Tamko la Rostam dhidi ya Mengi na yatokanayo - Page 123 - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jamii Intelligence


Jamii Intelligence Serious reports & Discussions on Corruption, Politics etc recommended to our clients! Detailed discussions which you need not to miss


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 30th April 2009, 10:11 AM  
Tamko la Rostam dhidi ya Mengi na yatokanayo
Companero Companero is offline 30th April 2009, 10:11 AM

Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:

"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"

Wakati huo huo gazeti hilo linaripoti kuwa mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, yeye ameshachukua hatua ya kufungua kesi dhidi ya Reginald Mengi ambapo anadai fidia. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni : Je, katika mpambano huu ile methali ya "wapiganapo tembo nyasi huumia" itatimia au nyasi ndio zitapata fursa ya kustawi zaidi? Je, mpambano huu utaishia kuwa mchezo wa kuigiza au utazitimizia hizo nyasi methali ya "avumaye baharini papa kumbe wengi wapo"?

TAMKO LAKE HILI HAPA:


__________________
"Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon

Last edited by Invisible; 30th April 2009 at 12:36 PM.. Reason: Enclosed the doc

 
Companero's Avatar
Companero
JF Senior Expert Member
Points: 568,593, Level: 100 Points: 568,593, Level: 100 Points: 568,593, Level: 100
Activity: 28% Activity: 28% Activity: 28%
Join Date: Sat Jul 2008
Posts: 1,840
Thanks: 211
Thanked 440 Times in 240 Posts
Views: 43675
Reply With Quote
  #1221  
Old 8th May 2009, 07:30 PM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is offline
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,761,988, Level: 100 Points: 12,761,988, Level: 100 Points: 12,761,988, Level: 100
Activity: 83% Activity: 83% Activity: 83%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,229
Thanks: 7,723
Thanked 4,133 Times in 1,153 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default Re: Rostam akabidhi vielelezo TAKUKURU

Lula wa Ndali Mwananzela - Raia Mwema

AMETIKISA kiberiti tena na waliotikisika wametisika. Alisema atazungumza waliotaka kusikia wamesikia. Waliokuwa wanajali atakachosema sasa hivi wanamuona shujaa!

Siyo mimi. Nilikataa mwaka jana kuwa Rostam ni mtu ambaye anaweza kuitikisa nchi kwa maneno yake. Niliandika wakati ule kuwa “Sipendi Rostam atikise kiberiti bungeni”. Baada ya majibu yake niliandika makala nyingine ya “Mtu mzima hatishiwi nyau”. Nadhani inabidi nibadili msimamo huo.

Mkutano wake na waandishi wa habari Jumapili iliyopita, umenihakikishia kabisa kuwa msimamo wangu wa awali ulikuwa na makosa. Sikujua kuwa Mbunge huyo ana nguvu kuliko serikali na ujasiri kuliko wa askari. Sasa nimetambua kwa uhakika kabisa Rostam ni mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye amekubuhu kwa kila kipimo.

Nimefikia hatima hiyo baada ya kusikia madai yake mazito aliyoyatoa dhidi ya serikali siku ya Jumapili, madai ambayo kimsingi yanaweza kuwa yamethibitisha tuhuma za ufisadi zinazotolewa juu yake. Yamethibitisha kuwa kama kiongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kama mfanyabiashara hana maadili ya uongozi kwani ameituhumu serikali ya chama chake hadharani na pasipo utata kuwa ni goi goi isiyofuata utawala wa sheria. Na zaidi ya yote amejiweka juu ya serikali hiyo.

Madai hayo mazito dhidi ya serikali yanapaswa kuangaliwa kwa ukaribu na kulaaniwa na kila Mtanzania. Ni madai ambayo ndani yake yamethibitisha kile ambacho wengine tumeamua tukikohofia kwa muda mrefu kuwa kuna tatizo ndani ya serikali. Ni madai mazito ambayo hayawezi kuachwa yapite bila kumulikwa kwa ukaribu.

Ninafahamu vizuri kuwa alisimama kumjibu Reginald Mengi aliyetangulia kutoa tuhuma dhidi yake na ya kuwa ukimsikiliza kwa karibu unaweza kabisa kuamini alikuwa anataja “ufisadi” wa Mengi. Na wala siandiki haya ili kumpamba Mengi.

Ukisogea kwa karibu na kuanza kuangalia kile alichosema utagundua kuwa Rostam amesimama akitoa tuhuma nzito dhidi ya serikali yetu, serikali ambayo tunaamini ilichaguliwa na wananchi na ipo kihalali. Tuhuma hizi ni nzito na haziwezi kuachwa zilivyo.

Kajisimamisha kinyume na serikali.

Kitu cha kwanza ambacho unaweza kukiona kwenye maelezo yake ni geresha ya heshima. Anatangaza kutambua kuwa mawaziri wa serikali wamekwisha kuzungumzia jambo hili pale anaposema “Naelewa kwamba tayari Serikali na vyombo vyake vimeshatoa kauli za kumuonya Mengi kuhusu kauli alizozitoa. Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utawala Bora, Mheshimiwa Sofia Simba, amemtahadharisha Mengi kwamba kitendo chake cha kutumia vibaya vyombo vyake vya habari kuwachafua washindani wake wa kibiashara hakikubaliki.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amesema Wizara yake inafanya uchunguzi wa matamshi ya Mengi kwa kuupitia mkanda wenye maelezo yake na ikibainika amevunja sheria atachukuliwa hatua.”

Anaendelea na kutoa mfano wa kauli ya Waziri Mkuu pamoja na msimamo wa Jeshi la Polisi. Kimsingi, alikiri kuwa serikali imeingilia kati na kama Mbunge aliyeapa kuilinda Katiba ya Tanzania alitakiwa akae kimya na kuviacha vyombo vya sheria kufanya kazi yake.

Rostam hakufanya hivyo kwani vyombo hivyo kwake viko chini yake. Anasema: “ Pamoja na kuheshimu na kuthamini maelezo hayo ambayo yamemuumbua Mengi, lakini bado nahisi binafsi nina wajibu wa kutoa maelezo ya kina kuhusu kiherehere hiki cha Mengi.”

Anachosema ni kuwa hata kama serikali imeingilia kati na imekwisha kutoa msimamo wake, yeye kama Rostam yuko juu ya serikali hiyo na hivyo haamini kuwa serikali inaweza kumdhibiti Mengi na hivyo anaongeza uzito wake binafsi kwenye suala hilo. Kwa nguvu gani aliyonayo?

Uwezo wa kuchagua msemaji wa Watanzania ameutoa wapi?

Katika tamko lake akahoji Mengi amepata wapi ridhaa ya kuzungumza na wananchi? Akauliza hivi “Mengi ambaye watu wanajiuliza amepata wapi uhalali wa kujifanya msemaji wa Watanzania wakati hawajawahi kumchagua katika nafasi yoyote na hivyo hana ridhaa yao.”

Anachojaribu kusema hapa ni kuwa kama mtu hajachaguliwa basi hawezi kuzungumza au kutoa kilio cha Watanzania. Kwamba, hadi uwe umewahi kuchaguliwa basi usijaribu kuwapinga mafisadi au kupambana nao kwani kwa kufanya hivyo hauna ridhaa.

Ina maana maoni ya wahariri wa magazeti, radio na televisheni, viongozi wa dini na watu wa taasisi mbalimbali hawana haki wala uwezo wa kuzungumza na kutoa kilio cha Watanzania kwa sababu moja tu kuwa hawakuchaguliwa! Anataka watu waamini kuwa ukichaguliwa ndiyo una ridhaa ya kutoa kilio cha sauti za Watanzania. Kweli?

Kama ni kweli tungemuuliza Mhe. Rostam, katika Bunge la Muungano ambapo yeye ni mjumbe wake ni lini alisimama kutetea maslahi ya Watanzania? Ni lini alikemea ufisadi wa Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, Tangold, au EPA? Ni lini yeye mchaguliwa wetu alisimama kutetea wale vijana waliotelekezwa na serikali ya chama chake kule Ukraine? Ni lini alisimama kutaka waliohusika wawajibishwe katika vifo vya watoto 19 kwenye mkoa wake wa Tabora?

Ni lini Rostam amesimama kuwatetea wanafunzi wa vyuo vyetu vikuu ambao kila mwaka wanalazimika kugoma kwa sababu ya uongozi mbovu na sera mbovu ya elimu ya juu? Kuchaguliwa peke yake si ridhaa ya wananchi kwani wengine wamechaguliwa baada ya hadaa ya wananchi hao! Kwani yeye mwenyewe alipitaje kwenye kura za maoni za CCM? Au tumkumbushe?

Ati Mengi ndiye amemfanya avunje ukimya.

Mheshimiwa mchaguliwa Rostam akionyesha kuwa ana uchungu na nchi hii alisema kwenye tamko lake: “…sidhani itakuwa ni haki kuendelea kukaa kimya na kumwacha (Mengi) afanikishe malengo yake hayo. Hatuwezi kukaa kimya maana kufanya hivyo kutakuja kuligharimu vibaya sana Taifa letu.”

Kwa haraka haraka unaweza kuamini kuwa tishio kubwa la nchi yetu ni Mengi! Kiasi kwamba hadi Rostam kuja kuzungumza basi Mengi anaitisha sana nchi hii. Ukweli ni kuwa, alichofanya Mengi kinawatisha mafisadi waliokubuhu nchini mwetu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakionewa haya hata kutajwa majina. Ndiyo sababu Rostam kaamua kuzungumza.
Hebu fikiria; hakuzungumza kwenye suala la Kagoda, hajazungumza juu ya wizi wa Benki Kuu, hajazungumza juu ya wizi wa rada, hajazungumza juu ya rafiki yake Andrew Chenge na suala la Vijisenti, hajazungumza suala la Richmond na Dowans, kote huko mchaguliwa amekaa kimya ati leo Mengi kumtaja ameamua kuvunja “ukimya” kwa maslahi ya nchi? Kwa sauti yake mwenyewe amethibitisha ufisadi wake.

Rostam amevunja ukimya si kwa sababu ana uchungu na nchi (yawezekana anao) lakini kwa sababu mirija yake iliyochomekwa kwa Watanzania inatishiwa kukatwa. Na hili linamtisha yeye na wengine.

Ugomvi wa Mengi na watu kadhaa

Mojawapo ya mifano inayotolewa mara nyingi ni ya “ugomvi wa Mengi” na watu mbalimbali na kuwa Mengi alitumia mambo hayo kuyafanya ya kitaifa.
Niliposikiliza na baadaye kusoma pole pole majina ya hao ambao Mengi aligongana nao ninaamini kuwa si tu alipaswa kugongana nao bali walikuwa ni watu sahihi kugongana nao (ukiondoa mmoja au wawili). Sitaawangalia kwa kirefu lakini majina yao yanafahamika. Wapo: Wilson Masilingi, Shamim Khan, Edward Lowassa, Basil Mramba, Habari Corporation, Yusuph Manji, Adam Malima, Tanil Somaiya, Lawrence Masha na mwenyewe Rostam Aziz.
Hili mbona ni genge la kushtua sana kugongana na mtu mmoja. Kwenye majina hayo naweza kuwaondoa watu wawili tu kuwa yawezekana mgongano wao ulikuwa wa kikazi lakini wengine wote aidha wamehusika na uporoja wa nchi yetu au bado wanahusika na uporaji huo!
Badala ya kuona kuwa mgongano huo ni wa Mengi dhidi ya hao kwa nini tusiuone kuwa ni mgongano wa watu kadhaa dhidi ya mtu mmoja? Inakuwaje, vigogo wa serikali na chama wote wawe wanagongana na mtu mmoja tu lakini hadi hivi sasa wameshindwa kumkamata kwa uhalifu au kumfikisha mahakamani na wamebakia kuziandama biashara zake?

Dhamira yake njema au kitu kingine?

Rostam ameelezea katika tamko lake sababu kubwa ya “kumuumbua” Mengi kuwa anafanya hivyo kwa sababu ya “kulinusuru Taifa lisije likatumbukia kule Mengi anakotaka kulipeleka.”

Nimesema hapo juu, juu ya kuvunja kwake ukimya. Hata hivyo, nitakuwa nina wazimu nikiamini kuwa Rostam amefanya hivyo ili “kulinusuru taifa”.
Ndugu zangu, Rostam ana nafasi ya kulinusuru Taifa kutoka mikononi mwa mafisadi wengine. Kwanza kabisa angetutendea mema kweli kama angetuambia Dowans ni kina nani na kwanini tusinunue mitambo yao; Rostam angeweza kutusaidia kweli kwa kupigana na ufisadi wa Benki Kuu au kwa kuleta mswada bungeni wa sheria ambayo ingeipa nguvu taasisi ya Usalama wa Taifa; au kwa kuleta mabadiliko ya Sheria ya Madini au mambo ya fedha.

Kama Mbunge ana nafasi ya kulinusuru Taifa akiwa bungeni na pia akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa. Sehemu hizo zote, Rostam hajasimama kujenga hoja au kuonekana akilitetea taifa.
Iweje leo aone tishio kubwa ni Mengi? Hivi haoni kilichotokea Benki Kuu? Wakati Dk. Daudi Ballali ametoroshwa kwenda Marekani mbona hakusimama kupiga kelele arudishwe? Saileth Vithlani yule dalali wa rada si ametoroka kwenda anakojua mbona Rostam hajapiga kelele? Hii dhamira yake njema ya “kulinusuru taifa” ina walakini. Haiwezekani mtu atake kulinusuru taifa wakati maslahi yake ndiyo yako hatarini.

Rostam angesema tu kuwa anafanya hivyo ili “kunusuru” biashara zake! Tungemuelewa wala tusingegongana.

Kwa maneno yake anakiri tabia yake mwenyewe.

Rostam anasema hivi katika maelezo yake “Wanasaikolojia wanasema mtu anapotuhumu wengine kuwa na tabia fulani, mara nyingi huwa yeye ndiye mwenye tabia hizo”.

Katika maelezo yake anamtuhumu Mengi kuwa ana “tamaa, uroho, wivu, chuki, fitina, ubaguzi na ubinafsi uliovuka mipaka” na kuwa ni “nyangumi wa ufisadi” nchini.

Kama maneno aliyoyasema kuhusu wanachosema wanasaikolojia je yawezekana kwa kile anachomtuhumu Mengi yeye naye ndiyo hicho hicho? Au anataka kusema kuwa ukweli wa maneno hayo ya wanasaikolojia yana ukweli kwa watu wengine wote isipokuwa Rostam? Kwa upendeleo gani alionao mbinguni?

Ukusanyaji wa taarifa za watu

Kati ya vitu ambavyo vimeonyesha ni jinsi gani Rostam ana nguvu na uwezo mkubwa ni pale ambapo ameweza kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali kuhusu kampuni za Mengi, fedha na masuala mbalimbali yanayohusiana nayo.

Ni wazi kuwa hakufanya kazi hiyo yote peke yake, na bila ya shaka, ana watu waliomsaidia kufanya hivyo. Hii ina maana kuwa Rostam mchaguliwa, mwanasiasa na mfanyabiashara safi ameweza kupata taarifa za kibenki (akaunti na kiasi cha fedha) za raia wa mitaani ambaye hajachaguliwa na mwananchi yeyote!

Hii ina maana ya kuwa Rostam ana watu hadi kwenye taasisi za benki na vyombo mbalimbali vya umma ambao wamemfanyia kazi hiyo. Siamini kama watakuwa wamefanya kazi hiyo bure!

Wakati Mengi alipotoa tuhuma zake hakutoa data! Wengi walifikiri ni kwa sababu hazipo lakini nina uhakika alijua kuja na data huwezi kuweka hadharani bila kuonyesha kuwa umevunja sheria kuzipata data hizo!
Ninatuhumu wazi wazi na hadharani kuwa Rostam, Mbunge wa Jamhuri ya Muungano amevunja sheria za mambo ya fedha na nyingine kwa kutoa taarifa za wateja wa benki.

Lakini pia kwa kufanya hivyo amethibitisha kuwa kama ameweza kupata taarifa zote hizo za makampuni ya Mengi ina maana anaweza kupata taarifa za Mtanzania yoyote yule anayejitokeza kumpinga, hizi ni nguvu za kutisha!

Ina maana ya kwamba, wale wanasiasa wote aliowasaidia kuingia madarakani wako mikononi mwake na siku wakimtibua tu atayaweka hadharani. Nakumbuka alivyomuumbua Mtikila kwa mkopo wa milioni tatu!

Uchungu wa bilioni 28 za mikopo

Kati ya vitu ambavyo vimenifurahisha lakini wakati huo huo kuthibitisha aina fulani ya unafiki ni pale anapoonyesha uchungu wa fedha ya mkopo halali ambao alidai kuwa Mengi anadaiwa.

Anasema hivi kuhusu mkopo huo: “Fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na hesabu ya riba zinafikia takriban bilioni 28. Hivi ndivyo Mengi alivyochangia kuifilisi NBC, benki ya wananchi masikini wa Tanzania. Fedha hizi zilizochukuliwa na Mengi, shilingi bilioni 28, zinaweza kujenga shule za sekondari 100 ambazo zingeweza kuwanufaisha watoto wa kimasikini wa Tanzania.”

Binafsi nilicheka na kutikisa kichwa! Rostam ana uchungu wa bilioni 28! Hivi zilipochotwa bilioni 133 toka EPA mbona Rostam hakusema kitu? Waliponunua dege kwa bilioni karibu 50 Rostam alikuwa wapi? Vipi kuhusu rada ya bilioni 40 wakati 21 zikigawiwa kwa makuwadi wa ufisadi Rostam mbona hakusimama kutetea? Rostam alikuwa wapi wakati wengine tunaongoza mapambano ya kupinga kutumia bilioni 60 kununua mitambo ya Dowans wakati Dowans waliingia nchini na kuandikishwa kwa taarifa za uongo?

Zaidi ya yote, ninajiuliza kama Rostam katika uwezo wote alionao ameweza kutupatia taarifa za akaunti za Mengi na madeni ya Mengi na yalitoka wapi na yakawa vipi, ameshindwa nini kujitolea kutumalizia suala la Kagoda?

Rostam ana uwezo na mbinu za kujua wamiliki wa Kagoda na fedha hizo zilienda vipi, wapi, na nani, kwanini DPP asimuombe Rostam kuendesha uchunguzi huo na kutoa taarifa kwa umma jinsi alivyofanya juzi? Hapo tu ndipo nitaamini kuwa kweli Rostam ana uchungu wa masikini wa nchi hii!

Hitimisho

Kimsingi ukweli unabakia kuwa ukweli, Rostam ni mtu mwenye nguvu nchini bila ya shaka kuliko mtu mwingine yeyote.

Asili ya nguvu zake hizo ni ujuzi wa mambo mbalimbali juu ya wanasiasa na watumishi mbalimbali. Ni yeye anayejua yaliyotokea wakati wa uchaguzi uliopita kwa vile alikuwa Meneja wa Kampeni).

Ninampa changamoto kuwa kama kweli yeye ni mzalendo wa kweli, ajitokeze na aeleze vyanzo vyote vya fedha za kampeni ya CCM.

Ninampa changamoto pia ajitokeze na kuliambia taifa ni makampuni mangapi yaliyo katika jina lake yeye mwenyewe ili angalau tujue anaposema ametoa ajira kwa watu 6000 tujue kweli ni yeye ndiye aliyefanya hivyo.

Zaidi ya yote, ninatoa changamoto kwa Rostam arudishe fedha yoyote ambayo hakuipata kihalali au anajua haikupatikana kihalali.

Vinginevyo, ninaamini kwa maneno yake mwenyewe na kwa kauli zake amethibitisha kabisa tuhuma za ufisadi wake. Amethibitisha ana nguvu za ajabu, anaweza kuitetemesha nchi na kwa hakika hakuna kiongozi yeyote wa serikali ya nchi hii anayeweza kumnyoshea kidole kwani wote wako mikononi mwake. Nina shaka inawezekana akawa na nguvu kuliko tunavyoweza kufikiria.

Labda siku moja kutakuwa na mtu jasiri ambaye atatuambia asili ya nguvu zake ili hatimaye tuweze kumdhibiti kama alivyodhibitiwa Samson. Vinginevyo, tukikubali hadaa zake kwa wananchi basi tusije kushangaa akiwashambulia mashujaa wa nchi hii!

Binafsi bado ninamuangalia kwani siamini kama anauwezo wa kulipigisha magoti taifa. Sijui labdo anao.

__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #1222  
Old 8th May 2009, 09:27 PM
Nemesis Nemesis is offline
Nemesis has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Wed Feb 2008
Posts: 2,051
Thanks: 84
Thanked 185 Times in 93 Posts
Rep Power: 67
Nemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the rough
Default Re: Rostam akabidhi vielelezo TAKUKURU

ummh! halafu alipewa kipindi maalumu TBC1, hebu tufikirie kwa pamoja nani aliyewahi kupewa kipindi maalumu kwenye TV ya taifa (toka TVT na sasa TBC) zaidi ya Rais na Waziri Mkuu? Je, Rostam ananguvu sana au zaidi ya Rais na Waziri Mkuu mpaka kupewa kipindi maalumu aongee upuuzi wake huu?

Mungu ibariki Tanzania
Reply With Quote
  #1223  
Old 8th May 2009, 09:31 PM
Dar Es Salaam's Avatar
Dar Es Salaam Dar Es Salaam is offline
Dar Es Salaam never gonna say never
JF Senior Expert Member
Points: 135,605, Level: 100 Points: 135,605, Level: 100 Points: 135,605, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sun Feb 2008
Posts: 1,432
Thanks: 1
Thanked 3 Times in 3 Posts
Rep Power: 0
Dar Es Salaam is infamous around these parts
Default Re: Breaking news;ROSTAM AKABIDHI VIELELEZO VYA MENGI TAKUKURU ;PATAMU

Quote:
View Post
Watz wengi wa kawaida wapo nyuma ya Mengi! Mengi analitambua hilo!

RA anaonekana ni fisadi mbele ya watu wa kawaida!
Mie simo!
__________________
Parti Pris
Reply With Quote
  #1224  
Old 8th May 2009, 09:32 PM
Dar Es Salaam's Avatar
Dar Es Salaam Dar Es Salaam is offline
Dar Es Salaam never gonna say never
JF Senior Expert Member
Points: 135,605, Level: 100 Points: 135,605, Level: 100 Points: 135,605, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sun Feb 2008
Posts: 1,432
Thanks: 1
Thanked 3 Times in 3 Posts
Rep Power: 0
Dar Es Salaam is infamous around these parts
Default Re: Rostam akabidhi vielelezo TAKUKURU

Quote:
View Post
ummh! halafu alipewa kipindi maalumu TBC1, hebu tufikirie kwa pamoja nani aliyewahi kupewa kipindi maalumu kwenye TV ya taifa (toka TVT na sasa TBC) zaidi ya Rais na Waziri Mkuu? Je, Rostam ananguvu sana au zaidi ya Rais na Waziri Mkuu mpaka kupewa kipindi maalumu aongee upuuzi wake huu?

Mungu ibariki Tanzania
Unaona donge?
__________________
Parti Pris
Reply With Quote
  #1225  
Old 8th May 2009, 09:37 PM
Nemesis Nemesis is offline
Nemesis has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Wed Feb 2008
Posts: 2,051
Thanks: 84
Thanked 185 Times in 93 Posts
Rep Power: 67
Nemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the rough
Default Re: Rostam akabidhi vielelezo TAKUKURU

Quote:
View Post
Unaona donge?
siyo kuona donge! jambo lisilo la kawaida linapotokea lazima uhoji. Exchange of bitter words btn two citizens haipaswi kushabikiwa na Serikali. Hata hivyo hoja yangu ni vipi Rostam apewe kipindi maalumu kwenye TV ya Taifa ili aogee upuuzi wake?

Mkuu nimeuliza swali ni nani aliyewahi kupewa kipindi maalumu TVT or TBC zaidi ya Rais na Waziri Mkuu?
Reply With Quote
  #1226  
Old 8th May 2009, 09:45 PM
Binti Maringo Binti Maringo is offline
Binti Maringo Thinking!
JF Senior Expert Member
Points: 710,591, Level: 100 Points: 710,591, Level: 100 Points: 710,591, Level: 100
Activity: 7% Activity: 7% Activity: 7%
 
Join Date: Wed Jul 2007
Posts: 2,609
Thanks: 46
Thanked 168 Times in 129 Posts
Rep Power: 28
Binti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enoughBinti Maringo will become famous soon enough
Send a message via MSN to Binti Maringo
Default Re: Breaking news;ROSTAM AKABIDHI VIELELEZO VYA MENGI TAKUKURU ;PATAMU

Quote:
View Post
Nyie subirini tu.. mtasikia Waziri Masha anasema Polissi wanafanyia kazi na Sofia Simba kumpongeza RA kwa kuisadia serikali.. na mwisho sitoshangaa mkasikia Mengi ametiwa pingu na watasema ni utawala wa sheria... what Rostam wants, Rostam gets! Hakuna mtu anayeweza kumkatalia kitu. Na huu yawezekana ukawa ni mwisho wa Mengi as we know it.

Niliuliza jana kama RA ana watu kwenye usalama.. majibu yake nayo yanatisha!

What do you mean by that?....Ni kwamba mwisho atauliwa au mwisho kwenye nini?Kwani mengi ni politician au business man?....
__________________
Nothing shall delay my miracles!...
Reply With Quote
  #1227  
Old 9th May 2009, 07:09 PM
Bulesi Bulesi is online now
Bulesi not satisfied until justice is done
JF Premium Member
Points: 109,241, Level: 100 Points: 109,241, Level: 100 Points: 109,241, Level: 100
Activity: 28% Activity: 28% Activity: 28%
 
Join Date: Wed May 2008
Posts: 1,365
Thanks: 114
Thanked 269 Times in 178 Posts
Rep Power: 24
Bulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enoughBulesi will become famous soon enough
Default Re: REGI MENGI: How dareful is he??

Quote:
View Post
naona mnapiga kelele nyingiii

hivi mnajua kama Rostam alikuwa SWAHIBA mkubwa sana wa MENGI?
GT acha spin zako usituharibie mjadala; toka lini Rostam na Mengi walikula meza moja? Swahiba wa Rostam ni LOWASSA na Gulam Dewji baba wa mbunge wa Singida mjini na ndio maana alimsaidia yule kijana kununua ubunge wa Singida mjini!!
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
dhidi, la, mengi, rostam, tamko, yatokanayo


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Barack Obama's 100 Days Press Conference SpK International Forum 7 2nd May 2009 04:09 AM
A Report on CIA Infiltration and Manipulation of the Mass Media Shy Habari na Hoja mchanganyiko 1 21st April 2009 02:46 PM
Ikulu yaahirisha Press Conference Halisi Matangazo madogomadogo 10 1st July 2008 05:24 PM
ANC 52nd National Conference - LIVE Invisible Habari na Hoja mchanganyiko 9 17th December 2007 03:47 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 12:34 AM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com