JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Njia gani za kutumia ili kuacha kabisa unywaji wa pombe?

  Report Post
  Page 1 of 39 123 11 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 766
  1. Makanyagio's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th June 2009
   Location : Nyakato Mwanza
   Posts : 119
   Rep Power : 659
   Likes Received
   14
   Likes Given
   2

   Default Njia gani za kutumia ili kuacha kabisa unywaji wa pombe?

   Wana JF,

   Kwa yeyote anejua dawa au mbinu ya kumfanya mlevi kuacha pombe. Nina ndugu yangu yeye bila kilevi cha pombe siku haiendi kabisaa na hii imekuwa inarudisha maendekleo yake nyuma.

   Wanaoijua tiba mnijuze niokoe maisha yake na familia yake.


   Baadhi ya majibu kutoka kwa wadau

   Quote By Nel Nelson View Post
   ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) NI NINI?

   Shirika la Afya Duniani (W.H.O) lilithibitisha kuwa ulevi sugu kuwa ni ugonjwa sugu tangu mwaka 1949. Baada ya hapo ugonjwa huu umeendelea kusababisha vifo vya maelfu ya watu duniani. Hapa Tanzania pia watu wengi wameathirika na ugonjwa huu.
   (Utafiti wa W.H.O umedhibitisha kuwa watu millioni 2 na nusu wanakufa kila mwaka kwa sababu ya unywaji wa pombe kupindukia)

   MAGONJWA SUGU NI YAPI? Ni kama Ukimwi (HIV AIDS), DIABATES (KISUKALI), KANSA (CANCER), PRESSURE (MAGONJWA YA MOYO). Kumbuka magonjwa sugu ya hatua za (awali, kati na mwisho) kwa maana nyingine hauna TIBA.

   HATUA YA KWANZA NI YEYE KUKUBALI KWAMBA ANA TATIZO NA YUKO TAYARI KUACHA YEYE MWENYEWE BILA SHINIKIZO LA MTU AU KITU CHOCHOTE.

   Kwahiyo mi nakushauri mtafutie huyu jamaa yako umoja wa watu walioacha au wenye nia ya kuacha ULEVI SUGU uitwao:
   Alcoholics Anonymous (A.A) ni ushirika wa wanaume na wanawake ambao wanashirikiana ujuzi, nguvu na matumaini kati yao ili waweze kutatua matatizo yao na kusaidia wengine kupona ulevi.

   Sharti pekee la uanachama ni nia ya kuacha ulevi. Hakuna ada ya kuwa mwanachama wa A.A, tunajitegemea wenyewe kwa michango yetu wenyewe. A.A haifungamani na madhehebu yoyote ya dini, siasa, shirika au taasisi na haitaki kujiingiza katika mabishano yoyote. Kadhalika A.A haiungi mkono wala kupinga chama chochote.
   Nia yetu ya msingi ni kukaa bila kulewa na kuwasaidia walevi wengine kupona kutokana na ulevi.
   A.A ni kwa ajili ya mlevi ambaye ana NIA YA KUACHA KUNYWA POMBE.

   Usisite kuwasiliana nami ili nikupatie maelekezo zaidi: +255 789 780 529,
   E-mail: [email protected]

   Nakutakia mafanikio mema.
   ===============

   Quote By EMT View Post
   Mkuu kabla ya kuamua kuacha kunywa pombe kuna maswali ya awali ya kujiuliza.
   1. Kwa nini unataka kuacha kunywa pombe? Watu wanaacha kwa sababu mbalimbali kama ukata etc.
   2. Mambo gani mazuri yanatokana na wewe kunywa pombe? Muhimu kujua ili kutafuta njia mbadala baada ya kuacha.
   3. Mambo gani mabaya yanayotokana na wewe kunywa pombe?
   4. Mambo gani mazuri unayategemea baada ya kuacha kunywa pombe?
   5. Mambo gani mabaya yanayoweza kutokana na wewe kuacha kunywa pombe?

   Kutokana na majibu ya maswali hapo juu, hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua. Zipo nyingi. Hizi ni baadhi tuu.

   1. Kama ni mnywaji sana ongea kwanza na daktari wako. Kuacha pombe ghafla kunaweza kukuletea madhara hasa kama ni mnywaji sana. Kuacha ghafla unaweza ku-suffer from panic attacks, anxiety, shakes, mapigo ya moyo kwenda mbio, au hata mwili kupungua. Kwa hiyo, kunaweza kuwa na umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kwanza jinsi ya kuacha.

   2. Badilisha attitude yako juu ya pombe. Kumbuka hakuna anayekulazimisha kuacha pombe (rafiki yako mkubwa ambae amekuwa na wewe kwa muda mrefu). Panga tarehe za kuacha. Be ambitious but reasonable. Kama ni mnywaji sana punguza kidogo kidogo. Ukiacha gafla unawezapatwa na symptoms. Ndio maana wanasizitiza kupata ushauri wa daktari ili aweze kukupangia kitaalamu jinsi ya kuacha pombe.

   3. Kama una pombe nyumbani, get rid all of them. Unaweza kusema itabidi uache pombe kidogo kwa ajili ya wageni. Lakini it is perfectly fine kumpa mgeni chai, soda au hata maji. Kama ni mgeni aliyezoea kuja kwako na kunywa pombe ukimwambia kuwa huna pombe ndani kwa sababu una mkakati wa kuacha kunywa, nadhani atakuelewa vyema.

   4. Rudi back to your feelings. Ukijiskia unataka kulia, then lia. Laugh when you can. Kula ukiwa na njaa. Lala ukiwa umechoka. Usitumie ule muda uliokuwa unautumia kunywa pombe kwa kwenda kulala. It won't help. Mwanzoni itaonekana ni weird but embrace it. Kuna uwezekano kwa sababu ya pombe hujawahi kujua hisia zako kwa muda mrefu. So, you will have to learn to curve.

   5. Usifanye kitu ambacho hauko tayari kukifanya. Kama unaenda kwenye sherehe na kuna pombe usinywe pombe kwa sababu wengine wanakunywa. Mwanzoni inaweza kuwa ngumu lakini you will need to rain check. Protecting your sobriety should be your first priority.

   6. Kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kwa muda na baadhi ya marafiki zako ambao ulikuwa unakunywa nao. Baadae utakuja kushangaa kuwa in fact marafiki ambao ulikuwa unakunywa nao walikuwa wanakunywa only occasionally, tena bia mbili tuu wakati wewe ulikuwa ulikuwa unakata bia tano.

   7. Kama nyumbani unatumia viungo vya kupikia ambavyo vinalazimisha kuwepo kwa bia au wine, then achana navyo. Pia kuna wale wanaosema nyamba choma haiendi bila bia. Itakubidi ukae mabli na nyama choma kwa muda. Wapo ambao wanachoma nyama na kuichanganya na bia wakati inachomwa. Itabidi uache kama unafanya hivyo.

   8. Tafuta kibox kidogo cha mbao cha kuhifadhia fedha. Kila unapofikiria kununua pombe, chukua hizo pesa na tumbukiza huko. Baadae utakujashangaa kiasi cha fedha ambazo ulikuwa unapotezea kwenye pombe. Ikishindikana basi tumia hizo fedha kupunguza stress kama kupata massage au jiunge na gym.

   9. Nununua ring ya bei rahisi na ivae kila wakati kama kielelezo kuwa haugusi tena pombe. Kama wewe ni Mkatoliki unaweza kuvaa Rozari kama kielelezo kuwa hutakunywa pombe wakati ukiwa umeivaa. Ukisikia hamu ya pombe tuu look at the ring.

   10. Kunywa maji kwa wingi. Hata kama ni kutembea na chupa za maji barabarani usiogope.

   11. Omba support kutoka kwa ndugu mme/mke kuhusu what you are going through and nini unachotaka ku-achieve.

   12. Kama kuna chama chochote cha watu wanaotaka kuacha pombe, jiunge nacho. Kama ukikuta chama chenyewe hakina mshiko, don't feel guilty. Its not your fault.

   13. Baada ya siku 90 ya kuwa sober, your whole outlook itabadilika na mwili wako utakuwa in full recovery mode. Utakuwa mtu tofauti na ulivyokuwa na kuna uwezekano weight yako ikapungua pia. Don't worry.

   14. Tengeneza list ya vitu ambavyo umefanya by using alcohol without alcohol, then celebrate maana list itakuwa ndefu.

   15. Furahia how it feel unapokwenda kulala jioni bila kupoteza network.

   16. Usijaribu kuwaelezea watu kuhusu kuacha kwako pombe. Watu wengi hawanywi pombe kama walivyokuwa wanakinywa zamani. Hawapo kama wewe na hawataweza kukuelewa kuwa una tatizo la kunywa pombe. Of course, wako ambao wana hilo tatizo. Either way kuna uwezekano wakakuambia huna tatizo. Mtu akitaka kukukaribisha pombe mwambie asante lakini nitakunywa soda; najaribu kupunguza weight. Kama ni watu wa karibu ipo siku watajua kweli wata-appreciate kwa wewe kuamua kuachana na pombe.

   17. Kubali na kumbuka kuwa pombe sio kitu muhimu maishani mwako kupita vyote.

   18. Kuwa na sababu nzuri ya kuacha pombe. Ni muhimu sana kuwa na sababu tena iwe ya msingi. Kama sababu ni pesa imepungua, kuna uwezakano ukarudia tena pombe kama pesa ikiongezeka. So ni bora kuwa na strong and valid reason.

   18. Usikwepe kwenda sehmu ambazo utakunywa pombe, kama kwenye sherehe, n.k. Badala yake nenda kwenye hizo sehemu ukiwa na attitude nzuri na kumbuka kuwa na good time bila hata kunywa pombe. You can have a good time bila kunywa pombe. Yes, you can. Tena utashangaa jinsi watu na heshima zao wanavyo-behave baada ya kulewa. Kwangu hii ndio sababu pekee iliyonifanya nisinywe pombe.

   19. Memorise a prayer, shairi, nk then rudia kulisema pale unapokuwa katika hatihati za ku-loose your control. It will keep your heard together. Kwa mfabo mtu ambaye anataka kuacha kuchukua rushwa anaweza ku-memorise baadhi ya sentensi kwenye speeches za Mwalimu Nyerere kama "Rushwa ni adui wa haki." Tafuta misemo ambayo inahusina na ulevi.

   20. Jipe mwenyewe zawadi kila siku au kila saa kwa kutokunywa. Sio lazima iwe zawadi kubwa. Just a simple treat kujipongeza.

   21. Nasistiza tena. Ongea na daktari wako. Kuacha pombe gafla kunaweza kukuletea madhara makubwa hasa kama ni mnywaji wa kupindukia.

   22. Fanya mazoezi. Mazoezi yatakufanya u-deal the stress na pia yatasaidia kutuliza ubongo wako na kuboresha afya yako kwa ujumla.

   23. Kulingana na ushauri wa daktari, meza vitamin B supplements kila siku kwa wiki ya kwanza ya kuacha pombe. Pombe inaadhiri uwezo wa mwili wako ku-absorb these. Upungufu wa Vitamin B unaweza kusababisha severe cognitive impairment. So, ongea na daktari wako juu ya hili na hasa kama unatumia medication nyingine.

   24. Kama ni mlevi sana jaribu ku-visualize jinsi unaakavyokuwa wakati ukiwa umelewa na jiulize kama unataka kuendelea kuwa vile.

   25. Kama unatoka kazini na kwenda moja kwa moja bar kunywa, jaribu kubadilisha routine kwa kufanya shughuli nyingine kama kutembelea ndugu na jamaa, kwenda gym au kanisani/msikitini. Ikishindikana kabisa then, jikite JF. JF is never boring na utafaidika zaidi ya kunywa pombe. Ni heri uwe mlevi ya JF kuliko mlevi wa pombe.

   26. Kula kwanza kabla ya kunywa. Hii itapunguza interest ya kutaka kunywa.

   27. Siku za mwanzoni punguza kiasi cha pombe unayokunywa. Halafu jaribu ku-imagine kutokana na kunywa mno jinsi unvyopoteza network, unavyojitapikia, kichwa kinauma, unachelewa kazini, nk.

   28. Don't give up. Wapo wanaosema wamekuwa wakinywa kwa muda mrefu sana kwa hiyo hawawezi kuacha, sijui wamejaribu kuacha mara nyingi lakini nimeshindwa, n.k. Hakuna age limit ya kuacha kunywa pombe. Unaweza kuacha katika umri wowote. It is never too late to quit drinking.

   29. Kama wewe ni mtu wa club sana, kuna strategy alikuwa anatumia rafiki yangu na ilimsadia. Kuwa yeye atakuwa dereva kila tukienda out. Kwa hiyo hatagusa pombe kabisa ili aturudishe nyumani salama. Ilimsaidia sana kutokunywa.

   29. Kumbuka kuacha kunywa pombe kutakuongezea urefu wa maisha yako hapa duniani. Pamoja na magojwa yanayosababishwa directly na unywaji wa pombe kupita kiasi, ukiwa mlevi kupindukia unaweza kufanya mmabo ya ajabu na kusabisha sio kifo chako tuu bali vifo kwa watu wengine pia kama ku-drive wakati umelewa.

   30. Don't let guilty affect you. Unaweza kuji-feel mshamba au guilty kwa kutokunywa pombe lakini usilaumu mwenyewe au mtu mwingine. Hakuna kitu muhimu kama wewe. You are of no use to anyone kama ukifa na magonjwa yanayosabishwa na ulevi. You must overthrow the oppressive rule of alcohol and start afresh, just as any country in revolution. Jiulize Libya waliweza kuachana na Gadaffi wewe kweli utashindwa kuachana na pombe? It will be hard and you must learn from the past, lakini kumbuka kuwa umenganywa na pombe kwa muda mrefu. Sasa ni muda wa kuanza kuyaishi maisha yako. Those around you will appreciate it too.

   Goodluck.

   Quote By Sanctus Mtsimbe View Post

   Alcoholism:   • Alcoholism is a psychological condition
   • Addiction to alcohol can affect one's life negatively
   • Family support and encouragement is critical to help quit drinking


   Symptoms to look for:


   • Depression
   • Anxiety
   • Irritability
   • Regular absence from work
   • Insomnia
   • Frequent intoxicated state


   Natural home remedy using carom seeds:


   1. Take 500 g of carom seeds
   2. Add them to 8 L of water
   3. Boil the mixture till about 2 L water is left
   4. Filter the mixture
   5. Drink 3-4 tbsp whenever you get a craving for alcohol


   Natural home remedy using apple juice:


   1. Drink 2 glasses of apple juice everyday to reduce the craving

   Kwa matatizo mengine tembelea:
   Mafanikio Na Afya Njema: Suluhu Ya Tatizo La Ulevi - Home Remedies for Alcoholism
   'There is no fair in this world'


  2. drphone's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th September 2009
   Posts : 3,553
   Rep Power : 1332
   Likes Received
   129
   Likes Given
   17

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   mwambie aokoke atapona kabisa yani shuhuda zipo nyingi
   THE BEST IS YET TO COME.

   THE GREATEST EXPERIENCE IS TO MEET YOURSELF AND FALL IN LOVE WITH YOURSELF.

  3. Jerome's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 9th September 2009
   Posts : 142
   Rep Power : 653
   Likes Received
   7
   Likes Given
   6

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   dawa yake siku atakapokunywa akaangusha gari watu wakavunja duka ataacha siku hiyohiyo kuna mifano mingi tu ya aina hiyo hakuna dawa zaidi,viginevyo ni maombi tu mpigieni maombi ya nguvu

  4. Juma Contena's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st May 2009
   Posts : 1,199
   Rep Power : 884
   Likes Received
   103
   Likes Given
   18

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   ajiunge na gym make sure he attends regulary, sio lazima abebe vyuma lakini he needs to feel good inside.
   the difference between fantasy and realism is that, one is based on wishful thinking and the other purely on facts.

   jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza......

  5. MaxShimba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2008
   Posts : 36,631
   Rep Power : 0
   Likes Received
   3918
   Likes Given
   679

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Makanyagio View Post
   Wana JF,
   Kwa yeyote anejua dawa au mbinu ya kumfanya mlevi kuacha pombe. Nina ndugu yangu yeye bila kilevi cha pombe siku haiendi kabisaa na hii imekuwa inarudisha maendekleo yake nyuma.
   Wanaoijua tiba mnijuze niokoe maisha yake na familia yake.
   Dawa ni Yesu Kristo.
   Yesu Kristo Ni Mungu
   Jesus Christ is My Sweetheart  6. Kamuzu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th October 2008
   Location : Vigwaza
   Posts : 915
   Rep Power : 855
   Likes Received
   192
   Likes Given
   71

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   nasikia maziwa ya nguruwe yakichanganywa na hiyo pombe halafu akainywa, atatapika sna na ndiyo mwisho wakunywa.

   .............................. ......
   Amani yetu inatumiwa vibaya

  7. Luteni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 2,288
   Rep Power : 1078
   Likes Received
   280
   Likes Given
   74

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   mwache aendelee siku atakayokosa hela ya pombe ndipo ataacha
   Luteni is a True Revolutionist.

  8. Omumura's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th August 2009
   Posts : 477
   Rep Power : 723
   Likes Received
   12
   Likes Given
   3

   Exclamation Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Kama ni mkristu mfungie kanisani, kama ni mwislamu mfungie msikitini na kama hayumo katika hizo dini mbili basi mwache alale kwenye kilabu cha pombe akizinduka amay be ataacha!

  9. Lekanjobe Kubinika's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2006
   Location : Tanzania
   Posts : 3,064
   Rep Power : 8932
   Likes Received
   511
   Likes Given
   856

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Mnyweshe bavaria, akizoea ataichukia harufu ya pombe. Wanahubiriwa sana kilabuni na kina Rose Mhando na Bahati Bukuku na kina Mwang'onda - Utanitambuaje......?


   Leka

  10. Ambassador's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd June 2008
   Posts : 909
   Rep Power : 872
   Likes Received
   38
   Likes Given
   75

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Nasikia ukinywa juisi ya limao asubuhi na jioni inapunguza hamu ya pombe mpaka inaisha kabisa. Imethibitishwa kisayansi.
   Watcha gonna do when they come for you?

  11. Baba_Enock's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2008
   Location : "On-board MH370"
   Posts : 6,667
   Rep Power : 2201
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   1914

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Makanyagio View Post
   Wana JF,
   Kwa yeyote anejua dawa au mbinu ya kumfanya mlevi kuacha pombe. Nina ndugu yangu yeye bila kilevi cha pombe siku haiendi kabisaa na hii imekuwa inarudisha maendekleo yake nyuma.
   Wanaoijua tiba mnijuze niokoe maisha yake na familia yake.
   Mwache apige kilaji - Maendeleo hayaji kwa kutokunywa pombe bali kwa kukosa mipango madhubuti ya maisha yako mwenyewe!

   "
   Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. "

  12. Makanyagio's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th June 2009
   Location : Nyakato Mwanza
   Posts : 119
   Rep Power : 659
   Likes Received
   14
   Likes Given
   2

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Kwanza niwape thanx. Pili tumeshajaribu mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumuombea, kumshauri, kumwekea vikwazo vya kiuchumi, lakini wapi. Ila Hii ya juisi ya limao ndo nimeisikia leo labda tujaribu hiyo, japo ni kazi kweli kweli maana unaweza kumpleka ng'ombe mpaka kisimani mziki ni kuyanywa hayo maji.
   'There is no fair in this world'

  13. Bigirita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : 3.0758° S, 37.3533° E
   Posts : 13,157
   Rep Power : 171804295
   Likes Received
   4129
   Likes Given
   5895

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Makanyagio View Post
   Wana JF,
   Kwa yeyote anejua dawa au mbinu ya kumfanya mlevi kuacha pombe. Nina ndugu yangu yeye bila kilevi cha pombe siku haiendi kabisaa na hii imekuwa inarudisha maendekleo yake nyuma.
   Wanaoijua tiba mnijuze niokoe maisha yake na familia yake.
   Kama ww unaona kilevi cha pombe ni kibaya
   basi mwambie atumie Bange!!
   * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

  14. Dreamliner's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th January 2010
   Location : Kijijini
   Posts : 2,015
   Rep Power : 1009
   Likes Received
   191
   Likes Given
   194

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Msiache kumpeleka kwenye maombi.. MUNGU sio kiziwi ipo siku atasikia maombi yenu..Pole sana!

  15. Bigirita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : 3.0758° S, 37.3533° E
   Posts : 13,157
   Rep Power : 171804295
   Likes Received
   4129
   Likes Given
   5895

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Dreamliner View Post
   Msiache kumpeleka kwenye maombi.. MUNGU sio kiziwi ipo siku atasikia maombi yenu..Pole sana!
   kwa nn wampeleke? kwani yy mbuzi, si aende mwenyewe!
   * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

  16. Masanilo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd October 2007
   Location : Swat valley, Keta Keta
   Posts : 22,185
   Rep Power : 85897712
   Likes Received
   4159
   Likes Given
   2484

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By gkundi View Post
   Kama ww unaona kilevi cha pombe ni kibaya
   basi mwambie atumie Bange!!
   Another great thinker!

   Kindness is the language which the deaf can hear and the blind can see - Mark Twain
   CCM is enemy of GOD

  17. Luteni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 2,288
   Rep Power : 1078
   Likes Received
   280
   Likes Given
   74

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Baba_Enock View Post
   Mwache apige kilaji - Maendeleo hayaji kwa kutokunywa pombe bali kwa kukosa mipango madhubuti ya maisha yako mwenyewe!

   Ni kweli kabisa jamaa ni genius ile kupata hela ya pombe kila siku inahitaji calculator kubwa lazima ziwe zinachemka kichwani wengine hatuyawezi nikikutana na jamaa huyo nampiga Kili moja ya bariiidiiii.
   Luteni is a True Revolutionist.

  18. Teamo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2009
   Location : KIJIWE SAMRI-BOM BOM
   Posts : 12,300
   Rep Power : 12057
   Likes Received
   914
   Likes Given
   678

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   dawa yake ni kuwa ''womaniser''
   '!....Ahadi za Kiongozi wako Zinatekelezekaa?..SASA NI WAKATI WA UWAJIBIKAJI....!'

  19. Bigirita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : 3.0758° S, 37.3533° E
   Posts : 13,157
   Rep Power : 171804295
   Likes Received
   4129
   Likes Given
   5895

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By Geoff View Post
   dawa yake ni kuwa ''womaniser''
   That is to say if you are a man you must be either of the two, and you cant be both

   Drink or F*
   Last edited by Bigirita; 21st January 2010 at 16:53. Reason: typo
   * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

  20. Teamo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2009
   Location : KIJIWE SAMRI-BOM BOM
   Posts : 12,300
   Rep Power : 12057
   Likes Received
   914
   Likes Given
   678

   Default Re: Msaada dawa ya kuacha pombe

   Quote By gkundi View Post
   That is to say if you are a man you must be either of the two, and you cant be both

   Drink or F*
   Naah!
   ukiwa cha-pombe utaishia kupiga mshindo mmoja na kulala!..utaishia kuzaa watoto wa kike.....!

   wasiokunywa wanasifiwa sana na lediiz
   '!....Ahadi za Kiongozi wako Zinatekelezekaa?..SASA NI WAKATI WA UWAJIBIKAJI....!'


  Page 1 of 39 123 11 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Nifanye nini ili kuacha kabisa mapenzi ??
   By NITIKE NDOSI in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
   Replies: 20
   Last Post: 3rd April 2015, 20:13
  2. Ni njia gani unaweza kutumia kumkamata aliekuibia Android Smartphone
   By Jakha in forum Tech, Gadgets & Science Forum
   Replies: 7
   Last Post: 18th January 2015, 17:42
  3. Replies: 8
   Last Post: 22nd April 2014, 18:36
  4. nitumie njia gani ili niweze kuzidownload hizi video
   By Ford89 in forum Tech, Gadgets & Science Forum
   Replies: 5
   Last Post: 17th March 2013, 09:57
  5. hivi wanaoiba katika benki kwa kutumia mtandao wanatumia njia gani?
   By sajolin in forum Tech, Gadgets & Science Forum
   Replies: 9
   Last Post: 13th April 2012, 14:06

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...