24
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3357
      Likes Received
      245
      Likes Given
      0

      Default

      unajua suala hili halihitaji petition kama hawataki DC then Globalization ita catch up nao then itakuwa ayaaaaaaaaaaaa jamani msahau yaliyopita and so on

    6. #25
      Eric Ongara's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th September 2006
      Posts : 244
      Rep Power : 701
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default

      Ni mada nzito hii,
      sina uelwa wa kutosha na eneo hili, ila kwa tafakari ya haraka naomba tusaidine kujibu mawswali haya yanayonitatiza

      Je kwa kuwa na uraia wa nchi mbili kuna baadhi ya haki unazipoteza? Kwa mfano,mtue aliepata uraia kwa kuomba hawezi kuwa raisi wa Tz, je kwa mtu mmwenye uraia wa nchi mbele inakuaje?

      Upo uwezekano ukawa kiongozi wa Marekani kisha baadae Tz?

      Je,hii haiwezi kutumika vibaya na raia wageni kupata kazi Tz? Maana sasa yapo madai kwamba kazi ambzo wa Tz wanaweza kufanya hakuna haja ya kuwapa wageni katika mtazamo wa kulinda soko la ajira la wazawa.

      Ikiwa tuna sheria hii, wageni hawawezi kutumia upenyo huu kupatia kazi na kuwaweka benchi watz?

      Ni vyema mjadala huu usiangalie faida za watz walioko ughaibuni peke yake,tukumbuke kwamba kuna wimbi kubwa la wageni linakuja afrika,maana muelekoe wa watu mara nyingi ni kuelekea kwenye mali.

      Nitaendelea kuchangia zaidi


    7. #26
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,698
      Rep Power : 2911
      Likes Received
      3891
      Likes Given
      12465

      Default

      Eric,
      Kwa kukusaidia kijuu juu tu, rais wa sasa wa Afghanistan ni raia wa Marekani. Kuna Wapoland wengi tu waliokuwa wamehamia Marekani ambao sasa wamerudi kwao baada ya ukomunisti kutokomea. Labda kwa Mtanzania, mathalan umechukua uraia wa Uingereza, baadaye ukarudi nyumbani, benefits zitakuwa kwamba hutapoteza haki yako kule bongo, pamoja na haki ya kugombea ubunge kule Moshi, if that is what you want. Ni hayo tu kwa mtizamo wangu finyu.

    8. Dua is offline
      Dua
      #27
      Dua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2006
      Posts : 3,534
      Rep Power : 1369
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default

      DUAL CITIZENSHIP


      Hili swala sio muhimu sana kwa sasa ukilinganisha na maswala ya EA Federation, Umeme and the like. Hawa jamaa wasijaribu ku-divert attention kwa sababu dual citzenship will come weather they like it or not.
      Dua la kuku halimpati mwewe

    9. #28
      Interested Observer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2006
      Posts : 976
      Rep Power : 877
      Likes Received
      92
      Likes Given
      102

      Default

      Hi Dua,

      Hebu fafanua hapa:
      "kwa sababu dual citzenship will come weather they like it or not".

      Mie siamini kabisa dual citzenship ni beneficial kwa waTanzania, how can your citizen benefit while they are 99% poor and uneducated (global perspective)?

    10. Dua is offline
      Dua
      #29
      Dua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2006
      Posts : 3,534
      Rep Power : 1369
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Dual Citizenship

      Quote By Interested Observer View Post
      Hi Dua,

      Hebu fafanua hapa:
      "kwa sababu dual citzenship will come weather they like it or not".

      Mie siamini kabisa dual citzenship ni beneficial kwa waTanzania, how can your citizen benefit while they are 99% poor and uneducated (global perspective)?

      Interested Observer

      Wellcome back I haven't seen your late postings

      I will give you a very simple example;

      Many Tanzanians are working overseas right now and they’ve married non-Tanzanians.

      Watoto wao watakuwa watanzania kwa upande wa baba (kama baba ni mtanzania na kwa kinamama ni tofauti inabidi wawe kwa upande wa baba tu [kuna ubaguzi hapa]), according to sheria zetu za sasa na vilevile itategemea nchi ambayo wapo- Mfano kama nchi hiyo iko kwenye Umoja wa jumuiya ya madola sheria zake zitakuwa hazipingani sana na za Tanzania i.e. mtoto huyu akimaliza miaka 10 katika nchi ile anaomba citizenship ambayo ni halali yake ambayo atapewa. Kwa hiyo tayari mtoto huyu ana citizenship mbili ingawa sisi Tanzania tunasema hatutaki.

      Sasa huyu mtoto akija Tanzania anachagua asafiri na passport ipi? Hiki ni kitu ambacho kipo sasa hivi kama huelewi ninakufahamisha.

      Kuhusu benefit kwa Tanzania – kwa sasa hivi mfano mdogo tu CRDB pale nyumbani watanzania wa nje ya nchi walideposit $2 million mwaka jana na hizi ni katika benki moja tu (one member mentioned this ... Kamundu), je zile ambazo watu wamepeleka kwa ndugu zao bila kupitia benki ni ngapi? Nchi nyingi tu zinanufaika na wananchi wake kufanya kazi nje, mfano India, Egypt na nyinginezo ambazo katika bajeti zao kuna kiasi ambacho kinajulikana kimetoka kwa raia wao wafanyao kazi nje.

      Sasa Tanzania badala ya kukopa kwa high interest kutoka IMF and the like wanaweza kutumia fedha za kigeni ambazo zinatokana na wananchi wake.

      Mfano wa mwisho UK wamekataa kuingia kwenye EU currency kwa sababu wanafaidika vilivyo na mapesa yaliyolundikwa na waizi kutoka Africa na kwingineko pamoja na wananchi wake walio nje na makampuni ambao wanaweka pesa zao kule. (kila jambo kubwa huanza na dogo – tunao watanzania ambao wamefungua makampuni nje na wengine watafuata kinachotakiwa ni kuwasaidia).

      Sio kwamba kila Tom Dick and Harry watataka dual citizenship, ni watu wachache tu ambao wana interest in both countries through marriage etc.

      I disagree with you that 99% of Tanzanians are uneducated, there are a lot of people educated and I don’t want to go in that line at the moment.
      Dua la kuku halimpati mwewe

    11. #30
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,698
      Rep Power : 2911
      Likes Received
      3891
      Likes Given
      12465

      Default

      Dua,
      Good points, good points!

    12. #31
      Pedro's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th November 2006
      Posts : 153
      Rep Power : 674
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      the bottom line, kuwa na uraia wa nchi mbili hahusiani hata kidogo na maendeleo ya nchi bali uhusiana na maendeleo ya mtu husika. Hata hivyo, kutokuwa nao hauhathiri maendeleo ya nchi wala hamuathiri asiyekuwa nao.Je uraia wa kuwa Mtanzania na Mkenya unafaida gani? au Mtanzania na Mmsumbiji? Of course, uraia wa namna hiyo unaozungumziwa zaidi ni ule wa Mtanzania/Mmarekani, Mtanzania/Mwingereza nk n.k

      Let me think of this a little bit more.. that is my first reaction.. nikifikiri zaidi I might come with some interesting ideas

      Mzee mwanakijiji hapo ninatofautiana na wewe kabisa, nchi nyingi zimefaidika sana na mfumo huu, mfano mkubwa kabisa ni India ambapo wahindi wote waliokuwa pale silicon valley USA wengine hata hawakuwa wazaliwa wa India ila ni wazazi wao ndio walikuwa wahindi, wao wameteremka kule india na kuanzisha silicon valley pale Bangalore, na India sasa hivi kutokana na wataalam kibao waliotoka nje unaambiwa uchumi wao unakuwa sio mchezo na vijana wanaomaliza shule pale india karibu wote wanapata ajira siku hizi!

      Nchi kama Pakistan hawana export nyingi isipokuwa wanakitu wanaita export of labour, yaani watu wao wanaofanya kazi nje ndio chanzo cha fedha za kigeni kwa asilimia kubwa tu, hii inatokana na jinsi wanavyotuma fedha za kigeni kwa watu wao na jinsi wanavyodeposit fedha zao pale vilevile.

      Kwa hiyo Dual citizenship ni bomba sana kwa watu binafsi na nji nzima kwa ujumla.

    13. #32
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,700
      Rep Power : 21825
      Likes Received
      750
      Likes Given
      3275

      Default

      Dua, well said,

      Hili jambo litapitishwa tu na serikali ili kuwalinda vigogo na watoto wao na ndugu zao kwani wengi tu tayari wana passport mbili mbili, kwa hiyo kinachofanyika hivi sasa serikalini ni paper work.

      Ni kweli watu walio nje wamewekeza sana nyumbani, njia moja wapo ikiwa ni kwa kutuma pesa nyumbani kwa ajili ya kazi na miradi mbali mbali, tena wakati hawana hiyo dual citizenship

      Sasa je, kuwa na uraia wa nchi mbili ndio kutaongezea nini?? labda mnieleweshe hapa.

      Binafsi nilifikiri ni vyema baada ya kukubali kuwa wananchi wetu walio nje wanaingizia pato serikali yetu, basi tuwawekee mazingira yatakayowarahisishia hao walio nje kuwekeza kwa mfano, kwanini tuendelee kuwapa FAIDA WESTERN UNION wakati tunaweza kuanzisha western union ya KITANZANIA??
      Tizameni hii link, hii ni kampuni ya Money transfer kama ilivyo WESTERN UNION, Kenya wameanzisha ya kwao, watu wa UCHUMI hebu mtueleweshe faida ya hii kitu, pengine na sisi TZ tukianzisha yetu itatufaa badala ya kufikiria mambo ambayo kimsingi hayatatusaidia

      https://remit.postapay.co.ke/info_tranfee.php

      Kenya (nao wana-debate kuhusu dual citizenship) pia waligundua kuwa wananchi wao walio nje wanaingiza sana pesa za kigeni Kenya na hivyo Posta ya Kenya wakaamua kuanzisha money transfer tena kwa rates ndogo kuliko za western union. Kwa hiyo hapo wenzetu wanaweza kutransfer pesa online kwa kutumia credit cards na agents wao pia.

      Mabenki ya nyumbani pia yangefungua huduma online ili watu tuweke pesa zetu kwenye benki za nyumbani online

      Sidhani kama tunahitaji dual citizenship ili tuwekeza/kutoa misaada nyumbani

      Kila la kheri Vigogo
      Last edited by Ogah; 30th November 2006 at 20:34.

    14. #33
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,042
      Rep Power : 1251
      Likes Received
      16
      Likes Given
      119

      Default

      Ogah
      Ni kweli watu walio nje wamewekeza sana nyumbani, njia moja wapo ikiwa ni kwa kutuma pesa nyumbani kwa ajili ya kazi na miradi mbali mbali, tena wakati hawana hiyo dual citizenship

      Sasa je, kuwa na uraia wa nchi mbili ndio kutaongezea nini??
      Well said Ogah...to add on that...

      Hili suala la DC ni nyeti sana kuliko lilivyochangiwa hapa so far. Security ni issue nyeti kuliko ambavyo wanabodi wamegusia hasa kwenye mambo ya Identity Theft.

      1. Hapa swali la msingi ni kuwa "Kwa sasa Tz hakuna DC je nini kinakosekana?"

      2. Watanzania wataohitaji DC ni asilimia ngapi kati ya waTz mil 37?

      3. Na...kama Sheria ya Arthi itabadilika na kuruhusu Arthi kuwa mali ya mtu binafsi, hawa wenye DC nao wataruhusiwa kumiliki arthi kama mali binafsi?


      Mimi nadhani haya ni maswali ya msingi ambayo inabidi tuyajibu huku tukiangalia mbele 25 to 100 years from now.
      Last edited by S. S. Phares; 30th November 2006 at 21:24.

    15. #34
      Tabasamu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 279
      Rep Power : 698
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      Ogah na Lordtical_Jnr,
      Hakika mmeuliza maswali ya maana sana kwenye hili jambo. Tunatakiwa kujua hasa kinachokosekana kwa sasa. Kusema tu kuhusu kuwekeza nyumbani haitoshi. Ni watu wangapi walioko nje hasa wenye pesa za kusema wanawekeza? Kama wapo nini kinashindikana kwa sasa wakati kuna watu wa nje wenye uraia wa nchi zao pekee wanakuja kuwekeza (kutuibia)?
      Binafsi sina tatizo na Dual citizenship, nashindwa kuelewa tu watu kuifanya mwarobaini wa matatizo yetu. Kiujumla ina faida kwa mtu binafsi anayeogpa kuukana Utanzania basi, maana nyumbani ni nyumbani tu, lakini siyo sababu za kiuchumi. Sababu za kusema eti mpaka mtu awe raia wa nchi mbili ndio akawekeze nyumbani ni nyembamba. Kwanza hakuna mazingira ya kuwekeza. Pili Mazingira ya kuwekeza yakipatikana, mtu yeyote anayeweza halafu akaacha ati kwa sababu hana dual citizenship huyo si muwekezaji.
      Tukiangalia watu wanachukulia dual citizenship kana kwamba katiba yetu ikishaturuhusu basi na huko nje moja kwa moja tumeruhusiwa, ndivyo kweli? Tunajua kuna hatua mbali mbali za kupitia na wengi wa WTZ walioko nje ni vigumu kupewa uraia huo. Hata tukikubaliana tuanzishe, je kama alivyouliza Lordtical_Jnr ni wangapi watakao nufaika na sheria hiyo? Sana sana kama mtu mmoja alivyowahi kusema ni Wahindi watakao tumia fursa hiyo, wanaingia Tanzania wananunua uraia (ndio) maana unananulika kisha wanatimkia majuu na kudai ni raia watanzania na watapata maana pesa ya kuanzia kama investors wanayo.
      Ila kama hata kama ni Watanzania elfu kumi watafaidika na hilo kwa sababu zao wenyewe, na kwa vile hilo halibadilishi chochote kwenye maisha ya Watanzania sioni kwani kusiwepo na hicho kitu.

    16. #35
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default

      Watanzania wenzangu,
      Swala la dual citizen ni muhimu kwa wale ambao tayari wana uraia nje na vigumu kwa mtu ambaye hana uraia nje kuliangalia kwa undani.
      Hii habari ya kuwekesha itakuja pale tutakapo kuwa na nafasi. Siwezi kuzungumzia nafsi ya mtu mwingine. Hivi leo tu kukosa Uraia umetufanya wengi tushindwe hata kutuma vitu nyumbani kwa sababu tayari tumeisha wekwa ktk fungu la wageni - Tax kubwa sana. Hivyo, vitu hivi vidogo iwe magari ama zana za ukulima, mashine za usindikaji matunda na n.k zingewasaidia sana familia na hata kuongeza ufanisi ktk uzalishaji pia serikali ingeweza kukusanya kodi zaidi wakati vitu hivi vikifanya kazi. Sasa tunaposimama hapa na kudai kama mtu anataka ku-invest nyumbani kwa nini anashindwa!.ndugu zangu sii rahisi kama mnavyofikiri hasa mnapokuwa nyie sii raia wa nje...Tunafungwa na mengi ktk sheria hii kwa hiyo ni bora kusimamisha kitu chako huku nje.
      Navyoona mimi haya ndiyo mawazo aliyokuwa akizungumzia Dr. Bundara...hapa mnatumia Fikra binafsi!...
      Ebu nambieni, kwa nini mtu kama mimi nipoteze uzawa wangu kwa sababu ya uraia nje ambao nimeupata kwa sababu ya kuishi huku muda mrefu!...Na tazama basi kila raia wa nje aliyeko Tanzania nakuhakikishia hapotezi Uraia wake wa uzawa huko alikotoka. Tuliyaona yote haya wakati wa Idd Amin!
      Jamani sisi Watanzania kama nyie na ndio maana tunakuwa wakereketwa hata ktk mijadala kama hii laa sivyo nadhani ipo haja ya nyie kutukatalia kabisa uanachama humu na pia kutuuliza kinachotuuma ni kipi hasa wakati sisi sio Watanzania.
      Tazameni wayahudi leo hii wako wapi?... China, India na mataifa mengi siku hizi wanafungua mabenki yao nchi za nje kuhudumia wazawa wao ambao wana uraia wa nchi mbili.. tena ukienda China town mji wowote ule north America, benki zao zinatoa huduma kwa kichina - wahudumu wote wachina.
      Leo hii vijana wetu wengi kama sii wote wafanya biashara nje, shopping zao ni Asia na hasa China, tukiwa na tawi la benki yetu huko Beijin ambalo litawasaidia vijana kupata mikopo na kikubwa zaidi kulingana na system za nje ni rahisi Watanzania wenye uraia China kukubaliwa kupata line of credit kwa sababu hawa watu record za credit zao zipo. Ni vigumu kwao kupata mikopo toka benki za China kwa biashara za Tanzania lakini itakuwa rahisi kwa benki yetu kumpa mtu mkopo kama atakuwa na biashara yake Bongo...tazamane Wanigeria ambao walikuwa na sheria kama yetu na waliuliza maswali hayahaya!... Lakini walipobadilisha mafedha yalimwagwa nchini mwao kishenzi (ingawa zilikuwa za wizi) hadi Marekani chini ya Mzee Bush walitaka fedha hizo ziwe freezed lakini hakufanikiwa.
      Mwisho wa yote, tunaolia na uraia wa nchi mbili ni sisi akina Yakhe walala hoi.. kwa sababu watu kama Mohammed Gire aliyewapachika hizo generator za umeme hana haja nayo. Na sijui mnamuweka kundi lipi maanake huyo huyo ni Mtanzania mara anajiita Asia - Amerikan. majuzi tu katunukiwa kama mfanya biashara bora ktk jumuiya yao ya Wa - Asia. Huyu mnamkuribisha kwa mikono miwili lakini Mkandara hapa aaaah!
      http://www.pagemedia.us/ahn/Asianofficials.htm.
      Tabasamu, mtoto wangu leo hana Utanzania kwa sababu tu kazaliwa nje na wazazi wenye uraia nje!...Najitahidi kumfundisha Kiswahili, culture zetu kumbe yote kazi bure? Babu na bibi zake wote wako Bongo leo unataka kunambia huoni faida ya sisi kuwa na roots zetu! Bob acheni roho hizo! who knows hawa mnaowakataa ndio kesho kutwa watakuwa viongozi Bongo. Nenda nchi za Asia ukaone jinsi vijana walivyorudi na kufanya mavitu makwao baada ya kusoma na kujijenga nje. Tupo nje kutafuta mtaji wa maisha kwani tulishindwa kupata malengo yetu wakati wa Nyerere, Mwinyi hadi Mkapa laa sivyo tungebanana wote humo.
      Kisha basi leo hii likinianguka janga hapa mshikaji hawa jamaa wanaweza kabisa kuninyang'anya huo Uraia.. Tumeyaona kwa hao waliokisiwa kuwa Al Kaeda, sasa hapo mshikaji wewe utanisaidia vipi kama sheria hii itaendelea kusimama.
      Last edited by Mkandara; 1st December 2006 at 02:16.
      Exploration of reality

    17. #36
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,700
      Rep Power : 21825
      Likes Received
      750
      Likes Given
      3275

      Default

      Bob Mkandara Calm down calm down,

      Dual Citizenship hiyo imeshapita, trust me, hapotei mtu hapa, kinachoangaliwa hivi sasa ni jinsi gani ya ku-accomodate hiyo sera, ndio maana watu wanakula perdiem huo nchi za watu eti wana-study mazingira yatakayolinda mazingira yetu.

      Pamoja na hayo, bado hatusiti kujiuliza na kuwapa ujumbe wanaopitisha hizi sera ikiwa kama challenge kwao, ili waweze ku-clear doubts zilizopo.

      wabeja

    18. #37
      Tabasamu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 279
      Rep Power : 698
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      Mkandara,
      Ukirejea tena post yangu nimesema wazi sina pingamizi kabisa na dual citizenship. Ni sawa kabisa kama wakiamua kuileta maana namini haimuumizi mtu yeyote. Napata taabu pale ninaposhindwa kufahamishwa kwamba Watanzania wameandaliwa vipi kufaidika na hatua hiyo. Maana siyo suala la kwamba tumeianzisha basi kila Mtanzania anapata. Maana hata ambao visa zao zime-expire nao pia wanataka dual citizenship. Hata mateja pale magogoni wanataka dual citizenship, je hiyo kitu ni rahisi kiasi hicho?

      Viongozi wetu wanataka kutupiga changa la macho kwa kutoshughulikia masuala muhimu waje kuishia kutwambia unaona tumeweza kupata dual citizenship ambayo haimsaidii kabunta (kuazima msamiati wako). Elimu kwetu inakufa hivihivi tutabakia na hizo sekondari ngumbaru maana idadi ya wanaoenda chuo kikuu inapungua, sasa nambie hata likiingia kwenye katiba ni nchi gani duniani inataka kujaza kabuntas. Ni na hakika watu kama wewe, kichuguu, mwl moshi mnahitaji hizo ni wazo zuri maana nyie ni Watanzania wenzetu hata kama mtu awe na pasi ya Vuanatu. Lakini ndiyo hapo mimi nadhani ni more personal than for national interest. Mnayoweza kuyafanya kwa jamii zenu nyumbani nina hakika mnayafanya sana.

      Labda tuseme mtu anapata priveledges kadhaa kwa kuwa raia wa nchi nyingine hasa zilizoendelea, ambazo asingepata kama si raia. Personal again

      Hilo la trekta usijali kwanza halitozwi kodi regardless nani analiingiza nchi. Kwa vitu vingine wewe mwambie mjomba, kaka, mpwa ajaze fomu za manunuzi kisha una-swipe kadi, maisha yanaendelea. Huhitaji kuwa una uraia wa nchi mbili. Ila don't get me wrong, nakubaliana kabisa na wazo hilo, nisichokubaliana nacho na sababu zinazotolewa.

    19. #38
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,042
      Rep Power : 1251
      Likes Received
      16
      Likes Given
      119

      Default

      Kwa yeyote atakayetaka nina soft copy ya Tanzania Law Reform Commission study iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya hii sheria ya DC. Send me private e-mail with your e-mail address and I will send you a copy.

    20. #39
      Interested Observer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2006
      Posts : 976
      Rep Power : 877
      Likes Received
      92
      Likes Given
      102

      Default

      Mkandara hapana usitupotoshe hapo, kuna baadhi ya nchi hizo ulizotaja hapo hazina DC, nchi kama China haina hiyo, na ukitaka uwe mchina lazima ukane u-Raia wa nchi ile unayotoka. Usichanganye Taiwan na Hong Kong maana hao siyo China proper.
      Kuhusu maelezo mengine, bado sioni hayo ynatosheleza, bado mie naona muda haujafika kwa Tanzania kuwa na DC, bado tuko nyuma mno, let go deep in our problems, we are talking too light!

    21. #40
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default

      Tabasamu,
      Tusitake kuchanganya vitu hapa jamani na hasa maelezo ya IO yananipa picha kwamba mnazungumzia watu wa nje kupewa uraia wetu TZ. Mimi nazungumzia Watanzania Wazawa wenye asili ya Utanzania ambao wame/naishi nchi za nje na wamepewa uraia huko. Hili swalia la mgeni kupewa uraia kwetu kila nchi zinatofautiana. Tunaweza tunga sheria zetu na zisifanane na nchi yeyote ile. Europe yenyewe kila nchi ina sheria zake tofauti kabisa na majirani zake. Lakini inapofikia kwa wazawa hili nchi nyingi zinafanana kisheria wakiamini MTU KWAO.
      Saudia hata uishi karne nzima lakini ukiwa huna asili, nasaba inayokuunganisha wewe na koo za Saudia mshikaji sii rahisi. Kuna special cases ambazo wanatoa uraia kwa watu wa nje lakini haohao saudia Msaudi akizaliwa nje acha kuishi nje ni raia bado wa Saudia. Kenya tu hapa majirani zetu wana sheria kali sana kwa wageni kupata uraia hali TZ ni rahisi sana kwa mtu wa kuja kuliko mzawa.

      Nd. Interested Observer,
      ebu nipe tafsiri ya kifungu hiki cha Overseas Chinese kina maana gani haswa labda tutaelewana vizuri.

      Overseas Chinese are Chinese people who live outside China. China, in this usage, usually refer to what is sometimes called "Greater China", including territory currently administered by the rival governments of the People's Republic of China (PRC) and the Republic of China (ROC) as per traditional definitions of the term prior to the Chinese Civil War, or only to the People's Republic of China by some. In addition, the government of the Republic of China granted residents of Hong Kong and Macau "overseas Chinese status" prior to their respective handover to Beijing rule, so the definition may be said to loosely extend to them.

      Kisha kuna kipande hiki:-
      Both the People's republic of China and the Republic of China maintain highly complex relationships with overseas Chinese populations. Both maintain cabinet level ministries to deal with overseas Chinese affairs, and many local governments within the PRC have overseas Chinese bureaus. Both the PRC and ROC have some legislative representation for overseas Chinese. In the case of the PRC, some seats in the National People's Congress are allocated for returned overseas Chinese. In the ROC's Legislative Yuan, there are eight seats allocated for overseas Chinese. These seats are apportioned to the political parties based on their vote totals on Taiwan, and then the parties assign the seats to overseas Chinese party Loyalists. Most of these members elected to the Legislative Yuan hold dual citizenship, but must renounce their foreign citizenship (at the American Institute in Taiwan for American citizens) before being sworn in.

      Navyojua mimi Wachina wengi nchi za nje hasa jirani waliukana Uchina na ndipo serikali yao ikawawekea vikwazo. Lakini kama unavyoona hata kugombea viti wanaruhusiwa isipokuwa wakichaguliwa ndipo huombwa kuutema uraia wa nje kabla ya kushika madaraka. Akina Yakhe sisi huku hatukuambiwa kuukana Utanzania ila tumeongezewa tu hilo ganda na sii vigumu hawa jamaa kulichukua ganda lao na wala hatutaki kugombea hivyo viti bali tunachodai ni haki yetu ya UZAWA..
      Wee unafikiri leo hii itokee vita kati yetu na hawa jamaa watakuja tuacha? Kweli wataamini sisi sio tena Watanzania eti kwa sababu tumeishi huku muda mrefu? ... Thubutu na watakuwa wajinga kweli kwa sababu mjomba siwezi kushika bunduki kupigana na Mbongo ila kinyume chake.
      Last edited by Mkandara; 3rd December 2006 at 09:26.
      Exploration of reality

    Page 2 of 24 FirstFirst 123412 ... LastLast

    Similar Topics

    1. DUAL citizenship Tanzania 2011
      By mbongopopo in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 42
      Last Post: 16th October 2012, 14:04
    2. Dual citizenship!
      By Jaguar in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 11th August 2011, 19:12
    3. Dual Citizenship
      By BAK in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 4th April 2007, 05:27

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...