Jamii IntelligenceSerious reports & Discussions on Corruption, Politics etc recommended to our clients! Detailed discussions which you need not to miss
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:
"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"
Wakati huo huo gazeti hilo linaripoti kuwa mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, yeye ameshachukua hatua ya kufungua kesi dhidi ya Reginald Mengi ambapo anadai fidia. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni : Je, katika mpambano huu ile methali ya "wapiganapo tembo nyasi huumia" itatimia au nyasi ndio zitapata fursa ya kustawi zaidi? Je, mpambano huu utaishia kuwa mchezo wa kuigiza au utazitimizia hizo nyasi methali ya "avumaye baharini papa kumbe wengi wapo"?
TAMKO LAKE HILI HAPA:
__________________
"Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon
Last edited by Invisible; 30th April 2009 at 11:36 AM..
Reason: Enclosed the doc
Hatutashinda vita hii kama hatutaangalia mchango wetu na wa wale wanaofanana na sisi katika kulifikisha taifa letu hapa lilipo. Uozo haukuanza na hawa tunaowazungumzia. Tumeuziwa ndege mbovu, vivuko vibovu, vyakula vibovu na wenzetu wakishirikiana katika uovu huo.Tumeuziwa skolaship na wenzetu hao na pale pasipopatikana mnunuzi, wenzetu hao walikuwa tayari asiende mtu. Wenzetu na sisi wenyewe tumeuzia serikali vifaa na bidhaa hewa, tumekataa kulipa kodi, tumehonga mapolisi na mahakimu, tumewahonga wasiojiweza ili tuchukue nafasi ya mwanao aliyefaulu mitihani, tumenunua na kurejesha risiti feki kwa safari ambazo hatukuenda n.k. n.k. Bila kujiangalia na kukubali kuwa katika uozo huu tumo wote hatufiki mbali. Naam, masuala ya EPA, Richmond .......yanaumiza lakini wakati tunawabana WOTE waliohusika ni lazima tupanue wigo na kutuma ujumbe kuwa kwenye vita hii hatutaangalia undugu, kabila, rangi, jinsia n.k. Kinyume cha hivyo huu mchezo wa musical chairs utaendelea hata kama hawa tunaowaita mafisadi papa watadhibitiwa!
Amandla.........
Aweethu...!
FM,
Ni kweli ulichandika. Wengi wetu tunadhani mabadiliko lazima yatokee kwa wengine kwanza. hatufikiri kwamba sisi ni sehemu ya wale wanaotakiwa kuleta mabadiliko kwa manufaa ya jamii yetu. Tunapozungumzia uadilifu, ni lazima uanzie kwa mmoja mmoja na hatimaye itatoa taswira ya taifa zima.
Leo hii kama tungekuwa tunapenda kutii sheria, hata za usalama bara barani tu za kufunga mkanda wa kiti cha gari, kuwa na kizima moto (vyote kwa faida na matumizi yako mwenyewe) je askari wa barabarani wangeanzia kuomba rushwa? na je kama tungeamua kupenda kulipa faini, (tena sh 20,000 tu), si ingesaidia kutujengea utamaduni mpya?
Tungekuwa tunaingia kazini saa 1.30, na kutoka saa 9 au 10, badala ya kupoteza muda mwingi stori za Arsenal na jinsi tulivyokuwa chakari jumamosi iliyopita, si tungekuwa kwenye utamaduni mpya?
Mbadikio ya kweli yanaanzia kwetu wenyewe, hata hapa JF!
Bado naona hakuna News hapa, atuoneshe documents za ufisadi wa Mengi siyo blah blah blah. Hana Jipya huyu baada ya kuona amechemsha kwa kutoa 48 Hrs kama mwenzake Masha sasa kaona ajifute sura kwa "mikono yenye Majivu". Hana jipya kuhusu Mengi mpaka hapo.
Documents kagawa kama njugu, uko wapi wewe! Haya Invisible tuwekee documents alizotowa RA hapo Kempinski, maana tuliochungulia TBC tumeona akionesha madocuments aliyosema katayarisha kuyagawa.
Come to your sense, hivi swala ni kulipia ama ni maudhui yaliyomo ndani ya Kipindi? Mbona mzee RICHMONDULI ( EL) alikatizwa alipo kuwa anataka kujisafisha alivyo pigwa chini? Unadhani hakuwa na Pesa ya kulipia?
Hii inafikisha ujumbe mwingine wa nani mtawala wa nchi hii.. Poor JK Raisi wa bendera! / (ceremonial president)
Kesi ya RA na ya EL ziko tofauti. EL alishambuliwa bungeni hivyo sehemu muafaka ya kujitetea kwanza ilikuwa bungeni na sio kwenye media.
RA kashambuliwa kwa TV hivyo ni muafaka kabisa kupewa airtime kwenye TV ajitetee.
On the other side, marudio ya TBC1 ambayo hata hivyo yalikuwa edited na kampuni inayojiita "I Plus Communications" yaliyonyofoa kipengele ambapo RA alikanusha kutajwa kwenye ripoti ya Mwakyembe.
Hata hivyo ITV wao walionesha kipengele hicho tu na kuachana na vipengele vingine ambapo bosi wao ameshushuliwa.
Kwa upande mwingine ujasiriamali wa Mengi nao ni wa kutia mashaka maana inaonesha anaposhindwa kibiashara anakimbilia kwenye uzalendo. Mengi ni msomi so I expected he could do better than that.
Sio RA tu, kuna wafanyibiashara wengine pia ambao wamemlalamikia Mengi kwa tabia ya kukimbilia kwenye uzawa pale anaposhindwa kunegotiate.
Ila RA ametoa kali kuhusu Mengi kulia faulo ya viwanja vya City center kwamba wanamiliki Wahindi tu ... kisha akapewa kiwanja na Mwinyi jirani na Souther Sun hotel ... then baadae akakiuza kwa ... (drum roll) ... MHINDI!
Na kitendo cha kuwaingiza mkenge wanahisa wa NICO kwa kuwauzia kiwanda bomu cha familia yake huko Moshi kwa kweli kinamuweka daraja moja na mafisadi. Huyu angekuwa CHADEMA ni wazi angehakikisha ndugu zake wanapewa viti maalumu Bungeni.
Mechi nzuri sana hii ... nasubiri kuona nani atakayeanza kutinga mahakamani.
__________________ Don't compare yourself with anyone in this world. If you do so, you are insulting yourself.
Guys this fourth phase gorvernment is full of flews ...kila siku maneno tu mara EPA,mengi ,mafisadi...can i ask? when will we get our holes back to job...
i am afraid usalama wa nchi unaelekea kubaya ...wananchi watagawanyika...
NAOMBA VYOMBO HUSIKA VIPIGE MARUFUKU WOTE MENGI..ROSTAM NA WENZAKE ...KUONGELEA HUU UBISHI..KAMA KWELI WANAPENDA NCHI HII KILA MMOJA APELEKE USHAHIDI WAKE KWA WAKATI WAKE BILA KUTAKA KAMERA,,
Usichanganye channel, RA anamjibu Mengi kama alivyomjibu Mtikila akaufyata na Mengi hali kadhalika, nilishawahi kuandika humu kuwa Mengi kawa pweza, anajipalilia mkaa yeye mwenyewe! na sasa ndio atakiona cha mtema kuni...Hii ni pati gazeti, senema kamili bado!
Guys this fourth phase gorvernment is full of flews ...kila siku maneno tu mara EPA,mengi ,mafisadi...can i ask? when will we get our holes back to job...
i am afraid usalama wa nchi unaelekea kubaya ...wananchi watagawanyika...
NAOMBA VYOMBO HUSIKA VIPIGE MARUFUKU WOTE MENGI..ROSTAM NA WENZAKE ...KUONGELEA HUU UBISHI..KAMA KWELI WANAPENDA NCHI HII KILA MMOJA APELEKE USHAHIDI WAKE KWA WAKATI WAKE BILA KUTAKA KAMERA,,
Wananchi wameshagawanyika mkuu...walalahoi wengi wanangojea siku Mengi aseme anagombea Urais au Ubunge.
__________________ "Our cherished rights of liberty and equality depend on the active participation of an awakened electorate.", Barack H. Obama. Presidential Announcement Speech, Springfield, Ill, Feb 10, 2007.
Guys this fourth phase gorvernment is full of flews ...kila siku maneno tu mara EPA,mengi ,mafisadi...can i ask? when will we get our holes back to job...
i am afraid usalama wa nchi unaelekea kubaya ...wananchi watagawanyika...
NAOMBA VYOMBO HUSIKA VIPIGE MARUFUKU WOTE MENGI..ROSTAM NA WENZAKE ...KUONGELEA HUU UBISHI..KAMA KWELI WANAPENDA NCHI HII KILA MMOJA APELEKE USHAHIDI WAKE KWA WAKATI WAKE BILA KUTAKA KAMERA,,
Unacho kisema ni sawa, lakini kwa jinsi ufisadi ulivo ota mizizi Tanzania, wacha kamera ziwepo ili watanzania wengi waone na waweze kupembua pumba na mchele, hii ita tusaidia sana kuongeza uamsho kwa wananchi kutambua kwamba tunaliwa nahivyo waweze kufanya maamzi sahihi katika sanduku la kura! Please please wacha iendelee.
Kwa upande mwingine wakisema iende kimya kimya, ndo hivo mafisadi wataiminya huko chini kwa chini wadanganyika tutaendelea kudanganywa kama kawa!
Na ukiangalia vyema Nia nyingine ya RA leo ni kuataka Mengi apeleke ushaidi wake Polisi ili wakaufisadi na mchezo uishe!
poor mengi .! He thought he had the president backing....now today the colours are clear showing rais yuko upande gani kwenye hii sinema......kama rostam hangekuwa na uungwaji mkono wa chama na serikali asingepata air time tbc ..hata kwa kulipia..
nadhani mnajuwa kamati kuu ya ccm imekaa jana ikulu....leo tumejuwa kuwa kamati kuu imeamua kumuunga mkono rostam.....rostam huwa yupo makini sana kabla ya kuongea ..hasa ikijulikana kuwa yeye ni mjumbe wa kamati kuu......angeweza kumjibu mengi kitambo...lakini amechagua kumjibu baada ya kutoka kwenye kikao cha kamati kuu....