Mara nyingi hua nasikia MTU akisema huu ni mwili wangu, sikio langu, pumzi yangu, moyo wangu, mawazo yangu, akili yangu, hisia zangu... Roho yangu n.k..
Sasa maswali ninayojiuliza:-
- mtu ni roho, mwili, hisia, au ni nini hasa?
- sababu hata mtu akifa bado maiti itaitwa mwili wa fulani. sasa yeye "fulani" yuko wapi?
- yeye ni kitu gani?
Kila kitu katika mwili wa mtu kinamilikiwa na huyu mtu...ndo maana "...angu" haziishi...so kama kila kitu ni changu..."mimi" mwenyewe nipo katika nafasi gani sababu mpaka pumzi bado ni yangu...zamani nikiwa mtoto nilidhani "mtu" ni roho lakini baadae nikaona haitoshi mtu kua ni roho sababu roho ni ya "mtu" so huyu "mtu" halisi ni nini hasa?
Naomba msaada wenu wana jf maana hii kitu inanisumbua sana kuielewa!!!

Reply With Quote



Follow Us Here