JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

  Report Post
  Page 20 of 50 FirstFirst ... 101819202122 30 ... LastLast
  Results 381 to 400 of 996
  1. alsaidy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd February 2009
   Posts : 317
   Rep Power : 716
   Likes Received
   49
   Likes Given
   152

   Default Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Hizi ni video za muhadhara wa Sheikh Mohamed Said alioutowa UDSM kwa MSAUDI. Natumai utafaidika nazo kwa kujuwa historia ya Waislamu Tanganyika.

   *Uislamu Tanganyika 1*

   Lecture of Mohamed Said at Dar-es-Salaam University about the role of Muslims in the struggle for the independence of Nyerere amemtaka Abdulwahid Sayks aandike historia ya mapambano ya ugombozi wa Tanganyika. Nyerere hakuyapenda yalioandikwa, kwani hayakumpa Nyerere umbele. Maandishi ya Sayks yamepuuzwa kwa muda wa kupindukia miaka 30. Hivi sasa maandishi haya yako kwa familia ya Sayks.   *Uislamu Tanganyika 2*
   Mohamed Said anasema uzalendo wa Tanganyika haukuanza na Nyerere. Viongozi wa Kiislamu wameanzisha Tanganyika African Association (TAA) tokea miaka ya 1920.   *Uislamu Tanganyika 3*
   Mohd Said anatuambia kwamba katika kupigania uhuru wa Tanganyika, Tanganyika Railway African Union ikiongozwa na Waislamu walifanya mgomo kwa muda wa siku 82. Huu mgomo umemtia woga Nyerere, na akakata shauri kuitia vyama vya wafanyakazi vyote chini ya mbavu zake.
   Juhudi zote za viongozi wa TANU na serekali ilikua kudharau Waislamu na juhudi za Waislamu katika kila lengo la nchi. Kama kua Tanganyika haina Waislamu kabisa.   *Uislamu Tanganyika 4*
   Mohd Said anatueleza kwamba gazeti la "African Events" lilizuiliwa kuuzwa Tanzania kwa sababu ya makala aliyoandika Mohamed Said kuhusu juhudi za Waislamu kupigania uhuru wa Tanganyika. Akafika kutishiwa. Zama za Nyerere Waislamu serekalini walifika kuficha majina yao ya Kislamu.
   *Uislamu Tanganyika 5*
   Viongozi wa TANU walizungumza maandishi ya Mohamed Said na wakataka kuchukulia hatua kali. Lakini Nyerere alikataa ili asipewew Mohamed umuhimu na umaarufu.
   Katika miaka ya 1950, jiji la Dar-es-Salaam lilikua na la Waislamu. Hata mabibi wa Kikristo walikua wakivaa mabuibui, kivazi cha Waislamu.
   *Uislamu Tanganyika 6*
   Mohamed Said anasimlia kwamba Nyerere aliunda kamati ya kuwajibu vitabu vya Ali Muhsin "Conflict & Harmony in Zanzibar" na cha Mohamed Said "The Life and Times of Abdulwahid Sykes".
   Tuhuma kubwa ya Mohamed Said kuwa Nyerere siokuwa kaficha juhudi za Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, bali amefanya kila juhudi kuwakandamiza Waislamu na Uislamu Tanganyika.   *Uislamu Tanganyika 7*   *Uislamu Tanganyika 8*
   Mohamed Said anaendelea kueleza. Nyerere aliogopa hili jambo la kura tatu litagawa TANU baina ya Waislamu na Wakristo. Nyerere mwisho aliweza kuifanya TANU ikubali kura tatu. Hapo ndipo Waislamu walipoteza nguvu zao. Hapo ndipo historia ya TANU ikawa ni Nyerere pekee.   *Uislamu Tanganyika 9*
   Mohamed Said anasema TAA ilikuwa imejaa Waislamu. Walitaka kuleta Wakristo ili kuleta umoja wa nchi yote. Hapo ndipo Nyerere alikubaliwa kwa urahisi katika TAA.
   Mohamed Said anajibu masuala haya:
   Suala: Je Mtemvu alikuwa sahihi katika suala la kura tatu
   Suala: Nini hali halisi ya Waislamu?
   Suala: Vipi Waislamu wamevunjwa?
   Suala: Vipi "East African Muslim Welfare Society" imevunjwa?   *Uislamu Tanganyika 10*
   Mohamed Said anaendelea kujibu vipi "East African Muslim Welfare Society"
   imevunjwa.   *Uislamu Tanganyika 11*
   Mohamed Said anaendelea kueleza vipi "East Africa Muslim Welfare Society"
   imevunjwa.

   "Being honest may not get you many friends but it will always get you the right ones" John Lennon

  2. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,574
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8258
   Likes Given
   8156

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Chuma,
   Huyo Jumbe alikataa kitu gani kwa Nyerere?.. ikiwa yeye aliweza kuivunja warsha ya waislaam akiwa makamu wa rais iweje tena ni kosa la Nyerere hali yeye Muislaam ambaye alikuwa na uwezo wa kukataa kama huyo Aziz..Nionyeshe hata hadithi moja ya Nyerere kuhusiana na waislaam ambayo kaifanya pasipo Waislaam wenyewe kuhusika kutoa maamuzi..

   Hii habari mimi siikubaliani nayo kwa sababu ina malengo makuu ya Udini, ni sawa na kesho Chadema washinde uchaguzi huu atokee Mchagga mmoja aanze kudai wao Wachagga ndio wameiwezesha Chadema kusimama kwa sababu tu ya waasisi wake ati ndio iwe historia ya chama kwa kuchukua kabila moja na sii Watanzania waliojiunga na Upinzani...Nina hakika Chadema wasingefika hapa walipo leo kama sii kuungana na watanzania wengine kupambana na CCM Kisiasa na sio kikabila, hii ndio argument yangu..

   Na ikumbukwe tu kwamba historia ya TANU ilianza tokea Kariakoo kama chombo cha kidini ambako asilimia kubwa kama sii yote ya wakazi na wanchama wake wakati huo walikuwa Waislaam. Lakini walipotaka kubadilika na kuwa chama cha kisiasa yalitokea Mapinduzi ndani ya chama cha kidini na AbdulWahid na Mwapachu kumpindua Kreist ktk uongozi na kukifanya chombo hicho kiwe cha kisiasa na sio cha kidini tena.

   kwa hiyo Historia ya Uislaam inakwisha baada ya Mapinduzi na Uzalendo unaingia kwani ndipo Wakristu walipojiunga kwa sababu lengo ni kupigania Uhuru. Kabla ya hapo mtu asikudanganye kwamba Waislaam walikuwa wakipigania Uhuru..Na nazidi kukataa hii habari ya Uislaam kwa sababu hata hao kina Mtenvu na wapinzani wa TAA wakati ule walikuwepo Waislaam, sasa iweje tuchukue moja la kufurahisha lakini lenye machungu tunawaachia Wakristu.

   Haya huyu Mohamed said anasema wazi yeye hakumuogopa Nyerer na aliandika kitabu chake Nyerere akiwa hai iweje mtu huyu kaweza kuandika mabaya yote ya Nyerere asifikichwe isipokuwa wale Mawaziri wenye wadhifa na hadhi kubwa Kitaifa wamwogope Nyerere ktk maswala ya kupinga kuonewa kwa waislaam. Na hata kama ilikuwa kweli navyojua mimi miaka ya 60 kufikia Uhuru hadi tunapata Uhuru asilimia kubwa ya viongozi wa chama wenye sauti ndani ya chama walikuwa Waislaam. Sioni ubavu wowote wa Nyerere kuweza kuwadidimiza Waislaam wakati ule zaidi ya Waislaam wenyewe kushindwa kutekeleza ya dini ndani ya siasa za chama.

   Yoote yazungumzwe lakini ukweli unasimama vipi.. Hadi mwalimu anaondoka madarakani ni asilimia chini ya 10 - ooh no to be exact only 5% ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba ndio walipata nafasi ya kwenda shule za Secondary. Tazameni record ya shule zetu utakuta kwamba ni mikoa ya Pwani tu ndio ilikuwa na wanafunzi wengi Waislaam wakati bara sii ajabu kabisa kukuta vijana wawili wa Kiislaam ktk darasa la wanafunzi 45.
   Na shule za bara alitoka mwanafunzi mmoja au wawili tu toka kila shule kwenda Secondary wakati Mkoa wa Pwani ulichukua hesabu kubwa ya wanafunzi walioingia secondary. Wakuu fikirieni asilimi 5 ya wnafunzi kwenda secondary utaweza vipi kuwaridhisha Umma..na sababu kubwa ni kwamba hatukuwa na nafasi za kutosha secondary kulingana na shule za msingi hivyo sii lazima watu wali fail mitihani isipokuwa nafasi ndizo zilikuwa adimu.

   Sasa mimi Mkerewe naweza kusema kwamba Nyerere aliwapendelea sana watu wa Pwani kuliko sisi bara ama kwa lugha nyingine aliwapendelea zaidi Waislaam (Wazaramo na Manyema) kuliko sisi Wakerewe na Wabara wavaa kaptula kwa kuwapa wao nafasi nyingi zaidi ya mikoa mingine. Hii sio lugha ya UTaifa, sii lugha ya watu wanaojiita Watanzania kama jamii moja isipokuwa ni lugha ya watu wanaojiona wao ni tofauti na wengine hivyo kuwafanya wao wabaguzi.

   Sasa nikuambieni navyoiona picha mimi.. Ubaguzi wa kidini umeanza wakati wa Mwinyi (awamu ya mwisho) na kushamiri baada ya Nyerere kuondoka. Na hakika naamini kabisa kwamba Kighoma Malima alifanyiwa Ufisadi kuondolewa kwa sababu mfumo wa Elimu yetu ulianza kubadilika ghafla na Udini kutumika zaidi kuingia elimu ya juu. Na hakika kama juhudi zake zilivyunjwa nguvu yoyote ile basi mhusika mkubwa ni alikuwa rais Mwinyi - Muislaam mwingine ambaye hakupenda kuona Waislaam wakifanikiwa.

   Aloandika Kighoma Malima yote yanahusiana na wakati huu (baada ya Nyerere), utawala huu wa CCM ambao umekuja kumbatia Udini zaidi kiasi kwamba alipotaka kujitoa na kuingia Upinzani alionekana mwiba wa takoni. Binafsi naamini kabisa Mkapa asingeweza kusimama na Malima ktk uchaguzi uliofuata hivyo waka Mkolimba kumaliza ubishi. Malima aliondolewa sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa alikuwa tishio la Upinzani kwa CCM (Siasa) na waliopitisha kuondolewa kwake wapo Waislaam.
   Haya ni mawazo yangu
   Last edited by Mkandara; 4th September 2010 at 06:20.
   Exploration of reality

  3. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Mkandara View Post
   Mkuu wangu Waislaam wanajiua wao wenyewe kama ilivyo asili ya mtu mweusi kwani leo hii na mabaya yoote ya viongozi wetu iwe CCM, bado wananchi wanaichagua CCM kama ndio dini yao kisha hutafuta wachawi nje haswa Wazungu wawekezaji. Na bila shaka wazungu nao wanataka maendeleo pia yao zaidi, hivyo wanayo kila haki ya kujineemesha kutokana na mipango yao.

   Wakristu wananeemeka kutokana na mipango yao, kamwe huwezi kuona Unafiki baina yao na kanisa hata kama iwe kuchagua baina ya Taifa na dini na haiwezi kutokea mgongano huo kwa sababu kila kitu kipo ktk vitabu. Lakini njoo kwa Waislaam, historia yoote aloandika Mohamed Said kwa asilimia kubwa waliochangia ugonvi na mabalaa ni Waislaam wenyewe tena basi hadi leo tuna migogoro ndani ya Bakwata, Bakwata na jumuiya za Kiiislaam, Masheikh na viongozi wengi wa dini ni balaa tupu kwa sababu Uislaam sio taasisi ila ni dini.

   Nyerere kisha kufa hayupo tena duniani mbona Waislaam bado wanashindwa kujipanga pamoja na kuweka maamuzi yenye manufaa kwao. Nina hakika hata tarehe ya Idd el Fitr/Hajj itakuwa mvutano wengine wakisema tusifuate Saudia sijui hatujauona mwezi na kadhalika. Ili mradi tu ni kubishana kila mmoja wetu anajua zaidi ya mwingine..

   Sasa mnapotaka kuufanya Uislaam kama taasisi inabidi mfuate misingi na taratibu za kuanzisha taasisi kwa kufuata vigezo fulani lakini sio kuumiziana sisi wenyewe kisha tunatafuta mchawi hali wachawi ni sisi wenyewe.
   Umenena Mkuu Mkandara.
   Hakuna mtu mwenye moyo mwema anayeshabikia mapungufu katika jamii, mradi hayako kwake
   Proper analysis ya tatizo ni muhimu ili kupata a proper solution.
   Mimi kama mtanzania hainipi faraja yoyote, nikiwa mkristo, nikiona katoto kadogo ka kiislamu kakikosa elimu, vile vile kwa katoto kadogo ka kikristo.
   Utatuzi wa tatizo lazima uanze kwa kujiangalia mwenyewe na jinsi unavyokabili mazingira yako.Charity begins at home.
   Nimetembelea nchi nyingi zisizo za kikristo(zikiwemo za kiislamu) na kushangaa sana maendeleo yao, umoja wao na utendaji kazi wao.
   Taasisi za kiislamu zikiwa na nguvu ya umoja, kwa kweli ni mengi sana wanaweza kufanya kama kujenga mashule , hospitali, vyuo vya ufundi nk.
   Huyu adui ujinga na umaskini hachagui dini wala kabila, mikakati tutakayoiweka kama taifa lazima vile vile sehemu nyingine zenye upungufu wa maendeleo, jambo ambalo sote tunalikubali kuwa ni tatizo.

  4. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Chuma View Post

   Mohammed Said kaandika tukio lingine la AGIP, Aziz...Nyerere alitoa order ya Kukamatwa Muft wa Tanganyika Shekh Hassan Bin Ameir...AGIP Aziz alikataa hio order...lkn nini kimefanyika...?Nyerere akafanya lake?

   Ukisoma vema kitabu utajua Fitna za Nyerere...ilikuwa ukimpinga order zake anakutengenezea Zengwe...unatiwa ndani au kusahaulika kabisa....so hao unaowataja walikuwa Rubber Stamp.
   Mkuu unamzungumzia yule IGP Aziz aliyeua mtu pale Salender kwa kumgonga.
   IGP Aziz hakusimama kumsaidia masikini mtu huyo, akawaagiza askari wake kwenda kuona "kitu" alichokigonga barabarani.
   Azizi hakufunguliwa mashtaka wala kufukuzwa kazi.
   Sana sana akishia kupewa kazi huko Marekani na Nyerere huyo huyo mnae mlaumu.
   Na hao ndo waadilifu mnaowaona wana mioyo ya kuigwa!

  5. Fundi Mchundo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th November 2007
   Posts : 4,693
   Rep Power : 2878
   Likes Received
   414
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Chuma View Post
   ...Fundi nafikiri unashindwa Kujua situation za wakati wa Mwalim na Hao unaowaita "Waislam"...hao wote unaosema walikuwa hawafuruki kwa Nyerere. Ikiwa Nyerere aliweza mficha Jumbe....hayo mengine madogo angeshindwaje? Hao walikuwa wapokea Order tu....!!!

   Mohammed Said kaandika tukio lingine la AGIP, Aziz...Nyerere alitoa order ya Kukamatwa Muft wa Tanganyika Shekh Hassan Bin Ameir...AGIP Aziz alikataa hio order...lkn nini kimefanyika...?Nyerere akafanya lake?

   Ukisoma vema kitabu utajua Fitna za Nyerere...ilikuwa ukimpinga order zake anakutengenezea Zengwe...unatiwa ndani au kusahaulika kabisa....so hao unaowataja walikuwa Rubber Stamp.

   Mzee Jumbe ameandika Kitabu..kitafute pia ukisome...!!!

   Hivi waweza kunieleza kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ktk Utawala wa Jakaya umezuiwa na Jakaya?....!!!
   Misamaha ya Kodi ya Makanisa imeruhusiwa kwa Serikali kupenda?.....Na hii ndio Christian Lobby anaiyozungumza Mohammed Said...!!!
   Mimi sipingi kuwa Nyerere aliwatia watu ndani. Wengi tu walitiwa ndani na wengine kupewa exile ya humo humo ndani. Ninachopinga ni kusema kuwa Nyerere alifanya hivyo kwa misingi ya dini. Kama kuna mtu aliyetofautiana nae kwa kiasi kikubwa ni mkatoliki mwenzake Oscar Kambona. Unataka kutuambia kuwa Nyerere alimtia ndani muislamu Bibi Titi peke yake kutokana na jaribio lile la kumpindua? Wengi wetu tunajua yaliyowakuta wakina Kasella Bantu. Lakini wakati huo huo aliwaachia wakina Sykes wafanye watakalo hapa nchini. Wakati neno kabaila lilikuwa kama tusi, wakina Sykes waliendesha biashara zao za travel agency, insurance agency na commission agents bila kubughudhiwa na mtu. Hao wakina Mwapachu wakapewa mashirika ya umma kuongoza. Wakina Rupia wakashika vyeo vya juu serikalini . Wakina Hamza Aziz wakaruhusiwa to get away with murder kama alivyosema Lole. Wote hawa wanavuna matunda ambayo waliowatangulia walipanda. Hakuna anao wa-begrudge hicho. Lakini kugeuka na kusema kuwa walionewa kama waislamu wakati watu kama wakina Vedasto Kyaruzi, Dr. Mwanjisi, Phombeah hakuna mtu anawajua au hata hatujawahi kusikia kama waliowafuata walipewa kifuta jasho. Nenda kamtembelee muasisi, mkatoliki mwenzake, Chief Patrick Kunambi ukaone maisha anayoishi halafu utuambie kuwa huyo Julius aliwapendelea wakatoliki wenzake!

   Kitu kibaya ambacho watu kama nyinyi mnachokifanya ni kuwashusha hao mnaojifanya kuwatetea na kuwatoa kwenye heshima wanayostahili ya UZALENDO na kuwafanya kama vile walikuwa WADINI. They deserve better.

   Amandla.......
   Fundi Utumbo

  6. Fundi Mchundo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th November 2007
   Posts : 4,693
   Rep Power : 2878
   Likes Received
   414
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Hivi waweza kunieleza kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ktk Utawala wa Jakaya umezuiwa na Jakaya?....!!!
   Misamaha ya Kodi ya Makanisa imeruhusiwa kwa Serikali kupenda?.....Na hii ndio Christian Lobby anaiyozungumza Mohammed Said...!!!
   Hamuoni hapa mnajitukana wenyewe. Iwaje vipi serikali ambayo Rais ni muislamu, makamu wa rais ni muislamu, mkuu wa polisi ni muislamu, mkuu wa usalama wataifa ni muislamu, waziri wa fedha ni muislamu n.k. washindwe kupitisha ajenda yao ambayo inakubalika na wengi kwa kuhofia tu hako ka Christian lobby? Hamuwezi kutambua kuwa masuala haya hayajfanikiwa kwa sababu tu kuna waislamu wengi tu ambao wameungana na wengine kuyapinga? Misaada ya kodi iliyoruhusiwa ni kwa ajili ya taasisi za dini. Sasa kama nyingi ya hizo taasisi ni za kikristu utawalaamu?

   Hapana, hizi shutma za jikoni hazitawasaidia kitu. Cha maana ni kukaa na kujiangalia na kukiri madhaifu yenu na kutafuta namna ya kuyaondoa badala ya kukimbilia kutafuta mchawi!

   Amandla.....
   Fundi Utumbo

  7. Fundi Mchundo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th November 2007
   Posts : 4,693
   Rep Power : 2878
   Likes Received
   414
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Chuma View Post
   Ushahidi gani tena wautaka?...Waislam hawataki Apology, wanataka HAKI itendeke....na hii ndio misconception kubwa mliyonayo mnafikiri waislam wanataka favor..waislam wanataka Haki itendeke.
   Ushahidi upi? Statistics kuwa wengi walioenda shule ni wakristu? Samahani kwa ndugu zangu wagogo, lakini utaniambia kweli unahitaji kufanya survey kujua kuwa wengi wa ombaomba Dar es Salaam kwa muda mrefu walikuwa wagogo? Sasa leo utataka kutuambia kuwa serikali iliwabagua wagogo ndiyo maana wakawa ombaomba? Kama kweli ni serikali ya haki kwa nini hatuoni wachaga waliopofuka wakitembeza vibakuli Dar? Statistics si ushahidi bali ni ishara ya kuwepo kwa tatizo. Kutokana na hizo statistics mgefanya utafiti na kupata ushahidi kuwa pamoja na kufanya vizuri kwenye mitihani waislamu hawachaguliwi kuendelea na masomo hapo ndipo tungezungumzia ushahidi.

   Wakristu hawatakuja hata siku moja ku-apologise kwa waislamu. Waislamu wanaongoja kuwa wapewe haki na wakristu watabaki daima nyuma maana mkristu hana uwezo wa kumpa haki hiyo! Mnaulizwa, ili muone kuwa HAKI inatendeka kwa waislamu mngetaka kifanywe nini mnabaki kujiuma midomo. Mkasaidiwa na kuulizwa " mnataka affirmative action?" Bado mmebaki na kigugumizi. Mkaulizwa, " je mnataka serikali iwazuie wakristu kusoma hadi waislamu watakapo-achieve parity", bado mna kigugumizi. Sasa kama wenyewe hamjui mnachokitaka, nani atawasaidia?

   Amandla......
   Last edited by Fundi Mchundo; 4th September 2010 at 17:10.
   Fundi Utumbo

  8. Mohamed Said's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2008
   Posts : 6,939
   Rep Power : 340144
   Likes Received
   5956
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   FM: Chanzo cha mnakasha huu ni DVD niliyozungumza kuiweka historia ya TANU katika mstari ambao mimi niliona unafaa. Nikiamini kuwa ninayoeleza yamekuwa yakiwatia hofu baadhi ya watu fulani kwa miaka mingi sana. Hofu hiyo ilikuwa inatokana na ukweli kuwa Nyerere hakuanzisha harakati za kujigomboa ingawa yeye mwenyewe alitaka sana historia ya TANU ianze na yeye. Katika kufanikisha hilo ikaandikwa historia ya TANU na Chuo cha Kivukoni. Mimi nikaja na kitabu changu ambacho kilieleza mambo kama yalivyokuwa kutokana na utafiti na kumbukumbu za akina Kleist Sykes, Abduwahid Sykes na Ally Sykes. Sikuishia hapo nilipata maelezo kutoka kwa Ally Mwinyi Tambwe, Zuberi Mtemvu, Titi Mohamed,Haidar Mwinyimvua, nk. Hawa walikuwa Dar es Salaam. Huko mikoani nilikutana na Bilal Rehani Waikela, Salum Mpunga, Mohamed Mangiringiri, Yusuf Olotu na wengineo wengi. Hata mimi nilishtuka kwa uvumbuzi wa hazina hizi na mambo waliyonieleza. Hawa niliobahatika kuwahoji wakawa wananipa habari za wazalendo wenzao waliotangulia mbele ya haki kama akina Maulid na Abdallah Kivuruga, Fundi Muhindi, Sheikh Yusuf Badi, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Kiyate Mshume, Mwinjuma Mwinyikambi...ni shida kutaja majina yote. Haikuwa shida kwangu na kwa hakika kwa yeyote yule kuona kuwa wapiganaji dhidi ya ukoloni walikuwa wanatoka katika jamii moja. Nikajiuliza na nikawauliza wapashaji habari wangu. Kulikoni? Nikapewa majibu na mimi nikatumia akili yangu kutazama jinsi ukoloni ulivyokuwa ukitawala. Nikapata majibu pia.

   Kilichojitokeza na kunitia hima niandike historia hii ni pale nilipokujaona kuwa historia hii inamkera Nyerere. Sasa hii ilikuwa miaka ya 1980 na Nyerere keshafahamika vyema kabisa. Nikaamua kuandika kitabu kitoe jibu kwa kitabu kile kilichoandikwa na Chuo cha Kivukoni ambacho ndicho kilikuwa kinachukuliwa kama historia rasmi ya nchi yetu kuhusu harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Kutokea hapa na baada ya clips zilizowekwa katika mtandao ndipo mjadala ukashamiri.

   Ombi langu kwa wana-ukumbi ni kuwa ikiwa kama kuna wazalendo ambao wamefanya mengi lakini historia imewasahau basi na ziandikwe habari zao ili kizazi kijacho kifaidike. Leo nafarajika sana ninapoalikwa kuzungumza hii historia iliyofanyiwa khiyana na hupata furaha kubwa ninapoona hadhira imetulia kimya wakinisikiliza na mwisho kusimama na kunipongeza.

   Ningependa kumaliza kwa kusema mzee wangu Ahmed Rashad Ali alipata kunambia kuwa rafiki yake, marehemu Abdulwahid Sykes kila yeye alipomlalamikia kuwa Nyerere anataka kujipa sifa isiyo yake kuwa yeye ndiye muaisisi wa TANU na harakati za uhuru Abdu Sykes alikuwa akisema, "Mwache bwana hakuna neno ikiwa yeye anataka sifa hii mwachie achukue si kitu." Hadi Abdu Sykes anaingia kaburini hakupata kusema kuwa yeye ndiye kilikuwa kichwa katika kuaisisi TANU wala kusema African Association alianzisha baba yake au hata kusema hata hiyo nyumba iliyokujaasisiwa TANU ilijengwa na baba yake. Leo hakuna kumbukumbu yoyote katika haya si Makumbusho ya Taifa wala pale ofisi ndogo ya CCM. Mimi naijua ofisi ya Abdu Sykes pale Lumumba ambayo aliitumia katika kipindi kifupi alipokuwa akiandika historia ya TANU iliyokataliwa na Nyerere. Kila nikipita pale husimama kwa muda na kusoma dua zimfikie yeye na wazalendo wengine waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa mali na nafsi zao. Naamini wana-ukumbi mmepata mengi kutoka kwangu na kama katika huu mnakasha labda nimekwaruza mtu basi anisamehe kwani hiyo haikuwa nia yangu. Jina langu lipo hapo sura yangu iko wazi popote mtakaponiona nisimamisheni angalau tunywe chai pamoja. Haya ndiyo mafunzo waliyotufunza wazee wetu.
   Last edited by Mohamed Said; 4th September 2010 at 17:52.

  9. Mohamed Said's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2008
   Posts : 6,939
   Rep Power : 340144
   Likes Received
   5956
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   FM: Sisi hatujawashusha wazee wetu hata kidogo. Sisi tumewatizama usoni wale waliotaka kuwashusha wazee wetu na kuwadhulumu haki yao na kuwapinga. Wengi katika wazee niliozungumzanao wamenambia wao wanamshukuru Allah kwa kuwapa nafasi ya kufanya yale waliyofanya kujaalia kuwa historia ya ukombozi wa Tanganyika ikawa inaendana na Uislam. Kama kuna aneona vibaya historia hii kunasibisshwa na wazalendo hawa na Uislam hili ni jambo ambalo ni tabu kufutika. Naweka hapa chini moja ya vipande ninavyovipenda katika kitabu changu:

   Kueleweka kwa nini Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere inahitajika uchambuzi kuelewa siasa za mfumo wa kikoloni katika Tanganyika. Mwaka wa 1951 Abdulwahid na Mwapachu walipokuwa wakishughulika kuifufua TAA, walijiwa na Ivor Bayldon, Brig. Scupham na V.M. Nazerali kuombwa kuunga mkono kuundwa kwa chama cha kisiasa kitakachojumuisha Watanganyika wa rangi zote. Hawa walikuwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria. Bayldon alikuwa mlowezi tajiri kutoka Nyanda za Juu za Kusini na alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini. Wajumbe wa Kiafrika wa Baraza la Kutunga Sheria walioliunga mkono wazo hili walikuwa Chifu Kidaha Makwaia na Liwali Yustino Mponda wa Newala . Watu wengine mashuhuri walioshauriwa na kuombwa kuunga mkono chama hiki walikuwa: Dr Joseph Mutahangarwa, Chifu Abdeli Shangali wa Machame, Chifu Mkuu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Haruna Msabila Lugusha, Dr Wilbard Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Dossa Aziz .

   Huu ulikuwa mchanganyiko wa Wazungu ambao tangu hapo walikuwa raia wa daraja la juu, baadhi yao kama Bayldon walikuwa walowezi; machifu kama vile Marealle, Waafrika wasomi kama Mwapachu; tabaka ya wafanyabiashara wa Kiasia kama Karimjee na watu wa mjini kama Dossa Aziz na Juma Mwindadi. Wote hawa walikuwa viongozi waliokuwa na wafuasi katika jumuiya zao. Katika barua Nazerali aliyomtumia Ally Sykes miaka miwili baada ya kudhihiri kuwa chama kile walichokusudia kisingeweza kuundwa, Kwenye sehemu moja alikuwa na haya ya kueleza: "Haja kubwa ilikuwa kuandaa kikundi cha watu walio wakweli, waaminifu na wenye imani katika maendeleo ya watu katika nchi yetu, pamoja na fursa sawa kwa wote."

   Abdulwahid wakati huo akiwa katibu pamoja na wanachama wa TAA wasingeweza kukubali wazo kama hilo. Ingawa kwa kiasi fulani malengo ya chama hicho kilichokusudiwa yalionekana yanafanana na malengo ya wananchi hivyo kudhihirisha barabara kile ambacho TAA ilikuwa ikikipigania, Waafrika wasingeweza kuachia azma ya wa Tanganyika kwa dhamira njema ya wasiokuwa Waafrika na ambao walikuwa wakishirikiana bega kwa bega na serikali ya kikoloni. Ilikuwa dhahiri kuwa Wazungu na Waasia nchini Tanganyika hawakutaka kukubali kuwa Tanganyika kwa hali yoyote ile ilikuwa nchi ya Waafrika. Kwa TAA kukubali kuundwa chama cha siasa kitakachojumuisha mataifa yote, kulikuwa sawa na kuyaweka maslahi ya Waafrika chini ya watu wachache. Miaka michache nyuma wazo kama hilo chini ya kile kilichojulikana kama Capricon Society lilianzishwa na wakoloni katika maeneo ya Tabora ambako kulikuwa na idadi kubwa ya Waafrika wasomi, wengi wao wakiwa Waalimu. Imani ya Capricon Society ilifungamana na dhana ya ëuhuru kwa Waafrika waliostaarabika-. Stephen Mhando aliyekuwa Dar es Salaam na akiwasiliana na George Magembe mjini Tabora alituma barua kwa uongozi wa TAA huko akiwatahadharisha juu ya mtego wa na Capricon. Ilikuwa dhahiri kuwa Tanganyika wakati ule ilikuwa ikitafuta mwelekeo wa kisiasa na haikuwa TAA peke yake iliyokuwa ikishughulika kutaka kuonyesha njia.

   Mara baada ya Nyerere kuchukua uongozi wa TAA chama kikaanza kusinzia, ushupavu na bidii iliyokuwepo wakati wa uongozi wa Abdulwahid vilitoweka. Kwa hakika ilikuwa wakati mmoja tukatika historia ya Dar es Salaam ambapo Mkristo Erikah Fiah, alikamata bendera dhidi ya serikaly ya kikoloni. Nyerere alikuwa akikaa nje ya mji na alikuwa akija Dar es Salaam mwishoni mwa juma tu. Kwa kiasi fulani hii iliathiri shughuli za chama. Kwa muda wanachama walionekana kama wamepoteza hamu ya chama. Wajumbe wa kamati ya utendaji mara nyingine hawakutokea kwenye mikutano ijapokuwa Dossa aliwapitia majumbani kwao na gari yake kuwachukua.

   Dossa anakumbuka kuwa alikuwa akisimama nje ya nyumba ya mwanakamati na kupiga honi. Mtoto au mke wa mwanakamati angetoka mlangoni kutoa habari kuwa hakuwapo, katoka ilhali yupo ndani. Kwa muda kidogo ilionekana kama Nyerere alikuwa kikwazo cha maendeleo ya TAA. Na huu ndiyo ulikuwa mwendo wa TAA, nguvu yake ilikuwa ikitegemea uwezo wa viongozi wake. Awamu ya kwanza ya uongozi wa Kleist Sykes na Mzee Bin Sudi katika makao makuu TAA ilipiga hatua kubwa. Vivyo hivyo katika zama za Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman katika tawi la Dodoma, TAA ilikuwa ikisikika sana na uongozi wake uliheshimiwa hata nje ya Tanganyika. Abdulwahid alikuwepo kama makamu wa rais lakini alipendelea kumwona Nyerere akiendesha ofisi na kufanya maamuzi yake mwenyewe kama rais. Akakihofia kufa kwa chama, Abdulwahid aliwataka shauri viongozi wenzake wa ndani katika TAA - Ally, Dossa, Tewa na Rupia kuwa kipi kifanyike ili kudhibiti hali ile iliyojitokeza. Ilikuwa dhahiri tatizo lilikuwa ni katika kubadilisha uongozi. Wanachama walikuwa hawana imani na uongozi mpya katika ngazi ya juu. Hili linaweza kueleweka ikifikirika kuwa ilikuwa ni miaka mitatu tu huko nyuma wakati Abdulwahid na Dr Kyaruzi walikifufua baada ya kupoteza mwelekeo baada ya Vita Kuu ya Pili. Iliamuliwa kuwa wazee Waislam wa mjini Dar es Salaam waombwe kumuunga mkono Nyerere.

   Wazee walifatwa na wakaelezwa kuwa uongozi wa TAA ulikuwa umemkubali Nyerere kama rais wa chama kama sehemu ya mpango wa kuigeuza TAA kuwa chama cha siasa cha umma Abdulwahid aliwaeleza wazee, miongoni mwao masheikh, kuwa nchi ilikuwa katika awamu yake ya mwisho ya harakati ambayo ilihitaji kuungwa mkono na kila Mwafrika wa Tanganyika bila kujali dini yake wala kabila. Hawa wazee walikuwa wanachama wa TAA lakini vilevile walikuwa wanachama au viongozi katika vyama vyao vya kikabila kama vile Batefera Union chama cha Wamanyema kilichokuwa kikiongozwa na Mzee bin Sudi, na Zaramo Union chini ya uongozi wa Makisi Mbwana. Baadhi ya wanachama waliokuwa katika vyama hivi walikuwa vilevile wanachama wa Al Jamiatul Islamiyya. Abdulwahid aliwaambia wazee kuwa makao makuu ya TAA yaliwahitajisana kuunga mkono chama, pamoja na wasomi kama Julius Nyerere waliochukuliwa kuwa watiifu kwa utawala wa kikoloni. Hawa wanaodhaniwa kuwa watiifu kwa utawala wa kikoloni ndiyo wanaofaa sana kugeuzwa waipinge serikali inayowadhulumu wananchi.

   Wazee waliafiki ushauri huu na wakaanza kumjenga Nyerere kama kiongozi wa kuwasemea na kuwaunganisha Waafrika wote wa Tanganyika. Mwanafunzi mmoja wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir anakumbuka kuwaona Abdulwahid, Dossa Aziz na Nyerere mara kadhaa katika miaka ya mwanzoni ya 1950 wakija kuonana na sheikh katika madrassa yake Kariakoo, Amani Street, nyumba nambari 36. Kwa kawaida Abdulwahid, Dossa Aziz na Nyerere walipokuja kumwona Mufti, Sheikh Hassan Bin Amir alikuwa akivunja darsa na kuwapa ruhusa wanafunzi wake ili upatikane utulivu wa maongezi. Kwa kawaida mashauriano yalikuwa yakifanyika mle mle ndani ya madrasa, Abdulwahid, Dossa na Nyerere wakiwa wamekaa chini kwenye jamvi wamekunja miguu. Wazee wengine mashuhuri waliomuunga mkono Nyerere walikuwa Sheikh Suleiman Takadir mwanachuoni wa Kiislamu aliyeelimika sana, akijulikana zaidi kwa jina la utani ëMakarios-, Jumbe Tambaza, mzee aliyekuwa akihodhi ardhi kubwa pale mjini; Mshume Kiyate, mzee muuza samaki aliyekuwa na kipato kizuri; Mwinyijuma Mwinyikambi, mzee aliyekuwa na viunga vya minazi na miembe; Rajabu Diwani, seremala hohe hahe lakini aliyejaaliwa ufasaha mkubwa wa kuzungumza; Makisi Mbwana, kiongozi wa Wazaramo mjini Dar es Salaam; Sheikh Haidari Mwinyimvua, fundi cherehani na mtu mwadilifu; Iddi Faizi Mafongo na Idd Tosiri ndugu wawili Wamanyema na binamu wa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo Khalifa wa tariqa ya Qadiriya. Iddi Faizi akiwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya na Iddi Tosiri mwanachama shupavu); Iddi Tulio, mzee mwenye heshima zake, Mashado Ramadhani Plantan, mhariri na mmiliki wa gazeti la Zuhra na kaka yake Schneider Abdillah Plantan, watoto wa Affande Plantan na wazee wengine wengi wa mjini.
   Last edited by Mohamed Said; 5th September 2010 at 01:05.

  10. Fundi Mchundo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th November 2007
   Posts : 4,693
   Rep Power : 2878
   Likes Received
   414
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Mohamed Said View Post
   FM: Chanzo cha mnakasha huu ni DVD niliyozungumza kuiweka historia ya TANU katika mstari ambao mimi niliona unafaa. Nikiamini kuwa ninayoeleza yamekuwa yakiwatia hofu baadhi ya watu fulani kwa miaka mingi sana. Hofu hiyo ilikuwa inatokana na ukweli kuwa Nyerere hakuanzisha harakati za kujigomboa ingawa yeye mwenyewe alitaka sana historia ya TANU ianze na yeye. Katika kufanikisha hilo ikaandikwa historia ya TANU na Chuo cha Kivukoni. Mimi nikaja na kitabu changu ambacho kilieleza mambo kama yalivyokuwa kutokana na utafiti na kumbukumbu za akina Kleist Sykes, Abduwahid Sykes na Ally Sykes. Sikuishia hapo nilipata maelezo kutoka kwa Ally Mwinyi Tambwe, Zuberi Mtemvu, Titi Mohamed,Haidar Mwinyimvua, nk. Hawa walikuwa Dar es Salaam. Huko mikoani nilikutana na Bilal Rehani Waikela, Salum Mpunga, Mohamed Mangiringiri, Yusuf Olotu na wengineo wengi. Hata mimi nilishtuka kwa uvumbuzi wa hazina hizi na mambo waliyonieleza. Hawa niliobahatika kuwahoji wakawa wananipa habari za wazalendo wenzao waliotangulia mbele ya haki kama akina Maulid na Abdallah Kivuruga, Fundi Muhindi, Sheikh Yusuf Badi, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Kiyate Mshume, Mwinjuma Mwinyikambi...ni shida kutaja majina yote. Haikuwa shida kwangu na kwa hakika kwa yeyote yule kuona kuwa wapiganaji dhidi ya ukoloni walikuwa wanatoka katika jamii moja. Nikajiuliza na nikawauliza wapashaji habari wangu. Kulikoni? Nikapewa majibu na mimi nikatumia akili yangu kutazama jinsi ukoloni ulivyokuwa ukitawala. Nikapata majibu pia.

   Kilichojitokeza na kunitia hima niandike historia hii ni pale nilipokujaona kuwa historia hii inamkera Nyerere. Sasa hii ilikuwa miaka ya 1980 na Nyerere keshafahamika vyema kabisa. Nikaamua kuandika kitabu kitoe jibu kwa kitabu kile kilichoandikwa na Chuo cha Kivukoni ambacho ndicho kilikuwa kinachukuliwa kama historia rasmi ya nchi yetu kuhusu harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Kutokea hapa na baada ya clips zilizowekwa katika mtandao ndipo mjadala ukashamiri.

   Ombi langu kwa wana-ukumbi ni kuwa ikiwa kama kuna wazalendo ambao wamefanya mengi lakini historia imewasahau basi na ziandikwe habari zao ili kizazi kijacho kifaidike. Leo nafarajika sana ninapoalikwa kuzungumza hii historia iliyofanyiwa khiyana na hupata furaha kubwa ninapoona hadhira imetulia kimya wakinisikiliza na mwisho kusimama na kunipongeza.

   Ningependa kumaliza kwa kusema mzee wangu Ahmed Rashad Ali alipata kunambia kuwa rafiki yake, marehemu Abdulwahid Sykes kila yeye alipomlalamikia kuwa Nyerere anataka kujipa sifa isiyo yake kuwa yeye ndiye muaisisi wa TANU na harakati za uhuru Abdu Sykes alikuwa akisema, "Mwache bwana hakuna neno ikiwa yeye anataka sifa hii mwachie achukue si kitu." Hadi Abdu Sykes anaingia kaburini hakupata kusema kuwa yeye ndiye kilikuwa kichwa katika kuaisisi TANU wala kusema African Association alianzisha baba yake au hata kusema hata hiyo nyumba iliyokujaasisiwa TANU ilijengwa na baba yake. Leo hakuna kumbukumbu yoyote katika haya si Makumbusho ya Taifa wala pale ofisi ndogo ya CCM. Mimi naijua ofisi ya Abdu Sykes pale Lumumba ambayo aliitumia katika kipindi kifupi alipokuwa akiandika historia ya TANU iliyokataliwa na Nyerere. Kila nikipita pale husimama kwa muda na kusoma dua zimfikie yeye na wazalendo wengine waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa mali na nafsi zao. Naamini wana-ukumbi mmepata mengi kutoka kwangu na kama katika huu mnakasha labda nimekwaruza mtu basi anisamehe kwani hiyo haikuwa nia yangu. Jina langu lipo hapo sura yangu iko wazi popote mtakaponiona nisimamisheni angalau tunywe chai pamoja. Haya ndiyo mafunzo waliyotufunza wazee wetu.
   Mimi ndio maana nasema historia jinsi ulivyoieleza haiwezi kusimama peke yake maana hakuna mahali ambapo inaelekea uliwahoji wale ambao pengine kumbukumbu zao zingekuwa tofauti na mawazo yako. Pamoja na wakristu kibao kuwepo katika harakati hizo, hakuna hata mmoja uliyemhoji!

   Mimi binafsi sijawahi kumsikia kuwa Nyerere akijisifia kuwa ni yeye peke yake ndiye aliyelanzisha TANU. Kuwa ni mmoja wa waasisi hiyo haina kificho! Sasa unataka kutuambia kuwa Abdu Sykes alikuwa anakana kuwa Nyerere hakuwa mmoja wa waasisi wa TANU? Unataka kutuambia kuwa TANU ilianzishwa na wakina Sykes peke yao? Mbona ndugu yao amekana dhana hiyo waziwazi na hakuchelea kumuita Nyerere baba wa taifa! Wewe una ukaribu gani na Abdu kuliko ndugu yake huyo wa damu? Huyo Nyerere unayedai kuwa alitaka sifa zote zimwendee, mpaka anaondoka madarakani ( kwa hiari yake bila kusukumizwa na mtu na kumwachia muislamu) hakuwa hata na mtaa wenye jina lake nchi nzima. Huyo Nyerere wa majigambo alikataa hata uwanja wa michezo kupewa jina lake? Huyo Nyerere wa majigambo mpaka anaondoka hakuwa hata na sanamu moja yenye jina lake mahali popote Tanzania ! Huyo Nyerere wa majigambo amekufa akiwa na nyumba ambayo alishindwa kulipia mkopo aliochukua kujengea. Huyo Nyerere unayemlaumu, hadi anafariki alikuwa anacheza bao na watu wa kawaida, alikuwa anakula ugali wa mtama nyumbani kwake na kulima kwa jembe la mkono! Kitu usichoelewwa ni kuwa wote tuliishi katika huo wakati Nyerere akiwa kwenye madarakani na tunajua alivyoishi. Huyo Nyerere unayetuhadithia sisi hatumtambui!

   Abdu Sykes hakusema kuwa yeye ndiye alikuwa kichwa katika TAA kwa sababu alijua ukweli kuwa haikuwa hivyo. Alikuwa kichwa katika vichwa. Wewe lini umemsikia Paul Rupia akitamba kuwa Baba yake ndiye alimpeleka Nyerere Marekani? Lini umemsikia akitamba kuwa kama si baba yake hata hizo kadi za uanachama zisingechapishwa? Kumbukumbu za mambo kama haya hayawekwi kwenye makumbusho ya taifa bali unayakuta kwenye National Archives. Na wote tunajua tulivyo watu wa ovyo katika utunzaji wa nyaraka. Si zinazowahusu wakina Sykes peke yao zilizopotea, kibao zaidi zimenyeshewa na mvua, kuliwa na mchwa n.k. Ni wengi kuliko hao unaowataja waliochangia uhuru wetu na it is a national disgrace wengi wao tumewasahau.

   Mtu yeyote aliyesoma historia anajua kuwa hauwezi kutegemea kitabu kimoja kama unataka kujua ukweli wa mambo yalivyotokea. Kitabu chako si cha kwanza kuandika historia ya nchi hii na kuwataja hao unaosema walisahauliwa. Chukua muda, google, na utagundua mengi zaidi ya hayo unayojua yameandikwa kuhusu historia yetu. Mkuu, kama unataka upate credibility inabidi uangalie zaid ya kitovu chako. Kwa kufanya hivyo, unafanya kosa lile lile ambalo unadai Nyerere alilifanya. Kosa la kutowathamini na kuwatendea haki wote waliochangia uhuru wetu bila kujali itikadi, rangi, dini au kabila lao. Kwenye hili hatuwezi kukubaliana hata siku moja!

   Amandla.......
   Fundi Utumbo

  11. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   I think it might be prudent that we might also hear from other writers as to what they have to say on Mwalimu,AFTER his death.
   Excerpts from Godfrey Mwakikagile book, "NYERERE AND AFRICA: END OF AN ERA: EXPANDED EDITION"

   "THE DEATH of Julius Nyerere in October 1999 marked the end of an era in more than one way.
   He was one of the pioneers in the struggle to end colonial rule after the end of World War II. He was also one of the first African leaders who led their countries to independence in the late fifties and in the sixties. And he was one of the last surviving leaders who spearheaded the struggle for African independence; among them, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Nnamdi Azikiwe, Sekou Toure, Modibo Keita, Patrice Lumumba and others. And he outlived most of them. The only surviving former African presidents who led their countries to independence in the sixties, and who outlived Nyerere, were Leopold Sedar Senghor, a Francophile, who died in France in December 2001 at the age of 95; Ahmed Ben Bella of Algeria, Dr. Kenneth Kaunda of Zambia, and Dr. Milton Obote of Uganda who were also his ideological compatriots like Dr. Nkrumah, Sekou Toure, Modibo Keita, and Lumumba.
   It was the era of “Big Men,” the founding fathers, and the life of Julius Nyerere as a political leader of international stature epitomized the best among them, despite a number of failures during their tenure. They will be remembered as the leaders who not only led their countries to independence but who also maintained national unity, especially in the early years after the end of colonial rule, laying the foundation for the nations we have across the continent today. They will also be remembered as the leaders who - besides Azikiwe and a few others - introduced the one-party system to fight tribalism and consolidate nationhood, and socialism to achieve economic development.
   Nyerere will be remembered for both, probably more than any other African leader. His one-party state was probably the most successful in transcending tribalism and maintaining national unity. Tribalism never became a prominent feature of national life in Tanzania under Nyerere, unlike in other African countries wracked by war and other conflicts. And besides Nkrumah, he was also the most articulate exponent and theoretician of one-party rule. A firm believer in socialism until his last days, he was also one of the strongest proponents of socialist policies for decades. And he lived and died as a socialist probably more than any other African leader. Even after his socialist policies failed to fuel and sustain Tanzania’s economic growth, he remained a firm believer in socialism, and responded to his critics in rhetorical terms: “They keep saying you’ve failed. But what is wrong with urging people to pull together? Did Christianity fail because the world isn’t all Christian?”1
   It is not the purpose of this chapter to examine the successes and failures of Nyerere’s socialist policies but to look at how life was under Nyerere in one of the poorest and most ethnically diverse countries in Africa and, indeed, in the entire world. These are my reflections on Tanzania, the land of my birth (it was then called Tanganyika and still a British colony), and on the life and death of Julius Nyerere, a leader my fellow countrymen and I came to know through the years as a patron saint of the masses and as one of the world’s most influential leaders in the twentieth century.
   His socialist policies were mostly a failure, but not his ideals of equality and social justice. My life in Tanzania, like that of millions of other Tanzanians, was shaped and guided by those ideals. It is these ideals which sustained Tanzania and earned it a reputation as one of the most stable and peaceful countries in Africa, and one of the most united; a rare feat on this turbulent continent.
   It was Nyerere’s biggest achievement."

   Nyereres only mistake was to dare to think over and above his own personal gains.Nyerere si tu aliendeleza umoja lakini alihakikisha mtu mwenye fikra tofauti za kuzuia umoja huo hapati nafasi.
   Leo tunaongelea tofauti za maendeleo ati kutokana na hila za Mwalimu, tunasahau kuwa asingeondoa uchifu kuna makabila yangejitangazia mipaka yao.
   Je ni wangapi wanafahamu kuwa Tanzania tunayoiona leo si ya 1950's ambapo kulikuwepo na Chagga Federation na vilevile Sukuma Federation,makibila ambayo tayari yalikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi.
   Kulikuwepo vyama vya ushirika vilivyosomesha wale tu wa kabila lao na shule nyingi za kidini ambazo japo hazikubagua waumini wengine , lakini primarily zilichukua watu wa sehemu zile tu.
   Having achieved peace for a long time we should not take it for granted.
   Last edited by Lole Gwakisa; 4th September 2010 at 19:30.

  12. #391
   Ogah's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Posts : 6,565
   Rep Power : 22247
   Likes Received
   1386
   Likes Given
   6173

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Mkandara View Post
   Chuma,
   Huyo Jumbe alikataa kitu gani kwa Nyerere?.. ikiwa yeye aliweza kuivunja warsha ya waislaam akiwa makamu wa rais iweje tena ni kosa la Nyerere hali yeye Muislaam ambaye alikuwa na uwezo wa kukataa kama huyo Aziz..Nionyeshe hata hadithi moja ya Nyerere kuhusiana na waislaam ambayo kaifanya pasipo Waislaam wenyewe kuhusika kutoa maamuzi..

   Hii habari mimi siikubaliani nayo kwa sababu ina malengo makuu ya Udini, ni sawa na kesho Chadema washinde uchaguzi huu atokee Mchagga mmoja aanze kudai wao Wachagga ndio wameiwezesha Chadema kusimama kwa sababu tu ya waasisi wake ati ndio iwe historia ya chama kwa kuchukua kabila moja na sii Watanzania waliojiunga na Upinzani...Nina hakika Chadema wasingefika hapa walipo leo kama sii kuungana na watanzania wengine kupambana na CCM Kisiasa na sio kikabila, hii ndio argument yangu..

   Na ikumbukwe tu kwamba historia ya TANU ilianza tokea Kariakoo kama chombo cha kidini ambako asilimia kubwa kama sii yote ya wakazi na wanchama wake wakati huo walikuwa Waislaam. Lakini walipotaka kubadilika na kuwa chama cha kisiasa yalitokea Mapinduzi ndani ya chama cha kidini na AbdulWahid na Mwapachu kumpindua Kreist ktk uongozi na kukifanya chombo hicho kiwe cha kisiasa na sio cha kidini tena.

   kwa hiyo Historia ya Uislaam inakwisha baada ya Mapinduzi na Uzalendo unaingia kwani ndipo Wakristu walipojiunga kwa sababu lengo ni kupigania Uhuru. Kabla ya hapo mtu asikudanganye kwamba Waislaam walikuwa wakipigania Uhuru..Na nazidi kukataa hii habari ya Uislaam kwa sababu hata hao kina Mtenvu na wapinzani wa TAA wakati ule walikuwepo Waislaam, sasa iweje tuchukue moja la kufurahisha lakini lenye machungu tunawaachia Wakristu.

   Haya huyu Mohamed said anasema wazi yeye hakumuogopa Nyerer na aliandika kitabu chake Nyerere akiwa hai iweje mtu huyu kaweza kuandika mabaya yote ya Nyerere asifikichwe isipokuwa wale Mawaziri wenye wadhifa na hadhi kubwa Kitaifa wamwogope Nyerere ktk maswala ya kupinga kuonewa kwa waislaam. Na hata kama ilikuwa kweli navyojua mimi miaka ya 60 kufikia Uhuru hadi tunapata Uhuru asilimia kubwa ya viongozi wa chama wenye sauti ndani ya chama walikuwa Waislaam. Sioni ubavu wowote wa Nyerere kuweza kuwadidimiza Waislaam wakati ule zaidi ya Waislaam wenyewe kushindwa kutekeleza ya dini ndani ya siasa za chama.

   Yoote yazungumzwe lakini ukweli unasimama vipi.. Hadi mwalimu anaondoka madarakani ni asilimia chini ya 10 - ooh no to be exact only 5% ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba ndio walipata nafasi ya kwenda shule za Secondary. Tazameni record ya shule zetu utakuta kwamba ni mikoa ya Pwani tu ndio ilikuwa na wanafunzi wengi Waislaam wakati bara sii ajabu kabisa kukuta vijana wawili wa Kiislaam ktk darasa la wanafunzi 45.
   Na shule za bara alitoka mwanafunzi mmoja au wawili tu toka kila shule kwenda Secondary wakati Mkoa wa Pwani ulichukua hesabu kubwa ya wanafunzi walioingia secondary. Wakuu fikirieni asilimi 5 ya wnafunzi kwenda secondary utaweza vipi kuwaridhisha Umma..na sababu kubwa ni kwamba hatukuwa na nafasi za kutosha secondary kulingana na shule za msingi hivyo sii lazima watu wali fail mitihani isipokuwa nafasi ndizo zilikuwa adimu.

   Sasa mimi Mkerewe naweza kusema kwamba Nyerere aliwapendelea sana watu wa Pwani kuliko sisi bara ama kwa lugha nyingine aliwapendelea zaidi Waislaam (Wazaramo na Manyema) kuliko sisi Wakerewe na Wabara wavaa kaptula kwa kuwapa wao nafasi nyingi zaidi ya mikoa mingine. Hii sio lugha ya UTaifa, sii lugha ya watu wanaojiita Watanzania kama jamii moja isipokuwa ni lugha ya watu wanaojiona wao ni tofauti na wengine hivyo kuwafanya wao wabaguzi.

   Sasa nikuambieni navyoiona picha mimi.. Ubaguzi wa kidini umeanza wakati wa Mwinyi (awamu ya mwisho) na kushamiri baada ya Nyerere kuondoka. Na hakika naamini kabisa kwamba Kighoma Malima alifanyiwa Ufisadi kuondolewa kwa sababu mfumo wa Elimu yetu ulianza kubadilika ghafla na Udini kutumika zaidi kuingia elimu ya juu. Na hakika kama juhudi zake zilivyunjwa nguvu yoyote ile basi mhusika mkubwa ni alikuwa rais Mwinyi - Muislaam mwingine ambaye hakupenda kuona Waislaam wakifanikiwa.

   Aloandika Kighoma Malima yote yanahusiana na wakati huu (baada ya Nyerere), utawala huu wa CCM ambao umekuja kumbatia Udini zaidi kiasi kwamba alipotaka kujitoa na kuingia Upinzani alionekana mwiba wa takoni. Binafsi naamini kabisa Mkapa asingeweza kusimama na Malima ktk uchaguzi uliofuata hivyo waka Mkolimba kumaliza ubishi. Malima aliondolewa sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa alikuwa tishio la Upinzani kwa CCM (Siasa) na waliopitisha kuondolewa kwake wapo Waislaam.
   Haya ni mawazo yangu
   This is what we call "Exploration of Reality"........Well said Bob

  13. Jasusi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th May 2006
   Posts : 12,055
   Rep Power : 173664484
   Likes Received
   4953
   Likes Given
   15529

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Mohammed,
   Unaweza kutupa ushahidi au source ya hii nukuu hapa chini? Kwa sababu vitabu vingine vya historia vina hitimisho tofauti na lako kuhusu uongozi wa Nyerere katika TAA na baadaye TANU

   Mara baada ya Nyerere kuchukua uongozi wa TAA chama kikaanza kusinzia, ushupavu na bidii iliyokuwepo wakati wa uongozi wa Abdulwahid vilitoweka. Kwa hakika ilikuwa wakati mmoja tukatika historia ya Dar es Salaam ambapo Mkristo Erikah Fiah, alikamata bendera dhidi ya serikaly ya kikoloni. Nyerere alikuwa akikaa nje ya mji na alikuwa akija Dar es Salaam mwishoni mwa juma tu. Kwa kiasi fulani hii iliathiri shughuli za chama. Kwa muda wanachama walionekana kama wamepoteza hamu ya chama. Wajumbe wa kamati ya utendaji mara nyingine hawakutokea kwenye mikutano ijapokuwa Dossa aliwapitia majumbani kwao na gari yake kuwachukua.

  14. #393
   Ogah's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Posts : 6,565
   Rep Power : 22247
   Likes Received
   1386
   Likes Given
   6173

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Ukombozi wa Tanganyika UNAENDANA NA UZALENDO WA WATANGANYIKA WOTE bila kujali UKABILA, UDINI WALA RANGI ZAO......PERIOD.............ha yo mengine tunashukuru kwa hadithi/historia.........za kutuambia Nyerere alikaa jamvini Nyumba No36 na kukunja miguu...............sijui nani alikuwa na miembe pale mjini........na mwingine alikuwa seremala na mwingine fundi mshona nguo...........ni vizuri kufahamu na kama kuna ameona kuna historia iliachawa basi na aandike yaliyoachwa ili tuwe na kumbukumbu iliyo sheheni kila aina ya mchango kwa ukombozi wa Tanganyika...............lakin i kutuambia fulani alikuwa mtanashati/msemaji sana.....sijui ili wengine tufanyeje

  15. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Wengi wetu tunajisahau kuwa katika historia ya Tanganyika kilichowasukuma baba zetu kupigania uhuru ni discrimination.
   Na discrimination iliyowaunganisha waafrika wengi ni ubaguzi wa rangi-racialism.

   Tusuisahau kwamba mwafrika wakati ule awe mkristo au mwislamu, alibaki kuwa a third class citizen baada ya wazungu(1st class) wahindi na waarabu(2nd class).Suala la udini wakati huo halikuwepo kabisa.
   Na hata katika kupigania uhuru kuna waliotaka vyama vya kisiasa viwe kwa class hizo,jambo ambalo TANU ililipinga.Zuberi Mtemvu yeye alipendelea waafrika wapigane kwa makundi kwa misingi ya race-rangi, hivyo aliondoka TANU.
   Tuone excerpts from Salma Maoulidi-Pambazuka News,
   "Africa: Racial And Religious Tolerance in Nyerere's Political Thought And Practice

   RACE, RACIALISM AND REPRESENTATION   Nyerere is credited for the level of racial tolerance reigning in Tanzania not witnessed in other countries in the region (Malambugi; Ssekitooleko; MacDonald; USAID). His politics of moderation and racial harmony ensured that the African majority lived in relative peace and harmony with minorities in the territory. A disposition of racial harmony is, however, deeply rooted in the history/herstory of the vanguard of the independence struggle, the Tanganyika African National Union (TANU). Her rallying motto was 'Uhuru na Umoja' ('Freedom and Unity'). Rather than encourage racialism, TANU promoted nationalism seeing people foremost as Tanganyikans.
   Yet, at the heart of the liberation struggle in both Tanganyika and Zanzibar was the question of race. Therefore, the integrationist racial politics in TANU did not always find wide support among adherents leading to fissures among the leadership and membership. Zuberi Mtemvu, formerly the TANU Secretary in the Eastern province, for example, did not approve of TANU's racial politics. On this account he broke away and the formed African National Congress (ANC), a party constituted on a racial platform. Her rallying slogan was 'Africa for Africans.' Another prominent party at the time, the United Tanganyika Party (UTP) - dubbed the governor's party - advocated for a representative system based on multiracialism.   TANU membership was open to all ethnicities and races and as a party of moderate racial politics, the TANU 1954 constitution stressed peace, equality, and racial harmony, while opposing tribalism, isolationism, and discrimination. TANU members were urged to fight the racialist habits of thought - a colonial heritage. During the 1958 elections TANU presented European as well as Asian candidates in different constituencies: Lady Chesham, a European, represented the Wahehe in the southern constituency of Iringa while Ms. Sophia Mustafa, an Asian, ran for the northern constituency in Arusha.
   This was later followed by Ms. Celia Paes, a Goan from Dar es Salaam, formerly the president of the Tanganyika Council of Women and Barbro Johansson, a European who stood for a seat in Mwanza. Together with three African women, these women formed the cream of Tanganyika's elected and nominated representative at independence. Their achievements are eclipsed by prominent non African figures in the first cabinet some of whom became close friends of Nyerere like Amir Jamal, Al-Noor Kassam and Derek Bryceson.
   INDOCTRINATING RACIAL EQUALITY
   To Nyerere, a self proclaimed African socialist, Socialism and Racialism are incompatible. The basis of socialism is a belief in human equality. Socialism is not for the benefit of black men, nor brown men, nor white men, nor yellow men. The purpose of socialism is the service of man (read humankind), regardless of color, size, shape, skill, ability or anything else.
   The Arusha Declaration of 1967, the then blue print for African socialism ('Ujamaa') in Tanzania, does not talk about racial groups or nationalities. It defines as friends those who stand for the interests of the workers and peasants, anywhere in the world. It urges against putting people in pre-arranged categories of race or national origin. Rather, it wants each individual judged according to her or his character and ability similar to Martin Luther King Jr.'s plea for people to be judged by the content of their character."

   Tusisahau vile vile kuwa msingi mkubwa wa Mapinduzi ya Zanzibar 1964 ni ubaguzi na kuundwa kwa vyama katika misingi ya race-ragi, tatizo ambalo linawasumbua wenzetu mpaka kesho.
   Leo hatuongelei kwa sana ubaguzi au ukabila kwa sana kwa sababu ni matatizo yaliyokwisha tatuliwa kwa kiasi kikubwa na Mwalimu.

  16. JokaKuu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st July 2006
   Posts : 10,413
   Rep Power : 85909134
   Likes Received
   7478
   Likes Given
   9151

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By Lole Gwakisa

   Nyereres only mistake was to dare to think over and above his own personal gains.Nyerere si tu aliendeleza umoja lakini alihakikisha mtu mwenye fikra tofauti za kuzuia umoja huo hapati nafasi.
   Leo tunaongelea tofauti za maendeleo ati kutokana na hila za Mwalimu, tunasahau kuwa asingeondoa uchifu kuna makabila yangejitangazia mipaka yao.
   Je ni wangapi wanafahamu kuwa Tanzania tunayoiona leo si ya 1950's ambapo kulikuwepo na Chagga Federation na vilevile Sukuma Federation,makibila ambayo tayari yalikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi.
   Kulikuwepo vyama vya ushirika vilivyosomesha wale tu wa kabila lao na shule nyingi za kidini ambazo japo hazikubagua waumini wengine , lakini primarily zilichukua watu wa sehemu zile tu.
   Having achieved peace for a long time we should not take it for granted.
   Lole Gwakisa,

   ..maeneo mbalimbali ya Tanganyika yaliishaanza kudai haki za namna mbalimbali za kujitawala. Sukuma Federation, Wachaga Union, etc etc ni ushahidi kwamba TAA/TANU siyo chama cha kwanza kudai haki za wazalendo wa Tanganyika.

   ..tofauti ya TAA/TANU na Sukuma Federation,Chaga Union etc, ni kwamba TAA/TANU ilikuwa chama cha kitaifa wakati hivyo vingine vilikuwa vya maeneo husika. Sababu iliyopelekea TAA/TANU kuwa cha kitaifa ni kwasababu kilianzishwa DSM ambayo ilibahatika kuwa na mchanganyiko wa watu toka maeneo mbalimbali.

   ..wanachama wa TAA/TANU wenyeji na wazaliwa wa Bara, ndiyo waliokipa chama hicho LEGITIMACY na kuweza kupata wanachama ktk maeneo ya interior Tanganyika. wengi wa wanachama hao walikuwa ni wasomi na walikuwa na mvuto na ushawishi kwa wenzao waliowaacha vijijini.

   ..sasa katika kusema hayo lazima tutambue mchango wa waanzilishi wa TAA/TANU kwa kusoma vyema alama za nyakati. waanzilishi hao waliweza kutumia DIVERSITY iliyokuwepo Dsm wakati ule kuanzisha chama cha kitaifa kilichoweza kuikomboa Tanganyika toka makucha ya Muingereza.

   ..vilevile ni lazima tupongeze vision ya waanzilishi wa vyama kama Sukuma Federation,Chaga Union, etc etc kwa kuweka pembeni tribal interests na kupigania maslahi ya Tanganyika nzima. kuna wanachama wa Chaga Union ambao walikwenda against their Paramount Chief ktk kuiunga mkono Tanu. kuna wengine, mfano Elias Kisenge, waliachia madaraka makubwa ya kikanda, na kuweka utaifa mbele, kwenda kuitumikia Tanu. Pia wapo wazalendo kama Paul Bomani, Clement George Kahama, waliotokea vyama vya ushirika na kuiunga mkono Tanu.

   ..Tusiwasahau Machifu kama Kidaha Makwaia waliotumia uzito wa nafasi zao kueneza Tanu ktk maeneo ya Wasukuma na Wanyawezi. Ushuhuda wa namna hii uko karibu toka kila pembe ya Tanzania.

   ..napingana na dhana ya kuvibeza na kuvipa jina baya la "ukabila" vyama vilivyoanzishwa na makabila mbalimbali kabla ya Tanu, na Uhuru. tuelewe kwamba Tanu ilienea nchi nzima kupitia mitandao ya vyama hivyo-hivyo ambavyo baadaye tumefundishwa kuvibeza.

   ..pia sikubaliani na dhana kwamba vyama vya ushirika vilikuwa vikiendeleza ukabila na kutoa nafasi za masomo kwa kutumia ukabila. kigezo cha kupewa nafasi za masomo kilikuwa ni uanachama na siyo kabila. vipo vyama vya ushirika ambavyo vilikuwa na wanachama wa kabila zaidi ya moja. pia shule zilizoanzishwa na vyama vya ushirika zilitoa elimu ya KI-SECULAR.

   ..wakati serikali inavunja vyama vya ushirika, wakubwa hawakusema kwamba tatizo lilikuwa vinaendekeza ukabila. pia hizo mamlaka za mazao walizounda zilisababisha matatizo makubwa kwa wakulima wa mazao mbalimbali.

   ..hatua ya kuvunja vyama vya ushirika imerudisha nyuma utamaduni wa wananchi kujitafutia maendeleo yao wenyewe. badala yake tumejenga taifa la watu wanaosubiri serikali iwafanyie kila kitu.

  17. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Quote By JokaKuu View Post

   Nakubaliana na wewe Mkuu katika observations zako.
   Jambo la msingi kabisa ni kuwa upiganiaji wa uhuru wetu hata baada ya vita kuu ya pili haukuanzia pwani peke yake. Hivyo basi kuondoa specific credit kwa kundi moja.
   Hii ni pamoja na ukweli kuwa kabla ya vyama vya siasa umoja ulioonekana ni wa vikundi au jumuiya zilizokaribu karibu na zenye uelewano kama makabila.
   Sikuliandika hilo kwa kulidegrade hapana , bali nikuweka mambo bayana kuwa ukombozi wa Tanganyika haukuanzia Dar es salaam peke yake.

   Suala la vyama vya ushirika ni complex kidogo.
   Vyama vya ushirika vilvyoanzishwa enzi za mkoloni viljipatia nguvu kubwa sana ya kiuchumi na kisiasa.
   Kama ulivyotoa mifano ya ukoo wa Bomani huko Nyanza, nguvu yao kubwa ilianzia chama cha ushirika, Victoria Federation of Cooperative Unions.
   Victoria Federatuion kwa wakati huo(1944-1955) ndio ilikuwa Ushirika wenye nguvu kuliko chama chochote barani Afrika.
   Vivyo hivyo KNCU Moshi na Rungwe Cooperative Unions ikiwa vyama vya kwanza kwanza nchini Tanganyika.
   Kimsingi ni kweli kuwa vyama hivi havikuwa vya kikabila lakini vilioperate in specific geographic boundaries ambazo vile vile zili zingira jamii na kabila husika.(Read a short history of Tanganyika, by John Iliffe)
   Siyo siri kuwa hadi siku za karibuni kama hujui kuongea kisukuma , kupata uongozi ndanu ya NCU itakuwa kazi kwako.Halikadhalika kwa vyama KNCU-Moshi ,RCU-Tukuyu nk.
   Vyama hivi vilisaidiana na serikali ya kikoloni kujenga mashule hata hospitali wakisaidiana na misheni.
   Hii ndio hali ilivyo kuwa.
   Nakubaliana nawewe mkuu JK kuwa kati ya makosa aliyofanya Mwalimu ni kuviua kiujumla vyama hivi.Hata serikali ilipojaribu kuvirudishia uhai tayari damage ya kimfumo ilikuwa too deep to be healed.
   Last edited by Lole Gwakisa; 4th September 2010 at 21:50.

  18. #397
   Ogah's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Posts : 6,565
   Rep Power : 22247
   Likes Received
   1386
   Likes Given
   6173

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   .......unajua kuna mijitu inajitafutia umaarufu kupitia mgongo wa dini.......kuandika vitabu na kutoa hadithi zisizo na msingi...............MIJITU YA AINA HII NI YA KUPIGWA VITA KAMA UKOMA.................kwa sababu ndio watakaosababisha UMOJA wetu kuwa tete kama bado haujawa............

  19. Mohamed Said's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2008
   Posts : 6,939
   Rep Power : 340144
   Likes Received
   5956
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Jasusi. Ahsante habari hiyo ni kutoka kwa Waziri Dossa Aziz. Katika kitabu zipo citation zote.

  20. Mohamed Said's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2008
   Posts : 6,939
   Rep Power : 340144
   Likes Received
   5956
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   LG: Ahsante nimesoma mchango wako nami nataka nipite humo humo ulipopita wewe kwa hiyo nakuwekea hapa chini moja ya vipande vyangu ambavyo huvipenda:

   Nyumba ya Abdulwahid ilikuwa vilevile sehemu ya kukutania hawa vijana wasomi pamoja wa wake zao, kwa kula pamoja na kuburudika. Halikadhalika Abdulwahid alikuwa na uhusiano mzuri na machifu wengi wa Tanganyika. Machifu hao wakiwa Dar es Salaam kuhudhuria Baraza la Kutunga Sheria, Abdulwahid alichukua fursa hiyo kuwakaribisha nyumbani kwake kwa chakula cha mchana au usiku na wakati mwingine aliwafanyia dhifa. Baadhi yao walikuwa Chifu Haruna Msabila Lugusha wa Sikonge, Mtanganyika wa kwanza kufuzu kama bwana shamba, Chifu Thomas Marealle wa Marangu, kwa sababu Abdulwahid alizoea kumtania kwa kumwita Marealle ëKing Tom-. Waingereza walitaka Waafrika waamini kuwa ufalme ni wao pekee, Wazungu ndiyo walikuwa na mfalme, malkia, wana na mabinti wa mfalme. Waafrika wangeweza kuwa na machifu tu. Chifu David Kidaha Makwaia wa Shinyanga na wengine vilevilewaliweza kuwa wageni wa Abdulwahid nyumbani kwake.

   Abdulwahid aliwakumbusha vijana wenzake kwamba hakuna kati yao aliyekuwa na wadhifa wowote katika TAA, ambapo mijadala yote iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwake juu ya Tanganyika ilipostahili kufanyika. Abdulwahid, akikumbuka ahadi iliyowekwa mwaka 1945 kule Imphal nchini Burma ya kuunda chama cha siasa, mara nyingi sana alijadiliana na marafiki zake Mwapachu, Dossa Aziz na kakake mdogo wake Ally kuhusu kutekeleza ile azma ya kuunda chama cha siasa ambacho kingewajumuisha watu wote wa Tanganyika. Inasemekana Mwapachu na wengine wachache kama Stephen Mhando walikuwa na shauku sana na wazo hili lakini vijana wengi, hususan wale waliokuwa watumishi serikalini walikuwa na mashaka iliyojaa hofu kuhusu wazo hilo.

   Ofisi ya Mwapachu pale Ilala ikawa kituo cha mijadala ya siasa nyakati za mchana. Jioni vikao hivyo vya majadiliano vilihamia Tanga Young Comrades Club. Hiki klikuwa kilabu maarufu cha kukutana, hasa kwa vijana maarufu na muhimu katika mji wa Dar es Salaam. Kilabu hiki kilikuwa New Street, Karibu na makao makuu ya TAA. Mijadala ya siasa nyumbani kwa Abdulwahid au katika ofisi ya Mwapachu Ilala au Tanga Club kidogo kidogo ikawa inaingia katika nadharia ya vile vijana wangeweza kuitoa TAA kutoka kwa wazee wale, ambao kwa hakika vijana waliwaona kama makapi ya utawala wa Kijerumaini. Wakati ule mwaka 1949, Mwalimu Thomas Plantan ndiye aliyekuwa rais wa TAA. Katibu wake alikuwa Clemet Mohammed Mtamila.

   Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu. Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua. Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.

   Mwaka wa 1952, akiwa na umri wa miaka ishirini na nne Abdulwahid alichaguliwa kuwa rais wa chama cha TAA. Kwa Chini ya miaka minne alitoka Chama cha Makuli kama katibu hadi katibu wa TAA na baadaye rais wake. Tajiriba ya Abdulwahid, alioipata akiwa katibu wa Chama cha Makuli chama ambacho wanachama wake walikuwa na elimu ndogo sana, ilikuwa lakini ulikuwa uzoefu huu uliyomrusha moja kwa moja hadi kufikia uongozi wa TAA, chama ambachokilikuwa na wasomi makini. Abdulwahid alikuwa bado kwenye mkondo akifuata nyayo za baba yake za kutumikia jamiii na kutawala siasa za Dar es Salaam kama kiongozi wa juu kabisa wa TAA. Hata hivyo, msingi wake wa siasa ulikuwa Dar es Salaam na ushawishi wake haukuvuka mipaka ya mji na matawi ya mijini ya TAA Tabora, Mwanza na Dodoma.
   Kleist, baba yake, alikuwa katibu muasisi wa African Association akiwa na umri wa miaka ishirini na tano. Abdulwahid alichaguliwa kuwa katibu wa TAA akiwa na umri wa miaka ishirini na sita. Kleist alikiongoza chama cha wafanyakazi kilichokuwa kikianza kuchanua nchini Tanganyika. Wakati huo alikuwa ameajiriwa na Tanganyika Railway wakati ambapo Abdulwahid aliongoza Chama cha Makuli kwa kuajiriwa na chama chenyewe. Kleist kamwe hakuchaguliwa kuwa rais wa African Association, si kwa sababu hakuwa na uwezo wa kazi hiyo, ila kwa sababu kama katibu, alikuwa mtu hodari kwa kupanga.

   Mara tu baada ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa TAA, Abdulwahid alifanya ziara rasmi Mwanza na kisha akaenda Nansio, katika kisiwa cha Ukerewe kumtembelea rafiki yake Mwapachu na kufungua ofisi ya tawi la TAA. Mwapachu alipewa uhamisho kwenda Nansio kama Assistant Welfare Officer. Katika kuonyesha mshikamano na kuunga mkono TAA, Mwapachu bila ya hofu kuwa angeliiudhi serikali, aliwahamasisha wananchi wa Nansio kumpa mapokezi makubwa rais wa TAA, Abdulwahid Sykes. Aiandaa mashua maalum kumvusha Abdulwahid kutoka Mwanza hadi pale kisiwani. Makaribisho ya kijadi yalifanywa pale bandarini kumpokea rais wa TAA na mkewe. Ndani ya mashua ile kutoka Mwanza alikuwa Michael Lukumbuzya aliyekuwa akirudi nyumbani kutoka Makerere College kwa likizo. Lukumbuzya ndiye aliyekuwa akitarajiwa kuja kutawala kisiwa hicho kama chifu katika siku za usoni. Lukumbuzya alistaajabishwa kwa zile sherehe pale kisiwani ambazo alikuwa anafanyiwa kijana mtanashati ambaye yeye hakuwa anamfahamu. Lukumbuzya alimuuliza Mwapachu huyo kijana aliyekuwa akipewa mapokezi yale ya heshima ni nani. Mwapachu alimjulisha kuwa huyo alikuwa Abdulwahid Sykes, rais wa TAA kutoka makao makuu Dar es Salaam. Abdulwahid na Mwapachu walijadili uwezekano wa kutuma ujumbe wa TAA kwenda kuzungumza mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York kuwasilisha suala la uhuru wa Tanganyika. Aliporudi makao makuu Abdulwahid alipendekeza kuundwa kwa sekretarieti ya kudumu katika ofisi ya New Street kushughulikia kazi za kila siku za chama. Alexander Tobias aliajiriwa kama mfanyakazi wa kwanza wa TAA. Tutakuja kuona hapo baadaye jinsi Alexander Tobias alipokuja kukisaliti chama cha TAA kwa Waingereza.

  21. Mohamed Said's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2008
   Posts : 6,939
   Rep Power : 340144
   Likes Received
   5956
   Likes Given
   286

   Default Re: Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

   Ogah: Ahsante kwa mchango wako nimeupenda ila tujadili hoja kwa hoja bila ghadhabu. Mimi naelewa mnavyojisikia kwa kusoma historia ya wazee wetu ambao kwa kipindi kirefu mchango wao haukuwa unajulikana. Umoja wa kweli utapatikana kwa katika misingi ya haki.

  Page 20 of 50 FirstFirst ... 101819202122 30 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Makabila yaliyogoma kupigania uhuru haya hapa
   By RICHEST in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 15
   Last Post: 22nd July 2011, 14:07
  2. CCM wakiri kusahau waasisi wa TANU
   By SubiriJibu in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 1
   Last Post: 8th July 2011, 13:08
  3. Replies: 16
   Last Post: 4th July 2011, 11:52

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...