Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Rupia ...hazina ya mjerumani

    Report Post
    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 21 to 40 of 62
    1. #1
      client3's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th August 2007
      Posts : 204
      Rep Power : 642
      Likes Received
      36
      Likes Given
      69

      Default Rupia ...hazina ya mjerumani

      Mwana jf
      Je umeshawahi kusikia visa na mikasa ya watu wanaotafuta rupia maarufu kama pesa au hazina ya mjerumani?
      binafsi nimekuwa nikisikia kuna watu huwa wanakwenda mahala ambapo wamepewa viashiria kuwa kuna rupia na huchimba kama wachimbavyo wachimbaji wa migodini...
      hii shughuli ni maarufu sana mkoani Mbeya na Njombe Iringa, nimewahi ona tukio la nyumba kubomoka baada ya watu waliokuwa wakichimba chini kwa chini kutokezea kwenye nyumba ya mzee mmoja huko Mbeya.
      Maswali yangu ni:
      1. je kuna ukweli wowote wa hili jambo?
      2. je rupia ni nini...ni pesa hasa au aina fulani ya kitu cha thamani?
      3. je rupia hutumiwaje baada ya kupatikana kwani kuna tetesi kuwa ina thamani kubwa sana.
      4. kuna mtu ashawahi kuiona hiyo rupia.

      nawasilisha.

    2. Miaka 50

    3. #21
      MAKOSHNELI's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 114
      Rep Power : 431
      Likes Received
      85
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By ipycalypse
      makoshneli mkuu mimi pia naishi hapa jijini mbeya uliyoyaeleza mengi nayajua so mfano bwana lena, soko la uhindini pia kuna mti kwa babu yangu inasemekana kuna rupia maeneo hayo kikweli hata tukienda kesho ilo eneo wamejaa nyuki na hawajawahi kuhama.
      mkuu kama nilivyoandika hapo juu wajerumani nadhan kwa uzoefu na elimu yangu naona ndio watu waliopata kuelimika zaidi hasa karne ya 17,18 na 19 coz mambo waliyoyafanya miaka hyo ya zamani with respect na technology+miundombinu ya wakati huo ni makubwa mno kwanzia ujenzi wa madaraja,nyumba,reli,meli,subm arine,migodi nk we just imagine mali zao walizificha kabla ya vita ya kwanza ya dunia but hadi leo pamoja na kuendelea kwa teknolojia bado huwezi ukatoa! So simple and clear sehem walizoficha mali zao walifanya mazindiko tena makubwa sasa miongoni mwa hayo mazindiko nikama nyuki au nyoka wa miaka yote yaani unakuta hiyo sehemu kuna nyuki au nyoka hafi wali haami hilo eneo,vi2 vingine nikama majini hasa chunusi sehem zenye maji kama mito na maziwa kama wewe ni mwenyeji wa mby nenda mabatini ile njia ya kuelekea itende jeshini unapokaribia kuingia eneo la jeshi kuna kota ya kwanza mkono wa kulia ipo pembezoni mwa mto ukiipita hiyo kota umbali kama wa mita 20 mtoni kuna shimo hapo na tayari zaid ya watu 4 walishawahi potelea hapo 1 akiwa ni mwanajeshi,jeshi walishaweka tangazo hapo kuwa ni marufuku mtu kufanya shughuli zozote eneo hilo ni hatari,eneo hilo kwa wakazi wa muda mrefu wa mabatini ukiwauliza "yorodani" ndio wapi watakusimulia vi2ko vya hapo coz zamani walikuwa wanakwenda hapo kufua na kubatiza waumini wao kabla hapajapigwa marufuku,mkuu yapo maeneo mengi sana hasa mkoa wa mby na wilaya zake zote na trick nyingine wajerumani waliyokuwa wanatumia hasa katika mashimo waliyofukia mali zao ni kuweka chupa zenye mecury so ukienda lazma utumie tochi kumulika sababu ya giza so on the way kumulika endapo utamulika ile chupa yenye mercury bulbu ya tochi inapasuka kutokana na reflection ya mercury

    4. #22
      chakarikamkopo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Posts : 73
      Rep Power : 366
      Likes Received
      31
      Likes Given
      22

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Binafsi nimeshiriki sana kwenye hiyo biashara......kuna ukweli fulani lakini sehemu kubwa ni utapeli kwasababu ya ujinga na kukosa elimu kwa watu wengi. Watu wengi wanangaika kutafuta hivyo vitu lakini ultimately hakuna mtu anayemtaja mnunuzi wa uhakika...wanunuzi wote ni wa kufikirika.

      Uzoefu wangu: NI kweli kuna hazina nyingi sana ambayo Wajerumani waliaacha Tz....wakati ule Msuya akiwa Waziri Mkuu katika ziara yake moja Ujereumani aliomba apewe ramani za sehemu ambazo wajerumani waliacha hazina ili zifukuliwe na zigawanywe. Jibu alilopewa ni kuwa hazina nyingi zilikuwa za watu binafsi wanaweza kushirikiana kwenye hazina za nchi ambazo nyingi zina vitu vya serikali....silaha, nk.

      Hazina ya serikali pale Mbeya Tukuyu ipo jengo la mkuu wa wilaya...hata kwa macho ukiangalia ile ofisi imejengwa juu ya mlima wa kutengenezwa kule chini ni shimo kubwa sana. Mlango wa kuingilia upo ofisi ya afisa utamaduni wa wilaya. hata ukitembea kwenye ofisi utaona kuna hali ya kuonyesha chini kuna mtikisiko wa uwazi. Mlango mwingine nadhani uko nyumba aliyokuwa akiishi OCD. Miaka kumi iliyopita shirika la moja la Ujerumani waliomba kukarabati boma la mkuu wa wilaya na waliomba ukarabati uanzie ofisi ya utamaduni. Watu wakamshtua aliyekuwa RAS wa mkoa Mbeya (name withheld) akazuia ukarabati huo

      Kule kijiji kwa akina Kapteni Komba kuna wageni wajerumani walichimba mashimbo kanisani na kwenye baadhi ya majengo ya kanisa hayo mashimo yalikuwepo hadi mwaka 2006 nilipopita hapo

      Kuna kijiji kimoja cha akina Joyce Mhaville (wa ITV) nimekisahau kule Njombe baada ya Isoliwaya kabla hujafika Mfriga kuna binti wa kizungu alikuja kama kama volunteer akakaa baada ya miezi kadhaa akawaita wanakijiji wamsaidie kuchimba shimo fulani akawaambia mkifika sehemu ngumu muache ili nililete vifaa vingine usiku huo akaenda peke yake akachukua cha kuchukua asubuhi wakakuta shimo tupu na binti akatoweka hadi kesho.....sehemu inaitwa Lupembe

      Kuna sehemu Mbeya inaitwa Ileya....pale kuna mzungu alikuwa tajiri sana yeye pia alificha mali zake jirani kabis na kanisa la Moravian hata alama za mawe alizoweka kuelekeza alipoficha mali zipo sema vile ni muda mfupi alama hizo zinapotea unapoingia kwenye vichaka. Baada ya kanisa la RC chini ya ''mtafutaji'' mashuhuri retired Afisa Usalama (name withheld) kushtukia hiyo dili waliamua kununua eneo lote hilo ili baadaye waanze kutafuta hizo mali wenyewe.

      Kifupi ni kuwa Nyerere aliamua kujenga magereza, JKT, Shule sehemu zote ambazo alihisi kuna hazina ya madini au wajerumani waliaacha mali zao

      The story goes on and on............................ .....

    5. #23
      Ipycalypse's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2011
      Location : Mjini hapa
      Posts : 1,172
      Rep Power : 638
      Likes Received
      248
      Likes Given
      148

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Mkuu MAKOSHNELI iyo njia ya Itende nimepita sana tena nilipokua primary ikitokea mitihani ya jumamosi inafanyika Kalobe primary basi nilikua nabana nauli napita itende mpaka kalobe me nilikua nakaa Forest. Ebu nipe maeneo mengine mkuu niendelee kupata ujuzi.

    6. #24
      Ipycalypse's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2011
      Location : Mjini hapa
      Posts : 1,172
      Rep Power : 638
      Likes Received
      248
      Likes Given
      148

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      chakarikamkopo Mkuu kama unaweza kuendelea na hayo maeneo mengine itakua vizuri kama ujuavyo watu wengi hawana hizi story ni vizuri ukaendelea na list pia itasaidia kupunguza maumivu ya siasa za Tz

    7. #25
      MAKOSHNELI's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 114
      Rep Power : 431
      Likes Received
      85
      Likes Given
      2

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      mkuu maeneo yapo mengi sana sehemu zingine nsizijui ila kama ukijiingiza katika hiyo ishu utakutana na jamaa kibao ambao kila kukicha mtakuwa mnagundua maeneo but kwa uzoefu wangu na kwa muda niliojihusishaga na hayo mambo sijawahi ona mtanzania katoa mali za wajerumani sehem walizozificha zaidi ya kumuona Lena na wajerumani wengine wanaokujaga tz kutoa refer post ya chakalikamkopo hapo juu,wengi wa watu huishia kutapeliwa,kufa na kufirisika huku wakitafuta hizo mali lakini hawapati,na unatakiwa kuzingatia kuwa ON YOUR WAY kwenda kutoa hazina ya mjerumani kuna 'DEALTH TRAP' kwa kiswahili ningesema MITEGO YA KIFO hasa kwa hazina zilizofukiwa ardhini,mfano ni PROXIMITY BOMBS,WIRE FUSED BOMBS,CABON CHAMBERS(VOIDS),MERCURY,ACIDY, MASHETANI,MAJI, NK ....so wao wakati wakiwa wanatoa huwa wanajua SAFE entry positions ambazo huwezi ukajua hadi uwe na ramani origina ya huyo aliyedesign hilo shimo,labda kwa kuongezea katika post ya chakalikamkopo nikwamba Nyerere alipokwendaga marekani immediately baada ya kupata uhuru kilichompeleka huko ni kwenda kuomba msaada wa ujenzi wa reli tokea DAR ES SALAAM hadi KAPIRI MPOSHI lakini wengi hawajui nikuwa ile trip ilikuja baada ya wanakijiji fulani wakishirikiana na baadhi ya maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakati huo walimkamata mjerumani mmoja ambaye alikutwa katokea katika pori la seluu akiwa na baadhi ya madini na baadhi ya ramani! sasa nikwamba katika pori la seluu ukiingilia KIBITI mkoani pwani takribani km kama 200 hivi kuna boma la zamani sana la mjerumani ambalo inasemekana mjerumani huyo alitokea hapo sasa kitu ambacho ni interested nikwamba moja ya ramani ambazo alikutwa nazo ni surveyed map ya reli ambayo wajerumani walifanya coz walikuwa na lengo la kuunganisha makoloni yao yote kwa njia ya reli kutokea germany east africa(tanganyika) hadi BOTSWANA na baadhi ya ramani zenyekuonyesha maeneo yaliyohifadhiwa hazina so zilipomfikia mchonga ndio akapata wazo la kujenga reli ya TAZARA! na akajenga shule,na kambi za jeshi sehemu ambazo kulikuwa na hivyo vitu but sio zote coz hakupata ramani zote,sasa katika kuhaha kutafuta watu wa kujenga akaenda kwa JF KENEDDY kuomba msaada ,jfk alipojua kuwa jamaa ni kichwa na kajua nini walichoacha wamarekani akamwambia usa haiko tayari kuisaidia tz kwa kipindi kile (coz tulikuwa upande wa china na russia) ila yeye binafsi AKAMPA NYERERE KITABU AMBACHO ALIAMBIWA AKISOME KITAMSAIDIA! inasadikiwa kile kitabu kilikuwa na ramani zote za Hazina wajerumani walikoficha na sehemu zenye madini ambazo wajerumani walifanya survey ambazo wamarekani walizipata baada ya kuipiga ujerumani ktk vita kuu ya 2 ya dunia CIA walipojua kuwa JFK kampa copy ya hicho kitabu WAKAMUIBIA JKN KABLA HAJAONDOKA IKULU YA WHITE HOUSE!,mchonga baada ya kuona hayo akaendazake china kuomba msaada wa kujenga reli tokea dar ha kapirimposhi zambia MAO wakati huo wameshibana sana na JKN ukawa msaada ambao hadi leo tunayo hiyo reli,sasa baada ya wachina kuja wao walipewa tu ile ramani ya mjerumani na kufanya survey kidogo tu na wakaanza ujenzi sasa marekani na uingereza wakahisi kuwa huenda wachina wanajua kuhusu hazina za mjerumani na wangeweza kutoa so nao ili wawe karibu kupeleleza nini kinaendelea wakaahidi kutoa msaada wa kujenga BOMBA LA MAFUTA NA BARABARA KUTOKEA DAR HADI ZAMBIA! na kama hujui kulishatokea mapigano kati ya wahandisi wa kichina na marekani, waingeleza sehemu ambazo hivi vitu viwili vilikuwa vinapishana mfano ni nipale usangu ambapo leri inavuka barabara hadi nyerere aliamua maeneo kama hayo ujenzi wa bomba na barabara urukwe serikari yenyewe itakuja kumalizia sjamaa wanatujua ndani nje nje ndani kila kitu thats y usishangae migodi mikubla inatoka canada ,usa na kwingine kote inakuja moja kwa moja tz hata hawahangaiki kufanya sijui upembuzi yakinifu nk ..............

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Ipycalypse's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2011
      Location : Mjini hapa
      Posts : 1,172
      Rep Power : 638
      Likes Received
      248
      Likes Given
      148

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      MAKOSHNELI hii iko deep sana ngoja nisave kabla wachakachuaji hawajaja. Thank you brother
      client3 likes this.

    10. #27
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,514
      Rep Power : 1794
      Likes Received
      654
      Likes Given
      0

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Jamaa nakupa pongezi kwa kudadavua uzuri sana,nilikuwa na ufahamu mdogo sana wa hazina za wajerumani,wengi wanaishia kufilisika,wengine kufa,bila kupata chochote

    11. #28
      MAKOSHNELI's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 114
      Rep Power : 431
      Likes Received
      85
      Likes Given
      2

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Labda kwa kuongezea zaidi kuna baadhi ya mambo najaribu ku connect dots kuanzia utawala wa mkapa hadi sasa nakumbuka mwishoni mwa utawala wake 2005 aliitwa akafanye ziara ujerumani,kilicho shtua mataifa mengi ni namna alivyopokelewa mkapa! Ilikuwa hv ndege ya mkapa wkt imeingia anga la ujerumani zilirushwa ndege za kivita 4 kwenda kumlaki mawinguni ! Zikaizunguka hyo ndege kila moja na upande wake then akapata mapokezi ya kutisha kuanzia airport had ikulu ya ujerumani ambako alikutana na raisi wa ujerumani kwa mazungumzo behind door,inasadikiwa moja ya mambo ambayo wajeruman waliyapa kipaumbele ni hizo mali zao walizoziacha inasadikiwa kuwa BWM alikubali hasa ukizingatia mchonga alikuwa katangulia mbele ya haki so hakukuwa na kipingamizi tena! Immediate wiki moja baada ya BWM kurejea marekani kupitia balozi wao dar wakatuma ujumbe mzito mkapa endapo akiwaruhusu wajerumani kurudi kuchukua mizigo yao tanzania tunge suffer kuanzia kunyimwa misaada hadi kuwa ukanda wa vita kama congo so mipango yote ya wajerumani ikaishia hapo! Ninavyowajua wajerumani sidhan kama ndo waligive up kirahisi hivyo hasa baada ya kushtukiwa na CIA so nadhan (sina uhakika sana najaribu ku connect dots) wamekuja na technic nyingine ya kukifadhili chama fulani cha upinzani ambacho viongozi wake wengi wa juu mbali na kuwa wamesoma huko pia wamekuwa wanakwenda huko mara kwa mara kuhudhuria makongamano mbali mbali!,na kumekuwa na tuhuma hasa kutoka chama tawala kuwa kunachama kinafadhiliwa na mataifa flani ya nje huko,Lakini ni mapema sana kuhisi hicho chama ila "TIME WILL TELL" kama wameshaandaliwa kuwa ma-puppet au ni misaada tu thats y marekani wakaenda kuweka CIA base na ubalozi mdogo kule mbalizi mbeya wakijifanya wanapaita UTENGULE COURT HOTEL kwa lengo la kumonitor pilikapilika za wajerumani!
      KWANINI MBEYA? Na sio mikoa mingine haya mambo yanatokea na kufanyika nitaendelea kudadavua next time
      client3 and Priya like this.

    12. #29
      SHIMBONONI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th September 2011
      Posts : 91
      Rep Power : 406
      Likes Received
      24
      Likes Given
      35

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Quote By Katavi
      Nimewahi sikia habari za rupia, kwa kweli zinatisha ni mambo ya uchawi na makafara.
      Mkuu,

      Taf usidanganyike na story za Rupia! Hilo ni game la Wajanja wanaotumia ujinga wetu kujipatia pesa! Me nilifuatilia sana suala hili kwa miaka kadhaa na nimepata hasara kubwa ya muda na raslimali! In fact nimezungushwa mikoa yote ya Tanzania, Rwanda, Burundi na Camerun! I got sense nilipokwenda kuonana na Ist Secretary at Germany embassy in Dar! NILIAMBIWA STOP FOOLING yourself! I stopped being a fool and became wise!
      client3 likes this.

    13. #30
      client3's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th August 2007
      Posts : 204
      Rep Power : 642
      Likes Received
      36
      Likes Given
      69

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Last edited by client3; 7th August 2012 at 22:36.

    14. #31
      mkali mimi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th August 2012
      Posts : 80
      Rep Power : 357
      Likes Received
      4
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By MAKOSHNELI
      Labda kwa kuongezea zaidi kuna baadhi ya mambo najaribu ku connect dots kuanzia utawala wa mkapa hadi sasa nakumbuka mwishoni mwa utawala wake 2005 aliitwa akafanye ziara ujerumani,kilicho shtua mataifa mengi ni namna alivyopokelewa mkapa! Ilikuwa hv ndege ya mkapa wkt imeingia anga la ujerumani zilirushwa ndege za kivita 4 kwenda kumlaki mawinguni ! Zikaizunguka hyo ndege kila moja na upande wake then akapata mapokezi ya kutisha kuanzia airport had ikulu ya ujerumani ambako alikutana na raisi wa ujerumani kwa mazungumzo behind door,inasadikiwa moja ya mambo ambayo wajeruman waliyapa kipaumbele ni hizo mali zao walizoziacha inasadikiwa kuwa BWM alikubali hasa ukizingatia mchonga alikuwa katangulia mbele ya haki so hakukuwa na kipingamizi tena! Immediate wiki moja baada ya BWM kurejea marekani kupitia balozi wao dar wakatuma ujumbe mzito mkapa endapo akiwaruhusu wajerumani kurudi kuchukua mizigo yao tanzania tunge suffer kuanzia kunyimwa misaada hadi kuwa ukanda wa vita kama congo so mipango yote ya wajerumani ikaishia hapo! Ninavyowajua wajerumani sidhan kama ndo waligive up kirahisi hivyo hasa baada ya kushtukiwa na CIA so nadhan (sina uhakika sana najaribu ku connect dots) wamekuja na technic nyingine ya kukifadhili chama fulani cha upinzani ambacho viongozi wake wengi wa juu mbali na kuwa wamesoma huko pia wamekuwa wanakwenda huko mara kwa mara kuhudhuria makongamano mbali mbali!,na kumekuwa na tuhuma hasa kutoka chama tawala kuwa kunachama kinafadhiliwa na mataifa flani ya nje huko,Lakini ni mapema sana kuhisi hicho chama ila "TIME WILL TELL" kama wameshaandaliwa kuwa ma-puppet au ni misaada tu thats y marekani wakaenda kuweka CIA base na ubalozi mdogo kule mbalizi mbeya wakijifanya wanapaita UTENGULE COURT HOTEL kwa lengo la kumonitor pilikapilika za wajerumani!
      KWANINI MBEYA? Na sio mikoa mingine haya mambo yanatokea na kufanyika nitaendelea kudadavua next time
      iko deep sana hii

    15. #32
      Mkekuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 700
      Rep Power : 499
      Likes Received
      84
      Likes Given
      0

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Hii darasa tosha.

    16. #33
      the muya best's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 22nd July 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By client3
      Mwana jf
      Je umeshawahi kusikia visa na mikasa ya watu wanaotafuta rupia maarufu kama pesa au hazina ya mjerumani?
      binafsi nimekuwa nikisikia kuna watu huwa wanakwenda mahala ambapo wamepewa viashiria kuwa kuna rupia na huchimba kama wachimbavyo wachimbaji wa migodini...
      hii shughuli ni maarufu sana mkoani Mbeya na Njombe Iringa, nimewahi ona tukio la nyumba kubomoka baada ya watu waliokuwa wakichimba chini kwa chini kutokezea kwenye nyumba ya mzee mmoja huko Mbeya.
      Maswali yangu ni:
      1. je kuna ukweli wowote wa hili jambo?
      2. je rupia ni nini...ni pesa hasa au aina fulani ya kitu cha thamani?
      3. je rupia hutumiwaje baada ya kupatikana kwani kuna tetesi kuwa ina thamani kubwa sana.
      4. kuna mtu ashawahi kuiona hiyo rupia.

      nawasilisha.
      Rupia nipesa

      S

    17. #34
      Shaffin Simbamwene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2008
      Posts : 628
      Rep Power : 878
      Likes Received
      150
      Likes Given
      49

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Quote By Kichuguu
      SOMA HII:

      The Balson Holdings Family Trust owns two type "B" 15 Rupien pieces - displayed below.This coin below was purchased by the Balson Holdings Family Trust from Heritage Coins in June 2005 (Item 13154) they noted: "lustrous AU and about as nice as we have seen one of these pieces". This piece is about as good as the "Tabora Pound", under siege conditions, gets. Value over US$4,000.
      This coin below, almost UNC for the series, is owned by the Balson Holdings Family Trust. It reflects the deterioration of the dies over time - in particular on the side of the elephant - see rim bottom right area and the rim bordering the eagle at 6 and 9 o'clock. Value over US$3,000.
      Swadakta mzee mwenzangu sasa nimerudi zizini.
      Je mwana wa kijij bado yumo humu?

    18. #35
      Shaffin Simbamwene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2008
      Posts : 628
      Rep Power : 878
      Likes Received
      150
      Likes Given
      49

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Quote By MAKOSHNELI
      Kanisa la mbozi mission na hospital yake
      3.Sehem nyingine ni lilipokuwa soko kuu la mbeya pale mbele ya benki ya NMB mbalizi road ambalo liliungua na linatarajiwa kujengwa soon,guess mkandarasi aliyeshinda tenda ya kujenga pale ni kutoka inchi gani? Makampuni makubwa ma5 yaliomba ,moja la israeli,jingine la austaria,jingine la ujerumani na mengine ya wachina! Wajeruman wameshinda tenda wataanza ujenzi any time baada ya bunge hili la bajeti i guess.
      3.Sehem nyingine utashangaa pale wajerumani walipokwenda kujenga matenki makubwa ya mradi wa maji ambao wameudhamini wenyewe kwa karibu 90% na waliutoa maalumu kwa mkoa wa mbeya tu! Ambao hauna shida sana ya maji ukilinganisha na mikoa ya kati na kusini mwa tz! Mradi huo utamaliza tatizo la maji mby kwa miaka 20! Ijayo imean hadi 2032! PALE UYOLE WALIPOJENGA HAYO MATENKI YAO YA MAJI PALIKUWA NA MASANDUKU YAO!
      MRADI HUU AWAMU YA KWANZA IMEKAMILIKA NA JK KAUZINDUA WIKI HII HII KAMA SIKOSEI!
      Awamu ya pili ya huu mradi ni kupeleka bomba la maji hadi tunduma umbali wa km 103! Ili wapitie na sehem zingine !
      4. LAKE NGOSI TUKUYU MBY!
      Zipo sehem kibao nikianza kuwatajia hapa sitazimaliza so tukirudi kwenye mada nikwamba kweli rupia ya mjerumani inamambo tatizo ni namna ya kuipata coz sehem zote ilizofichwa wajerumani walikuwa wanafanya makafara ya watu kuanzia 10 na kuendelea ambao hubaki hapo kama majini kulinda ila wao wanavyokuwa wanakuja kuchukua huwa kuna maneno flani huyatamka na hayo madudu hutambua mwenye mali kaja either mtoto au mjukuu wake! So huwa hayasumbua tofaut na mswahl ukienda pale na hii ki2 ikapelekea wengi kwenda kwa waganga ambako hupewa masharti ya kutafuta viungo vya binadamu hasa albino!
      Nadhan mkuu umenielewa kama unamaswali zaidi ni pm namba yako ntakujuza zaid
      source: mimi mwenyewe ninafanya kazi za uchimbaji madini hasa dhahabu nipo matundas chunya na pia ni graduate ktk fani ya mining enggrng UDSM
      Duh...Mambo ya dachi yalikuwa balaa.
      Nilidhani ushirikina ni mswahili pekee kumbe hata nyeupe wamo zizini.

    19. #36
      Mupirocin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Location : Tanzania
      Posts : 1,562
      Rep Power : 805
      Likes Received
      523
      Likes Given
      408

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Thanks alot i learned some thing, wadau vp kuhusu Peramiho hapa hapa bado wanaishi hawa wajerumani

    20. #37
      mpalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th September 2010
      Location : MZINGIZINGI
      Posts : 1,537
      Rep Power : 747
      Likes Received
      405
      Likes Given
      359

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      mkuu unatisha tupetupe maudambwidambwi ayo
      Quote By MAKOSHNELI
      Labda kwa kuongezea zaidi kuna baadhi ya mambo najaribu ku connect dots kuanzia utawala wa mkapa hadi sasa nakumbuka mwishoni mwa utawala wake 2005 aliitwa akafanye ziara ujerumani,kilicho shtua mataifa mengi ni namna alivyopokelewa mkapa! Ilikuwa hv ndege ya mkapa wkt imeingia anga la ujerumani zilirushwa ndege za kivita 4 kwenda kumlaki mawinguni ! Zikaizunguka hyo ndege kila moja na upande wake then akapata mapokezi ya kutisha kuanzia airport had ikulu ya ujerumani ambako alikutana na raisi wa ujerumani kwa mazungumzo behind door,inasadikiwa moja ya mambo ambayo wajeruman waliyapa kipaumbele ni hizo mali zao walizoziacha inasadikiwa kuwa BWM alikubali hasa ukizingatia mchonga alikuwa katangulia mbele ya haki so hakukuwa na kipingamizi tena! Immediate wiki moja baada ya BWM kurejea marekani kupitia balozi wao dar wakatuma ujumbe mzito mkapa endapo akiwaruhusu wajerumani kurudi kuchukua mizigo yao tanzania tunge suffer kuanzia kunyimwa misaada hadi kuwa ukanda wa vita kama congo so mipango yote ya wajerumani ikaishia hapo! Ninavyowajua wajerumani sidhan kama ndo waligive up kirahisi hivyo hasa baada ya kushtukiwa na CIA so nadhan (sina uhakika sana najaribu ku connect dots) wamekuja na technic nyingine ya kukifadhili chama fulani cha upinzani ambacho viongozi wake wengi wa juu mbali na kuwa wamesoma huko pia wamekuwa wanakwenda huko mara kwa mara kuhudhuria makongamano mbali mbali!,na kumekuwa na tuhuma hasa kutoka chama tawala kuwa kunachama kinafadhiliwa na mataifa flani ya nje huko,Lakini ni mapema sana kuhisi hicho chama ila "TIME WILL TELL" kama wameshaandaliwa kuwa ma-puppet au ni misaada tu thats y marekani wakaenda kuweka CIA base na ubalozi mdogo kule mbalizi mbeya wakijifanya wanapaita UTENGULE COURT HOTEL kwa lengo la kumonitor pilikapilika za wajerumani!
      KWANINI MBEYA? Na sio mikoa mingine haya mambo yanatokea na kufanyika nitaendelea kudadavua next time

    21. #38
      mpalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th September 2010
      Location : MZINGIZINGI
      Posts : 1,537
      Rep Power : 747
      Likes Received
      405
      Likes Given
      359

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Quote By MAKOSHNELI
      Kanisa la mbozi mission na hospital yake
      3.Sehem nyingine ni lilipokuwa soko kuu la mbeya pale mbele ya benki ya NMB mbalizi road ambalo liliungua na linatarajiwa kujengwa soon,guess mkandarasi aliyeshinda tenda ya kujenga pale ni kutoka inchi gani? Makampuni makubwa ma5 yaliomba ,moja la israeli,jingine la austaria,jingine la ujerumani na mengine ya wachina! Wajeruman wameshinda tenda wataanza ujenzi any time baada ya bunge hili la bajeti i guess.
      3.Sehem nyingine utashangaa pale wajerumani walipokwenda kujenga matenki makubwa ya mradi wa maji ambao wameudhamini wenyewe kwa karibu 90% na waliutoa maalumu kwa mkoa wa mbeya tu! Ambao hauna shida sana ya maji ukilinganisha na mikoa ya kati na kusini mwa tz! Mradi huo utamaliza tatizo la maji mby kwa miaka 20! Ijayo imean hadi 2032! PALE UYOLE WALIPOJENGA HAYO MATENKI YAO YA MAJI PALIKUWA NA MASANDUKU YAO!
      MRADI HUU AWAMU YA KWANZA IMEKAMILIKA NA JK KAUZINDUA WIKI HII HII KAMA SIKOSEI!
      Awamu ya pili ya huu mradi ni kupeleka bomba la maji hadi tunduma umbali wa km 103! Ili wapitie na sehem zingine !
      4. LAKE NGOSI TUKUYU MBY!
      Zipo sehem kibao nikianza kuwatajia hapa sitazimaliza so tukirudi kwenye mada nikwamba kweli rupia ya mjerumani inamambo tatizo ni namna ya kuipata coz sehem zote ilizofichwa wajerumani walikuwa wanafanya makafara ya watu kuanzia 10 na kuendelea ambao hubaki hapo kama majini kulinda ila wao wanavyokuwa wanakuja kuchukua huwa kuna maneno flani huyatamka na hayo madudu hutambua mwenye mali kaja either mtoto au mjukuu wake! So huwa hayasumbua tofaut na mswahl ukienda pale na hii ki2 ikapelekea wengi kwenda kwa waganga ambako hupewa masharti ya kutafuta viungo vya binadamu hasa albino!
      Nadhan mkuu umenielewa kama unamaswali zaidi ni pm namba yako ntakujuza zaid
      source: mimi mwenyewe ninafanya kazi za uchimbaji madini hasa dhahabu nipo matundas chunya na pia ni graduate ktk fani ya mining enggrng UDSM
      tupe na zingine kk....kuna boma wilayani Ulanga-Mahenge ambalo lilifanyiwa ukarabati miaka ya tisini kuna tetes napo kulikuwa na mzigo wao

    22. #39
      mpalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th September 2010
      Location : MZINGIZINGI
      Posts : 1,537
      Rep Power : 747
      Likes Received
      405
      Likes Given
      359

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Quote By SHIMBONONI
      Mkuu,

      Taf usidanganyike na story za Rupia! Hilo ni game la Wajanja wanaotumia ujinga wetu kujipatia pesa! Me nilifuatilia sana suala hili kwa miaka kadhaa na nimepata hasara kubwa ya muda na raslimali! In fact nimezungushwa mikoa yote ya Tanzania, Rwanda, Burundi na Camerun! I got sense nilipokwenda kuonana na Ist Secretary at Germany embassy in Dar! NILIAMBIWA STOP FOOLING yourself! I stopped being a fool and became wise!
      asa kama kweli kuna mali ulitaka wakupe siri zao

    23. #40
      Mpitagwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 927
      Rep Power : 552
      Likes Received
      319
      Likes Given
      204

      Default Re: Rupia ...hazina ya mjerumani

      Nitakuja Mpitagwa mwenyewe kuwaondoa hao nyuki na tuitoe hiyo rupia tutengeze hela.

    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...